Hakimiliki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 09 Mar 2026 20:09:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Hakimiliki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba kuendesha operesheni ya jezi feki https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/simba-kuendesha-operesheni-ya-jezi-feki/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/simba-kuendesha-operesheni-ya-jezi-feki/#respond Sun, 08 Mar 2026 09:57:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14407 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imeendelea kutoa malalamiko yake kuhusu kuwapo kwa jezi feki zenye nembo ya klabu hiyo zinazoendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini na kuahidi kuendesha oeperesheni maalum.Taarifa ya klabu ya Simba iliyotolewa Jumamosi Machi 7, 2026 imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na mzabuni wa jezi, Kampuni ya Jayrutty Investment […]

The post Simba kuendesha operesheni ya jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imeendelea kutoa malalamiko yake kuhusu kuwapo kwa jezi feki zenye nembo ya klabu hiyo zinazoendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini na kuahidi kuendesha oeperesheni maalum.
Taarifa ya klabu ya Simba iliyotolewa Jumamosi Machi 7, 2026 imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na mzabuni wa jezi, Kampuni ya Jayrutty Investment imebaini kuwapo kwa jezi hizo sokoni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Simba na Jayrutty, jezi hizo ni zile ambazo zilitumiwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu yaani pre season.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa jezi hizo hazikuandaliwa kwa ajili ya mashabiki bali ni wachezaji pekee kwa ajili ya kipindi cha pre season.
Uongozi wa Simba na Jayrutty wamebainisha kuwa hakuinufaishi timu wala mzabuni badala yake wanaonufaika ni wezi kwani kitendo hicho ni uhujumu uchumi si kwa klabu tu bali hata nchi.
Katika kukabiliana na tatizo klabu kupitia taarifa hiyo imeahidi kuendesha operesheni maalum ya kukamata jezi feki itakayoanza Jumatatu ya Machi 9, 2026.

“Kuanzia sasa yeyote atakayekutwa anatengeneza, kuuza au kununua jezi hizo atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.


Hii si taarifa ya kwanza kwa Simba na Jayrutty kulalamikia kuwapo kwa jezi feki, Desemba mwaka jana, Simba kupitia msemaji wa klabu hiyo, Ahmed Ally walitoa taarifa ya punguzo la bei ya jezi sambamba na kutoa tahadhari ya kuwapo kwa jezi feki katika mikoa kadhaa nchini.

The post Simba kuendesha operesheni ya jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/simba-kuendesha-operesheni-ya-jezi-feki/feed/ 0
Simba wakataa jezi feki, washusha bei https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/simba-wakataa-jezi-feki-washusha-bei/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/simba-wakataa-jezi-feki-washusha-bei/#respond Wed, 17 Dec 2025 12:20:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14183 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba kwa kushirikiana na Kampuni ya JayRutty imetangaza punguzo la bei ya jezi zake katika kipindi cha Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya huku wakihimiza kukataa jezi feki.Punguzo hilo lililotangazwa Jumanne hii Desemba 16, 2025 linahusisha bei ya jezi kutoka Sh 45,000 hadi Sh 12,000 kwa jezi za ligi […]

The post Simba wakataa jezi feki, washusha bei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba kwa kushirikiana na Kampuni ya JayRutty imetangaza punguzo la bei ya jezi zake katika kipindi cha Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya huku wakihimiza kukataa jezi feki.
Punguzo hilo lililotangazwa Jumanne hii Desemba 16, 2025 linahusisha bei ya jezi kutoka Sh 45,000 hadi Sh 12,000 kwa jezi za ligi na kimataifa kwa jezi za watu wazima na za watoto ambazo pia zitakuwa mitaani.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo, Ahmed Ally, uamuzi huo ni katika hatua ya klabu kutaka kwenda sawa na dunia inavyokwenda lakini hapo hapo wanapambana na jezi feki.
Ally alisema kwamba kama kuna wanachama wa Simba walikuwa wakinunua jezi feki kwa Sh 15,000 sasa wataipata jezi ambayo ni original yaani si feki kwa Sh 12,000.
Alisema kwamba huu ni wakati wa kuvaa jezi original na kufafanua kwamba bei ya punguzo inaanza Desemba 16, 2025 na itakwenda hadi Januari 30, 2026 muda ambao ni sawa na siku 45 kwa wateja kufaidika na ofa hiyo.
Akizungumzia upatikanaji wa jezi hizo, Ally alisema wameamua kurahisha mambo ambapo wateja wataipata kupitia mitandao ya simu kwa kulipia kupitia namba 61223807 na baada ya hapo watakwenda kwenye ofisi ya Shirika la Posta au ofisi za JayRutty.
Kwa mujibu wa Ally, mteja ataruhusisiwa kununua jezi kwa idadi yoyote anayotaka na kuchagua rangi au saizi inayompendezea wakati akifika kwenye ofisi kuchukua jezi zake.
Katika kipindi cha siku 45 za ofa hiyo, Ally alisema kwamba mteja pia anaweza kukopa na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo kabla haijafika mwisho.

“Unaweza kupata jezi hata kwa kukopa, mitandao yote ya simu wanakopesha wateja, ni fursa ambayo hatupaswi kuichezea, huu ndio wakati wa kila Mwanasimba kununua jezi yake original,” alisema Ally.

The post Simba wakataa jezi feki, washusha bei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/simba-wakataa-jezi-feki-washusha-bei/feed/ 0
Simba wamedhamiria kukataa jezi feki https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/simba-wamedhamiria-kukataa-jezi-feki/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/simba-wamedhamiria-kukataa-jezi-feki/#respond Tue, 04 Nov 2025 15:18:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14057 Na Hassan KinguKlabu ya Simba inaonekana imedhamiria kuikataa kwa nguvu zote biashara ya jezi feki, ni kama vile klabu hiyo imeamua kuanzisha vita dhidi ya wanaosambaza na kuuza jezi hizo ambazo zinawanyima mapato.Ni hatua ya kupongezwa lakini hapo hapo ni muhimu kutambua ukweli kwamba vita au mapambano ya aina hii hayajawahi kuwa kitu rahisi si […]

The post Simba wamedhamiria kukataa jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Klabu ya Simba inaonekana imedhamiria kuikataa kwa nguvu zote biashara ya jezi feki, ni kama vile klabu hiyo imeamua kuanzisha vita dhidi ya wanaosambaza na kuuza jezi hizo ambazo zinawanyima mapato.
Ni hatua ya kupongezwa lakini hapo hapo ni muhimu kutambua ukweli kwamba vita au mapambano ya aina hii hayajawahi kuwa kitu rahisi si Tanzania tu bali hata kwingineko Afrika au duniani kwa ujumla.
Biashara ya jezi feki ni kubwa, ni aina ya biashara ambayo baadhi ya watu wanajaribu kuihalalisha na wameihalalisha kwa namna ambavyo wamekuwa wakiifanya kwa muda mrefu bila kujali.
Sababu mojawapo inayowafanya watu hawa kuihalalisha biashara hii ni ukweli kwamba wanaoibiwa wanatumia nguvu ndogo au hawajaonesha utayari wa kupambana nao kwa kutumia nguvu kubwa.
Klabu ya Simba kwa kushirikiana na wadhamini wao Kampuni ya Jayrutty hadi sasa wameonesha dalili zote za utayari na kufanya kila linalowezekana kukabiliana na uuzwaji na usambazaji wa jezi feki.
Hata hivyo kama nilivyosema awali ni muhimu kutambua ukweli kwamba Simba peke yao bado hawatoshi kumaliza tatizo hili bali klabu zote kuanzia mahasimu wao Yanga na klabu nyingine za ligi kuu ni muhimu kushiriki kwa pamoja katika vita hii.
Ukweli kwamba kuna watu wamejihalalishia biashara hii na wana nguvu za kiuchumi ndio unaonifanya niamini kuwa klabu zote hasa za ligi kuu pamoja na wadau wa soka wana kila sababu ya kushiriki katika vita hii.

Mafanikio ya vita hii ni mafanikio ya michezo, ni mafanikio ya soka, serikali na jamii ya watanzania kwa kuwa sehemu kubwa ya jezi feki huwa hazilipiwi kodi.
Kwa hali hiyo unapopiga vita jezi feki unakuwa umepambana katika kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi lakini la muhimu zaidi ni kwamba unasaidia maendeleo ya klabu kiuchumi na soka kwa ujumla wake.
Ikumbukwe kwamba wanaouza jezi kihalali ni wanamichezo hivyo wana nafasi pia ya kuunga mkono michezo mingine kadri wanavyopata faida na faida yao itapatikana zaidi jezi feki zikidhibitiwa.
Na hapa ndipo tunapouona ukweli kwamba vita ya jezi feki si sahihi kuwa ya Simba na washirika wao yaani Jayrutty badala yake ni vita ya wanamichezo, watanzania na wote wanaopenda haki.
Kama nilivyosema kwamba kuna kundi kubwa la watu ambao limejihalalishia biashara hii kwa imani kwamba wana haki ya kununua jezi na kuzitengeneza upya chini ya ubora na kuziuza kwa faida wakati mwingine faida kubwa kuliko klabu husika au mdhamini.
Hili si jambo sahihi kibiashara na katika misingi ya haki halikubaliki na ndio maana nasisitiza kwa klabu zote kusimama kidete katika vita hii.
Simba wameanza ni vyema kwa namna ambavyo wanafanya kampeni zao mikoani zenye lengo la kukataa jezi feki, juhudi zao ni vyema zikiungwa mkono, peke yao vita hii ni ngumu na inawapa nguvu wanaoifanya kuona kwamba wanapambana na nguvu ndogo kwa maana ya Simba peke yao.
Na ndio maana nasisitiza tena na tena kwamba wadau wote wa soka kwa pamoja kuanzia klabu, TFF, serikali na wengineo nguvu yao inahitajika katika hiki kinachofanywa na Simba kwa kushirikiana na Jayrutty.
Kinachoonekana sasa mbele ya wengi ni kama vile jukumu la kuzikataa jezi feki ni la ofisa habari wa Simba, Ahmed Ally na kundi lao la Simba kwa kushirikiana na Jayrutty au waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye hivi karibuni ameonekana kuunga mkono juhudi hizo wakati si kweli.
Ni muhimu nguvu iongezeke, wadau washirikiane kwa pamoja kuwakumbusha watanzania kuthamini na kuheshimu hakimiliki kwa maana ya kwamba wenye haki ya kuuza jezi ya Simba ni watu maalum kwa makubaliano maalum na si kila mtu.

The post Simba wamedhamiria kukataa jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/simba-wamedhamiria-kukataa-jezi-feki/feed/ 0
Simba wabaini jezi feki https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/simba-wabaini-jezi-feki/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/simba-wabaini-jezi-feki/#respond Tue, 23 Sep 2025 19:37:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13936 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Simba na Kampuni ya Jayrutty Investment umebaini kuwapo kwa jezi feki katikaza Simba mikoa ya Morogoro, Singida, Mwanza na Geita.Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Simba ugunduzi wa jezi hizo feki umetokana na opertesheni maalum ambayo imefanywa kwa ushirikiano kati ya klabu hiyo na polisi na tayari baadhi […]

The post Simba wabaini jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Simba na Kampuni ya Jayrutty Investment umebaini kuwapo kwa jezi feki katikaza Simba mikoa ya Morogoro, Singida, Mwanza na Geita.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Simba ugunduzi wa jezi hizo feki umetokana na opertesheni maalum ambayo imefanywa kwa ushirikiano kati ya klabu hiyo na polisi na tayari baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa na wanatarajia kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katika taarifa hiyo, Simba wamebainisha kuwa uzalishaji, uuzaji, usambazaji na utumiaji wa jezi ambazo hazijazalishwa na Jayrutty ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.
“Hatua zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzalisha, kuuza, kusambaza ama kutumia jezi na bidhaa feki kwani vitendo hivyo ni uhujumu wa wazi dhidi ya klabu ya Simba,” ilieleza taarifa hiyo.
Simba pia wameahidi kuweka ulinzi mkali kote Tanzania kwa lengo la kudhibiti na kukamata wahusika wote wa bidhaa feki na kuwataka wanasimba na raia wote kutoshiriki katika matumizi ya bidhaa feki.
Katika taarifa hiyo, Simba na Jayrutty pia wametaka mtu yeyote atakayebaini uwepo wa jezi na bidhaa feki mahala popote atoe taarifa kituo chochote cha polisi au apige simu namba, 0752 111 181 au 0784 128 220 na 0742 771 311.
Simba kwa kushirikiana na Jayrutty pia wameahidi zawadi nono kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa jezi feki.

The post Simba wabaini jezi feki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/simba-wabaini-jezi-feki/feed/ 0
Marufuku kuuza jezi zenye nembo ya Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/10/18/marufuku-kuuza-jezi-zenye-nembo-ya-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/18/marufuku-kuuza-jezi-zenye-nembo-ya-yanga/#respond Fri, 18 Oct 2024 06:44:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12015 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote au taasisi kutengeneza, kuagiza au kusambaza bidhaa zozote zenye nembo ya Yanga bila ruhusa.Taarifa ya klabu hiyo kutoka idara ya sheria iliyopatikana Alhamisi hii, pia imefafanua kuwa ni kinyume cha sheria kwa wafanyabiashara wa jumla na rejareja kuuza bidhaa […]

The post Marufuku kuuza jezi zenye nembo ya Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote au taasisi kutengeneza, kuagiza au kusambaza bidhaa zozote zenye nembo ya Yanga bila ruhusa.
Taarifa ya klabu hiyo kutoka idara ya sheria iliyopatikana Alhamisi hii, pia imefafanua kuwa ni kinyume cha sheria kwa wafanyabiashara wa jumla na rejareja kuuza bidhaa zozote zenye nembo ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bidhaa hizo ili ziweze kuuzwa na wafanyabiashara hao ni lazima ziwe zimesambazwa na mshirika rasmi wa klabu hiyo ambaye ni kampuni ya GSM.
Agizo la klabu hiyo limekuja ikiwa takriban mwaka mmoja umepita tangu polisi jijini Dar es Salaam wakamate kontena mbili zenye jezi zinazodaiwa kuwa na nembo ya Yanga, Simba, Azam FC na Taifa Stars.
Sambamba na katazo la kuuza na kusambaza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo, taarifa ya Yanga pia imepiga marufuku kwa taasisi yoyote kutumia nembo ya Yanga kwenye matangazo yake ya aina yoyote bila ridhaa ya klabu hiyo.
Yanga wameeleza kuwa vitendo hivyo ni ukiukwaji wa hakimiliki za klabu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayehusika.
Katika kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na wananchi wote, klabu hiyo imeahidi kutoa zawadi nono kwa yeyote atakayetoa taarifa za kuwabaini wanaojihusisha na shughuli hizo ambazo klabu hiyo umezitaja kuwa ni haramu.

The post Marufuku kuuza jezi zenye nembo ya Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/18/marufuku-kuuza-jezi-zenye-nembo-ya-yanga/feed/ 0
Jezi feki zamuibua Waziri Ndumbaro https://www.greensports.co.tz/2023/10/27/jezi-feki-zamuibua-waziri-ndumbaro/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/27/jezi-feki-zamuibua-waziri-ndumbaro/#respond Fri, 27 Oct 2023 17:00:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8259 Na mwandishi wetuWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Nadumbaro (pichani) amesema hawatakuwa na msamaha kwa wanaojihusisha na utengenezaji jezi feki nchini kwa kuwa ni kati ya watu wanaozorotesha uchumi wa nchi nzima.Ndumbaro ameyasema hayo ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuelezwa kukamatwa kwa jezi bandia za Simba, Yanga na timu ya taifa, Taifa […]

The post Jezi feki zamuibua Waziri Ndumbaro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Nadumbaro (pichani) amesema hawatakuwa na msamaha kwa wanaojihusisha na utengenezaji jezi feki nchini kwa kuwa ni kati ya watu wanaozorotesha uchumi wa nchi nzima.
Ndumbaro ameyasema hayo ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuelezwa kukamatwa kwa jezi bandia za Simba, Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars maeneo ya Chang’ombe na Temeke, Dar es Salaam zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh bilioni mbili.
“Kama wizara kwanza tumesikitishwa sana na vitendo vya uharamia uliofanywa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi yetu, tufahamu kwamba kutengeneza bidhaa bandia kwanza unaathiri uchumi wa nchi, unakiuka sheria za ushindani, hakimiliki na nembo pia, mbaya zaidi unaathiri uchumi wa nchi, klabu na sekta ya michezo kwa ujumla,” alisema Ndumbaro.
Waziri huyo alisema vitendo hivyo pia vinarudisha nyuma juhudi za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye anajipambanua kuinyanyua michezo nchini ili klabu ziwe na fedha na mapato mazuri ya kuendeleza michezo kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Alisema pamoja na mambo mengine lakini faida muhimu katika michezo ni ajira, biashara na uchumi, hivyo anayejaribu kuchezea vitu hivyo vitatu watamchukulia hatua stahiki ili watambue kwamba mali za klabu, mali za mpira sio vitu vya kuvichezeachezea.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji kwa kuwa masuala ya ushindani wa haki yako chini ya dhamana yake, tayari ameshachukua hatua, anaendelea na hatua za mwisho ili haki itendeke,” alisema Dk Ndumbaro.


“Na sisi Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo tunamuunga mkono Kijaji, tunamuahidi kushirikiana naye kupigania haki na maslahi ya klabu za Tanzania na timu za taifa na kuhakikisha yeyote anayefanya uharamia katika jezi, nembo na vifaa vingine vya klabu atachukuliwa hatua stahiki, kwenye hili hatuna mchezo ili wajue mali za klabu, mali za mpira sio vya mchezo mchezo,” alisema Ndumbaro.

The post Jezi feki zamuibua Waziri Ndumbaro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/27/jezi-feki-zamuibua-waziri-ndumbaro/feed/ 0
Bocco kulipwa Sh 200 milioni https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/#respond Sat, 09 Sep 2023 11:39:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7703 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa timu ya Simba, John Bocco anatarajia kulipwa Sh Milioni 200 baada ya Mahakama Kuu Tanzania kuitaka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Princess Leisure kumlipa mchezaji huyo kiasi hicho cha fedha.Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba na mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatakiwa kulipwa kiasi hicho […]

The post Bocco kulipwa Sh 200 milioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa timu ya Simba, John Bocco anatarajia kulipwa Sh Milioni 200 baada ya Mahakama Kuu Tanzania kuitaka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Princess Leisure kumlipa mchezaji huyo kiasi hicho cha fedha.
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba na mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kampuni hiyo kutumia picha zake katika matangazo yao.
Hukumu hiyo ilitolewa Agosti 31 na Jaji Irvin Mugeta iliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha licha ya kuwa katika madai ya awali, Bocco alitaka alipwe Sh bilioni 1 kama fidia ya kutumia picha hizo bila ya makubaliano.
Bocco aliyewakilishwa na mawakili Innocent Michael na Gadi Kabele, katika madai yake alidai kwamba kitendo cha kampuni hiyo kutumia picha yake kilimaanisha kwamba alivunja mkataba na klabu ya Simba ambayo ilijiandaa kumchukulia hatua za kinidhamu.
Mchezaji huyo pia alidai kwamba hakuwahi kuipa idhini kampuni hiyo kutumia picha yake na hawakuwa na makubaliano katika jambo hilo.
Jaji Mugeta wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alihitimisha kwa kuitaka kampuni hiyo kumlipa fidia mchezaji huyo.
Baadhi ya picha zilizotumika na kuonekana katika mtandao wa Instagram ni ile iliyokuwa na tangazo lililowakumbusha mashabiki kuhusu uhondo wa Ligi Kuu NBC.
Tangu kutolewa kwa hukumu hiyo na habari kusambaa kwenye vyanzo mbalimbali vya habari, imesababisha kuibuka kwa mjadala kuhusu hakimiliki na matumizi sahihi ya picha za wanamichezo na wasanii pale picha hizo zinapotumika kibiashara.

The post Bocco kulipwa Sh 200 milioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/feed/ 0
Hakimiliki yamtia matatani Bieber https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/hakimiliki-yamtia-matatani-bieber/ https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/hakimiliki-yamtia-matatani-bieber/#respond Sun, 24 Apr 2022 13:08:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=592 Wanamuziki Justin Bieber na Dan + Shay wameshitakiwa kwa kosa la kwenda kinyume na taratibu za hakimiliki katika kibao chao 10,000 Hours.Bierber, mkali wa miondoko ya pop na mwenzake wa muziki wa Country wameshitakiwa na makampuni ya International Manufacturing Concepts, Melomega music na Sound Gems wakidaiwa kuiba baadhi ya mashairi katika kibao hicho.Sehemu ya mashairi […]

The post Hakimiliki yamtia matatani Bieber first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Justin Bieber

Wanamuziki Justin Bieber na Dan + Shay wameshitakiwa kwa kosa la kwenda kinyume na taratibu za hakimiliki katika kibao chao 10,000 Hours.
Bierber, mkali wa miondoko ya pop na mwenzake wa muziki wa Country wameshitakiwa na makampuni ya International Manufacturing Concepts, Melomega music na Sound Gems wakidaiwa kuiba baadhi ya mashairi katika kibao hicho.
Sehemu ya mashairi yanayodaiwa kuibwa ni yale ya kibao cha mwaka 1973 cha The First Time Baby Is A Holiday, ambayo awali yaliandikwa na Palmer Rakes na Frank Fioravanti.
Kampuni hizo zilidai kwamba zinamiliki wimbo huo na kutaka kutambuliwa katika kibao cha 10,000 Hours pamoja na kulipwa fidia, heshima yao pamoja na malipo ya ada ya mwanasheria na kuomba kuzuiwa usambazaji wa aina yoyote wa kibao cha 10,000 Hours.
Oktoba 2019, Bieber na Dan + Shay walitoa kibao cha 10,000 Hours ikiwa ni siku nne tu baada ya Bieber kufunga ndoa kwa mara ya pili na Hailey Baldwin pamoja na kufanya sherehe za kidini mjini South Carolina na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu.
Mwaka 2021, Bieber na Dan+ Shay walitwaa tuzo ya Grammy kupitia kibao cha 10,000 Hours katika kipengele cha wimbo bora katika miondoko ya country. Hata hivyo Bieber na Dan hawajasema lolote kuhusu madai hayo.

The post Hakimiliki yamtia matatani Bieber first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/hakimiliki-yamtia-matatani-bieber/feed/ 0
Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/#respond Thu, 11 Nov 2021 11:00:39 +0000 https://greensports.co.tz/?p=422 Na mwandishi wetu Msanii wa miondoko ya Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuna wakati alilazimika kuzunguka mitaani kukamata wezi wa kazi zake za muziki waliokua wakizidurufu na kuziua bila ya ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria ya hakimiliki. Sugu ambaye pia amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia mwaka […]

The post Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu

Msanii wa miondoko ya Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuna wakati alilazimika kuzunguka mitaani kukamata wezi wa kazi zake za muziki waliokua wakizidurufu na kuziua bila ya ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria ya hakimiliki.

Sugu ambaye pia amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 alisema kwamba hali hiyo ilitokana na mazingira ya wakati huo na nia ya kulinda kilicho chake.

Katika tukio moja, Sugu alimkamata machinga jijini Dar es Salaam akiuza kaseti zilizokuwa na wimbo wake wa Day Worker lakini baada ya kutafakari alisita kumpeleka polisi kwa alichodai kuwa mtu huyo ni Day Worker yaani anayefanya kazi za kawaida ikiwamo vibarua.

“Achana na hiyo ya chinga, mimi nilishakwenda kwenye duka la mtu mmoja nikamkuta anauza kazi zangu kumuuliza akaniambia yeye ni mfanyabiashara analetewa bidhaa na kuziuza, akanitolea mfano wa mtu anayeuza suruali kwamba analetewa tu na watu aziuze hajui wanaomuuzia bidhaa hizo wanazitoa wapi,’’ alisema Sugu.

Alisema kwamba ni muhimu kwa wasanii kupambana katika kulinda kazi zao na kutolea mfano wa mtu aliyejenga nyumba mahali ambapo kituo cha polisi kiko mbali akisema kwamba mtu huyo ni lazima ajipe jukumu la kulinda mali zake kabla ya kulalamika kwamba polisi wako mbali.

Akizungumzia wingi wa wasanii kwa sasa, Sugu alisema kwamba pamoja na wingi huo lakini kuna tatizo la kukosekana umoja, “tatizo ninaloliona sasa ni ukosefu wa umoja, wasanii hawana umoja.”

Akifafanua kuhusu umoja, Sugu alisema kwamba akiwa bungeni aliwahi kuwasilisha hoja ya kutaka wasanii wa muziki walipwe na vituo vya redio na televisheni kwa kutumia kazi zao lakini hapo hapo akatokea msanii mwingine mkubwa na kumpinga.

 Sugu pia aliizungumzia sheria ya Hakimiliki akishangaa na kuhoji ni  kwa nini masuala yanayohusu hakimiliki yapo Wizara ya Viwanda na BIashara wakati wasanii walio wengi ndio wahusika katika sheria hiyo.

“Hii sheria ilitakiwa kuwa wizara inayohusika na sanaa kwani huko kuna wahusika walio wengi wanaoguswa na mambo ya hakimiliki,’’ alisema Sugu.

The post Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/feed/ 0