Mangungu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 09 Feb 2026 19:33:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mangungu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba: Waliomfanyia fujo Mangungu waadhibiwe https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/simba-waliomfanyia-fujo-mangungu-waadhibiwe/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/simba-waliomfanyia-fujo-mangungu-waadhibiwe/#respond Mon, 02 Feb 2026 18:31:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14316 Na mwandishi wetuUongozi wa klabu ya Simba umelitaka jeshi la polisi nchini kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kumfanyia fujo mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu.Mangungu alijikuta katika kadhia hiyo kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa soka ambao walimbughudhi na kumtolea lugha chafu baada ya mechi yao na Esperance ya Tunisia iliyoisha kwa sare ya […]

The post Simba: Waliomfanyia fujo Mangungu waadhibiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa klabu ya Simba umelitaka jeshi la polisi nchini kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kumfanyia fujo mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu.
Mangungu alijikuta katika kadhia hiyo kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa soka ambao walimbughudhi na kumtolea lugha chafu baada ya mechi yao na Esperance ya Tunisia iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Matokeo ya mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumapili Januari Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam yamewakera baadhi ya mashabiki ambao inaaminika waliamua kumalizia hasira zao kwa Mangungu.
Katika tukio hilo, Mangungu alijikuta akizongwa na kama si juhudi za maofisa usalama wa uwanjani hapo huenda hali ingeweza kuwa mbaya kwa kiongozi huyo kwa namna ambavyo idadi ya mashabiki ilikuwa kubwa.
Taarifa ya klabu ya Simba iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo, Crecentius Magori muda mfupi baada ya mechi hiyo, ilieleza kusikitishwa na tukio hilo na kulitaja kuwa si la kiungwana na halikubaliki.
Magori katika taarifa hiyo alisema kuwa sambamba na kutoa pole kwa Mangungu lakini pia alifafanua kuwa tukio hilo halitafumbiwa macho.
Alilitaka jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika au kula njama katika tukio hilo dhidi ya Mangungu na bodi ya klabu hiyo haitavumilia wala kubariki mtu yeyote atakayeharibu taswira ya klabu kwa namna yoyote.
Mashabiki wengi wanaoaminika kuwa wa Simba walikerwa na matokeo ya sare ya 2-2 ambayo yamezidi kufifisha kama si kufuta matumaini ya timu hiyo kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post Simba: Waliomfanyia fujo Mangungu waadhibiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/simba-waliomfanyia-fujo-mangungu-waadhibiwe/feed/ 0
Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/#respond Sun, 14 Dec 2025 18:06:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14171 Hassan KinguSimba haipo vizuri, mwenendo wa timu kiujumla hauridhishi, utata ulianza kuonekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya timu hiyo kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.Kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, tena mabao ya jioni ni jambo jingine lililoongeza machungu na hasira za mashabiki ambao msimu uliopita waliishuhudia timu yao ikifikia […]

The post Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Hassan Kingu
Simba haipo vizuri, mwenendo wa timu kiujumla hauridhishi, utata ulianza kuonekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya timu hiyo kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.
Kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, tena mabao ya jioni ni jambo jingine lililoongeza machungu na hasira za mashabiki ambao msimu uliopita waliishuhudia timu yao ikifikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Matarajio ya msimu huu yalikuwa juu, yalianza kuzungumzwa wakati wa usajili, imani ikajengeka timu itafanya vizuri kwenye Ligi Kuu NBC na Ligi ya Mabingwa lakini matumaini yanafifia siku hadi siku.
Katika kupambana kuweka mambo sawa, Simba imeanza au inaendelea kumsaka mchawi wake, mchawi wa siku zote alikuwa Murtaza Mangungu, mwenyekiti wa klabu hiyo, na sasa mchawi mwingine ni kocha Suleiman Matola.
Ingekuwa miaka ya nyuma Mangungu angekuwa tayari ameondolewa kupitia mkutano mkuu lakini zama hizi jambo hilo ni ngumu na huenda lisipate baraka za mamlaka.
Kwa hiyo Mangungu amepenya kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni, licha ya kusakamwa na kuwekwa katika hali tete lakini alikuwa makini dhidi ya jaribio lolote la kumuondoa na mwisho wa siku akamaliza mkutano kimtindo.
Kuhusu suala la Mangungu kilichobaki sasa ni mkutano wa uchaguzi, hapo ndipo atakapoondolewa kupitia kura za wanachama, tofauti na hivyo kuondoka kwake kunabaki kuwa jambo gumu.
Walioamini mkutano ungemng’oa Mangungu wamefeli wasubiri kura na kwenye kura ni kama ataamua kukaa kando vinginevyo ni vigumu kutabiri kama atashinda au atashindwa, hilo litategemea mengi ikiwamo aina ya wapinzani atakaokutana nao au mwenyewe kujiweka kando au kuwekwa kando na katiba.
Kuhusu Matola ambaye naye anatajwa na kuhusishwa na mwenendo mbaya wa Simba hasa baada ya timu hiyo kufungwa na Azam yeye ni tofauti na Mangungu, Matola anaweza kuondoka au kuondolewa wakati wowote.


Uamuzi dhidi ya Matola unahusisha watu wachache na ndio maana imekuwa rahisi kusikia watu kwenye mitandao wakimjadili katika namna mbaya na wengine kudiriki kusema kwamba siku zake ndani ya Simba zinahesabika.
Majina haya mawili kwa siku za karibuni yamekuwa yakitajwa sana hasa mitandaoni wakinangwa na kuonekana ndio msingi wa tatizo ndani ya Simba.
Kwa hali ilivyo mitandaoni kama kuna mtu labda ni mgeni na mambo ya soka la Tanzania na hajui kinachoendelea anaweza kujiambia kwamba ni kwa nini watu hao wawili hawaondoki ili Simba iwe bora.
Kwa upande mwingine napata tabu kuamini kuwa Matola na Mangungu pekee ndio tatizo la Simba badala yake naona kuna mambo muhimu kuyafanyia tafakuri na kuyapatia majibu badala ya kuwajadili na kuwasakama watu hao wawili.
Hao watu wawili wanaotajwa msimu uliopita walikuwa Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika huku matumaini yakiwa juu kwamba timu hiyo ilikuwa na uwezo wa kuweka historia kwa kubeba taji hilo.
Kilichotarajiwa ni kwamba Simba iliyofikia fainali Shirikisho Afrika msimu uliopita ingeendeleza mafanikio msimu huu lakini dalili za jambo hilo hazionekani.
Nionavyo kabla ya kuanza na Mangungu au Matola ambao walikuwa na timu hiyo msimu uliopita ni vyema kujiuliza kuhusu usajili, je timu ya msimu uliopita na hii ya sasa ipi bora?
Hili ni swali au hoja ngumu na ya kiufundi ambayo inahitaji tafakuri kabla ya kuijibu na ndio maana wengi hatuitaki badala yake yanatafutwa maswali au hoja rahisi yenye majibu rahisi kama vile Mangungu tatizo na sasa Matola tatizo.
Baada ya kikosi hoja au swali la pili kwangu ni kuhusu kocha, je Simba wana mpango gani katika kupata kocha mwenye hadhi au uwezo unaolingana na ule wa Fadlu Davids ambaye aliifikisha timu hiyo fainali ya Shirikisho Afrika?.
Fadlu si tu aliifikisha timu fainali bali hata aina ya soka lake ilivutia na ni sababu kubwa ya kuwapo matumaini kwamba Simba ya msimu huu ingekuwa moto chini ya kocha huyo lakini hali imekuwa tofauti, Fadlu ameondoka wakati anahitajika.
Kwa mantiki hiyo badala ya Mangungu na Matola, tafakuri au swali ambalo wana Simba wanapaswa kujiuliza na kutafuta majibu iwe katika hayo mambo mawili, kwanza kikosi na pili kuhusu kocha wa hadhi ya Fadlu.
Kinyume na hapo kwangu naona ni sawa na kujiuliza swali rahisi na kujipa jibu rahisi ambalo katu haliwezi kuisaidia timu.

The post Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/feed/ 0
Eti tatizo Simba ni Mangungu https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/#respond Sun, 13 Jul 2025 20:56:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13724 Na Hassan KinguMsimu wa 2024-25 umeisha, naiangalia Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika, ikafungwa na RS Berkane mabao 2-0 na kushindwa kubeba taji la michuano hiyo.Simba hiyo hiyo, iliyoishia nafasi ya pili Ligi Kuu NBC na kufungwa mabao 2-0 na Yanga, mashabiki wanaamini timu yao imefeli na tatizo ni mwenyekiti wao, Murtaza Mangungu.Ndoto na […]

The post Eti tatizo Simba ni Mangungu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Msimu wa 2024-25 umeisha, naiangalia Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika, ikafungwa na RS Berkane mabao 2-0 na kushindwa kubeba taji la michuano hiyo.
Simba hiyo hiyo, iliyoishia nafasi ya pili Ligi Kuu NBC na kufungwa mabao 2-0 na Yanga, mashabiki wanaamini timu yao imefeli na tatizo ni mwenyekiti wao, Murtaza Mangungu.
Ndoto na matumaini ya Simba kubeba taji hilo ziliyeyuka kama ambavyo ziliyeyuka ndoto za kubeba taji la Ligi Kuu NBC ambalo liliishia mikononi mwa mahasimu wao Yanga.
Kama hiyo haitoshi, mahasimu wao Yanga wakaendelea kuwapa vipigo kwa mara ya tano mfululizo huku wakilibeba taji la ligi hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Simba ambayo imefikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika haikuambulia hata taji moja katika msimu wa 2024-25 huku ni kufeli na wenyewe wanaaminishana kwamba aliyewafelisha ni Mangungu.
Nyimbo za hatumtaki Mangungu zimesikika kwenye mitandao ya kijamii na ukizisikiliza nyimbo hizo unaweza kujiaminisha moja kwa moja kuwa Simba haina tatizo jingine isipokuwa Mangungu. Huu ni uwongo wa wazi.
Kwa mtu asiyefahamu kuhusu Mangungu pia anaweza kudhani kwamba Mangungu ndiye kocha wa timu au ndiye ofisa mtendaji mkuu yaani CEO, kumbe sivyo Mangungu ni mwenyekiti wa klabu.
Mara ya mwisho Simba kufikia hatua ya fainali kwenye michuano ya klabu barani Afrika inayoandaliwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ilikuwa mwaka 1993, miaka takriban 31 iliyopita, tulidhani kwamba kufikia hatua hiyo msimu huu ni mafanikio, hapana ni kufeli na sababu ni Mangungu.
Kwa kilichotokea katika Simba msimu huu baadhi yetu tunaamini tatizo si Mangungu bali tatizo ni lile lile, mafanikio ya Yanga na vipigo mara nne mfululizo.
Klabu hizi mbili zina tabia ya kuteswa na mafanikio ya mmoja wao kiasi cha kujinyima hata kufurahia mafanikio mengine ya kihistoria waliyofikia.


Kuhusu Mangungu ni ama wanachama wamejazwa na maadui zake mitazamo ya kuamini kuwa yeye ndiye tatizo, iwe ni kwa kulipwa au kutolipwa au hawajatafakari kwa kina wanachokizungumza kuhusu kiongozi huyo.
Inawezekana kuna watu wenye nguvu ndani ya Simba ambao hawamtaki Mangungu kwa hiyo hatua iliyofikia Simba katika msimu wa 2024-25 inageuzwa kuwa ni kufeli, tena kufeli kubaya na eneo sahihi la kumshughulikia Mangungu ni hilo.
Si vibaya kusema kwamba Simba imefeli hasa kwa kuwa haijapata taji lakini si sahihi kugeuza nongwa kufeli kwa aina ya msimu huu na kuuaminisha umma uamini kwamba tatizo alikuwa ni Mangungu.
Mtazamo wa Simba kufeli unaweza kuzungumziwa katika kukosa mataji, kufungwa na Yanga lakini huu hauwezi kuwa msimu wa hovyo kwa Simba badala yake unaweza kutajwa kuwa ni msimu ambao Simba imeteleza.
Katika kuteleza huko ni vyema kuangalia matatizo kwa mapana yake badala ya kumuangalia Mangungu na kujiaminisha kwamba ndiye tatizo na labda akiondoka mambo yatakuwa salama, huku ni kumpa Mangungu sifa ambazo hana.
Klabu yenye kocha, CEO, bodi na viongozi wengine lukuki wanaohusika moja kwa moja na maendeleo ya timu, hao wote hawana tatizo isipokuwa mwenye tatizo ni Mangungu pekee, bila shaka atakuwa na nguvu ya kipekee na anaogopwa.
Wakati Simba inasonga mbele hatua moja hadi nyingine kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki walikuwa wakijivunia na hakuna aliyewahi kusema kwamba Mangungu ana msaada au amechangia kufikisha Simba ilipofikia.
Ni kama vile Mangungu alikuwa anasubiriwa Simba ishindwe, tena bila kujali imeshindwaje na katika hatua ipi ndipo waanze kumshutumu kwamba hatakiwi na ndiye tatizo.
Badala ya kuhangaika na Mangungu pekee, Simba waanze mipango ya kuboresha kikosi, warekebishe mapungufu yaliyowafanya wafike fainali na wasichukue taji la Shirikisho Afrika, wahakikishe wanakuwa na kikosi kipana kama cha Yanga.
Kama kuna kitu Simba wanatakiwa kujifunza kwa Yanga basi ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi kipana na cha ushindani.
Baada ya hapo wasichoke, waendelee kujiuliza, baada ya kushika nafasi ya pili kwenye ligi, msimu ujao watawezaje kubeba taji na kama kuifunga Yanga kwao ndio kila kitu pia waweke mkakati huo.
Huyu Mangungu kama kweli wamemchoka na ndiye tatizo basi wasubiri kumtoa kwenye uchaguzi, mambo ya kupinduana kwa sasa hayana nafasi au yamepitwa na wakati.

The post Eti tatizo Simba ni Mangungu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/feed/ 0
Mangungu akana Mo kuinunua Simba https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/#respond Thu, 07 Mar 2024 18:37:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10070 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema si kweli kuwa mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliinunua klabu hiyo miaka mitano iliyopita kama ilivyoelezwa hivi karibuni.Mangungu alipokuwa akizungumza na kituo cha redio cha EFM Jumatano hii, alisema: “Simba SC ipo, kitu ambacho kimejitokeza ni kwamba nadhani ni uelewa wa watu wengi hata Wanasimba […]

The post Mangungu akana Mo kuinunua Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema si kweli kuwa mwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliinunua klabu hiyo miaka mitano iliyopita kama ilivyoelezwa hivi karibuni.
Mangungu alipokuwa akizungumza na kituo cha redio cha EFM Jumatano hii, alisema: “Simba SC ipo, kitu ambacho kimejitokeza ni kwamba nadhani ni uelewa wa watu wengi hata Wanasimba wenyewe kuhusu mabadiliko yaliyofanyika ndani.
“Simba SC kama ilivyo kwa timu nyingine ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo wa ridhaa baada ya mabadiliko ya maendeleo na changamoto nyingi za kiuendeshaji, Mohammed Dewji ni mmoja wa waliojitolea sana kuisaidia klabu,” alisema Mangungu.
Alieleza kuwa Dewji kipindi ambacho hakuwa sehemu ya Simba alikuwa anatoa michango yake kama watu wengine wanaochangia lakini baadaye akatoa wazo la kutengeneza mfumo ambao watawekeza ili klabu iwe ya kiushindani zaidi
“Hivyo kwa makubaliano ya awali tuliunda chombo ambacho kiliitwa Simba SC Company Limited, ambayo ndio ambayo imegawanya muundo wa shea wa asilimia 51/49 ambapo mwanzoni ilikuwa 50/50.
“Lakini masharti yaliyowekwa na serikali yalilazimisha kuwa lazima upande wa wanachama uwe wenye hisa nyingi chombo hicho kipo na kwa uelewa wangu na ndivyo ukweli ulivyo,” alisisitiza Mangungu.
Aliongeza kuwa kuna makubaliano ya uendeshaji na Simba SC imetoa mali zake na nguvu zake kuwekeza na mwekezaji amewekeza fedha ambazo zitakuwa mtaji unaounganishwa kwa pamoja kwa ajili ya kuendesha klabu na mambo mengine.
“Mchakato huo umeanza na umefikia hatua za mwisho kwa maana kwamba kwa kuwa klabu yetu ilikuwa inaendeshwa kwa ridhaa kuna taratibu zilikuwa zinapaswa kufikiwa kwa mujibu wa taratibu za kiserikali kwa upande wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambayo ni Wizara pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na upande wa FCC (Tume ya Ushindani).
“Maana mtaji ukizidi Shilingi bilioni tano lazima FCC wasimamie huo mchakato, hivi sasa tuko hatua ya mwisho ya kuingiza mali zetu, Simba ina bodi ya udhamini ambao ndio walioingia mkataba na mwekezaji mwenza ambaye ni Dewji,” alisema Mangungu.
Alisema baada ya kukamilisha hayo ndio wanaenda FCC kuangalia kama kila kitu ambacho kilichotakiwa kimekamilika ndipo mchakato ukamilike.

The post Mangungu akana Mo kuinunua Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/07/mangungu-akana-mo-kuinunua-simba/feed/ 0
Mangungu awapotezea wanaomkosoa https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mangungu-awapotezea-wanaomkosoa/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mangungu-awapotezea-wanaomkosoa/#respond Mon, 11 Dec 2023 18:34:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8823 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ameeleza kuwa hana la kufanya kwa wanaomkosoa na kumpigia kelele katika uongozi wake kwani anaendelea na ujenzi wa timu hiyo kufanya vizuri.Mangungu ameeleza hayo baada ya kuibuka hoja kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wakimtaka ajiuzulu kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo […]

The post Mangungu awapotezea wanaomkosoa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ameeleza kuwa hana la kufanya kwa wanaomkosoa na kumpigia kelele katika uongozi wake kwani anaendelea na ujenzi wa timu hiyo kufanya vizuri.
Mangungu ameeleza hayo baada ya kuibuka hoja kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wakimtaka ajiuzulu kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo hasa baada ya kufungwa mabao 5-1 na Yanga Novemba 5, mwaka huu.
Kiongozi huyo alisema kwake anaona ni kawaida kukosolewa kibinadamu kwani haiwezekani akakubalika na watu wote na zaidi wanaofanya hivyo wanatumia haki yao ya msingi hivyo ni suala ambalo linaeleweka kibinadamu na lipo siku zote.
“Ni kawaida kwa maisha ya biandamu, huwezi ukakubalika, ukapokelewa na watu wote na huwezi ukakataliwa au ukakosolewa na watu wote.

“Wanaokosoa wanatumia haki yao, mara nyingine mtu akikosoa anapata furaha, basi kama ni jambo linalompa furaha aendelee kukosoa lakini kimsingi tunaendelea kuhakikisha tunajenga mazingira mazuri ya timu yetu kufanya vizuri,” alisema Mangungu.


Kuhusu mwenendo wa Simba kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na mechi dhidi ya Wydad AC, Mangungu alisema hana wasiwasi na timu hiyo kwani ina uzoefu wa kutosha na magumu ya michuano hiyo, hivyo anaamini itakaa sawa na watapata mafanikio muda si mrefu.
Katika hatua ya makundi msimu huu, Simba imetoa sare mechi mbili na kufungwa moja na hivyo kuburuza mkia kwenye Kundi B ikiwa na pointi mbili. ASEC Mimosas inaongoza kwa pointi saba, ikifuatiwa na Jwaneng Galaxy yenye nne na Wydad AC yenye pointi tatu.

The post Mangungu awapotezea wanaomkosoa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mangungu-awapotezea-wanaomkosoa/feed/ 0
Mangungu amjibu Okwa https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/mangungu-amjibu-okwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/mangungu-amjibu-okwa/#respond Tue, 27 Jun 2023 20:16:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6738 Na mwandishi wetuSiku chache baada ya Nelson Okwa kuachwa Simba na kuwashutumu viongozi kwa kuwapangia makocha wachezaji katika mechi, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amewaomba mashabiki kutowasikiliza wachezaji wanaoachwa.Mangungu (pichani) badala yake amewaomba mashabiki hao kubariki maamuzi ya viongozi wao ambao wana lengo la kuwajengea timu ya ushindi.Juzi, mmoja wa wachezaji aliyeachwa kwenye kikosi chao, […]

The post Mangungu amjibu Okwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku chache baada ya Nelson Okwa kuachwa Simba na kuwashutumu viongozi kwa kuwapangia makocha wachezaji katika mechi, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amewaomba mashabiki kutowasikiliza wachezaji wanaoachwa.
Mangungu (pichani) badala yake amewaomba mashabiki hao kubariki maamuzi ya viongozi wao ambao wana lengo la kuwajengea timu ya ushindi.
Juzi, mmoja wa wachezaji aliyeachwa kwenye kikosi chao, Okwa raia wa Nigeria aliwashutumu viongozi wa Simba akidai wamekuwa wakiwapangia makocha wachezaji katika mechi.
Mangungu alieleza kusikitishwa na kauli za Okwa lakini akawataka mashabiki pia kumpuuza sababu mchezaji huyo ni kati ya wachezaji waliopewa nafasi kubwa lakini hakuonesha kile walichokitarajia.
“Hatukatai kukoselewa sababu ndio maana nzuri ya kutambua madhaifu yetu lakini wanachama na mashabiki wetu hawapaswi kuzipa nafasi hizo kelele badala yake watuache viongozi wao tupambane kwa ajili ya kuwajengea kikosi bora kitakachowapa mafanikio msimu ujao,” alisema Mangungu.
Kiongozi huyo alisema tangu kuanza kwa mchakato wa mabadiliko, Simba ndio timu ambayo inaendeshwa kwa uwazi mkubwa nchini ndio maana anapingana na tuhuma za mchezaji huyo sababu aliyeondolewa kwenye timu hayuko peke yake.
Alisema malengo ya Simba ni makubwa na yanahitaji mchezaji ambaye yupo tayari kupigania na kuvuja jasho kwa ajili ya walichokikusudia.

“Sasa ikitokea mtu anapewa nafasi na anashindwa kuonesha msaada wake lazima tutamuondoa ili kuleta mtu sahihi,” alisema Mangungu.


Katika hatua nyingine Mangungu pia amewaomba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuongeza mshikamano ili kujenga umoja utakaowawezesha kutimiza malengo yao msimu ujao.

The post Mangungu amjibu Okwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/mangungu-amjibu-okwa/feed/ 0
Mangungu atangaza kuisuka upya Simba https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/mangungu-atangaza-kuisuka-upya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/mangungu-atangaza-kuisuka-upya-simba/#respond Tue, 16 May 2023 18:38:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6185 Na mwandishi wetuMwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema tayari wameanza mchakato wa kukisuka upya kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri na kurudisha ufalme wao kuanzia msimu ujao.Simba inatarajia kumaliza msimu wa pili mfululizo bila taji lolote, kitendo ambacho kimewakera viongozi wa timu hiyo na sasa wameamua kulitumia dirisha kubwa la usajili kukiboresha maradufu kikosi […]

The post Mangungu atangaza kuisuka upya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema tayari wameanza mchakato wa kukisuka upya kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri na kurudisha ufalme wao kuanzia msimu ujao.
Simba inatarajia kumaliza msimu wa pili mfululizo bila taji lolote, kitendo ambacho kimewakera viongozi wa timu hiyo na sasa wameamua kulitumia dirisha kubwa la usajili kukiboresha maradufu kikosi chao.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa tayari kumekuwa na vikao kati yake na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na benchi la ufundi kujadili njia sahihi za kupata wachezaji ambao watakiimarisha kikosi chao na kubeba mataji msimu ujao.

“Jambo la msingi ni kuwa tumechukua kilichotokea kama changamoto na kufanya tathmini ya wapi tumekosea na tunatarajia kufanya maboresho makubwa ya kikosi chetu, tunasubiri ripoti ya benchi la ufundi kujua ni mchezaji gani atakuwa sehemu ya mahitaji kwa msimu ujao na yupi atalazimika kuondoka,” alisema Mangungu.


Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa wamepanga kufanya usajili mkubwa wa wachezaji wapya pamoja na mipango ya kambi bora ya kabla ya msimu kuhakikisha wanarejesha utawala wao msimu ujao na hilo linawezekana kutokana na mikakati waliyoianza ya usajili.
Simba itashiriki michuano ya Super Cup mwezi Agosti, mwaka huu na mwenyekiti huyo ameeleza kuwa kipimo cha mafanikio ya msimu ujao wanataka kuyaona kupitia michuano hiyo.

The post Mangungu atangaza kuisuka upya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/16/mangungu-atangaza-kuisuka-upya-simba/feed/ 0