Mashabiki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 21 May 2023 18:01:49 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mashabiki - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mashabiki 12 wafariki uwanjani El Salvador https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mashabiki-12-wafariki-uwanjani-el-salvador/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mashabiki-12-wafariki-uwanjani-el-salvador/#respond Sun, 21 May 2023 18:01:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6249 San Salvador, El SalvadorMashabiki 12 wa soka wamefariki dunia nchini El Salvador na wengine 90 kujeruhiwa baada ya kutokea msongamano wakati wa kuingia kwenye Uwanja wa Cuscatlan mjini San Salvador.Tukio hilo limetoka jana Jumamosi wakati wa mechi baina ya timu za Alianza na FAS chanzo kikidaiwa kuwa ni baadhi ya mageti ya uwanja huo kufungwa […]

The post Mashabiki 12 wafariki uwanjani El Salvador first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

San Salvador, El Salvador
Mashabiki 12 wa soka wamefariki dunia nchini El Salvador na wengine 90 kujeruhiwa baada ya kutokea msongamano wakati wa kuingia kwenye Uwanja wa Cuscatlan mjini San Salvador.
Tukio hilo limetoka jana Jumamosi wakati wa mechi baina ya timu za Alianza na FAS chanzo kikidaiwa kuwa ni baadhi ya mageti ya uwanja huo kufungwa na kubaki machache.
Katika kinachoaminika kuwa ni jitihada za kuingia uwanjani baadhi ya mashabiki walikosa hewa, baadhi yao wakianguka na kuzimia na wengine kufariki.
Baada ya tukio hilo, Rais Nayib Bukele alisema utaanzishwa uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ambalo awali taarifa ya polisi ilidai kwamba watu waliofariki wanaume walikuwa saba na wanawake wawili wa umri uliozidi miaka 18 lakini taarifa ya baadaye ilitaja idadi ya waliofariki kufikia 12.
Inadaiwa kwamba baadhi ya mashabiki walikuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani huku pia zikiwapo taarifa kwamba wapo mashabiki waliouziwa tiketi feki za mechi hiyo.
Watu wa huduma ya kwanza walionekana wakiwasaidia waliozidiwa huku baadhi ya mashabiki wakiwa vifua wazi na kuwapepea baadhi ya majeruhi kwa kutumia mashati yao.
Na ingawa watu 90 wanadaiwa kuwa majeruhi lakini Waziri wa Afya wa El Salvador, Francisco Alabi alisema kwamba sehemu kubwa ya majeruhi waliofikishwa hospitali wako vizuri na hakuna taarifa yoyote ya kifo iliyoripotiwa hospitali.
Taarifa ya Shirikisho la Soka la El Salvador ilitangaza kuahirishwa kwa mechi zote za soka za wikiendi na kusikitishwa na kilichotokea kwenye mechi hiyo.

The post Mashabiki 12 wafariki uwanjani El Salvador first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mashabiki-12-wafariki-uwanjani-el-salvador/feed/ 0
Yanga yawaita mashabiki Kwa Mkapa https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/yanga-yawaita-mashabiki-kwa-mkapa/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/yanga-yawaita-mashabiki-kwa-mkapa/#respond Wed, 26 Apr 2023 19:43:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5949 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga imewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Rivers United ya Nigeria ili kuwemo katika rekodi ya walioshuhudia timu hiyo ikipenya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema leo Jumatano kuwa kuna uwezekano mkubwa msimu huu wakapata […]

The post Yanga yawaita mashabiki Kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Rivers United ya Nigeria ili kuwemo katika rekodi ya walioshuhudia timu hiyo ikipenya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema leo Jumatano kuwa kuna uwezekano mkubwa msimu huu wakapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye nusu fainali hiyo hivyo licha ya mashabiki kujitokeza kuiunga mkono timu lakini pia kuwemo kwenye historia hiyo.
Yanga itaumana na Rivers Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ikiwa tayari na faida ya ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Uyo, Nigeria wikiendi iliyopita.
Na kwenye mechi hiyo ya marejeano, Rivers inahitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kusonga mbele wakati Yanga ikihitaji sare pekee kutinga nusu fainali.
“Kuna uwezekano mkubwa sana nchi ikapata mwakilishi wa nusu fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho, ni jambo kubwa kwa nchi, basi Wananchi nao wajitokeze kwa wingi kuhakikisha wanakuwa sehemu ya historia ya siku ya tarehe 30.

“Miaka kadhaa mbele mtu aweze kusema kwamba siku timu imekwenda hatua ya nusu fainali na mimi nilikuwepo kuishangilia lakini pia wajitokeze kuendelea kuwapa hamasa wachezaji wetu kuonesha kwamba tuko pamoja nao katika kuipambania timu,” alisema Haji.


Pamoja na hayo, Haji alisisitiza kuelekea mechi hiyo uongozi mzima pamoja na benchi la ufundi wamekubaliana kwamba bado hawajamaliza mechi ya robo fainali kwani wanazitegemea dakika 90 nyingine za mechi ya Jumapili hii kujihakikishia hilo, hivyo hawatabweteka.
“Unajua mechi hizi ni dakika 180, tushamaliza 90 za kwanza na sasa tunahitaji subira na kujipanga upya tena kwa 90 nyingine za pili ambazo ndiyo zitatoa jibu kwa hiyo uongozi, benchi la ufundi tumekubaliana bado hatujapita, tusibweteke na maandalizi yaendelee kama vile huu ndiyo mchezo wa kwanza wa robo,” alisema Haji.
Kuonesha Yanga inaihitaji kucheza hatua hiyo, baada ya juzi kurejea nchini, hawakupumzika ambapo kikosi kimeendelea na kambi ya maandalizi ya mchezo wao huo.

The post Yanga yawaita mashabiki Kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/yanga-yawaita-mashabiki-kwa-mkapa/feed/ 0