Mwamnyeto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 06 May 2024 19:29:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mwamnyeto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mwamnyeto: Mashabiki Yanga wanatupa nguvu https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/mwamnyeto-mashabiki-yanga-wanatupa-nguvu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/mwamnyeto-mashabiki-yanga-wanatupa-nguvu/#respond Mon, 06 May 2024 19:29:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10858 Na mwandishi wetuNahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kwa sasa kikubwa kinachowapa nguvu ya kupambana ni namna mashabiki wao wanavyohitaji ushindi katika kila mchezo na kufanya kila mechi iliyo mbele yao iwe kama fainali.Mwamnyeto amezungumzia hayo baada ya timu hiyo jana Jumapili kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa kwenye mchezo uliopigwa […]

The post Mwamnyeto: Mashabiki Yanga wanatupa nguvu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kwa sasa kikubwa kinachowapa nguvu ya kupambana ni namna mashabiki wao wanavyohitaji ushindi katika kila mchezo na kufanya kila mechi iliyo mbele yao iwe kama fainali.
Mwamnyeto amezungumzia hayo baada ya timu hiyo jana Jumapili kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuendelea kujichimbia kileleni ikifikisha pointi 65 baada ya mechi 25, ikiiacha Azam katika nafasi ya pili kwa pointi 54 ilizovuna katika mechi 24 na Simba iliyopo nafasi ya tatu kwa pointi 50 baada ya mechi zake 23.

“Kikubwa kinachotupa nguvu ni mashabiki wetu, kila mechi wanataka ushindi na mpaka sasa tuko kwenye mwelekeo wa kuchukua ubingwa, kwa hiyo kwetu wachezaji tunafanya kila mchezo kuwa ni fainali, mfano tumekuja Kigoma kucheza na timu ngumu ya Mashujaa, ndio imepanda daraja lakini ina wachezaji wazoefu na wapambanaji lakini mwisho tumefanikiwa kushinda,” alisema Mwamnyeto.


Beki huyo alisema hata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakizungumza kauli moja ya ushindi na pointi tatu na hiyo ndio azma yao kubwa na kisha wataangalia mwisho wa ligi kilichopatikana.
Yanga inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo Jumatatu ikitokea Kigoma ambapo wachezaji watatawanyika nyumbani kwao kisha kesho Jumanne kuanza maandalizi ya mchezo wao wa keshokutwa dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

The post Mwamnyeto: Mashabiki Yanga wanatupa nguvu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/mwamnyeto-mashabiki-yanga-wanatupa-nguvu/feed/ 0
Mwamnyeto ataka rekodi ya mataji https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwamnyeto-ataka-rekodi-ya-mataji/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwamnyeto-ataka-rekodi-ya-mataji/#respond Tue, 13 Feb 2024 06:09:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9703 Na mwandishi wetuNahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema anataka kuweka rekodi kwa kuwa miongoni mwa manahodha wa timu hiyo waliobeba ubingwa mara tatu mfululizo.Akizungumza na GreenSports, nahodha huyo alisema pamoja na kuwa lengo mama la kila mchezaji ni kuipigania timu kufikia malengo iliyopanga mwanzoni mwa msimu lakini akiwa kama nahodha taji la tatu litakuwa na […]

The post Mwamnyeto ataka rekodi ya mataji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema anataka kuweka rekodi kwa kuwa miongoni mwa manahodha wa timu hiyo waliobeba ubingwa mara tatu mfululizo.
Akizungumza na GreenSports, nahodha huyo alisema pamoja na kuwa lengo mama la kila mchezaji ni kuipigania timu kufikia malengo iliyopanga mwanzoni mwa msimu lakini akiwa kama nahodha taji la tatu litakuwa na maana kubwa kwake.

“Nataka kuwemo kwenye rekodi ya kuwa nahodha niliyebeba mataji matatu mfululizo nikiwa na Yanga na hayo ndio malengo ya kila mmoja wetu kuipigania timu kutimiza kile tulichokikusudia ambacho ni kutetea mataji yote,” alisema Mwamnyeto.


Alisema kwa namna walivyojipanga, anaamini hilo litatimia kwani wana kikosi imara chenye wachezaji wenye uchu wa mafanikio.
Mbali na Mwamnyeto, manahodha wengine waliobeba mataji zaidi ya matatu waliopita kwenye kikosi cha Yanga ni Fredy Mbuna aliyebeba mataji 13 kwa vipindi tofauti na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyebeba mataji manne ya ligi lakini kwa misimu tofauti.
Yanga imekamilisha mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa kileleni mwa msimamo wakikusanya pointi 40 katika michezo 15.

The post Mwamnyeto ataka rekodi ya mataji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/mwamnyeto-ataka-rekodi-ya-mataji/feed/ 0
Mwamnyeto ataka Yanga waisahau Simba https://www.greensports.co.tz/2023/04/19/mwamnyeto-ataka-yanga-waisahau-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/19/mwamnyeto-ataka-yanga-waisahau-simba/#respond Wed, 19 Apr 2023 05:25:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5862 Na mwandishi wetuKipigo cha mabao 2-0 ambacho Yanga ilikipata Jumapili iliyopita dhidi ya Simba kimemuibua nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto akiwataka wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kusahau yaliyopita.Mwamnyeto badala yake amewataka wote kuelekeza akili zao kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.Yanga ilipokea kichapo […]

The post Mwamnyeto ataka Yanga waisahau Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipigo cha mabao 2-0 ambacho Yanga ilikipata Jumapili iliyopita dhidi ya Simba kimemuibua nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto akiwataka wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kusahau yaliyopita.
Mwamnyeto badala yake amewataka wote kuelekeza akili zao kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.
Yanga ilipokea kichapo cha mabao 2-0, kutoka kwa watani zao katika mchezo wa Ligi Kuu NBC uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, matokeo ambayo yameonesha kupunguza ari ya baadhi ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.
Mwamnyeto amesema kuwa wanapaswa kusahau yaliyopita na kuweka nguvu kwenye mchezo unaowakabili ili kushinda na kuandika historia kwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

“Kufungwa ni sehemu ya mchezo ingawa kufungwa na mtani inauma lakini tunapaswa kukubaliana na uhalisia, imeshatokea na sasa ni vyema tukahamisha fikra zetu kwenye mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ambao unahitaji utimamu wa akili na mwili,” alisema Mwamnyeto.


Beki huyo alisema kuhusu kipigo cha Simba anamini uwezo wa kulipiza kisasi wanao endapo watakutana nao kwa mara nyingine kwenye mashindano ya Kombe la FA (ASFC) lakini kwa sasa ni vyema wakasahau yaliyopita.
Alisema maumivu ya kufungwa na Simba hayalingani na yale ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali na Rivers United hivyo ni bora wakaweka pembeni matokeo ya mchezo dhidi ya watani zao na kuwawaza zaidi wapinzani wao wa Caf.
Yanga Jumapili ijayo itakuwa ugenini Nigeria ikiumana na Rivers United huo ukiwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Dar es Saalam Aprili 30, mwaka huu.

The post Mwamnyeto ataka Yanga waisahau Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/19/mwamnyeto-ataka-yanga-waisahau-simba/feed/ 0
Mwamnyeto azungumzia vita ya namba Yanga https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/mwamnyeto-azungumzia-vita-ya-namba/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/mwamnyeto-azungumzia-vita-ya-namba/#respond Wed, 03 Aug 2022 12:31:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2112 Na mwandishi wetuWakati Yanga ikiendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya msimu ujao, beki wa kati wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto amekiri ndani ya kikosi hicho kumekuwa na ushindani mkubwa kila nafasi akiamini kocha wa timu hiyo, Nasredine Nabi atakuwa na kazi kubwa.Mwamnyeto amewasili juzi katika kambi ya timu hiyo, Avic Town iliyoko Kigamboni […]

The post Mwamnyeto azungumzia vita ya namba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wakati Yanga ikiendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya msimu ujao, beki wa kati wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto amekiri ndani ya kikosi hicho kumekuwa na ushindani mkubwa kila nafasi akiamini kocha wa timu hiyo, Nasredine Nabi atakuwa na kazi kubwa.
Mwamnyeto amewasili juzi katika kambi ya timu hiyo, Avic Town iliyoko Kigamboni akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa na mechi za kufuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Akifafanua kuhusu hali hiyo, Mwamnyeto alisema kuwa imetokana na kuongezeka wachezaji wale waliokuwepo awali na uwepo wa wachezaji wapya mahiri waliosajiliwa na timu hiyo hivi karibuni.
“Kwa sasa kumekuwa na wakati mgumu kidogo kwa sababu wachezaji wote kwa sasa ni wazuri na kila mchezaji anaonyesha kwamba anataka kucheza kwa hiyo sisi kama wachezaji tunafanya majukumu yetu ya kujiweka vizuri zaidi, kazi kwake mwalimu nani ataanza nani atakaa benchi, si kazi yetu tunamwachia mwalimu,” alisema Mwamnyeto.
Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu NBC Bara na Kombe la FA, ilimaliza ligi bila kupoteza mchezo ikiwa na kikosi imara na sasa imeongeza wachezaji wapya Stephane Aziz Ki, Joyce Lomalisa, Lazarous Kambole, Gael Bigirimana na Bernard Morrison wanaotajwa kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na viwango wanavyoendelea kuonyesha.

The post Mwamnyeto azungumzia vita ya namba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/mwamnyeto-azungumzia-vita-ya-namba/feed/ 0