Noni Madueke - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 25 Sep 2025 15:10:05 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Noni Madueke - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Madueke nje wiki nane https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/madueke-nje-wiki-nane/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/madueke-nje-wiki-nane/#respond Tue, 23 Sep 2025 19:49:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13945 London, EnglandArsenal huenda ikamkosa mshambuliaji wake, Noni Madueke kwa kipindi cha wiki sita hadi nane kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata katika mechi ya juzi Jumapili dhidi ya Man City iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.Madueke, 23 ambaye amejiunga na Arsenal akitokea Chelsea katika majira ya kiangazi, alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko na amekuwa akifanyiwa […]

The post Madueke nje wiki nane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal huenda ikamkosa mshambuliaji wake, Noni Madueke kwa kipindi cha wiki sita hadi nane kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata katika mechi ya juzi Jumapili dhidi ya Man City iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Madueke, 23 ambaye amejiunga na Arsenal akitokea Chelsea katika majira ya kiangazi, alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko na amekuwa akifanyiwa vipimo kujua ukubwa wa tatizo lililomkuta.
Habari za ndani zinadai kwamba upo uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyo kukosa mechi za Arsenal kwa wiki sita hadi nane ingawa taarifa rasmi bado hazijatolewa.
Habari hizo zinakuwa pigo kubwa kwa kocha wa Arsenal Mikel Arteta na kocha wa England, Thomas Tuchel baada ya mchezaji huyo kuanza vizuri msimu huu na kuibua matumaini makubwa kwa makocha hao.
Ikitokea Madueke kuwa nje kwa kipindi cha wiki nane maana yake ni kwamba atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi Novemba na hivyo kumfanya akose baadhi ya mechi muhimu za Arsenal za Ligi ya Mabingwa Ulaya na zile za Ligi Kuu England.
Kwa upande wa England mshambuliaji huyo huenda akazikosa mechi zijazo dhidi ya Wales na Latvia hapo hapo kukiwa na wasi wasi kama atakuwa tayari kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Albania zitakazochezwa katikati ya mwezi Novemba.
Arsenal itaumana na Sunderland Novemba 8 katika mechi ya Ligi Kuu England na kama ataikosa mechi hiyo basi mashabiki wa timu hiyo wamtarajie mchezaji huyo katika mechi ya London Derby dhidi ya Tottenham ambayo itachezwa Novemba 23.

The post Madueke nje wiki nane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/madueke-nje-wiki-nane/feed/ 0
Arsenal yamsajili Madueke https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/arsenal-yamsajili-madueke/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/arsenal-yamsajili-madueke/#respond Sat, 19 Jul 2025 12:47:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13752 London, EnglandArsenal imekamilisha usajili wa winga, Noni Madueke kutoka klabu ya Chelsea kwa ada ya Pauni 48.5 milioni.Usajili wa Madueke umeonekana kushangaza kwani mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Chelsea waliokuwa na timu hiyo nchini Marekani kwenye fainali za michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia.Madueke, 23, hata hivyo aliondoka kwenye kambi ya Chelsea […]

The post Arsenal yamsajili Madueke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal imekamilisha usajili wa winga, Noni Madueke kutoka klabu ya Chelsea kwa ada ya Pauni 48.5 milioni.
Usajili wa Madueke umeonekana kushangaza kwani mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Chelsea waliokuwa na timu hiyo nchini Marekani kwenye fainali za michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia.
Madueke, 23, hata hivyo aliondoka kwenye kambi ya Chelsea kabla ya timu hiyo kucheza mechi ya fainali dhidi ya PSG iliyopigwa Jumapili na Chelsea kutoka na ushindi wa 3-0 na kubeba taji la michuano hiyo.
Arsenal imempa Madueke mkataba wa miaka mitano ambao ada yake kwa ujumla pamoja na malipo mengine inaweza kufikia Pauni 50 milioni.

“Nimefurahi na najiona mwenye baraka kuwa hapa, ahsanteni kwenu wote mliofanikisha mimi kuwa hapa, nasubiri kwa hamu kuingia uwanjani na kuanza kulipa imani mliyonionesha, litakuwa jambo la kipekee,” alisema Madueke.


Madueke alijiunga na Chelsea Januari 2023 akitokea PSV Eindhoven kwa ada ya Pauni 30 milioni na hadi anaondoka ameichezea timu hiyo maea 92 na kufunga mabao 20.
Kabla ya kujiunga na PSV aliyodumu nayo miaka minne na nusu, Madueke ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Enland, alianza kucheza katika akademi za Crystal Palace na baadaye Tottenham.
Madueke amezoeleka kucheza katika wingi ya kulia ambayo amezoeleka kucheza Bukayo Saka ingawa pia anamudu wingi ya kushoto.

The post Arsenal yamsajili Madueke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/19/arsenal-yamsajili-madueke/feed/ 0
Chelsea yamsajili Madueke https://www.greensports.co.tz/2023/01/21/chelsea-yamsajili-madueke/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/21/chelsea-yamsajili-madueke/#respond Sat, 21 Jan 2023 09:34:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4840 London, EnglandChelsea jana Ijumaa jioni ilikamilisha usajili wa winga, Noni Madueke (pichani juu) kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi ambaye amesaini mkataba wa miaka saba na nusu.Madueke, mwenye miaka 20, usajili wake unatajwa kuigharimu Chelsea Dola 38 milioni ambapo katika mkataba wake kuna kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.Makubaliano baina ya Chelsea na PSV yalifikiwa […]

The post Chelsea yamsajili Madueke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chelsea jana Ijumaa jioni ilikamilisha usajili wa winga, Noni Madueke (pichani juu) kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi ambaye amesaini mkataba wa miaka saba na nusu.
Madueke, mwenye miaka 20, usajili wake unatajwa kuigharimu Chelsea Dola 38 milioni ambapo katika mkataba wake kuna kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.
Makubaliano baina ya Chelsea na PSV yalifikiwa Alhamisi na klabu hiyo kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa England kusafiri hadi London kukamilisha taratibu nyingine za usajili.

“Nina furaha kusaini katika moja ya klabu kubwa duniani, kurudi England na kucheza katika Ligi Kuu England ni ndoto kwangu na familia yangu na sina cha kusubiri kabla ya kuanza kucheza England,” alisema Madueke.

“Navutiwa na mambo yajayo ya klabu hii, dira ya mmiliki kwa mambo yajayo na kuwa katika klabu kama hii na hatimaye kushinda mataji ya kiwango cha juu,” alisema Madueke.
Mmiliki na mwenyekiti wa Chelsea, Todd Boehly na wakurugenzi wa bodi walielezea kufurahishwa na usajili wa Madueke hasa kwa kuwa tayari amethibitisha uwezo wake miaka michache iliyopita akiwa PSV akicheza kwenye ligi ngumu na wana furaha kwa uamuzi wake wa kuichagua Chelsea ikiwa ni hatua nyingine katika maisha yake ya soka.
Madueke alijiunga na timu ya vijana ya PSV mwaka 2018 na kucheza kikosi cha wakubwa cha timu hiyo miaka miwili baadaye na hadi sasa ana rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 20 na kutoa asisti 14 katika mechi 80.
Usajili wa Madueke unakua wa sita kwa Chelsea tangu dirisha dogo lifunguliwe Januari mwaka huu, hivi karibuni klabu hiyo iliwasajili Mykhailo Mudryk kutoka Shakhtar Donetsk na Joao Felix kutoka Atletico Madrid.

The post Chelsea yamsajili Madueke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/21/chelsea-yamsajili-madueke/feed/ 0