Richarlison - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 14 Sep 2023 14:13:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Richarlison - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Richarlison asaka tiba ya kisaikolojia https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/richarlison-asaka-tiba-ya-kisaikolojia/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/richarlison-asaka-tiba-ya-kisaikolojia/#respond Thu, 14 Sep 2023 14:13:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7754 Rio de Janeiro, BrazilMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema anajiandaa kutafuta msaada wa kisaikolojia atakaporudi England baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.Richarlison alionekana kwenye picha mbalimbali Jumamosi iliyopita akitokwa machozi baada ya kutolewa wakati akiiwakilisha Brazil katika mechi na Bolivia ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, mechi ambayo Brazil ilishinda kwa mabao 5-1.Baadaye […]

The post Richarlison asaka tiba ya kisaikolojia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema anajiandaa kutafuta msaada wa kisaikolojia atakaporudi England baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Richarlison alionekana kwenye picha mbalimbali Jumamosi iliyopita akitokwa machozi baada ya kutolewa wakati akiiwakilisha Brazil katika mechi na Bolivia ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, mechi ambayo Brazil ilishinda kwa mabao 5-1.
Baadaye mchezaji huyo alisema kwamba hali hiyo ilimtokea kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza ndani na nje ya uwanja ambayo yapo nje ya taratibu zake.
Richarlison amefunga mabao manne tu katika mechi 40 alizoichezea Spurs tangu ajiunge na timu hiyo majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Everton kwa ada ya Pauni 60 milioni.
“Nimepitia kipindi kigumu mno nje ya uwanja katika miezi hii mitano iliyopita, walau kwa sasa mambo yameanza kuwa mazuri nyumbani, watu ambao macho yao yalikuwa kwenye pesa zangu tu kwa sasa hawapo tena karibu na mimi,” alisema Richarlison.
“Mambo sasa yameanza kwenda vizuri, na naamini nitakuwa na mwendelezo mzuri Tottenham, na mambo yatawezekana kwa mara nyingine,” alisema.

“Nikirudi England naenda kutafuta msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wataalam, ili nijiimarishe zaidi kifikra, hiyo ndiyo hali halisi, nataka kurudi katika ubora nikiwa imara,” alisema.


Richarlison alishindwa kuitumia nafasi aliyoipata katika mechi na Bolivia na baadaye kutolewa dakika ya 71 na juzi Jumanne alitolewa dakika ya 64 katika mechi dhidi ya Peru, mechi ambayo Brazil ilishinda kwa bao 1-0.
Richarlison ambaye hivi karibuni ilidaiwa ameachana na wakala wake wa siku nyingi, Renato Velasco, alisema kwamba hali ya huzuni aliyokuwa nayo haikutokana na kucheza vibaya na si kweli kwamba mechi na Bolivia ilimkataa.
“Kwa mawazo yangu sikucheza vibaya mechi na Bolivia, bali ilikuwa ni katika kuguswa na matukio ya nje ya uwanja yaliyo nje ya taratibu zangu, ambayo yamenitawala na kushindwa kujiongoza, si kwa sababu ya lolote nililofanya bali ni kwa sababu ya watu walio karibu nami,” alisema Richarlison.
Richarlison alisema kwamba anaamini atakuwa katika timu ya Brazil kwenye mechi ijayo na hilo ndilo jambo analolifanyia kazi na pia anataka kuweka mambo sawa na Spurs kwa kuzungumza na viongozi.
Brazil itacheza mechi nyingine ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Venezuela itakayopigwa Oktiba 13 na siku tano baadaye itacheza na Uruguay wakati kwenye Ligi Kuu England, Spurs ya Richarlison, Jumamosi itakuwa mwenyeji wa Sheffield United.

The post Richarlison asaka tiba ya kisaikolojia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/14/richarlison-asaka-tiba-ya-kisaikolojia/feed/ 0
Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/#respond Mon, 10 Jul 2023 05:53:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6892 London, EnglandMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema kwamba kocha wa zamani wa timu hiyo, Antonio Conte alimkaripia kwa takriban saa mbili wakati wakiwa kwenye kikao cha timu hiyo.Richarlison ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Spurs msimu uliopita wa 2022-23 chini ya Conte kabla […]

The post Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema kwamba kocha wa zamani wa timu hiyo, Antonio Conte alimkaripia kwa takriban saa mbili wakati wakiwa kwenye kikao cha timu hiyo.
Richarlison ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Spurs msimu uliopita wa 2022-23 chini ya Conte kabla ya kocha huyo kutimuliwa mwezi Machi.
Utata baina ya Richarlison na Conte ulianza baada ya mchezaji huyo kumshushia lawama kocha huyo baada ya Spurs kutolewa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo baadaye Conte alisema kwamba mchezaji huyo ni mbinafsi.
Richarlison hata hivyo alikiri kwamba alikosea kumlaumu kocha wake hadharani na kujikuta akipewa adhabu mbele ya wachezaji wenzake.
“Ni kweli nilifanya upuuzi mimi mwenyewe kwa kusema katika mahojiano baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa lakini baadaye nilimuomba radhi,” alisema Richarlison.
“Nilifikia hatua ya kumwambia kwamba hata kama anataka kuniadhibu anaweza kufanya hivyo, tulimaliza lile pale,” alisema.
“Lakini alitaka pia aoneshe ukali wake mbele ya wachezaji, ni kama kusema kwamba yupo imara na ndiye kiongozi, hiyo ndiyo namna yake ya kukabiliana na watu, na kundi la wachezaji na alitumia kama saa mbili kunishambulia mimi tu kwenye kikao mbele ya kila mtu,” alisema Richarlison.
Richarlison alisema kwamba baada ya tukio lile baadhi ya wachezaji walimwambia asifanye tena alichokifanya na kila mmoja alitaka kuondoka.
Conte alimsajili Richarlison kutoka Everton mwanzoni mwa msimu wa 2022-23 lakini mchezaji huyo alipitia kipindi kigumu kidogo, hakuwa katika kiwango chake bora baada ya kuandamwa na majeraha hadi kuishia kufunga bao moja tu katika Ligi Kuu England.
Richarlison, 26, hata hivyo alisema kwamba baada ya Conte kutimuliwa Spurs aliwasiliana naye na kumuomba radhi. “Nilimtumia ujumbe wa kumuomba radhi kwa sababu ni mtu ambaye aliniajiri na sikumsaidia kwa kiwango alichofikiria, jambo pekee nililoona linafaa kulifanya ni kumuomba radhi.”

The post Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/feed/ 0