Michezo ya Olimpiki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 04 Apr 2024 20:39:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Michezo ya Olimpiki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/#respond Thu, 04 Apr 2024 20:39:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10516 Lausanne, UswisiKamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema inahitaji kupata bodi mpya sahihi ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi vinginevyo iufute mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles, Marekani mwaka 2028.IOC ilitangaza kulivua Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (IBA) haki ya kusimamia ngumi katika Michezo ya Olimpili ya Tokyo mwaka 2021 na […]

The post Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lausanne, Uswisi
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesema inahitaji kupata bodi mpya sahihi ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi vinginevyo iufute mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles, Marekani mwaka 2028.
IOC ilitangaza kulivua Shirikisho la Kimataifa la Ngumi (IBA) haki ya kusimamia ngumi katika Michezo ya Olimpili ya Tokyo mwaka 2021 na ile ya Paris ambayo inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Juzi Jumanne Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhisho wa Michezo (CAS) ilitangaza kuunga mkono maamuzi ya IOC ya kutoitambua IBA na hata kuitoa moja kwa moja katika Olimpiki.
Kwa kipindi kirefu IOC imeelezea wasiwasi wake kuhusu uongozi wa IBA na nidhamu ya usimamizi katika mapambano ya ngumi namna mapambano hayo yanavyosimamiwa na majaji wake.
Mwaka jana viongozi wa IOC walimlalamikia Rais wa IBA-Urusi, Umar Kremlev kwa kutumia lugha za shari na vitisho kwa maofisa waandamizi wa IOC.
IOC imewataka viongozi wa mashirikisho ya ngumi kwa kila nchi na kamati za olimpiki kila nchi kusaidia kuundwa bodi mpya ya kimataifa ya kusimamia mchezo wa ngumi kwa lengo la kuupa nafasi mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles.
Katika agizo hilo IOC imetaka kuona inakuwa na mshirika wa ngumi kwenye Olimpiki ambaye ni bodi mpya ya kimataifa ya mchezo huo mapema mwaka 2025 ili kuupa nafasi mchezo huo kwenye Olimpiki.
IOC haijataja jina la bodi mpya lakini inadhaniwa huenda ikawa ni World Boxing, umoja ambao unaundwa na maofisa wa Marekani na Uingereza ambao mwaka jana walijitoa IBA na kumteua, Boris van der Vorst wa Uholanzi kuwa rais wao.

The post Ngumi kufutwa kwenye Olimpiki? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ngumi-kufutwa-kwenye-olimpiki/feed/ 0
Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/#respond Thu, 28 Dec 2023 14:10:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9042 Paris, UfaransaWenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 wameahidi kuifanya michezo hiyo kuwa ya mfano wa kipekee katika kuhakikisha haihusishi uharibifu wa mazingira ikiwamo kupunguza kiwango cha hewa ukaa kwa asilimia 50.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Paris 2024, Tony Estanguet amesema kwamba Michezo ya Olimpiki mwakani itakuwa mfano mpya wa kipekee katika kuandaa michezo ya […]

The post Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 wameahidi kuifanya michezo hiyo kuwa ya mfano wa kipekee katika kuhakikisha haihusishi uharibifu wa mazingira ikiwamo kupunguza kiwango cha hewa ukaa kwa asilimia 50.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Paris 2024, Tony Estanguet amesema kwamba Michezo ya Olimpiki mwakani itakuwa mfano mpya wa kipekee katika kuandaa michezo ya aina hiyo duniani kote.
Estanguet alinukuliwa na BBC akisema kwamba Paris inataka kuwa mfano wa sehemu nyingine duniani katika kuandaa Michezo ya Olimpiki katika namna ambayo mazingira yatalindwa.

“Tunataka kudhihirisha kwamba Paris na Ufaransa wanaweza kuwa wenyeji wa michezo ambayo itakuwa katika namna tofauti na ambavyo imekuwa ikifanyika siku za nyuma” alisema Estanguet katika mazungumzo yake na BBC.


Michezo ya Olimiki itafanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 mwakani katika jiji la Paris na kufuatiwa na Michezo ya Olimpiki Maalum au Paralympics inayohusisha walemavu wa viungo ambayo itafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8.
Moja ya malengo ya waandaji ni kuhakikisha kunakuwa na mpango maalum wenye nia ya kupunguza hewa ukaa kwa asilimia 50 zaidi ya ilivyokuwa katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 na 2016.
Paris hata hivyo wana kazi kubwa ya kufikia malengo hayo hasa baada ya Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 ambayo ilifanyika mwaka 2021 ambayo iliweka rekodi kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha hewa ukaa.
Tafiti hata hivyo zilionesha kwamba Tokyo walifanikiwa kwa sababu ya ugonjwa wa korona ambao kwanza ulisababisha michezo hiyo kufanyika mwaka 2021 badala ya 2022 lakini pia ugonjwa huo ulisababisha mashabiki na hata washiriki kuwa wachache kutokana na zuio la kusafiri.
Michezo ya Olimpiki ni aina ya tamasha kubwa la michezo duniani linaloongoza duniani kwa kushirikisha michezo na wanamichezo wengi kutoka mataifa karibu yote duniani.

The post Olimpiki Paris wapania kupunguza hewa ukaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/olimpiki-paris-wapania-kupunguza-hewa-ukaa/feed/ 0