Taifa Stars - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 31 May 2026 12:19:01 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Taifa Stars - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/#respond Sun, 31 May 2026 12:18:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14668 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaita katika kikosi chake wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys.Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa Mei 29, 2026 iliwataja wachezaji hao kuwa ni Kassim Juma na Luqman Mbalasalu ambao watajiunga katika kikosi hicho […]

The post Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaita katika kikosi chake wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa Mei 29, 2026 iliwataja wachezaji hao kuwa ni Kassim Juma na Luqman Mbalasalu ambao watajiunga katika kikosi hicho baada ya Juni 2, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa dhidi ya Uganda Cranes, Ijumaa, Juni 5, 2026.
Baada ya mechi hiyo, Stars itaingia tena uwanjani Jumanne, Juni 9, 2026 kwa mechi yake ya pili dhidi ya timu ya Rwanda, mechi zote hizo zitachezwa mjini Marakech, Morocco.
Wachezaji wengine wa timu hiyo waliotajwa katika kikosi cha Gamondi, wameanza kuingia kambini tangu Ijumaa iliyopita.
Kwa upande wa Serengeti Boys, timu hiyo itacheza mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) chini ya miaka 17 dhidi ya Senegal, mechi itakayochezwa mjini Rabat, Morocco, usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026 kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan.

The post Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/feed/ 0
Stars yapata ushindi wa kishindo https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/stars-yapata-ushindi-wa-kishindo/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/stars-yapata-ushindi-wa-kishindo/#respond Mon, 30 Mar 2026 19:19:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14502 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars imeibuka na ushindi wa kishindo kwa kuichapa timu ya Macau mabao 6-0 katika mwendelezo wa mechi maalum za Fifa (Fifa Series) mjini Kigali, Rwanda.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili Machi 29, 2026, Stars ilitawala kwa kiwango kikubwa mchezo huo baada ya kushindwa kutamba katika mechi yake ya […]

The post Stars yapata ushindi wa kishindo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars imeibuka na ushindi wa kishindo kwa kuichapa timu ya Macau mabao 6-0 katika mwendelezo wa mechi maalum za Fifa (Fifa Series) mjini Kigali, Rwanda.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili Machi 29, 2026, Stars ilitawala kwa kiwango kikubwa mchezo huo baada ya kushindwa kutamba katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Liechtenstein ilipolala kwa bao 1-0.
Ukurasa wa mabao ya Stars ulianza kufunguliwa dakika ya 15 ya mchezo kwa bao la kuzawadiwa baada ya Amancio kujifunga katika harakati za kuokooa na dakika 10 baadaye, Bakari Mwamnyeto akaiongezea Stars bao la pili.
Mudathir Yahya aliongeza bao la tatu kwa Stars muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko na hivyo kufanya timu zende mapumziko, Stars wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili Stars iliendeleza moto wake na kuandika bao la nne dakika ya 56 lililofungwa na Paul Peter wakati bao la tano lilifungwa na Novatus Dismas dakika ya 74 na Allarakhia akakamilisha idadi ya mabao sita dakika tatu kabla ya mpira kumalizika.
Hii ni mechi ya sita kwa kocha Miguel Gamondi tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa timu hiyo siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) zilizofanyika kuanzia Desemba mwaka jana nchini Morocco.
Chini ya Gamondi, Stars imecheza mechi nne za Afcon 2025 na kuishia hatua ya 16 bora kabla ya kutolewa na wenyeji Morocco na mechi nyingine mbili za michuano ya Fifa Series.

The post Stars yapata ushindi wa kishindo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/stars-yapata-ushindi-wa-kishindo/feed/ 0
Stars yakwama Fifa Series https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/stars-yakwama-fifa-series/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/stars-yakwama-fifa-series/#respond Sat, 28 Mar 2026 15:19:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14490 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars imeanza vibaya mechi maalum za Fifa (Fifa Series) kwa kupigwa bao 1-0 na timu ya Liechtenstein, mechi iliyochezwa Alhamisi Machi 26, 2026 kwenye Uwanja wa Pele mjini Kigali, Rwanda.Bao pekee lililoizamisha Stars lilifungwa katika dakika ya 54 na Ferhat Saglam aliyemalizia kwa kuujaza wavuni mpira ulioanzia […]

The post Stars yakwama Fifa Series first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars imeanza vibaya mechi maalum za Fifa (Fifa Series) kwa kupigwa bao 1-0 na timu ya Liechtenstein, mechi iliyochezwa Alhamisi Machi 26, 2026 kwenye Uwanja wa Pele mjini Kigali, Rwanda.
Bao pekee lililoizamisha Stars lilifungwa katika dakika ya 54 na Ferhat Saglam aliyemalizia kwa kuujaza wavuni mpira ulioanzia kwa Nicolas Hasler baada ya Liechtenstein kucheza pasi kadhaa langoni mwa Stars.
Kuingia kwa bao hilo hakukuwakatisha tamaa wachezaji wa Stars ambao kwa muda mrefu walionesha uhai wakitengeneza nafasi kadhaa ingawa tatizo la umaliziaji lilijidhihirisha katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi ya Stars ambayo mengi yalitokea kwa mawinga pia yalikutana na kizingiti kwenye safu ya ulinzi ya Liechtenstein ambayo ilikuwa macho kudhibiti kila hatari iliyoelekezwa kwenye lango lao.
Baada ya matokeo hayo, Stars sasa inasubiri kuumana na Macau, mechi itakayochezwa Jumapili Machi 29 kwenye uwanja huo huo, mechi ambayo itatoa mshindi wa tatu wakati mechi ya fainali pia itapigwa siku hiyo hiyo kwa mechi kati ya Liechtenstein na Aruba.

The post Stars yakwama Fifa Series first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/stars-yakwama-fifa-series/feed/ 0
Gamondi amuita Manula Stars https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/gamondi-amuita-manula-stars/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/gamondi-amuita-manula-stars/#respond Thu, 19 Mar 2026 07:37:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14459 Na mwandishi wetuKocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi amemuita katika kikosi chake kipa mzoefu wa Azam FC, Aishi Manula.Manula ambaye pia amewahi kutamba na timu ya Simba, katika mechi za karibuni ameanza kuonesha ubora wake jambo ambalo linaaminika kumshawishi kocha huyo Mtaliano kumuita katika kikosi hicho.Wachezaji wengine walioitwa katika timu […]

The post Gamondi amuita Manula Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi amemuita katika kikosi chake kipa mzoefu wa Azam FC, Aishi Manula.
Manula ambaye pia amewahi kutamba na timu ya Simba, katika mechi za karibuni ameanza kuonesha ubora wake jambo ambalo linaaminika kumshawishi kocha huyo Mtaliano kumuita katika kikosi hicho.
Wachezaji wengine walioitwa katika timu hiyo itakayoingia kambini Machi 22, 2026 ni Mohamed Mussa (Mashujaa FC), Zubeir Foba (Azam), Yona Amosi (Pamba Jiji), Bakari Msimu (Coastal Union), Twalib Nuru (Azam) na Haji Mnoga (Sallford City-UK).
Wengine ni Elias Lameck (Azam), Nickson Kibabage (Simba), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Mohamed Hussein (Yanga) Ibrahim Abdullah Bacca (Yanga), Yusuph Kagoma (Simba), Kelvin Nashon (Pamba Jiji), Mudathir Yahya (Yanga) na Alphonce Mabula (Shamakhi-Azerbaijan).
Katika orodha hiyo pia wamo Novatus Dismas (Goztepe FC-Uturuki), Feisal Salum (Azam), Simon Msuva (Al Taraba-Iraq), Idd Suleiman Nado (Azam), Kelvin John (Aalborg BK-Denmark), Charles M’mombwa (Floriana FC-Malta), Suleiman Mwalimu (Simba), Paul Peter (JTK Tanzania) na Tarryn Allarakhia (Rochdalle AFC-UK).

The post Gamondi amuita Manula Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/gamondi-amuita-manula-stars/feed/ 0
Taifa Stars yafa kiume https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/#respond Sun, 04 Jan 2026 19:49:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14252 Rabat, MoroccoUmewahi kusikia hadithi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufa kiume, achana na hadithi zote za nyuma, hadithi ya kweli imetokea leo Jumapili Januari 4, 2026 kwa timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Morocco kwenye fainali za Afcon 2025.Stars ikiumana na wenyeji Morocco katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) imekubali […]

The post Taifa Stars yafa kiume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Umewahi kusikia hadithi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufa kiume, achana na hadithi zote za nyuma, hadithi ya kweli imetokea leo Jumapili Januari 4, 2026 kwa timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Morocco kwenye fainali za Afcon 2025.
Stars ikiumana na wenyeji Morocco katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) imekubali kipigo hicho na hivyo kuaga fainali hizo huku ikiweka rekodi ya kipekee kwa kupambana kisawasawa na Morocco ambao ni wenyeji wa fainali hizo.
Matarajio ya Stars kufungwa mabao mengi yalitoweka na hadi dakika 90 zinamalizika Morocco, timu lenye hadhi na heshima yake katika soka, Afrika na duniani kote, ilishikwa kila kona na kujikuta ikiambulia bao hilo pekee.
Morocco ambao kwa ushindi huo wamefuzu hatua ya robo fainali, waliuanza mchezo kwa kufanya mashambulizi na kuongoza kwa umiliki wa mpira kwa zaidi ya asilimia 70 katika kipindi chote cha kwanza lakini nidhamu ya safu ya ulinzi ya Stars ilikuwa kikwazo.
Safu hiyo ya ulinzi ya Stars ilifanikiwa kuwavuruga Morocco mbele ya maelfu ya mashabiki wao ambao licha ya kushangilia kwa muda mwingi, hawakuamini kuona timu zikitoka uwanjani kwenda mapumziko bila kufungana.
Moja ya nafasi ambazo Morocco walizitengeneza lakini hazikuweza kuwapatia bao ni katika dakika ya 24 baada ya Ismail Saibari kuuwahi mpira wa juu na kuujaza wavuni kwa kichwa lakini mwamuzi alikataa bao hilo baada ya kutumia VAR kwa madai kwamba mfungaji aliotea.
Stars ambao wanajivunia rekodi ya kufikia hatua ya mtoano ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza, nao walifanya mashambulizi kadhaa kwa nidhamu ya hali ya juu, mfano katika kipindi hicho Simon Msuva akiwa ndani ya 18 alishindwa kuunganisha vyema krosi ya Seleman Abdallah.
Kipindi cha pili juhudi za Morocco zilizaa matunda dakika ya 63 baada ya kupata bao hilo pekee lililotokana na shuti la chini lililopigwa na mshambuliaji wa Real Madrid, Brahim Diaz na kujaa wavuni huku kipa Hussein Masalanga akiishia kuugusa mpira huo na mkono wake wa kushoto.
Stars, licha ya kufungwa bao hilo lakini waliendelea kuonesha upambanaji bila kujali aina ya mpinzani waliyekuwa wakishindana naye na katika dakika za lala salama, Iddi Nado aliangushwa na beki wa Morocco, Adam Masina wakati akiambaa na mpira kuelekea lango la Morocco.
Kuangushwa kwa mchezaji huyu kuliibua malalamiko kwa wachezaji na benchi la Stars wakitaka wapewe penalti au VAR itumike ili kujua undani wa tukio hilo lakini mwamuzi wa mechi hiyo, Boubou Traore alikataa kutoa penalti.
Wakati Stars ikiziaga fainali hizo ikiwa kifua mbele, Morocco sasa wanasubiri kuumana na mshindi wa mechi kati ya Afrika Kusini na Cameroon katika mechi ya robo fainali.

The post Taifa Stars yafa kiume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/feed/ 0
Stars wananifikirisha ya Chipolopolo https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:22:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14247 Na Hassan KinguTimu ya taifa ya Morocco imekamilika kila idara, historia yake inatisha, si Afrika tu bali duniani kote, tayari imeonesha ubora wake kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa kufika hatua ya nusu fainali.Unapozungumzia Kombe la Dunia maana yake ni kwamba unazungumzia mashindano makubwa ya soka duniani, Morocco wameonesha ubora wao katika michuano […]

The post Stars wananifikirisha ya Chipolopolo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Timu ya taifa ya Morocco imekamilika kila idara, historia yake inatisha, si Afrika tu bali duniani kote, tayari imeonesha ubora wake kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa kufika hatua ya nusu fainali.
Unapozungumzia Kombe la Dunia maana yake ni kwamba unazungumzia mashindano makubwa ya soka duniani, Morocco wameonesha ubora wao katika michuano hiyo na kuingia katika orodha ya timu tishio.
Morocco ni timu ya kwanza barani Afrika kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia, hii ni rekodi ya kipekee na ya kujivunia si kwa Morocco tu bali hata Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linajivunia rekodi hiyo.
Katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea nchini Morocco, wenyeji hao Morocco ni timu inayopewa nafasi kubwa kama si nafasi ya kwanza kubeba taji hilo au kulibakisha nyumbani.
Morocco hiyo ambayo inatisha Afrika yenye rekodi za kutisha kuanzia kwenye Afcon yenyewe, Jumapili hii ya Januari 4, 2026 itacheza na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, timu ambayo haikuwamo katika timu zinazopewa nafasi ya japo kufikia hatua ya robo fainali.
Si robo fainali tu, Taifa Stars haikuwamo hata katika timu ambazo ungeweza kuzitaja kuwa zitavuka hatua ya makundi, ni timu ambayo ilihusishwa na mechi tatu za makundi na baada ya hapo kurudi nyumbani.
Kilichotokea ni tofauti na matarajio ya wengi, hata baadhi ya mashabiki wachache wa Tanzania ambao pengine hawakupenda kuona timu hiyo inafanikiwa wameshangazwa na hatua ambayo timu imefikia.
Huenda hata wachezaji wenyewe hawakutarajia kama wangefanya vizuri kiasi cha kufuzu kucheza hatua ya mtoano (16 bora) na hilo linathibitishwa na hali ya furaha waliyokuwa nayo baada ya kufuzu kiasi cha kuimba kibao cha ‘Sisi ndio wale wale mliotukataa mkasema hatufiki mbali…’
Kimsingi Taifa Stars iliingia katika Afcon ikiwa kile kinachoitwa ‘underdogs’ unaweza kusema ni timu dhaifu lakini leo imepiga hatua na sasa inasubiri kukabiliana na Morocco au miamba ya soka barani Afrika.

Wanachokutana nacho Stars leo kinanikumbusha tukio la mwaka 2012, timu ya taifa ya Zambia ikiwa chini ya kocha Mfaransa, Renard Herve ililishangaza bara la Afrika, haikuwa timu iliyotajwa au kupewa nafasi ya kufika mbali, mafanikio pekee ambayo ilihusishwa nayo ni kupambana hadi kufika hatua ya robo fainali.
Hali ikawa tofauti, Zambia au Chipolopolo (pichani) ilipiga hatua moja baada ya nyingine ikiwapangua vigogo na mwishowe ikafika fainali na kubeba taji hilo katika michuano iliyofanyika Guinea ya Ikweta na Gabon.
Katika fainali za 2012 kuna ukweli kwamba baadhi ya nchi mahiri katika soka Afrika zilikuwa na matatizo ya kisiasa kuanzia Misri, Libya na Algeria, hapo hapo timu za Nigeria, Afrika Kusini na Cameroon zilishindwa kufuzu.
Kwa baadhi ya wachambuzi hali hiyo ilijengewa hoja kwamba ndio sababu mojawapo ya Zambia kufanya vizuri hadi kubeba taji la michuano hiyo lakini kimsingi kilichowawezesha Zambia kubeba taji ni uwezo na kujiamini kwa wachezaji.
Kujiamini huko ndiko kulikoifanya timu hiyo ipenye hadi kubeba taji katika michuano ambayo pia ilishirikisha mataifa mengine mahiri katika soka la Afrika kuanzia Morocco, Senegal na wenyeji Guinea na Gabon.
Kubwa kuliko yote ni ushindi wao katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast, taifa ambalo lina heshima yake katika soka la Afrika na kabla ya mechi ndiyo timu iliyotajwa na wachambuzi na hata wacheza kama kuwa ndiyo ambayo ingebeba taji hilo na kuwa taji lao la nne kwa wakati huo.
Hali hata hivyo ikawa kinyume, Zambia wakaishangaza Afrika, wakawashangaza wachambuzi na wacheza kamari, wakaushangaza ulimwengu kwa kutoka sare na Ivory Coast kabla ya kuwatoa kwenye penalti na kubeba taji.
Sijui ni kwa nini na huenda si mimi peke yangu, historia ya Chipolopolo hadi kuibwaga Ivory Coast na kubeba taji la Afcon 2012 inanifikirisha wakati huu Taifa Stars ikijiandaa kuikabili Morocco.

The post Stars wananifikirisha ya Chipolopolo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/feed/ 0
Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/#respond Tue, 30 Dec 2025 20:10:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14233 Rabat, MoroccoTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mara ya kwanza imeingia hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia, mechi iliyochezwa leo Jumanne, Desemba 30, 2025.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kufikia hatua hiyo baada ya kuishia […]

The post Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mara ya kwanza imeingia hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia, mechi iliyochezwa leo Jumanne, Desemba 30, 2025.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kufikia hatua hiyo baada ya kuishia hatua ya makundi katika fainali zote ilizofuzu kuanzia mwaka 1980 ilipofuzu kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Mechi dhidi ya Tunisia ndiyo ya mwisho kwa Stars katika mechi zake za Kundi C na imemaliza ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Nigeria iliyoshika usukani, Tunisia ya pili na Uganda ikiburuza mkia katika kundi hilo.
Stars imemaliza na pointi mbili, Nigeria tisa na Tunisia nne wakati Uganda haina pointi hata moja na kuiacha Stars ikifuzu kupitia kundi la best loosers na sasa inasubiri kuumana na wenyeji Morocco.
Tunisia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 42 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Ismail Gharbi baada ya Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ kumkaba shingoni Hazem Mastouri wa Tunisia aliyekuwa akiuwahi mpira wa juu uliopigwa na Hannibal Mejbri kuelekea kwenye lango la Stars.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Jacques Ndala Ngambo baada ya kujiridhisha kupitia VAR na picha kurudiwa zikimuonesha Bacca alivyomzuia Mastouri kwa kumkaba shingoni ndani ya eneo la penalti na mwamuzi kumpa kadi ya njano beki huyo wa Yanga.
Stars walisawazisha bao hilo dakika ya 54 mfungaji akiwa Feisal Salum au Fei Toto ambaye alifumua shuti la chinichini akiwa nje ya eneo la 18 na kumuacha kipa wa Tunisia, Aymen Dahmen akiruka bila mafanikio.
Tunisia waliuanza mchezo vizuri wakitawala kila eneo na Stars kujikuta wakifanya kazi ya kuzuia mashambulizi na katika dakika ya 11, Gharbi alifumua shuti lililogonga mwamba wa juu kwenye kona na kurudi uwanjani na kuwaacha mashabiki wa Stars wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kipa wa Stars, Hussein Masalanga aliruka akijaribu kuufuata mpira huo lakini aliishia kuuangalia kwa macho ukigonga mwamba kabla ya kurudi uwanjani.


Stars nao walianza kujiamini huku Mbwana Samatta na Simon Msuva wakionekana kuwa tishio kwenye lango la Tunisia ambao hatimaye walianza kucheza kwa tahadhari zaidi.
Kocha wa Stars, Miguel Gamondi ambaye timu yake ilianza mchezo kwa kujihami, kipindi cha pili alionekana kubadili mbinu ambazo zilisaidia kuifanya Stars icheze pasi na kulisogelea lango la Tunisia mara kadhaa na haikushangaza kwa timu hiyo kupata bao.
Katika kipindi hicho, Gamondi alianza kwa kumtoa Samatta na nafasi yake kuingia Seleman Mwalimu, baadaye akamtoa Mohamed Hussein Zimbwe na kuingia Paschal Msindo.
Mabadiliko hayo yaliendelea kwa kuwatoa, Fei Toto, Msuva na Haji Mnoga na nafasi zao kuingia Charles M’mombwa, Tarryn Allarakhia na Shomari Kapombe.
Stars sasa ina kazi ngumu ya kuwakabili wenyeji Morocco, mechi ambayo itachezwa Jumapili ijayo ya Januari 4, 2026 wakati siku moja kabla Tunisia wao wataumana na Mali.

The post Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/feed/ 0
Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/#respond Sat, 27 Dec 2025 20:50:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14226 Rabat, MoroccoTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na […]

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.
Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na kumshinda kipa mkongwe wa Cranes, Dennis Onyango.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi baada ya Baba Alhassan wa Cranes, kuunawa mpira uliopigwa na Alphonce Mabula na Alhassan kujichanganya katika harakati za kuokoa na kujikuta akiuzuia mpira huo kwa mkono ingawa kipa wake aliokoa.
Cranes baada ya kufungwa bao hilo walianza kulisakama lango la Stars mara kwa mara huku Stars wakiwa na kazi ya kuzuia kabla ya mambo kuharibika dakika ya 69 baada ya Cranes kupata bao la kusawazisha.
Bao hilo lilitokana na mpira ulioanzia kwa kipa Onyango aliyetoa pasi ndefu kabla ya kupigwa krosi ambayo ilipigwa na Denis Omedi na Uche Ikpeazu akaujaza mpira wavuni kwa kichwa.
Kuingia kwa bao hilo ni kama vile kuliwaamsha Cranes ambao dakika chache baadaye nusura waandike bao la pili baada ya kupata penalti iliyotokana na makosa ya Haji Mnoga aliyemshika mchezaji mmoja wa Cranes lakini mpigaji wa penalti, Allan Okelo akaupaisha mpira.
Cranes ndio waliouanza mpira kwa kasi kwa kupeleka mashambulizi ya mapema yaliyoanzia kwa beki wa kushoto Abdul Aziz Kayondo ambaye alikuwa akipanda na kupiga krosi chonganishi ambazo hata hivyo ziliokolewa na kipa Zubeir Foba.
Stars nao walijibu mapigo na kutengeneza nafasi kadhaa ikiwamo dakika ya 41 baada ya Kelvin John akiwa katika nafasi nzuri lakini mpira alioupiga ulipaa juu ya lango la Cranes.


Katika mechi ya leo, kocha wa Stars Miguel Gamondi alianza kwa kumuweka benchi nahodha Mbwana Samatta kabla ya kumuingiza dakika ya 63 akichukua nafasi ya Kelvin John.
Mechi ya leo ilikuwa na neema mara mbili kwa Msuva kwani licha ya kufunga bao lililoibeba Stars pia ndiye aliyetajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kwa matokeo hayo, Stars na Cranes ambazo zimepangwa kundi moja na timu za Nigeria na Tunisia, sasa zitakuwa na kazi ya kuhakikisha zinashinda mechi zao za mwisho zilizobaki ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya mtoano (16 bora).
Timu hizo zimepoteza mechi zao za kwanza, Stars ikilala kwa Nigeria na Cranes mbele ya Tunisia na katika mechi zao za mwisho hatua ya makundi zitakazochezwa Jumanne Desemba 30, 2025, Stars itaivaa Tunisia na Cranes itaumana na Nigeria.

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/feed/ 0
Nigeria yailaza Taifa Stars 2-1 https://www.greensports.co.tz/2025/12/24/nigeria-yailaza-taifa-stars-2-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/24/nigeria-yailaza-taifa-stars-2-1/#respond Wed, 24 Dec 2025 20:16:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14217 Rabat, Morocco.Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) nchini Morocco kwa kuchezea kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Nigeria au Super Eagles.Katika mechi hiyo ya kwanza kwa timu zote iliyopigwa Jumanne hii Desemba 23, 2025 kwenye dimba la El Barid mjini Rabat, Nigeria ndio […]

The post Nigeria yailaza Taifa Stars 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) nchini Morocco kwa kuchezea kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Nigeria au Super Eagles.
Katika mechi hiyo ya kwanza kwa timu zote iliyopigwa Jumanne hii Desemba 23, 2025 kwenye dimba la El Barid mjini Rabat, Nigeria ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Semiu Ajayi dakika ya 35.
Stars ilipambana na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 50 kupitia kwa Charles M’Mombwa aliyeyatumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Nigeria hadi kupata bao hilo lililoibua matumaini kwa mashabiki wa Tanzania.
Nigeria hata hivyo walizima matumaini ya Watanzania dakika mbili baadye walipoongeza bao la pili na la ushindi kupitia kwa Ademola Lookman na hivyo kujihakikishia ushindi katika mechi yao ya kwanza.
Stars na Nigeria zipo Kundi C na timu za Tunisia na Uganda, katika kundi hilo kila timu imebakisha mechi mbili kabla ya kujua hatma zao kama ni kuaga michuano mapema au kuendelea katika hatua inayofuata.
Stars itaumana na Uganda Jumamosi ya Desemba 27, 2025 siku ambayo pia Nigeria itaumana na Tunisia na Stars itamalizia na mechi dhidi ya Tunisia siku tatu baadaye, siku ambayo pia Uganda itacheza na Nigeria.
Akizungumza baada ya mechi, kocha wa Nigeria, Eric Chelle alisema mechi ilikuwa muhimu na kubwa kwa timu yake na anaamini ni muhimu kupata ushindi katika mechi ya kwanza.
Kwa upande wake kocha wa Stars, Miguel Gamondi alisema yaliyopita yamepita na hakuna wa kuwazuia katika kujiamini na kuipigania ndoto yao.

The post Nigeria yailaza Taifa Stars 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/24/nigeria-yailaza-taifa-stars-2-1/feed/ 0
Waziri ataka mafanikio zaidi Stars https://www.greensports.co.tz/2025/12/18/waziri-ataka-mafanikio-zaidi-stars/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/18/waziri-ataka-mafanikio-zaidi-stars/#respond Thu, 18 Dec 2025 20:23:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14202 Na mwandishi wetuWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars’ inayoshiriki Afcon 2025 kuhakikisha wanapata mafanikio zaidi ya yale ya CHAN.Waziri Kabudi alitoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 18, 2025 akiwa kwenye kambi ya timu hiyo jijini Cairo nchini Misri wakati akiwakabidhi wachezaji hao […]

The post Waziri ataka mafanikio zaidi Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamagamba Kabudi amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Tafa Stars’ inayoshiriki Afcon 2025 kuhakikisha wanapata mafanikio zaidi ya yale ya CHAN.
Waziri Kabudi alitoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 18, 2025 akiwa kwenye kambi ya timu hiyo jijini Cairo nchini Misri wakati akiwakabidhi wachezaji hao bendera ya taifa huku akiwataka wachezaji hao kuwa fahari ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo vya Shirikisho la Saoka Tanzania (TFF) Waziri Kabudi alifafanua kuwa katika CHAN, Stars iliishia hatua ya robo fainali hivyo ni muhimu kwenda mbele zaidi.
Michuano ya CHAN inayohusisha nchi za mataifa ya Afrika hushirikisha wachezaji wa ligi za ndani, ilifanyika hivi karibuni kwa pamoja katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Waziri Kabudi pia aliwaambia wachezaji wa Stars kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anawatakia kila la kheri na amemuhakikishia kuwa mafanikio ya CHAN hayakuwa madogo na huko Morocco wanawatakia mafanikio makubwa zaidi.
Katika fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025, Stars imepangwa Kundi C na timu za Uganda, Tunisia na Nigeria na itacheza mechi yake ya kwanza Jumanne, Desemba 23 dhidi ya Nigeria.

The post Waziri ataka mafanikio zaidi Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/18/waziri-ataka-mafanikio-zaidi-stars/feed/ 0