Yanga-Azam FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 03 Jul 2026 22:16:02 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Yanga-Azam FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/#respond Thu, 25 Jun 2026 05:27:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14732 Na mwandishi wetuMahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba wameendelea kukoleza vita ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC baada ya kila mmoja kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi zilizochezwa Jumatano Juni 24, 2026.Yanga walikua kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar walitoka na ushindi huo dhidi ya Azam FC wakati Simba ushindi wao […]

The post Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba wameendelea kukoleza vita ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC baada ya kila mmoja kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi zilizochezwa Jumatano Juni 24, 2026.
Yanga walikua kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar walitoka na ushindi huo dhidi ya Azam FC wakati Simba ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ulipatikana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Matokeo hayo yameiwezesha kila timu kuvuna pointi tatu, Yanga wakiendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 69 katika michezo 28 waliyocheza hadi sasa.
Kwa upande wa Simba wameendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili wakifikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 kama ilivyo Yanga na hivyo kuzidiwa kwa pointi mbili tu.
Yanga ambao Jumapili iliyopita walitolewa na Azam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 3-2, walikuja tofauti katika mechi ya ligi na kucheza kwa kiwango cha juu.
Ushindi wa Yanga ulianza kupatikana dakika ya 41 kwa bao lililofungwa na Ibrahim Bacca aliyemalizia kazi ya Prince Dube ambaye pia ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Baada ya bao hilo, mpira ulizidi kuwa wa ushindani kwa pande zote, Yanga wakisaka bao la kuongeza huku Azam wakipambana kusawazisha lakini hadi dakika 45 zinamalizika hakuna bao jingine lililopatikana.
Kipindi cha pili timu zote zilikianza kwa nguvu mpya na kuonesha nia ya kutaka bao lakini walikuwa Yanga waliopata bao dakika ya 71 lililofungwa kwa penalti na Depu baada ya mchezaji huyo kuchezewa rafu ndani ya eneo la 18.
Dakika nane baada ya kuingia bao hilo, Pacome Zouzoua aliwainua vitini mashabiki wa Yanga alipofunga bao la tatu akiutumia mpira uliopigwa na Dube na kuokolewa.
Kwa upande wa Simba bao lao la kwanza lilipatikana mapema dakika ya tisa mfungaji akiwa ni beki wa kati wa timu hiyo, Rushine De Reuck aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, bao lililodumu kwa dakika 45 za kwanza.


Kipindi cha pili, Simba waliendelea kuutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 77, bao lililofungwa na Seleman Mwalimu akiitumia pasi ya Anicett Oura.
Karamu ya mabao ya Simba katika mechi hiyo ilihitimishwa dakika ya 90 ya mchezo huo kwa bao lililofungwa na Oura.
Matokeo hayo yanazidi kukoleza vita ya mahasimu hao wa soka nchini Tanzania katika kuliwania taji la ligi kwa msimu huu wa 2025-26 unaoelekea ukingoni huku kila timu ikiwa na mechi mbili mkononi.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi hiyo ni kama ifuatavyo
KMC 2-3 Namungo FC
Dodoma Jiji 0–0 JKT
Fountain Gate 0-1 Mashujaa
TRA Unite 1-1 Coastal Union
Pamba Jiji 02 Mbeya City
Singida BS 3-1 Prisons

The post Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/feed/ 0
Azam yenye wachezaji 10 yaitesa Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/azam-yenye-wachezaji-10-yaitesa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/azam-yenye-wachezaji-10-yaitesa-yanga/#respond Mon, 22 Jun 2026 14:45:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14724 Na mwandishi wetuIkicheza na wachezaji 10 uwanjani, Azam FC imeibuka kidedea kwa kuichapa Yanga mabao 3-2 na kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho, michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB.Matokeo ya mechi hiyo ya nusu fainali iliyopigwa Jumapili Juni 20, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, yanaifanya Yanga kulitema rasmi taji la michuano […]

The post Azam yenye wachezaji 10 yaitesa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ikicheza na wachezaji 10 uwanjani, Azam FC imeibuka kidedea kwa kuichapa Yanga mabao 3-2 na kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho, michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB.
Matokeo ya mechi hiyo ya nusu fainali iliyopigwa Jumapili Juni 20, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, yanaifanya Yanga kulitema rasmi taji la michuano hiyo walilolimiliki kwa misimu minne.
Ushindi wa Azam kwa Yanga ulipatikana baada ya timu hizo kutoana jasho kwa dakika 120 huku Azam ikipata pigo dakika ya 70 baada ya beki wake Yoro Diaby kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kadi hiyo ilitolewa na mwamuzi baada ya Diaby kumchezea rafu Prince Dube wa Yanga lakini licha ya upungufu huo, Azam walifanikiwa kumaliza dakika 90 kwa sare ya 2-2 kabla ya kutumia dakika nyingine 30 kupata bao la ushindi.
Azam walianza kuzitikisa nyavu za Yanga dakika ya 27 kwa bao la Himid Mao ambaye pia ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kupewa tuzo na kitita cha Sh milioni 1 na wadhamini wa michuano hiyo, Benki ya CRDB.
Mao akionesha kiwango cha juu kwenye mechi hiyo, alifunga bao hilo baada ya kuunganishiwa pasi na kiungo Jean Jacques Ngita.
Yanga walijibu mapigo kwa kusawazisha bao hilo kabla ya timu kwenda mapumziko mfungaji akiwa ni Dube baada ya kuunganishiwa pasi na Allan Okelo.

Azam walionesha umakini kwa kufunga bao la pili katika dakika ya 85 licha ya kuwa 10 uwanjani, bao lililofungwa na Elias Lawi aliyeutumia mpira wa kona uliopigwa na nyota wa zamani wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto alifufua matumaini ya timu yake alipofunga bao la kusawazisha akiitumia pasi ya Okello na ndipo dakika 30 zilipoongezwa baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika matokeo yakiwa sare ya mabao 2-2.
Walikuwa ni Azam walioneemeka na dakika hizo kwa kufunga bao la tatu lililowekwa kimiani dakika ya 112 na Japhet Kitambala aliyeneemeka na makosa ya beki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca.
Azam sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali na Simba ambao katika mehi nyingine ya nusu fainali waliichapa Coastal Union ya Tanga mabao 4-0.

The post Azam yenye wachezaji 10 yaitesa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/azam-yenye-wachezaji-10-yaitesa-yanga/feed/ 0
Yanga yaipiga Azam, yafuzu fainali Muungano https://www.greensports.co.tz/2026/04/26/yanga-yaipiga-azam-yafuzu-fainali-muungano/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/26/yanga-yaipiga-azam-yafuzu-fainali-muungano/#respond Sun, 26 Apr 2026 16:07:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14559 Na mwandishi wetuMabingwa watetezi Yanga wamefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Muungano baada ya kuichapa Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa Jumamosi Aprili 25, 2026 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.Yanga ilianza kuziona nyavu za Azam katika dakika ya sita kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo kutoka Zimbabwe, Prince Dube […]

The post Yanga yaipiga Azam, yafuzu fainali Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabingwa watetezi Yanga wamefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Muungano baada ya kuichapa Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa Jumamosi Aprili 25, 2026 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Yanga ilianza kuziona nyavu za Azam katika dakika ya sita kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo kutoka Zimbabwe, Prince Dube akitumia pasi ya Alan Okelo.
Kasi ya Yanga kusaka bao la pili ilizaa matunda katika dakika ya 25 kwa bao lililofungwa na kiungo wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Maxi Nzengeli aliyeitumia pasi ya Dube kufunga bao hilo.
Bao pekee la Azam lilifungwa na Feisal Salum au Fei Toto katika dakika ya 77, bao ambalo alilifunga akinufaika na makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga waliochelewa kuokoa mpira katika eneo lao.
Kwa ushindi huo Yanga inasubiri kuumana na mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali kati ya Simba na Mlandege ambayo itachezwa Jumapili Aprili 26 saa mbili usiku kwenye uwanja huo huo.
Mechi ya fainali ya Kombe la Muungano inatarajia kuchezwa Jumatano Aprili 29, 2026 kwenye uwanja huo huo wa New Amaan kuanzia saa mbili usiku.

The post Yanga yaipiga Azam, yafuzu fainali Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/26/yanga-yaipiga-azam-yafuzu-fainali-muungano/feed/ 0
Yanga, Azam zashindwa kufungana https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/yanga-azam-zashindwa-kufungana/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/yanga-azam-zashindwa-kufungana/#respond Mon, 16 Mar 2026 16:29:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14445 Na mwandishi wetuVinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Jumapili Machi 15, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Matokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 36 wakati Azam nao wamechupa hadi nafasi ya […]

The post Yanga, Azam zashindwa kufungana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Vinara wa Ligi Kuu NBC, Yanga wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Jumapili Machi 15, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 36 wakati Azam nao wamechupa hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 28.
Ikiwatumia washambuliaji wake mahiri Depu na Prince Dube, Yanga ilipata wakati mgumu kuipenya safu ya ulinzi ya Azam iliyoongozwa na kipa mkongwe Aishi Manula.
Katika harakati za kusaka mbinu za kuipenya ngome ya Azam, Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuingia kiungo fundi, Pacome Zouzoua ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini mabadiliko hayo hayakuzaa bao.
Baada ya matokeo hayo mjadala umeanza kuibuka kuhusu Yanga ikionekana kama imeanza kupoteza makali yake hasa baada ya kutoka sare kama hiyo na mahasimu wao Simba na baadaye kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Prisons.
Mjadala huo hata hivyo hauwezi kufuta ukweli kwamba timu hiyo inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Azam inayoshika nafasi ya pili baada ya kila timu kucheza mechi 14.

The post Yanga, Azam zashindwa kufungana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/yanga-azam-zashindwa-kufungana/feed/ 0