Raphael Varane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 21 Dec 2023 09:07:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Raphael Varane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Real Madrid yamtaka Varane https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/real-madrid-yamtaka-varane/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/real-madrid-yamtaka-varane/#respond Thu, 21 Dec 2023 09:07:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8970 Madrid, HispaniaReal Madrid inatajwa kuanza hesabu za kumsajili kwa mara ya pili beki wa Man United, Raphael Varane ili kuziba pengo la David Alaba ambaye kwa sasa ni majeruhi.Taarifa ya chanzo kimoja cha habari iliyopatikana leo Alhamisi ilieleza kuwa Real Madrid ambayo imefuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inataka kuimarisha safu yake […]

The post Real Madrid yamtaka Varane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Real Madrid inatajwa kuanza hesabu za kumsajili kwa mara ya pili beki wa Man United, Raphael Varane ili kuziba pengo la David Alaba ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Taarifa ya chanzo kimoja cha habari iliyopatikana leo Alhamisi ilieleza kuwa Real Madrid ambayo imefuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya Alaba kuwa majeruhi na jina la Varane limeingia katika hesabu zao.
Varane aliyekuwa na timu ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, ambaye amewahi kuichezea Real Madrid kabla ya kuihama mwaka 2021 na kusajiliwa na Man United, zipo habari kwamba kwa sasa hafurahii mambo ndani ya klabu hiyo.
Mwenendo mzima wa Man United na mfumo wa kocha Ten Hag ni kati ya mambo ambayo yanatajwa kutomfurahisha Varane na hivyo anaweza kushawishika kurudi kwa mara nyingine katika jiji la Madrid.
Habari zaidi hata hivyo zinadai kwamba kocha Ten Hag haonekani kuwa tayari kumruhusu beki huyo ambaye mkataba wake unafikia ukomo mwakani aondoke kwa kuwa yumo katika mipango yake na timu hiyo.
Ten Hag pia hataki kiungo wake Mbrazil, Casemiro aondoke licha ya wachezaji hao wawili wote kudaiwa kwamba kuna timu zinawataka na huenda wakaondoka wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari.

The post Real Madrid yamtaka Varane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/21/real-madrid-yamtaka-varane/feed/ 0
Varane ajipanga kuondoka Old Trafford https://www.greensports.co.tz/2023/12/14/varane-ajipanga-kuondoka-old-trafford/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/14/varane-ajipanga-kuondoka-old-trafford/#respond Thu, 14 Dec 2023 07:05:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8866 Manchester, EnglandMan United huenda ikamkosa beki wake Raphael Varane ambaye anatajwa kuwa na mpango wa kuihama timu hiyo yenye makazi yake Old Trafford akiwa mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kukamkilika.Habari za ndani zinadai kuwa mchezaji huyo hafurahii maisha ya Man United ikidaiwa kuwa picha haziendi na kocha wake Erik ten Hag na kwa […]

The post Varane ajipanga kuondoka Old Trafford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man United huenda ikamkosa beki wake Raphael Varane ambaye anatajwa kuwa na mpango wa kuihama timu hiyo yenye makazi yake Old Trafford akiwa mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kukamkilika.
Habari za ndani zinadai kuwa mchezaji huyo hafurahii maisha ya Man United ikidaiwa kuwa picha haziendi na kocha wake Erik ten Hag na kwa muda mrefu amekuwa akipiga hesabu za kuondoka katika timu hiyo.
Mkataba wa Varane na Man United unatajwa kufikia mwisho majira ya kiangazi au kabla ya hapo, hivyo huenda Man United ikamkosa mchezaji huyu bila kupata chochote kama ataondoka akiwa huru.
Mambo si mazuri kwa sasa ndani ya kikosi cha Man United ambapo kocha wa timu hiyo, Ten Hag anapitia kipindi kigumu hasa baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Baadhi ya wachezaji akiwamo Varane inadaiwa hawafurahii mambo yanavyokwenda chini ya himaya ya Ten Hag ikiwamo mfumo wake wa kuiongoza timu pamoja na mbinu anazotumia.
Varane, 30, beki ambaye pia ametamba kwa muda mrefu katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha kwanza cha Man United hivyo suala la kuondoka katika timu hiyo ni jambo ambalo limekuwa likizungumzwa sana katika siku za karibuni.

The post Varane ajipanga kuondoka Old Trafford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/14/varane-ajipanga-kuondoka-old-trafford/feed/ 0
Varane afichua siri ya kustaafu mapema Ufaransa https://www.greensports.co.tz/2023/02/04/varane-afichua-siri-ya-kustaafu-mapema-ufaransa/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/04/varane-afichua-siri-ya-kustaafu-mapema-ufaransa/#respond Sat, 04 Feb 2023 15:03:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5005 Manchester, EnglandBeki wa kati ya Man United, Raphael Varane amesema kwamba uamuzi wake wa kustaafu mapema kuichezea timu ya Taifa ya Ufaransa umetokana na ratiba kuwa ngumu na yenye kumchosha.Varane ndio kwanza ana miaka 29 na juzi Alhamisi alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo akiwa na rekodi ya kuichezea mechi 93, akishika nafasi ya 13 kati […]

The post Varane afichua siri ya kustaafu mapema Ufaransa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa kati ya Man United, Raphael Varane amesema kwamba uamuzi wake wa kustaafu mapema kuichezea timu ya Taifa ya Ufaransa umetokana na ratiba kuwa ngumu na yenye kumchosha.
Varane ndio kwanza ana miaka 29 na juzi Alhamisi alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo akiwa na rekodi ya kuichezea mechi 93, akishika nafasi ya 13 kati ya wachezaji walioichezea timu hiyo mechi nyingi.
Mwaka 2018 alikuwa na timu ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia nchini Urusi na Desemba mwaka jana alikuwamo katika kikosi kilichofikia hatua ya fainali ya michuano hiyo lakini walishindwa kutamba mbele ya Argentina waliobeba kombe hilo.
Baada ya kutangaza kustaafu, Varane alilalamikia ratiba ngumu ya michuano mbalimbali na hivyo ili kujipunguzia mzigo akaamua kustaafu timu ya Taifa.
“Nilijitoa kwa kila kitu, kimwili na kiakili lakini mwishowe unakuwa mfano wa mashine ya kufulia nguo, unacheza kila mara bila kupumzika,” alisema Varane.

“Tuna ratiba iliyobeba michuano mingi na mnacheza bila kupumzika kwa sasa najiona kama mzigo umenizidia,” alisisitiza Varane ambaye alianza kuichezea Ufaransa mara ya kwanza mwaka 2013.


Wakati Varane akistaafu kuichezea timu hiyo akiwa na miaka 29, nahodha na kipa wa timu hiyo, Hugo Lloris yeye alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo mwezi uliopita akiwa na miaka 36.
Tatizo la ratiba ya michuano kuwa ngumu kwa wachezaji liliwahi pia kuzungumzwa na kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois ambaye mwaka 2021 alililalamikia Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) kwa kuwa na ratiba ngumu kwa wachezaji.
Kipa huyo alinukuliwa akisema kwamba wachezaji wanafanywa kama ‘maroboti’ kwa kubebeshwa kalenda ya soka ngumu na yenye mashindano mengi.

The post Varane afichua siri ya kustaafu mapema Ufaransa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/04/varane-afichua-siri-ya-kustaafu-mapema-ufaransa/feed/ 0
Varane astaafu kimataifa https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/varane-astaafu-kimataifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/varane-astaafu-kimataifa/#respond Fri, 03 Feb 2023 06:04:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4984 Manchester, EnglandBeki wa kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Manchester United, Raphael Varane ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya Taifa.Varane (pichani) ambaye alikuwa na kikosi cha timu ya Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, anastaafu akiwa ameifungia Ufaransa mabao matano katika mechi 93 tangu aichezee timu hiyo mara […]

The post Varane astaafu kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Manchester United, Raphael Varane ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya Taifa.
Varane (pichani) ambaye alikuwa na kikosi cha timu ya Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, anastaafu akiwa ameifungia Ufaransa mabao matano katika mechi 93 tangu aichezee timu hiyo mara ya kwanza mwaka 2013.
Anakuwa mchezaji wa pili wa Ufaransa kustaafu timu ya Taifa kwa siku za karibuni akiwa ametanguliwa na kipa na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Hugo Lloris ambaye alitangaza kutaafu mwezi uliopita.
Mara ya mwisho, Varane alikuwa na kikosi cha Ufaransa kwenye fainali za Kombe la Dunia za Qatar 2022 ingawa walishindwa kutamba mbele ya Argentina waliobeba taji wakiilaza Ufaransa kwa penalti 4-2 baada ya sare ya mabao 3-3 katika dakika 120.
Varane anajivunia kuiwakilisha Ufaransa kwa kipindi kirefu hadi sasa anaamua kustaafu “Kuiwakilisha nchi yetu kwa muongo mmoja (miaka 10) ni moja ya heshima kubwa katika maisha yangu.”

“Kila wakati nikivaa jezi hii ya kipekee ya bluu naona ufahari wa aina yake, wajibu wa kujitoa kwa kila kitu, kucheza nikiuridhisha moyo wangu na kushinda kila wakati ninapokuwa uwanjani,” alisema Varane.


“Nimekuwa nikilitafakari jambo hilo kwa miezi kadhaa sasa na hatimaye kuamua kwamba huu ni wakati sahihi kwangu kustaafu soka la kimataifa,” aliongeza.
Varane ambaye alikuwa akitajwatajwa kuwa mrithi wa Lloris katika nafasi ya unahodha wa timu hiyo, moja ya kumbukumbu zake kubwa za utotoni ni wachezaji mastaa waliokuwa na timu ya Ufaransa iliyobeba taji la dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa.
“Nikiwa mdogo nakumbuka kuifuatilia timu ya Ufaransa ya mwaka 1998, wachezaji hawa walitupa uzoefu na mvuto wa kipekee,” alisema.
“Nilijiwa na ndoto za kuwa shujaa na miaka 20 baadaye niliishi ndoto hiyo na kujikuta katika tukio la kipekee katika maisha yangu, tukio ambalo limenifanya nijivunie hasa, tulipeleka nyumbani Kombe la Dunia,” alisema.
“Kamwe sitokaa nisahau, bado nakumbuka mvuto na hamasa ya siku hiyo ya Julai 15, 2018, lilikuwa ni tukio la aina yake na la kuendelea kukumbukwa katika maisha yangu,” aliongeza Varane ambaye alijiunga na Man United Agosti 2021 akitokea Real Madrid.

The post Varane astaafu kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/03/varane-astaafu-kimataifa/feed/ 0