Sadio Mane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 01 Aug 2023 19:29:38 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Sadio Mane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mane amfuata Ronaldo Al Nassr https://www.greensports.co.tz/2023/08/01/mane-amfuata-ronaldo-al-nassr/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/01/mane-amfuata-ronaldo-al-nassr/#respond Tue, 01 Aug 2023 19:29:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7213 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameachana na timu hiyo na kujiunga na Al-Nassr ya Saudi Arabia ambayo pia anachezea nyota wa zamani wa Man United na Real Madrid, Cristiano Ronaldo.Mane, (pichani) mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, ameifungia Bayern mabao 12 katika mechi 38 za msimu wa 2022-23 huku akiwa katika msimu mgumu ulioandamana […]

The post Mane amfuata Ronaldo Al Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameachana na timu hiyo na kujiunga na Al-Nassr ya Saudi Arabia ambayo pia anachezea nyota wa zamani wa Man United na Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Mane, (pichani) mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, ameifungia Bayern mabao 12 katika mechi 38 za msimu wa 2022-23 huku akiwa katika msimu mgumu ulioandamana na majanga ya kuwa majeruhi.
Mchezaji huyo pia Aprili mwaka huu alijikuta akiwa gumzo kwenye vyombo vya habari akidaiwa kumpiga mchezaji mwenzake, Leroy Sane wakiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kupoteza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City.
Katika siku za karibuni, Mane mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama Bayern na ikaelezwa kwamba alikuwa akiwaniwa na timu za Saudi Arabia huku Bayern ikidaiwa kwamba imerudisha pesa ilizotumia kumnunua mshambuliaji huyo kutoka Liverpool mwanzoni mwa msimu wa 2022-23.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayern, Jan-Christian Dreesen aliwahi kusema kwamba Mane ambaye pia aliwahi kuichezea Southampton hakuwa na msimu rahisi tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Liverpool.
“Na ndio maana sote pamoja tumeamua kwamba afungue ukurasa mpya wa maisha yake ya soka na kuanza upya katika klabu nyingine, tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika changamoto mpya na Al-Nassr,” alisema Dreesen.
Mapema leo Jumanne, kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alisema kwamba yeye na Mane walikubaliana kwa pamoja kwamba kilichotokea hakikuwa kitu kizuri.
“Tulikumbatiana kwa muda mrefu na kwa pamoja tulikubaliana kwamba hatujapenda kilichotokea wakati huu lakini tunafikiri ni katika mazingira yaliyo mema,” alisema Tuchel.

“Kuna wakati mambo hayaendi vizuri kama ambavyo mtu anataka, mimi binafsi nimekuwa na uhusiano mazuri na Mane na itabaki kuwa hivyo, naelewa kabisa ameumizwa na hata mimi siwezi kufurahia mambo yakiwa katika namna hiyo,” aliongeza Tuchel.


The post Mane amfuata Ronaldo Al Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/01/mane-amfuata-ronaldo-al-nassr/feed/ 0
Sadio Mane ampongeza Pape Sakho https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/#respond Tue, 25 Jul 2023 12:45:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7109 Na mwandishi wetuMshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 2022, Sadio Mane amempongeza aliyekuwa winga wa Simba, Pape Sakho kwa kujiunga na timu ya Union Sportive Quevillaise ya Ligi Daraja la Pili Ufaransa.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, mshambuliaji huyo anayekipiga Beyern Munich ya Ujerumani alisema anajisikia furaha kuona ndoto za Sakho […]

The post Sadio Mane ampongeza Pape Sakho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 2022, Sadio Mane amempongeza aliyekuwa winga wa Simba, Pape Sakho kwa kujiunga na timu ya Union Sportive Quevillaise ya Ligi Daraja la Pili Ufaransa.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, mshambuliaji huyo anayekipiga Beyern Munich ya Ujerumani alisema anajisikia furaha kuona ndoto za Sakho za kucheza Ulaya zimetimia.
Kwa upande wake Sakho raia wa Senegal kama ilivyo kwa Mane ambaye tayari ametambulishwa Union Sportive Quevillaise, alimshukuru Mane kwa ushirikiano aliompa na kumfanikishia kufika hapo alipo.
“Asante kaka kwa kufanikisha dili hili, nakukubali sana na siku zote utabaki kuwa mfano mzuri kwangu,” alisema Sakho ambaye naye ni mshindi wa tuzo ya bao bora la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2021-22.
Sakho (pichani juu) aliyeitumikia Simba kwa misimu miwili alisema baada ya dili lake la kujiunga na timu hiyo ya Ufaransa yupo katika wakati mgumu kuagana na watu wake wa karibu lakini hakuna namna sababu mchezo wa mpira ndivyo ulivyo.

“Nimeishiwa maneno ya kusema lakini siku zote Simba itabaki kuwa familia yangu, mchezo wa soka ni mchezo wa kupanda viwango, nami nimechagua kusogea mbele kwa faida yangu binafsi,” alisema Sakho.


Mchezaji huyo pia ameushukuru uongozi wa Simba, kwa ushirikiano na upendo mkubwa waliompa tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Teungueth ya kwao na ameitakia timu hiyo mafanikio mema na kushinda mataji yote itakayoshiriki msimu ujao.

The post Sadio Mane ampongeza Pape Sakho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/feed/ 0
Saudi Arabia kwamvutia Mane https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/#respond Tue, 25 Jul 2023 05:22:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7098 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameanza kuipigia hesabu ofa ya klabu ya Al-Nasr ya Saudi Arabia ambayo imeonesha nia ya kumsajili.Mane alijiunga na Bayern kabla ya msimu uliopita wa 2022-23 kwa ada ya Pauni 35 milioni akitokea Liverpool lakini hakuweza kuonesha makali aliyokuwa nayo wakati akiwa Liverpool na zipo habari kwamba Bayern ipo […]

The post Saudi Arabia kwamvutia Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ameanza kuipigia hesabu ofa ya klabu ya Al-Nasr ya Saudi Arabia ambayo imeonesha nia ya kumsajili.
Mane alijiunga na Bayern kabla ya msimu uliopita wa 2022-23 kwa ada ya Pauni 35 milioni akitokea Liverpool lakini hakuweza kuonesha makali aliyokuwa nayo wakati akiwa Liverpool na zipo habari kwamba Bayern ipo tayari kumpiga bei.
Kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel anaonekana kupoteza matumaini na mchezaji huyo na hivyo yupo tayari kufanya biashara na klabu yoyote itakayojitokeza wakati Mane naye inadaiwa tayari amefanya mazungumzo ya awali na mabosi wa Al-Nasr.
Akiwa Liverpool, Mane alijipatia mafanikio kwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England kabla ya kutimkia Bayern akidai kwamba ulikuwa wakati sahihi kwake kupata changamoto mpya ingawa mambo hayakwenda kama yalivyotarajiwa.
Kibaya zaidi, Mane aliingia katika mzozo na mchezaji mwenzake wa Bayern, Leroy Sane akidaiwa kumpiga ngumi Aprili mwaka huu baada ya timu hiyo kushindwa kutamba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City.
Tukio hilo lilimfanya aondolewe kwenye kikosi cha Bayern na kutozwa faini ingawa baadaye alirudishwa lakini hadi mwisho wa msimu aliishia kufunga mabao 12 katika mechi 38.
Kocha Tuchel aliwahi kusema kwamba mambo hayajawa rahisi kwa Mane kwenye kikosi cha kwanza na ushindani umekuwa mkubwa mno kwake na mchezaji huyo anafahamu hilo na anaujua msimamo wa klabu.
Ikitokea mpango wa Mane kwenda klabu ya Al-Nasr ukafanikiwa, mchezaji huyo atakuwa ameungana na winga wa zamani wa klabu za Real Madrid na Mancheter United, Cristiano Ronaldo.

The post Saudi Arabia kwamvutia Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/saudi-arabia-kwamvutia-mane/feed/ 0
Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/#respond Fri, 19 May 2023 08:08:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6210 London, EnglandKlabu za Newcastle na Man United zimeingia vitani kila moja ikiwania kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane (pichani) ambaye mambo yake si mazuri katika klabu hiyo.Mane mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita alitamba na Liverpool na ndiye aliyeiwezesha timu ya Senegal kutwaa taji la Mataifa ya Afrika, tangu atue Bayern msimu huu […]

The post Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu za Newcastle na Man United zimeingia vitani kila moja ikiwania kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane (pichani) ambaye mambo yake si mazuri katika klabu hiyo.
Mane mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita alitamba na Liverpool na ndiye aliyeiwezesha timu ya Senegal kutwaa taji la Mataifa ya Afrika, tangu atue Bayern msimu huu amekuwa na wakati mgumu.
Kasi yake ya upachikaji mabao iliyozoeleka inaonekana kupotea huku akiandamwa na majanga ya hapa na pale ikiwamo tukio la hivi karibuni la kumpiga ngumi mchezaji mwenzake, Leroy Sane.
Baada ya tukio hilo lililotokea kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City na Bayern kulala kwa mabao 3-0, Bayern ilimsimamisha Mane na akakosa mechi moja.
Baada ya tukio hilo habari mpya zilianza kuibuka kwamba Bayern inajiandaa kumpiga bei na sasa Man United na Newcastle zimeonekana kuwa mstari wa mbele kila moja ikiitaka saini ya mchezaji huyo.
Man United na Newcastle zote zipo vizuri kwenye Ligi Kuu England (EPL) katika kupigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao hivyo kama kigezo cha Mane kitakuwa na michuano hiyo, atakuwa huru kuchagua mojawapo ya timu hizo.
Katika EPL, Newcastle inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 katika mechi 36 wakati Man United inashika nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 35.

The post Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/19/sadio-mane-aziingiza-vitani-man-utd-newcastle/feed/ 0
Bayern yamsimamisha Sadio Mane https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/bayern-yamsimamisha-sadio-mane/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/bayern-yamsimamisha-sadio-mane/#respond Fri, 14 Apr 2023 06:19:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5799 Munich, UjerumaniBayern Munich imemsimamisha mshambuliaji wake, Sadio Mane anayedaiwa kumpiga ngumi mchezaji mwenzake, Leroy Sane baada ya mechi na Man City huku kukiwa na habari kwamba huenda mchezaji huyo akauzwa.Katika mechi hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Jumanne iliyopita na Bayern kulala kwa mabao 3-0, uliibuka mzozo wa maneno baina ya […]

The post Bayern yamsimamisha Sadio Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Bayern Munich imemsimamisha mshambuliaji wake, Sadio Mane anayedaiwa kumpiga ngumi mchezaji mwenzake, Leroy Sane baada ya mechi na Man City huku kukiwa na habari kwamba huenda mchezaji huyo akauzwa.
Katika mechi hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Jumanne iliyopita na Bayern kulala kwa mabao 3-0, uliibuka mzozo wa maneno baina ya wachezaji hao uwanjani na baadaye kuendelea kuzozana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Inadaiwa kwamba baadaye hali ilikuwa tete kiasi cha wachezaji hao kushikana hali iliyowalazimu wachezaji wenzao kufanya kazi ya kuamua ugomvi.
Baada ya tukio hilo, Bayern ilitoa taarifa fupi ya hatua za kinidhamu dhidi ya mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool ambaye pia ni mchezaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Senegal.

“Sadio Mane, 31, hatokuwa katika kikosi cha Bayern kitakachoumana na 1899 Hoffenheim Jumamosi na sababu ni utovu wa nidhamu wa mchezaji huyo baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Man City, na zaidi ya hilo atatozwa faini.” ilieleza taarifa ya Bayern kuhusu Mane.


Habari zaidi zinadai kwamba Mane (pchani kushoto) alichukizwa na kauli alizotolewa na Sane baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Man City kwenye dimba la Etihad.
Bayern haijatoa taarifa nyingine yoyote kuhusu tukio hilo huku ikidaiwa kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel leo Ijumaa huenda akazungumza na waandshi wa habari na kuligusia suala hilo.
Kipigo cha mabao 3-0 ni kikubwa mno kwa Bayern, mara ya mwisho kupata kipigo kama hicho ilikuwa mwaka 2017 mbele ya PSG.
Bayern inajiandaa kurudiana na Man City Aprili 19 mwaka huu katika mechi ambayo itahitaji kupata ushindi wa zaidi ya mabao 3-0 ili kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

The post Bayern yamsimamisha Sadio Mane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/14/bayern-yamsimamisha-sadio-mane/feed/ 0