Walid Regragui - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 01 Feb 2024 19:10:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Walid Regragui - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/#respond Thu, 01 Feb 2024 19:10:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9549 Abidjan, Ivory CoastKocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon hatua ya 16 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini.Morocco au Atlas Lion ilishindwa kutamba juzi Jumanne mbele ya Afrika Kusini na kutolewa kimaajabu jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa ni […]

The post Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon hatua ya 16 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini.
Morocco au Atlas Lion ilishindwa kutamba juzi Jumanne mbele ya Afrika Kusini na kutolewa kimaajabu jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa ni moja ya timu zilizopewa nafasi ya kubeba taji hilo.
Timu hiyo ilianza kwa kuadhibiwa kwa bao la Evidence Makgopa dakika takriban 10 baada ya kuanza kipindi cha pili kabla ya Teboho Mokoena kumalizia bao la pili katika dakika za lala salama.
Morocco mbali na nyota wake, Achraf Hakimi kukosa penalti lakini pia ilimaliza mechi na wachezaji 10 baada ya kiungo wake, Sofyan Amrabat kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
“Labda tungeweza kumaliza mechi katika nusu ya kwanza, lakini katika hatua tuliyofikia unaweza kuadhibiwa kwa nafasi yoyote unayoipoteza,” alisema Regragui.

“Penalti umetuuma sana na hakika hatukufanya kila kitu tulichotakiwa kukifanya lakini mimi nabeba lawama zote,’ alisema Regragui.


Matumaini ya Morocco yalikuwa ni kubeba taji la Afcon kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo mwaka 1976 na mafanikio yao ya kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 yalifanya matumaini ya kubeba taji hilo kuwa makubwa zaidi.
“Tutajifunza kutokana na mkwamo huu ambao hatukuutarajia, hili ni jambo la kuumiza kwa mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono kwa kiasi kikubwa,” alisema Regragui.

The post Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/feed/ 0
Kocha Morocco achunguzwa kwa ubaguzi https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/kocha-morocco-achunguzwa-kwa-ubaguzi/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/kocha-morocco-achunguzwa-kwa-ubaguzi/#respond Wed, 24 Jan 2024 05:58:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9395 Abidjan, Ivory CoastShirikisho la Soka Afrika (Caf) limeanza uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi kati ya kocha wa Morocco, Walid Regragui na beki wa DR Congo, Chancel Mbemba wanaodaiwa kuzozana hadi kutaka kupigana mara baada ya mechi baina ya timu hizo.Sambamba na hilo, Caf pia inachunguza madai ya udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na wachezaji wa […]

The post Kocha Morocco achunguzwa kwa ubaguzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limeanza uchunguzi wa tuhuma za ubaguzi wa rangi kati ya kocha wa Morocco, Walid Regragui na beki wa DR Congo, Chancel Mbemba wanaodaiwa kuzozana hadi kutaka kupigana mara baada ya mechi baina ya timu hizo.
Sambamba na hilo, Caf pia inachunguza madai ya udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na wachezaji wa timu ya Morocco mara baada ya mechi hiyo ya Kundi F katika fainali za Afcon zinazoendelea..
Morocco na DR Congo ziliumana Jumapili iliyopita katika mechi ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 na baada ya mechi hiyo kuliibuka vita ya maneno baina ya Mbemba na Regragui na kufuatiwa na kutaka kushikana na kutoleana kauli za vitisho.
Taarifa ya Caf iliyotolewa Jumatatu ilithibitisha kuwapo mpango wa kufanyia uchunguzi sakata hilo licha ya Shirikisho la Soka Morocco nalo kuamua kulipooza tukio zima.
Katika tukio hilo, Mbemba na Regragui walilazimika kutenganishwa baada ya kutoleana maneno makali ingawa baadaye kocha huyo alimfuata Mbemba aliyekuwa katika harakati za kufanya maombi kwa lengo la kutaka kumpa mkono.
Mbemba anayeichezea klabu ya Marseille ya Ufaransa alionekana kutokuwa tayari kupeana mkono na kocha huyo akieleza kwamba hakupenda kitendo cha kocha huyo kujaribu kumshawishi mwamuzi kwa kutaka atoe kadi nyekundu.
“Nimeamua kukaa kimya, ni bora, kila mtu ananifahamua mimi, naheshimu kila mtu lakini sikuwahi kuwaza kama ningesikia neno lile kutoka kwa kocha, kwamba neno lile lingetoka mdomoni mwake,” alisema Mbemba.
“Nilimuheshimu kocha lakini video zipo wazi kwenye televisheni, nilitumia muda wangu kumtukuza Mungu,” alisema Mbemba ambaye pia kuna madai kwamba alitolewa kauli za kibaguzi uwanjani hapo na baadaye kupitia mitandao ya kijamii.
Katika taarifa yake, Rais wa Shirikisho la Soka DR Congo (Fecofa), Dieudonne Sambi Nsele-Lutu alisema kwamba kilichofanyika kwa nahodha wao hakikubaliki.

“Haikubaliki kwa nahodha wetu kufanyiwa mashambulizi ya kibaguzi, kutolewa kauli zisizofaa kutoka kwa wachezaji wa Morocco na kocha wao jambo lililoendelea hata wakati tukielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo,” alisema Nsele-Lutu.


Kwa upande wake kocha wa Morocco, Regragui alionekana kushangazwa na madai ya Mbemba kwamba alitoa kauli za ubaguzi wa rangi.
“Anataka kuonesha kwamba kauli yangu ni ya kibaguzi, si uungwana hasa kwa kuwa amezungumza mambo ya dini katika kauli zake, ajaribu kuwa muungwana, nilimpa mkono akaanza kufoka kama mnavyoweza kuona kwenye picha na video zilizopo kila kona,” alisema Regragui.
Morocco leo Jumatano itakamilisha mechi yake ya Kundi F dhidi ya Zambia na ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne wakati DR Congo yenye pointi mbili nayo leo itakamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kuumana na Tanzania.

The post Kocha Morocco achunguzwa kwa ubaguzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/24/kocha-morocco-achunguzwa-kwa-ubaguzi/feed/ 0