TRA United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 May 2026 14:44:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TRA United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Watoza kodi waichapa Azam 4-1 https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/#respond Fri, 08 May 2026 19:18:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14619 Na mwandishi wetuTimu ya TRA United au Watoza Kodi, imetoa kichapo cha mabao 4-1 kwa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, leo Ijumaa, Mei 8, 2026.Azam waliuanza mchezo kwa kasi wakionesha dhamira ya kusaka pointi tatu na kasi yao ilizaa matunda mapema dakika ya saba […]

The post Watoza kodi waichapa Azam 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya TRA United au Watoza Kodi, imetoa kichapo cha mabao 4-1 kwa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, leo Ijumaa, Mei 8, 2026.
Azam waliuanza mchezo kwa kasi wakionesha dhamira ya kusaka pointi tatu na kasi yao ilizaa matunda mapema dakika ya saba walipopata bao lao pekee lililofungwa na Japhet Kitambala aliyeitumia pasi ya Sadio Kanoute.
Iliwachukua dakika 12 TRA kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa Ally Ng’anzi aliyeyatumia vizuri mapungufu ya safu ya ulinzi ya Azam kuipatia TRA bao la kusawazisha kwa pasi ya Ally Mapaka.
Kuingia bao hilo hakukuwasumbua Azam ambao waliendelea kuonesha uhai ingawa kadri muda ulivyokwenda ndivyo kasi ya TRA ilivyoongezeka na Azam kujikuta wakipachikwa mabao mawili ya haraka haraka.
Mabao hayo yalifungwa na Amy Mapaka katika dakika ya 41 na Mapaka tena akaongeza bao la pili dakika ya 44 na kuifanya TRA iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.
Karamu ya mabao ya TRA ilikamilishwa dakika ya 64 kwa bao lililofungwa na Ramadhan Chobwedo aliyefumua shuti kali lililomshinda kipa Aishi Manula wa Azam.
Matokeo hayo mbali ya kuvuruga mbio za Azam katika kulisaka taji la ligi hiyo, pia yanakuwa yameivunja rekodi ya Azam ya kutopoteza mechi zake za ligi msimu huu.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Namungo wakiwa nyumbani Lindi walishindwa kuwadhibiti wageni wao Mashujaa na kujikuta wakitoka sare ya bila kufungana.

The post Watoza kodi waichapa Azam 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/feed/ 0
Matokeo ya sare yaongezeka Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/#respond Thu, 19 Mar 2026 13:00:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14462 Na mwandishi wetuMatokeo ya sare ya 0-0 yameendelea kushika kasi kwa timu ya Yanga katika Ligi Kuu NBC baada ya kupata matokeo hayo mara nyingine katika mechi na TRA United iliyopigwa Jumatano Machi 18, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Hii ni sare ya tatu katika mechi za hivi karibuni za timu hiyo baada […]

The post Matokeo ya sare yaongezeka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Matokeo ya sare ya 0-0 yameendelea kushika kasi kwa timu ya Yanga katika Ligi Kuu NBC baada ya kupata matokeo hayo mara nyingine katika mechi na TRA United iliyopigwa Jumatano Machi 18, 2026 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Hii ni sare ya tatu katika mechi za hivi karibuni za timu hiyo baada ya kupata matokeo kama hayo dhidi ya Simba na Azam FC na sasa TRA United.
Yanga hata hivyo ilicheza mechi hiyo bila ya wachezaji wake kadhaa tegemeo kina Dickson Job, Ibrahim Bacca, Depu na wengineo na kama hiyo haitoshi timu hiyo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Prince Dube kushindwa kumaliza mchezo.
Dube aliyeianza mechi kwa matumaini makubwa aliishia dakika ya 21 na nafasi yake kuingia Emmanuel Mwanengo ambaye dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili alipata nafasi ya kufunga lakini mpira wa kichwa alioupiga uliokolewa.
Safu ya ulinzi ya Yanga pamoja na kuwakosa nyota wake mahiri lakini ikiwa chini ya kipa Djigui Diarra, Bakari Mwamnyeto na Frank Assinki ilifanikiwa kudhibiti mashambulizi ya hapa na pale ya TRA.
TRA kwa muda mrefu ilipambana ikitengeneza mashambulizi kutokea pembeni yakiongozwa na Ramadhan Chobwedo na Joseph Akandwabo lakini uimara wa mabeki wa pembeni wa Yanga, Mohamed Hussein aliyekuwa upande wa kushoto na Israel Mwenda aliyekuwa kulia walidhibiti mashambulizi hayo.
Mwenda naye hakuweza kumaliza dakika zote 90 kwani mapema kipindi cha pili alitolewa na nafasi yake kuingia Yao Kouassi ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Mambo yaliwaendea kombo TRA na kulazimika kucheza na wachezaji 10 kwa takriban dakika 20 baada ya Mzamiru Yassin kupewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje ingawa TRA walijipanga vizuri kwa dakika zilizobaki na kuidhibiti Yanga.
Mara baada ya dakika 90 kukamilika, Yanga walionekana kuwa katika hali ya huzuni wakati kwa TRA ilikuwa shangwe wakifurahia matokeo ya sare dhidi ya Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo.
Sare hiyo hata hivyo haijaweza kuishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, badala yake timu hiyo inaendelea kushika usukani ikiwa na pointi 37 katika michezo 15 ikijivunia kutopoteza mchezo hata mmoja.

The post Matokeo ya sare yaongezeka Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/matokeo-ya-sare-yaongezeka-yanga/feed/ 0