Mendy - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 20 Jul 2023 11:41:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mendy - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Benjamin Mendy asajiliwa Lorient https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/benjamin-mendy-asajiliwa-lorient/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/benjamin-mendy-asajiliwa-lorient/#respond Thu, 20 Jul 2023 11:41:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7029 Lorient, UfaransaBeki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Lorient ya Ufaransa ikiwa ni siku tano tangu afutiwe mashtaka ya kubaka na udhalilishaji wa kijinsia.Mendy ambaye ni beki wa kushoto mkataba wake na Man City ulifikia ukomo hivi karibuni ingawa klabu hiyo ilimsimamisha tangu ahusishwe na tuhuma […]

The post Benjamin Mendy asajiliwa Lorient first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lorient, Ufaransa
Beki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Lorient ya Ufaransa ikiwa ni siku tano tangu afutiwe mashtaka ya kubaka na udhalilishaji wa kijinsia.
Mendy ambaye ni beki wa kushoto mkataba wake na Man City ulifikia ukomo hivi karibuni ingawa klabu hiyo ilimsimamisha tangu ahusishwe na tuhuma za kubaka na kudhalilisha wasichana.
Baada ya kuandamwa na kashfa hiyo akituhumiwa kwa makosa tofauti ya kubaka na kudhalilisha, Januari mwaka huu Mendy alifutiwa mashitaka sita yote yakiwa ni ya udhalilishaji kijinsia, kabla ya Ijumaa iliyopita kufutiwa mashtaka mawili ya kubaka msichana na kutaka kukaba msichana mwingine.
Mwaka 2017, Mendy alikuwa gumzo kila kona akiwa beki wa bei mbaya zaidi duniani baada ya Man City kumnunua kwa Pauni 52 milioni kutoka klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Katika msimu wake wa kwanza aliiwezesha Man City kubeba taji la Ligi Kuu England lakini pia alikuwamo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichobeba taji la dunia mwaka 2018 nchini Russia.
Mara ya mwisho kucheza mechi ya ushindani ilikuwa Agosti 2021 alipoiwakilisha Man City dhidi ya Tottenham lakini alikamatwa baadaye mwezi huo na kuwekwa ndani kwa miezi mitano kabla ya shauri lake kuanza kusikilizwa Agosti mwaka jana.
Mendy aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi ambapo baada ya uamuzi huo mshambuliaji wa Uholanzi, Memphis Depay na Vinicius Jr wa Real Madrid walitumia mitandao ya kijamii kutoa kauli za kumtia moyo.

The post Benjamin Mendy asajiliwa Lorient first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/benjamin-mendy-asajiliwa-lorient/feed/ 0
Mendy afutiwa kesi ya ubakaji https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/mendy-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/mendy-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/#respond Sat, 15 Jul 2023 08:42:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6976 Manchester, EnglandBeki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy (pichani) amefutiwa tena tuhuma nyingine za kumbaka msichana wa miaka 24 na kutaka kumbaka msichana mwingine wa miaka 29.Mendy mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa timu ya Taifa ya Ufaransa alidaiwa kufanya makosa hayo Oktoba 2020 katika mjengo wake wa kifahari na […]

The post Mendy afutiwa kesi ya ubakaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy (pichani) amefutiwa tena tuhuma nyingine za kumbaka msichana wa miaka 24 na kutaka kumbaka msichana mwingine wa miaka 29.
Mendy mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa timu ya Taifa ya Ufaransa alidaiwa kufanya makosa hayo Oktoba 2020 katika mjengo wake wa kifahari na kujikuta akiondolewa katika kikosi cha Man City.
Uamuzi huo wa mahakama ya Chester Crown uliofikiwa jana Ijumaa ni nyingine kubwa kwa mchezaji huyo ambaye Januari mwaka huu alifutiwa makosa mengine sita ya tuhuma za kubaka na udhalilishaji kijinsia.
Baada ya mahakama kumfutia makosa hayo katika shauri lililoendeshwa kwa kipindi cha wiki tatu, Mendy alijikuta akimwaga chozi.
Majaji sita wanaume na sita wanawake walifikia uamuzi huo baada ya mashauriano ya takriban saa tatu kabla ya kutangaza kumfutia mchezaji huyo tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Mendy ambaye amekuwa akiandamwa na tuhuma hizo kwa takriban miaka miwili sasa, mkataba wake na Man City ulifikia ukomo mapema mwezi huu.
Katika mshtaka ya awali Mendy alikuwa na tuhuma za makosa sita ya kubaka na moja la udhalilishaji kijinsia ambayo alidaiwa kuwafanyia wasichana wanne.
Wakati kesi hiyo ikiendelea muendesha mashtaka mmoja aliiambia mahakama kwamba Mendy alikuwa na tabia ya kufanya sherehe za kifahari nyumbani kwake na kutumia nafasi hiyo kuwanasa wageni wasichana akitumia utajiri na umaarufu wake uliomfanya awe mtu asiyekubali kuambiwa hapana.

The post Mendy afutiwa kesi ya ubakaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/15/mendy-afutiwa-kesi-ya-ubakaji/feed/ 0
Mendy akana tena kubaka https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/mendy-akana-tena-kubaka/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/mendy-akana-tena-kubaka/#respond Wed, 10 Aug 2022 20:04:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2319 Manchester, EnglandBeki wa klabu ya Manchester City aliyesimamishwa, Benjamin Mendy amekana tuhuma nyingine za ubakaji zinazomkabili katika mahakama ya Chester Crown.Mendy mwenye umri wa miaka 28 sasa anakuwa amekana kuhusika katika makosa manane ya ubakaji, moja la udhalilishaji kijinsia na moja la kuwa na dhamira ya kubaka, matukio anayodaiwa kuwafanyia wanawake saba nyumbani kwake kati […]

The post Mendy akana tena kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Beki wa klabu ya Manchester City aliyesimamishwa, Benjamin Mendy amekana tuhuma nyingine za ubakaji zinazomkabili katika mahakama ya Chester Crown.
Mendy mwenye umri wa miaka 28 sasa anakuwa amekana kuhusika katika makosa manane ya ubakaji, moja la udhalilishaji kijinsia na moja la kuwa na dhamira ya kubaka, matukio anayodaiwa kuwafanyia wanawake saba nyumbani kwake kati ya Oktoba 2018 na Agosti 2021.
Mtu mwingine anayehusika katika kesi hiyo ni Louis Saha Matturie mwenye umri wa miaka 40 ambaye naye kama Mendy amekana kuhusika katika mashitaka hayo wakati kesi yao ikitarajiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu.
Mendy aliyejiunga na Man City mwaka 2017 akitokea Monaco na kuichezea timu hiyo mechi 50 za Ligi Kuu England, mara tu baada ya kuhusishwa na tuhuma hizo alijikuta akisimamishwa na timu yake ingawa kwa sasa yeye na mwenzake wapo nje kwa dhamana.

The post Mendy akana tena kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/10/mendy-akana-tena-kubaka/feed/ 0