tenisi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 06 Jul 2023 20:45:51 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.7 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg tenisi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/#respond Thu, 06 Jul 2023 20:45:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6832 London, EnglandWanaharakati za mazingira wa kundi la Just Stop Oil jana Jumatano waliandamana na kufanya vurugu kwenye mashindano ya tenisi ya Wimbledon kwa kuvamia sehemu ya kuchezea na kutupa maganda ya machungwa.Tukio la kwanza la wanamazingira hao lilitokea wakati wa mechi kati ya Sho Shimabukuro na Grigor Dimitrov hali iliyosababisha mechi hiyo kusimama kwa muda.Katika […]

The post Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Wanaharakati za mazingira wa kundi la Just Stop Oil jana Jumatano waliandamana na kufanya vurugu kwenye mashindano ya tenisi ya Wimbledon kwa kuvamia sehemu ya kuchezea na kutupa maganda ya machungwa.
Tukio la kwanza la wanamazingira hao lilitokea wakati wa mechi kati ya Sho Shimabukuro na Grigor Dimitrov hali iliyosababisha mechi hiyo kusimama kwa muda.
Katika tukio la pili wanamazingira hao walisababisha mechi nyingine kati ya Katie Boulter na Daria Saville kusimama kwa muda huku uwanja ikiwa umetapakaa maganda ya machungwa.
Hata hivyo tukio hilo lililoongozwa na waandamanaji wawili walioingia sehemu za kuchezea tenisi halikuchukua muda kwani wana usalama waliwadhibiti na baadaye wachezaji wakasaidia kusafisha uwanja uliotapakaa maganda ya machungwa.
Baadaye taarifa ya polisi ilithibitisha kukamatwa kwa waandamanaji wawili waliokuwa mstari wa mbele mmoja mwanaume na mwingine mwanamke ambao umri wao wote ni miaka zaidi ya 60.
Ulinzi ulikuwa mkali safari hii kuliko mwaka jana ingawa baadhi ya mashabiki wamelalamikia ulinzi huo kwa namna ulivyowachelewesha kuingia uwanjani kwani muda mwingi ulitumika kukagua mashabiki.
Muungano wa kundi la Just Stop Oil linalohusisha wanamazingira wamekuwa wakifanya vurugu katika michezo mbalimbali zikiwamo mechi za soka za Ligi Kuu England pamoja na zile za ligi ya rugby.
Miongoni mwa madai ya wanamazingira wa Just Stop Oil ni pamoja na kuitaka Serikali ya Uingereza iache kutoa leseni mpya katika miradi ya gesi, mafuta na makaa ya mawe.

The post Wanamazingira wavamia mashindano ya tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/wanamazingira-wavuruga-mashindano-ya-tenisi/feed/ 0
Serena Williams kustaafu tenisi https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/serena-williams-kustaafu-tenisi/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/serena-williams-kustaafu-tenisi/#respond Wed, 10 Aug 2022 11:45:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2307 New York, MarekaniNyota wa mchezo wa tenisi duniani, Serena Williams ametoa kauli inayoashiria kujiandaa kustaafu mchezo huo licha ya kutokuwa wazi na kusema kwamba baada ya Mashindano ya Wazi ya Marekani (US Open) atajitenga kidogo na mchezo huo.Akiandika katika Jarida la Vogue, Serena mwenye umri wa miaka 40 sasa na kinara wa Grand Slam mara […]

The post Serena Williams kustaafu tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Nyota wa mchezo wa tenisi duniani, Serena Williams ametoa kauli inayoashiria kujiandaa kustaafu mchezo huo licha ya kutokuwa wazi na kusema kwamba baada ya Mashindano ya Wazi ya Marekani (US Open) atajitenga kidogo na mchezo huo.
Akiandika katika Jarida la Vogue, Serena mwenye umri wa miaka 40 sasa na kinara wa Grand Slam mara 23 alisema kwamba anajipanga kwenda kufanya mambo mengine muhimu na kwamba safari hiyo inaanza hapo hapo akasema kwamba halipendi neno kustaafu.
Juni mwaka huu Serena aliibukia kwenye michuano ya tenisi ya Wimbledon baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu akiandamwa na majeraha, alisema kwamba atashiriki katika Mashindano ya Wazi ya Marekani akiwa na rekodi ya kushinda mashindano hayo kwa mtu mmoja mmoja mataji sita kuliko mcheza tenisi mwanamke yeyote na akishika nafasi ya pili kwa rekodi ya jumla ya mashindano hayo akiwa ametanguliwa na Margaret Court.
“Bahati mbaya sikuweza kushinda Michezo ya Wimbledon mwaka huu na sijui kama nitakuwa tayari kushinda ile ya New York lakini nitajaribu,” alisema.
“Najua kuna hamasa kutoka kwa mashabiki kwamba ningeweza kuifikia rekodi ya Margaret siku ile London, na labda kuipiku rekodi hiyo New York, na baada ya hapo kupewa taji na kufanya sherehe, nalijua hilo, ni hamasa nzuri ingawa siangalii hilo,” alisema.
“Ninapata tabu sana kuaga, ni jambo baya duniani lakini tafadhali eleweni kwamba ninawashukuru katika namna ambayo siwezi kuieleza kwa maneno,” aliongeza.
Serena alisema kwamba amekuwa akisita yeye mwenyewe kujiambia au kumwambia mtu mwingine yeyote kwamba analazimika kujiweka kando na tenisi.
“Ni jambo gumu, Alexis, mume wangu na mimi hatukuwahi kuzungumza hili, ni kama mada haramu, pia siwezi hata kuwa na mazungumzo ya aina hii na mama au baba, najikuta katika wakati mgumu, koo linakwama na najikuta nikianza kulia, kuna watu wengi nawajua ambao hufurahia kulizungumza hili na wako tayari kulipokea, natamani nami ningekuwa katika hali kama hiyo,” alisema.
Kutokana na mafanikio yao kwenye mchezo wa tenisi, Serena na dada yake, Venus wanatajwa kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo huo kwa kuuongezea umaarufu duniani ikiwamo kutoa hamasa kwa wachezaji wa baadaye huku pia wakidaiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutetea masuala ya haki za kijinsia.

The post Serena Williams kustaafu tenisi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/serena-williams-kustaafu-tenisi/feed/ 0