Real Madrid - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 31 May 2026 08:46:25 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Real Madrid - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mourinho asaini mkataba Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/#respond Sun, 31 May 2026 08:46:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14658 Madrid, HispaniaJose Mourinho au Speacial One anadaiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Real Madrid ingawa atatangazwa rasmi baada ya uchaguzi wa rais wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 7, 2026.Hii itakuwa mara ya pili kwa Mourinho kuinoa timu hiyo ingawa uhalali wa mkataba wake upo njia panda na kila kitu kitajulikana rasmi baada […]

The post Mourinho asaini mkataba Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Jose Mourinho au Speacial One anadaiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Real Madrid ingawa atatangazwa rasmi baada ya uchaguzi wa rais wa klabu hiyo utakaofanyika Juni 7, 2026.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Mourinho kuinoa timu hiyo ingawa uhalali wa mkataba wake upo njia panda na kila kitu kitajulikana rasmi baada ya rais wa sasa, Florentino Perez kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo.
Mourinho, 63, amekuwa akihusishwa katika nafasi hiyo mara kadhaa tangu kuondoka kwa Xabi Alonso Januari mwaka huu na nafasi yake kukabidhiwa kocha wa muda, Alvaro Arbeloa.
Kwa kukubali kuinoa Real Madrid, Mourinho anaachana na klabu ya Benfica ambayo alianza kuinoa Septemba mwaka jana na ameiwezesha kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Ureno maarufu Primera Liga msimu huu.
Akiwa na Real Madrid mara ya kwanza kati ya mwaka 2010 hadi 2013, kocha huyo kutoka Ureno aliiwezesha timu hiyo kutwaa mataji ya La Liga, Copa del Rey na Spanish Super Cup.
Mourinho pia amewahi kuzinoa timu za FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Tottenham, Man United, AS Roma na Fenerbahce.
Msimu huu wa 2025-26 na msimu uliopita imekuwa migumu kwa Real Madrid ikimaliza bila taji lolote na msimu huu imeuaga kwa kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mahasimu wao Barcelona katika El Clasico.
Perez, 79, anaamini Mourinho ana uwezo wa kurudisha heshima Real Madrid ingawa bado ana kazi ya kuchuana katika kiti cha urais wa klabu hiyo na Enrique Riquelme, bilionea aliyewekeza katika nishati jadidifu.
Tangu mwaka 2009, Perez amekuwa Real Madrid akikosa mpinzani tishio katika kiti cha urais na kabla ya hapo aliiongoza klabu hiyo kati ya mwaka 2000 na 2006, safari hii licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda urais, ujasiri wa Riquelme unaacha maswali mengi.

The post Mourinho asaini mkataba Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/mourinho-asaini-mkataba-real-madrid/feed/ 0
Man United, Arsenal zamsaka Rodrygo https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/man-united-arsenal-zamsaka-rodrygo/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/man-united-arsenal-zamsaka-rodrygo/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:10:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14240 Madrid, HispaniaHabari ya winga wa Real Madrid, Rodrygo kutaka kuachana na timu hiyo imeibuka kwa mara nyingine na tayari timu za Arsenal, Man United na Liverpool zimeonesha nia ya kuitaka huduma ya mchezaji huyo.Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuonesha nia ya kutaka kuihama timu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa hafurahishwi na […]

The post Man United, Arsenal zamsaka Rodrygo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Habari ya winga wa Real Madrid, Rodrygo kutaka kuachana na timu hiyo imeibuka kwa mara nyingine na tayari timu za Arsenal, Man United na Liverpool zimeonesha nia ya kuitaka huduma ya mchezaji huyo.
Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuonesha nia ya kutaka kuihama timu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa hafurahishwi na mambo yanavyokwenda ikiwamo uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Rodrygo 24, kwa sasa ana mkataba na Real Madrid ambao unafikia ukomo mwaka 2028 na kinachoonekana ni kama vile klabu hiyo inasita kumruhusu nyota huyo aondoke kwani hata habari hiyo ilivyojitokeza huko nyuma jaribio hilo halikufanikiwa.
Nyota huyo ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Brazil, inaonekana safari hii amedhamiria kutafuta changamoto nje ya klabu hiyo licha ya mabosi wake kuwa wagumu kumruhusu.
Mashabiki na wachambuzi wengi wanamuona Rodrygo kuwa ni aina ya mchezaji mwenye kipaji ambacho kinakuwa bora na aliwahi kufananishwa na mastaa wengine wa Brazil, Neymar na Robinho.

The post Man United, Arsenal zamsaka Rodrygo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/man-united-arsenal-zamsaka-rodrygo/feed/ 0
Alonso atambia umoja Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/alonso-atambia-umoja-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/alonso-atambia-umoja-real-madrid/#respond Mon, 15 Dec 2025 09:33:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14179 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Xabi Alonso amepongeza kuwapo kwa umoja katika timu yake baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Alaves katika mechi ya La Liga iliyopigwa jana Jumapili Desemba 14, 2025.Alonso anapitia kipindi kigumu ndani ya timu hiyo kutokana na matokeo mabaya ya hivi karibuni kikiwamo kipigo cha mabao 2-1 mbele ya […]

The post Alonso atambia umoja Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso amepongeza kuwapo kwa umoja katika timu yake baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Alaves katika mechi ya La Liga iliyopigwa jana Jumapili Desemba 14, 2025.
Alonso anapitia kipindi kigumu ndani ya timu hiyo kutokana na matokeo mabaya ya hivi karibuni kikiwamo kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Man City katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kylian Mbappe, mshambuliaji aliyekuwa majeruhi aliifungia Madrid bao la kwanza, Alaves waliokuwa nyumbani wakasawazisha kupitia Carlos Vicente kabla ya Rodrygo kuipatia Madrid bao la pili kwa pasi ya Vinicius Junior.
Ushindi huo mbali na kumpa ahueni Alonso aliyekuwa akihusishwa na mipango ya kutimuliwa pia umeifanya Madrid kuwasogelea mahasimu wao Barca wanaoshika usukani katika La Liga kwa kupunguza idadi ya pointi kufikia nne.
Matokeo mabaya ya Real Madrid kwenye La Liga hususan kipigo cha mabao 2-0 mbele ya Celta Vigo yalianza kuibua hisia za kuitoa timu hiyo kwenye mbio za kusaka taji la La Liga huku kukiwa na habari kwamba mabosi walianza kuijadili nafasi ya Alonso.
Sambamba na matokeo mabaya, Alonso pia alianza kujadiliwa kuhusu uhusiano wake na wachezaji mastaa mmojawao akiwa Vinicius tangu mchezaji huyo aoneshe hasira za waziwazi baada ya kocha kumtaka aende benchi katika mechi dhidi ya Barca maarufu Clasico.

“Sisi sote tupo pamoja, tunapambana pamoja katika hatua nzuri na huu ni wakati mzuri, timu ilipambana vizuri na kwa mara nyingine tuko tayari kusonga mbele, umoja ni kitu muhimu,” alisema Alonso baada ya ushindi dhidi ya Alaves.


Kabla ya mapumziko ya Krismasi, Madrid watacheza mechi mbili ambazo pia zitakuwa kipimo kingine muhimu kwa Alonso, keshokutwa Jumatano wataumana na Talavera de la Reina katika Copa del Rey na mwishoni mwa wiki watakuwa na kibarua mbele ya Sevilla katika La Liga.

The post Alonso atambia umoja Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/15/alonso-atambia-umoja-real-madrid/feed/ 0
Alonso: Wachezaji wapo nami https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/alonso-wachezaji-wapo-nami/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/alonso-wachezaji-wapo-nami/#respond Wed, 10 Dec 2025 18:56:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14163 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Xabi Alonso amesisitiza kuwa anaendelea kuungwa mkono na wachezaji wake na yuko katika hali ya utulivu wakati huu zikiwapo habari kwamba kibarua chake kipo njia panda.Madrid itaumana na Man City Jumatano hii Novemba 10, 2025, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi ambayo matokeo mabaya kwa timu hiyo huenda […]

The post Alonso: Wachezaji wapo nami first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso amesisitiza kuwa anaendelea kuungwa mkono na wachezaji wake na yuko katika hali ya utulivu wakati huu zikiwapo habari kwamba kibarua chake kipo njia panda.
Madrid itaumana na Man City Jumatano hii Novemba 10, 2025, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi ambayo matokeo mabaya kwa timu hiyo huenda yakawa sababu tosha ya kutimuliwa kwa Alonso.
Mwenendo wa Madrid katika mechi za karibuni si mzuri, timu hiyo imeshinda mechi moja kati ya tano zilizopita ikiwamo Jumapili ilipolala kwa mabao 2-0 mbele ya Celta Vigo hali ambayo ilizidisha presha kwa Alonso.
Habari zaidi zinadai kwamba baada ya matokeo dhidi ya Celta Vigo, rais wa klabu hiyo, Florentino Pérez alifanya kikao na wajumbe wa bodi kujadili mwelekeo wa Alonso kukiwa na hofu kuhusu uongozi wake na viwango vya wachezaji tegemeo wa timu hiyo.
Kwa upande wake Alonso alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo anaungwa mkono na wachezaji wake, kocha huyo alijibu, ndiyo na kufafanua kuwa kuna umoja katika kikosi chake.

“Timu ipo katika hali ya umoja, inashawishi, kila mmoja anaamini tutashinda kesho (Jumatano) hakuna mwenye shaka lakini katika hilo ni lazima tucheze kwa mwenendo mzuri, tuwe imara na washindani,” alisema Alonso.


Naye kiungo wa Madrid, Aurélien Tchouameni alipozungumza baadaye alisema matokeo mabaya ikiwamo kufungwa bao 1-0 na Liverpool katika ligi ya mabingwa na sare tatu dhidi ya Rayo Vallecano, Elche na Girona kabla ya kupoteza mbele ya Celta Vigo, tatizo si Alonso.
Tchouameni alifafanua kuwa katika mechi na Celta Vigo, kocha alikuwa na mpango mzuri lakini mwisho wa siku ni wao wachezaji ndio wanaokuwa uwanjani kama wakiwa katika kiwango chao wanakuwa na nafasi nzuri ya kushinda na wakipoteza kunakuwa na tatizo baina yao uwanjani na si kocha.

The post Alonso: Wachezaji wapo nami first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/alonso-wachezaji-wapo-nami/feed/ 0
Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/#respond Sun, 26 Oct 2025 19:57:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14039 Madrid, HispaniaReal Madrid imetoka kifua mbele dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwa kuwachapa mabao 2-1, leo Jumapili Oktoba 26, 2025, mechi ambayo baada ya dakika 90 ilitawaliwa na mzozo wa wachezaji Lamine Yamal na Vinicius Junior au Vini Jr.Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kylian Mbappe kwa pasi […]

The post Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Real Madrid imetoka kifua mbele dhidi ya mahasimu wao Barcelona kwa kuwachapa mabao 2-1, leo Jumapili Oktoba 26, 2025, mechi ambayo baada ya dakika 90 ilitawaliwa na mzozo wa wachezaji Lamine Yamal na Vinicius Junior au Vini Jr.
Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Kylian Mbappe kwa pasi ya Jude Bellingham ambaye aliivuruga safu ya ulinzi ya Barca kabla ya kutoa pasi iliyozaa bao hilo.
Barca walikuja juu na kusawazisha bao hilo dakika ya 38 kwa bao la Fermín López ambaye aliitumia pasi ya Marcus Rashford, mshambuliaji wa Man United anayeichezea Barca kwa mkopo.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Jude Bellingham aliipatia Real bao la pili na la ushindi baada ya kuinasa pasi ya Éder Milita.
Real walionesha kila dalili za kutoka na ushindi katika mechi hiyo, dakika ya pili tu ya mchezo, Vini Jr aliangushwa ndani ya eneo la penalti na mwamuzi kuipa Real penalti lakini ilifutwa baada ya mapitio ya VAR.
Picha ya VAR ilibaini kwamba kabla ya kuanguka, Vini Jr alimkwatua Lamine Yamal mgunni na hivyo maamuzi hayo kubadilishwa.
Ushindi huo ni hatua nzuri kwa Real kwani ni kama vile imefuta uteja baada ya kufungwa na Barca katika mechi zote nne za msimu uliopita.
Nje ya matokeo hayo ambayo yanaifanya Real kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga, tukio la Yamal na Vini Jr limeendelea kuteka hisia za mashabiki wa timu hizo mbili.
Tukio hilo lililotokea baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo liliibuka kwa kinachoaminika kuwa ni vita ya maneno baina ya wachezaji hao tegemeo kwa timu zote.

Awali mzozo ulianza kati ya Yamal na Dani Carvajal kubadilishana kauli za hasira lakini wakati Yamal akielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, Vini Jr ni kama aliuwasha moto upya kwa kumvaa Yamal kwa maneno.
Vini alianza kwa kumwambia Yamal kuwa ni mchezaji mwenye kutoa pasi za kisigino tu kabla ya kuongeza kwa kumwambia kuwa anaongea sana na kumtaka aongee baada ya matokeo hayo.
Kauli ya Vini Jr inaaminika kutokana na alichokisema Yamal kabla ya mechi hiyo kwamba Real wana tabia ya kufanya matukio ya kudanganya katika mechi zao.
Kauli za Yamal ni kama vile zilipuuzwa na wachezaji wa Real ingawa hali ilikuwa tofauti kwa mashabiki ambao kwa muda mwingi walikuwa wakimzomea mchezaji huyo.

The post Real yailaza Barca, Vini Jr, Yamal wazozana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/26/real-yailaza-barca-vini-jr-yamal-wazozana/feed/ 0
Florian Wirtz atua Liverpool https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/#respond Fri, 13 Jun 2025 18:44:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13598 Liverpool, EnglandMabingwa wa Ligi Kuu England (EPL) Liverpool, wamekubali kumsajili kiungo mshambuliaji Florian Wirtz (pichani juu) kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 100 milioni.Ada ya mchezaji huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 22, imeweka rekodi kwa klabu ya Liverpool wakati kwa England ni CHelsea iliyoweka rekodi ya juu mwaka 2023 ilipomsajili Enzo […]

The post Florian Wirtz atua Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Liverpool, England
Mabingwa wa Ligi Kuu England (EPL) Liverpool, wamekubali kumsajili kiungo mshambuliaji Florian Wirtz (pichani juu) kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 100 milioni.
Ada ya mchezaji huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 22, imeweka rekodi kwa klabu ya Liverpool wakati kwa England ni CHelsea iliyoweka rekodi ya juu mwaka 2023 ilipomsajili Enzo Fernandez kutoka Benfica kwa ada ya Pauni milioni 107.
Hadi kumpata Wirtz, Liverpool ililazmika kushindana na Chelsea ambao walionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kama ilivyokuwa kwa Bayern Munich ambao nao walitajwa kumtaka.
Wirtz hata hivyo inaaminika aliweka wazi msimamo wake wa kuitaka Liverpool ambao walianza majadiliano na Leverkusen na kufikia muafaka licha ya klabu hiyo kuwasilisha ofa ya awali ya Pauni 126 milioni.
Kabla ya kujiunga na Leverkusen mwaka 2020, Wirtz ambaye pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara 31 na kuifungia mabao saba, aliwahi kuzichezea timu za SV Grün-Weiß na FC Cologne za Ujerumani.
Akiwa na Leverkusen ameifungia timu hiyo mabao 57 katika mechi 197 na mwaka 2024 alitoa mchango mkubwa kwa timu hyo hadi kubeba taji la Ligi Kuu Ujerumani maarufu Bundesliga.
Kwa sasa Liverpool pia ipo katika mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth, Milos Kerkez kwa ada inayotajwa kufikia Pauni milioni 45.
Wakati huo huo, klabu ya Real Madrid ya Hispania nayo inadaiwa kukamilisha usajili wa kinda wa River Plate ya Argentina, Franco Mastantuono (pichani chini) ambaye ni kiungo na mshambuliaji.
Mastantuono, 17, kwa sasa yuko nchini Marekani na klabu yake ya River Plate ambayo ataiwakilisha kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia itakayoanza kutimua vumbi Jumapili Juni 15, 2025 nchini Marekani.

Real Madrid ilionesha nia ya kumtaka nyota huyo takriban miaka miwili iliyopita kabla ya kuamua kukamilisha mpango huo mwaka huu wakati klabu kadhaa Ulaya ikiwamo PSG nazo zikidaiwa kumtolea macho.
Mastantuono ambaye Agosti 14 mwaka huu atatimiza miaka 18, atajiunga rasmi na timu yake hiyo mpya miezi miwili ijayo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2025-26.
Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa jimbo la Buenos Aires, Juni 5 mwaka huu aliichezea kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa ya Argentina katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Chile, mechi ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.

The post Florian Wirtz atua Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/feed/ 0
Ancelotti: Real Madrid tupo shwari https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/#respond Sun, 20 Apr 2025 08:41:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13283 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekana kuwapo mgogoro wa chinichini katika klabu hiyo huku akiweka wazi kwamba mambo yake ya baadaye yatajadiliwa mwisho wa msimu huu.Nafasi ya Ancelotti imekuwa mjadala katika siku za karibuni hasa baada ya timu hiyo kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutolewa na Arsenal.Real […]

The post Ancelotti: Real Madrid tupo shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekana kuwapo mgogoro wa chinichini katika klabu hiyo huku akiweka wazi kwamba mambo yake ya baadaye yatajadiliwa mwisho wa msimu huu.
Nafasi ya Ancelotti imekuwa mjadala katika siku za karibuni hasa baada ya timu hiyo kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutolewa na Arsenal.
Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabéu Jumatano iliyopita ililala kwa mabao 2-1 mbele ya Arsenal hiyo ni badaa ya kulala ugenini kwa mabao 3-0 na hivyo kutolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 5-1.
Kocha huyo Mtaliano tangu ajiunge kwa mara ya pili na Real Madrid mwaka 2021 ameweza kujiwekea rekodi nzuri ya kubeba mataji ya La Liga mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.
Msimu huu hata hivyo umekuwa mgumu kwa Ancelotti, timu yake imetolewa kwenye ligi ya mabingwa, michuano ambayo ina hadhi ya juu Ulaya na dunia kote wakati huo huo inahaha kubeba taji la La Liga.
Real Madrid msimu huu imepoteza mechi kadhaa katika namna ambayo haikutarajiwa, wiki ijayo itacheza mechi ya fainali Kombe la Mfalme, taji inalotakiwa ilipiganie walau itoke na kitu msimu huu.

“Nimezungumza na wachezaji na viongozi, sote tunafikiria katika mtazamo mmoja ambao ni kuendelea kupigania mataji yaliyobaki,” alisema Ancelotti.


Ancelotti alisisitiza kwamba hakuna mgogoro wowote na klabu na kwamba wote wapo katika safari moja na yeyote anayesema kuna mgogoro na klabu au rais (Florentino Perez) huyo hasemi ukweli.
Mkataba wa Ancelotti na Real Madrid unafikia ukomo mwaka 2026 ingawa kumekuwapo habari kwamba klabu hiyo inataka kuachana na kocha huyo ambaye pia inadaiwa anawindwa kwa udi na uvumba kwenye timu ya taifa ya Brazil.

The post Ancelotti: Real Madrid tupo shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/feed/ 0
Marcelo aipasha Arsenal, ‘Real Madrid ni Real Madrid’ https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/marcelo-aiambia-arsenal-real-madrid-ni-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/marcelo-aiambia-arsenal-real-madrid-ni-real-madrid/#respond Tue, 15 Apr 2025 19:14:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13256 Mexico City, MexicoBeki wa zamani wa Real Madrid, Marcelo amesema timu hiyo si ya kufutwa moja kwa moja wakati huu ikiwa na kibarua kigumu cha kupindua meza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.Real Madrid ina kazi ngumu ya kuupanda mlima baada ya kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Arsenal Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Enmirates katika […]

The post Marcelo aipasha Arsenal, ‘Real Madrid ni Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Mexico City, Mexico
Beki wa zamani wa Real Madrid, Marcelo amesema timu hiyo si ya kufutwa moja kwa moja wakati huu ikiwa na kibarua kigumu cha kupindua meza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Real Madrid ina kazi ngumu ya kuupanda mlima baada ya kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Arsenal Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Enmirates katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Marceloa ambaye ana rekodi ya kubeba mataji matano ya ligi ya mabingwa akiwa na Real Madrid anaamini hakuna jukumu ambalo ni kubwa zaidi kwa klabu hiyo.
“Huwezi kuifuta moja kwa moja Real Madrid, ingawa mabao matatu ni mengi lakini wakati wote huwa naifikiria Real Madrid na nina imani kubwa kwa timu hiyo kwamba inaweza kujibu mapigo, Real Madrid ni Real Madrid na inaweza kushinda,” alisema Marcelo.
Marcelo ambaye kwa sasa yuko nchini Mexico akijiandaa kucheza mechi ya El Clasico ambayo itahusisha wachezaji wa zamani wa Real Madrid na Barcelona, alisema katika mechi ya marudiano, Real Madrid itakuwa na faida ya kuwa nyumbani kwenye dimba la Bernabeu.

“Mechi ya marudiano itakuwa Bernabéu, mashabiki wataiunga mkono kwa nguvu na wachezaji wanaamini inawezekana, ingawa ni kweli hatujui nini kitatokea bali tuna imani na Real Madrid kujibu mapigo,” alisema Marcelo.

Marcelo aliongeza kwa kusema kuwa anadhani ushindi upo katika damu za wachezaji wa Real Madrid na ni kama vile ni jambo ambalo wanafundishwa mara tu wanapoanza kuvaa jezi ya timu hiyo.
“Nafikiri mara tu tunapojiunga na Real Madrid tunafundishwa kutokata tamaa na hilo kwa wakati wote linakuwa kwenye damu zetu, ni kufanya juhudi, kuvumilia, kujitoa kila siku pamoja na kuungwa mkono na mashabiki, ni kati ya vitu vinavyosaidia mambo yaende,” alisema Marcelo.

The post Marcelo aipasha Arsenal, ‘Real Madrid ni Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/marcelo-aiambia-arsenal-real-madrid-ni-real-madrid/feed/ 0
Ancelotti: Ni pigo kubwa https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/#respond Sun, 02 Mar 2025 09:16:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13076 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekiri timu yake imepata pigo kubwa katika mbio za kusaka taji la La Liga baada ya kufungwa mabao 2-1 na Real Betis jana Jumamosi.Katika mechi hiyo, Real Madrid ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa naBrahim Díaz lakini Betis walisawazisha kupitia kwa Johnny Cardoso na kuzifanya timu ziende […]

The post Ancelotti: Ni pigo kubwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekiri timu yake imepata pigo kubwa katika mbio za kusaka taji la La Liga baada ya kufungwa mabao 2-1 na Real Betis jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo, Real Madrid ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na
Brahim Díaz lakini Betis walisawazisha kupitia kwa Johnny Cardoso na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili, nyota wa zamani wa Real Madrid, Isco aliifungia Betis bao la pili kwa penalti na kuifanya Real Madrid ipoteze pointi tatu na kujiweka pagumu katika mbio za kulisaka taji hilo dhidi ya timu za Barcelona na Atlético Madrid.
Akizungumzia matokeo hayo, Ancelotti alisema mechi ilikuwa mbaya kwao licha ya kuanza vizuri lakini hawakuweza kuendelea na kasi yao hivyo kushindwa na timu ambayo ilicheza vizuri na ilikuwa haki yao kushinda.

“Hili ni pigo kubwa, lazima tuchukue hatua, kupoteza mechi katika hatua hii ya msimu ni pigo, hatukufanya vizuri, tulipoteza mpira mara 27 katika kipindi cha kwanza, hicho ni kiasi kikubwa,” alisema Ancelotti.


Ancelloti pengine baada ya kuona mambo yanakuwa magumu dakika ya 75 alimtoa Kylian Mbappe na kumuingiza Endrick, mabadiliko ambayo hayakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo.
Kocha huyo hata hivyo baadaye alisema kwamba Mbappe alikuwa na tatizo la jino na hata mazoezi hakufanya vizuri na alimtoa na kumuingiza Endrick ili kuepusha matatizo zaidi.
Real Madrid kwa sasa inapigania mataji matatu, Jumatano iliyopita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad katika nusu fainali ya Copa del Rey na keshokutwa Jumanne itacheza mechi ya hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

The post Ancelotti: Ni pigo kubwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/feed/ 0
Real Madrid kuikabili Liverpool Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2024/08/29/real-madrid-kuikabili-liverpool-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/29/real-madrid-kuikabili-liverpool-ligi-ya-mabingwa/#respond Thu, 29 Aug 2024 19:19:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11840 Monaco, UfaransaReal Madrid itazianza kampeni za kulitetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Liverpool katika mfumo mpya wa michuano hiyo ambao umefuta utaratibu wa timu kuanzia hatua ya makundi.Kwa mujibu wa droo iliyofanywa leo Alhamisi na Uefa, timu nyingine za England za Man City na Arsenal zote zitacheza na PSG wakati Aston […]

The post Real Madrid kuikabili Liverpool Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Monaco, Ufaransa
Real Madrid itazianza kampeni za kulitetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Liverpool katika mfumo mpya wa michuano hiyo ambao umefuta utaratibu wa timu kuanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa droo iliyofanywa leo Alhamisi na Uefa, timu nyingine za England za Man City na Arsenal zote zitacheza na PSG wakati Aston Villa itakuwa na Celtic ambao ni mabingwa wa Scotland.
Katika mfumo huo mpya utakaoanza msimu huu wa 2024-25 kwa wanaume ukiwa na timu 36, kila timu itacheza mechi nane za awali, nne nyumbani na nne ugenini na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Septemba 17 na 19 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mfumo huo mpya, idadi ya mechi sasa zitaongezeka kutoka 125 za awali hadi 189 wakati timu 16 za juu zitacheza hatua ya 16 bora.
Namna ratiba ya kila mechi itakavyokuwa itajulikana keshokutwa Jumamosi baada ya droo za michuano mingine ya klabu barani Ulaya ya Europa Ligi na Conference Ligi kufanyika lakini hadi sasa kila timu inawajua wapinzani wake kama ifuatavyo…
Aston Villa
Bayern Munich (H)
Leipzig (A)
Juventus (H)
Club Bruges (A)
Celtic (H)
Young Boys (A)
Bologna (H)
Monaco (A)
Arsenal
Paris St-Germain (H)
Inter Milan (A)
Shakhtar Donetsk (H)
Atalanta (A)
Dinamo Zagreb (H)
Sporting Lisbon (A)
Monaco (H)
Girona (A)
Celtic
Aston Villa (A)
Leipzig (H)
Borussia Dortmund (A)
Club Bruges (H)
Atalanta (A)
Young Boys (H)
Dinamo Zagreb (A)
Slovan Bratislava (H)
Liverpool
Real Madrid (H)
Leipzig (A)
Leverkusen (H)
AC Milan (A)
Lille (H)
PSV Eindhoven (A)
Bologna (H)
Girona (A)
Manchester City
Inter Milan (H)
Paris St-Germain (A)
Club Brugge (H)
Juventus (A)
Feyenoord (H)
Sporting Lisbon (A)
Sparta Prague (H)
Slovan Bratislava (A)

The post Real Madrid kuikabili Liverpool Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/29/real-madrid-kuikabili-liverpool-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0