Pape Sakho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 23 Nov 2023 12:54:59 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Pape Sakho - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Sakho aiponza Simba, Fifa yaizuia kusajili https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/sakho-aiponza-simba-fifa-yaizuia-kusajili/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/sakho-aiponza-simba-fifa-yaizuia-kusajili/#respond Thu, 23 Nov 2023 12:54:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8599 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imepigwa marufuku kufanya usajili wa wachezaji hadi itakapoilipa klabu ya Teungueth ya Senegal pesa za usajili wa mchezaji Pape Sakho iliyomsajili kutoka timu hiyo.Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana leo Alhamisi, uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya klabu ya Teungueth kushinda […]

The post Sakho aiponza Simba, Fifa yaizuia kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imepigwa marufuku kufanya usajili wa wachezaji hadi itakapoilipa klabu ya Teungueth ya Senegal pesa za usajili wa mchezaji Pape Sakho iliyomsajili kutoka timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana leo Alhamisi, uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya klabu ya Teungueth kushinda kesi ya madai ya mauzo ya mchezaji huyo.
Sakho ambaye kwa sasa anaichezea Quevilly Metropole ya Ufaransa, aliichezea Simba kabla ya kutimkia Ufaransa ambapo katika madai yao, Teungueth walitaka Simba iwalipe sehemu ya malipo baada ya kumuuza mchezaji huyo katika klabu ya Quevilly.
Simba ilipewa siku 45 kuhakikisha inafanya malipo hayo lakini haikufanya hivyo na hatimaye uamuzi mgumu umefikiwa na sasa watalazimika kukamilisha malipo hayo kama watahitaji kukiongezea nguvu kikosi chao ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kikiwa katika hatua ya makundi.
Uamuzi wa Fifa kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo, unahusu usajili wa wachezaji kimataifa lakini TFF wameiongezea nguvu adhabu hiyo kwa kuipiga marufuku Simba kufanya usajili wa ndani.
Sakho akiwa na Simba takriban misimu miwili iliyopita alitoa mchango mkubwa katika timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC, Ligi ya Mabingwa Afrika na michuano mingine akiwa mmoja wa wachezaji muhimu.
Mchezaji huyo pia aling’ara Afrika katika tuzo za wanamichezo bora Afrika kwa kubeba tuzo ya bao bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika katika hafla iliyofanyika mjini Rabat, Morocco.
Tuzo hiyo aliipata baada ya kufunga bao zuri la ‘tik-taka’ katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, mechi ambayo Simba ilitoka na ushindi wa mabao 3-1.

The post Sakho aiponza Simba, Fifa yaizuia kusajili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/23/sakho-aiponza-simba-fifa-yaizuia-kusajili/feed/ 0
Sadio Mane ampongeza Pape Sakho https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/#respond Tue, 25 Jul 2023 12:45:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7109 Na mwandishi wetuMshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 2022, Sadio Mane amempongeza aliyekuwa winga wa Simba, Pape Sakho kwa kujiunga na timu ya Union Sportive Quevillaise ya Ligi Daraja la Pili Ufaransa.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, mshambuliaji huyo anayekipiga Beyern Munich ya Ujerumani alisema anajisikia furaha kuona ndoto za Sakho […]

The post Sadio Mane ampongeza Pape Sakho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 2022, Sadio Mane amempongeza aliyekuwa winga wa Simba, Pape Sakho kwa kujiunga na timu ya Union Sportive Quevillaise ya Ligi Daraja la Pili Ufaransa.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, mshambuliaji huyo anayekipiga Beyern Munich ya Ujerumani alisema anajisikia furaha kuona ndoto za Sakho za kucheza Ulaya zimetimia.
Kwa upande wake Sakho raia wa Senegal kama ilivyo kwa Mane ambaye tayari ametambulishwa Union Sportive Quevillaise, alimshukuru Mane kwa ushirikiano aliompa na kumfanikishia kufika hapo alipo.
“Asante kaka kwa kufanikisha dili hili, nakukubali sana na siku zote utabaki kuwa mfano mzuri kwangu,” alisema Sakho ambaye naye ni mshindi wa tuzo ya bao bora la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2021-22.
Sakho (pichani juu) aliyeitumikia Simba kwa misimu miwili alisema baada ya dili lake la kujiunga na timu hiyo ya Ufaransa yupo katika wakati mgumu kuagana na watu wake wa karibu lakini hakuna namna sababu mchezo wa mpira ndivyo ulivyo.

“Nimeishiwa maneno ya kusema lakini siku zote Simba itabaki kuwa familia yangu, mchezo wa soka ni mchezo wa kupanda viwango, nami nimechagua kusogea mbele kwa faida yangu binafsi,” alisema Sakho.


Mchezaji huyo pia ameushukuru uongozi wa Simba, kwa ushirikiano na upendo mkubwa waliompa tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Teungueth ya kwao na ameitakia timu hiyo mafanikio mema na kushinda mataji yote itakayoshiriki msimu ujao.

The post Sadio Mane ampongeza Pape Sakho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/sadio-mane-ampongeza-pape-sakho/feed/ 0
Pape Sakho aitwa timu ya Taifa https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/#respond Sun, 04 Jun 2023 07:28:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6432 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Benin.Sakho (pichani) ameitwa kwenye kikosi hicho na kocha mkuu wa timu hiyo, Aliou Cisse kwa mara ya pili baada ya awali kuitwa Machi mwaka huu walipokuwa wakijiandaa kuuamana […]

The post Pape Sakho aitwa timu ya Taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Benin.
Sakho (pichani) ameitwa kwenye kikosi hicho na kocha mkuu wa timu hiyo, Aliou Cisse kwa mara ya pili baada ya awali kuitwa Machi mwaka huu walipokuwa wakijiandaa kuuamana na timu ya taifa ya Msumbiji.
Senegal iliyoita jumla ya wachezaji 26 itavaana na Benin ikiwa ugenini Juni 17 mjini Cotonou kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Brazil Juni 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa José Alvalade mjini Lisbon, Ureno.
Cisse hata hivyo amewatema mshambuliaji wa Lorient, Bamba Dieng na kipa wa Chelsea, Edouard Mendy katika kikosi hicho na kuwajumuisha winga Ismail Jacobs wa AS Monaco, kiungo Pape Gueye (Sevilla) na Cheikhou Kouyate (Nottingham Forest) aliyerejea kikosini baada ya awali kukosekana kutokana na majeraha.
Baadhi ya nyota wengine walioitwa kwenye kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Afcon ni Sadio Mane wa Bayern Munich, Kalidou Koulibaly (Chelsea), Gana Gueye (Everton), Ismaila Sarr (Watford) na Abdou Diallo (RB Leipzig).
Senegal inaongoza Kundi L ikiwa na pointi 10, ikifuatiwa na Msumbiji yenye pointi nne, Rwanda ya tatu ikiwa na pointi tatu huku Benin ikiburuza mkia kwa pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi nne.

The post Pape Sakho aitwa timu ya Taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/pape-sakho-aitwa-timu-ya-taifa/feed/ 0
Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/#respond Fri, 17 Mar 2023 19:28:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5518 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Msumbiji.Hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuitwa kwenye timu ya taifa tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Teungueth ya […]

The post Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Msumbiji.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuitwa kwenye timu ya taifa tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Teungueth ya nyumbani kwao Senegal.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Senegal, vinaeleza kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Aliou Cisse amemjumuisha Sakho baada ya kuvutiwa na kiwango chake anachokionesha akiwa na Simba kwenye michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Ni mchezaji mwenye kipaji cha juu ukitaka kuthibitisha hilo msimu uliopita aliibuka mshindi wa bao bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, naamini anaweza kutusaidia kufikia malengo yetu dhidi ya Msumbuji,” alisema Cisse.
Katika orodha ya wachezaji 24, Sakho ataungana na baadhi ya nyota wengine wa timu hiyo wakiwemo mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane, Gana Gueye anayekipiga Everton, Bamba Dieng anayecheza Lorient ya Ufaransa, Kalidou Coulibally wa Chelsea.
Sakho anaungana na wachezaji wengine wa Simba Henock Inonga (DR Congo), Clatous Chama (Zambia), Aishi Manula, Mzamiru Yassin, Beno Kakolanya ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za Afcon zinazotarajiwa kufanyika Ivory Coast.

The post Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/sakho-aitwa-timu-ya-taifa-senegal/feed/ 0