US Monastir - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 20 Mar 2023 07:38:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg US Monastir - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yatua robo fainali https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/yanga-yatua-robo-fainali/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/yanga-yatua-robo-fainali/#respond Sun, 19 Mar 2023 19:36:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5540 Na mwandishi wetuMabao ya Kennedy Musonda na Fiston Mayele, leo Jumapili yameiwezesha Yanga kutoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga inakuwa timu ya pili ya Tanzania kufuzu hatua hiyo katika mashindano ya klabu Afrika baada ya Simba nao kufuzu hatua […]

The post Yanga yatua robo fainali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabao ya Kennedy Musonda na Fiston Mayele, leo Jumapili yameiwezesha Yanga kutoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga inakuwa timu ya pili ya Tanzania kufuzu hatua hiyo katika mashindano ya klabu Afrika baada ya Simba nao kufuzu hatua kama hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika takriban saa 24 zilizopita.
Musonda aliipatia Yanga bao la kwanza katika dakika ya 33 akiitumia vizuri krosi iliyochongwa na Jesus Moloko na kuifanya timu hiyo iende mapumziko ikiwa mbele.
Dakika 14 baada ya kuanza kipindi cha pili, Mayele aliwainua kwenye viti mashabiki wa Yanga alipoandika bao la pili akiitumia pasi ya Musonda.
Ushindi huo mbali na kuiwezesha Yanga kufuzu robo fainali pia unaifanya timu hiyo kuongoza Kundi D licha ya kuwa sawa kwa pointi na US Monastir, (pointi 10) Yanga inaneemeka na wastani mzuri wa mabao.
Katika mechi nyingine ya Kundi D iliyochezwa leo, mambo hayakuwa mazuri kwa TP Mazembe ya DR Congo ambayo ikiwa ugenini nchini Mali ilichapwa na Real Bamako mabao 2-1.
Matokeo hayo yanaifanya Mazembe kuburuza mkia katika kundi hilo ikiwa na pointi tatu wakati Real Bamako inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano.

The post Yanga yatua robo fainali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/yanga-yatua-robo-fainali/feed/ 0
Nabi: Kikosi kipo tayari https://www.greensports.co.tz/2023/03/18/nabi-kikosi-kipo-tayari/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/18/nabi-kikosi-kipo-tayari/#respond Sat, 18 Mar 2023 19:43:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5528 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kikosi chake kipo tayari kupigania ushindi dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga kesho Jumapili itaumana na timu hiyo ya Tunisia ikiwa ni mechi yao ya tano huku ikihitaji pointi tatu ili kufikisha pointi 10 na […]

The post Nabi: Kikosi kipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kikosi chake kipo tayari kupigania ushindi dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga kesho Jumapili itaumana na timu hiyo ya Tunisia ikiwa ni mechi yao ya tano huku ikihitaji pointi tatu ili kufikisha pointi 10 na kuwafikia Monastir pamoja na kufuzu hatua hiyo kutoka Kundi D.
Katika kundi hilo, TP Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa pointi tatu huku Real Bamako ya Mali ikiburuza mkia ikiwa na pointi mbili.
Nabi amefafanua leo Jumamosi kuwa walipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Monastir katika mechi ya ugenini lakini tayari wamejifunza kwa aina ya mabao waliyofungwa na wamewasoma vizuri Monastir kuelekea mtanange huo.
“Mechi yetu ya kesho ni muhimu sana kwetu sababu tukipata matokeo mazuri tunafuzu moja kwa moja robo fainali lakini mechi ni ngumu sababu Monastir hawajaja kutembea hapa, wamekuja kucheza na kutafuta matokeo maana wanahitaji kumaliza wakiwa wanaongoza kundi.

“Upande wetu tumejiandaa vizuri kwa umakini, kisaikolojia na mechi hiyo na tunataka matokeo. Tunafahamu aina ya mabao waliyotufunga mwanzo, tumejifunza zaidi, tumeona video zao, ingawa tunajua watabadilika tena lakini tumewafahamu vizuri,” alisema Nabi.


Kwa upande wake kocha wa Monastir, Darko Navic alisema wamejiandaa vizuri na wako tayari kimchezo, wakihitaji ushindi ili kuendelea kujenga kujiamini kwa timu hiyo japo watacheza kwa presha kulingana na ugumu wa mechi yenyewe.
“Kwetu matokeo ni kitu muhimu, tutahitaji matokeo kikosi kiendelee kujiamini zaidi, tumejiandaa vya kutosha na tunafahamu mechi ni ngumu kiuhalisia lakini tutacheza kawaida kwa ajili ya kuitazama zaidi robo fainali,” alisema Navic.
Katika mechi nne za awali, Yanga ilipoteza dhidi ya Monastir kabla ya kuifunga Mazembe mabao 3-1 kisha ikatoka sare ya 1-1 na Bamako kabla ya kuichapa mabao 2-0 kwenye mechi ya marudiano.

The post Nabi: Kikosi kipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/18/nabi-kikosi-kipo-tayari/feed/ 0
Yanga yakwama Tunisia https://www.greensports.co.tz/2023/02/12/yanga-yakwama-tunisia/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/12/yanga-yakwama-tunisia/#respond Sun, 12 Feb 2023 18:54:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5105 Tunis, TunisiaYanga leo Jumapili imeanza na mguu mbaya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na US Monastir ya Tunisia katika mechi ya Kundi D.Mabao yaliyoizamisha Yanga iliyokuwa ugenini yote yalipatikana kipindi cha kwanza yakifungwa kwa kichwa na Mohammed Sagrawi aliyefunga la kwanza na Boubacar Traore aliyefunga la pili.Baada […]

The post Yanga yakwama Tunisia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tunis, Tunisia
Yanga leo Jumapili imeanza na mguu mbaya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na US Monastir ya Tunisia katika mechi ya Kundi D.
Mabao yaliyoizamisha Yanga iliyokuwa ugenini yote yalipatikana kipindi cha kwanza yakifungwa kwa kichwa na Mohammed Sagrawi aliyefunga la kwanza na Boubacar Traore aliyefunga la pili.
Baada ya kufunga mabao, Monastir wakishangiliwa na mashabiki wachache, walifanya mashambulizi machache na kutumia muda mwingi kujihami na kuchelewesha muda na hadi mapumziko Yanga waliumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa licha ya kuwa nyuma kwa mabao mawili.
Yanga ilikianza kipindi cha pili kwa kushambulia, dakika moja tu baada ya kuanza kipindi hicho, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ alimpenyezea pasi Fiston Mayale ambaye alifumua shuti lakini kipa wa Monastir alikuwa makini na kuokoa mpira huo.
Monastir walijibu shambulizi hilo dakika chache baadaye ambapo Traore akiwa karibu na lango la Yanga aliupiga mpira ambao kama si umahiri wa kipa Djigui Diarra, Monastir wangepata bao la tatu.
Shambulizi hilo lilimsababishia kadi ya njano, Traore ambaye baada ya Diarra kuudaka mpira na kukimbia nao hatua chache ili awapasie wachezaji wake, Traore alimzuia njiani na ndipo mwamuzi alipompa kadi hapo hapo.
Dakika ya 58, Stephan Aziz Ki alipiga mpira wa adhabu ambao kipa wa Monastir aliuokoa na kuangukia ndani ya lango lake kabla ya kulala chini akilalamika kuumia baada ya kuokoa mpira huo.
Baada ya shambulio hilo Yanga waliendelea kuutawala mchezo lakini dakika ya 69, Monastir walifanya shambulizi jingine baada ya Yusuf Omar kuwatoka mabeki wawili wa Yanga lakini mpira alioupiga uliokolewa na Diarra.
Dakika ya 82, Mayele nusura aipatie Yanga bao baada ya kuunganishiwa pasi na Kennedy Musonda lakini shuti alilopiga lilitoka nje.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyochezwa leo, TP Mazembe ya DR Congo ilitoka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Real Bamako ya Mali.
Yanga sasa inajiandaa kucheza mechi yake ya pili ya kundi hilo, Februari 19 ikiwa nyumbani dhidi ya Mazembe wakati Monastir itakuwa ugenini Mali dhidi ya Real Bamako.

The post Yanga yakwama Tunisia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/12/yanga-yakwama-tunisia/feed/ 0