Lewandowski - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 12 Aug 2025 18:40:43 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Lewandowski - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Lewandowski aliitamani Man United https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/lewandowski-aliitamani-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/lewandowski-aliitamani-man-united/#respond Tue, 12 Aug 2025 18:40:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13818 Barcelona, HispaniaMshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski amebainisha kuwa alitamani kusaini na klabu ya Manchester United mwaka 2012 ili kufanya kazi na kocha wa wakati huo, Sir Alex Ferguson.Mpango wa mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo ya Old Trafford hata hivyo haukuweza kufanikiwa baada ya klabu yake ya wakati huo, Borussia Dortmund kuzuia usajili huo.Lewandowski hata […]

The post Lewandowski aliitamani Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski amebainisha kuwa alitamani kusaini na klabu ya Manchester United mwaka 2012 ili kufanya kazi na kocha wa wakati huo, Sir Alex Ferguson.
Mpango wa mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo ya Old Trafford hata hivyo haukuweza kufanikiwa baada ya klabu yake ya wakati huo, Borussia Dortmund kuzuia usajili huo.
Lewandowski hata hivyo alibaki Ujerumani baada ya kusajiliwa na klabu ya Bayern Munich mwaka 2014 akiwa mchezaji huru.
“Kuhusu kwenda Manchester United niliamua na kusema sawa, nilitaka kujiunga na Manchester United ili kuonana na Alex Ferguson,” alisema.
Lewandowski alifafanua kuwa licha ya kuikubali Man United, Dortmund walikataa kumuuza kwa sababu walifahamu kama angebaki pengine wangeweza kupata pesa zaidi na hivyo alitakiwa kusubiri labda kwa mwaka mmoja au miwili.
Wakati mchezaji huyo akitamani kwenda Man United, Dortmund ilikuwa ikinolewa na kocha Jurgen Klopp ambaye baadaye alihamia Liverpool na kujipatia mafanikio.
Lewandowski ambaye pia aliwahi kutakiwa na klabu ya Blackburn Rovers pia ya England kwa sasa ana fikra tofauti kuhusu kushindwa kwake kucheza soka katika Ligi Kuu England.
“Labda ni jambo la kujuta kwa kutocheza katika Ligi Kuu England lakini nikiangalia huko nilipotoka hadi kucheza Bayern Munich, Dortmund na sasa Barcelona nalazimika kusema kwamba nina furaha katika maisha yangu ya soka,” alisema.

The post Lewandowski aliitamani Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/lewandowski-aliitamani-man-united/feed/ 0
Lewandowski adai amesalitiwa https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/lewandowski-adai-amesalitiwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/lewandowski-adai-amesalitiwa/#respond Tue, 10 Jun 2025 10:06:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13569 Warsaw, PolandMshambuliaji Robert Lewandowski amemshutumu kocha wa timu ya taifa ya Poland kwa kumsaliti baada ya kumvua unahodha na mchezaji huyo kuamua kuachana na timu ya taifa.Kocha wa timu ya taifa ya Poland, Michal Probierz alifanya uamuzi wa kumvua unahodha wa timu ya taifa mshambuliaji huyo wa Barca na nafasi hiyo kumpa Piotr Zielinski.“Kocha amemuarifu […]

The post Lewandowski adai amesalitiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Warsaw, Poland
Mshambuliaji Robert Lewandowski amemshutumu kocha wa timu ya taifa ya Poland kwa kumsaliti baada ya kumvua unahodha na mchezaji huyo kuamua kuachana na timu ya taifa.
Kocha wa timu ya taifa ya Poland, Michal Probierz alifanya uamuzi wa kumvua unahodha wa timu ya taifa mshambuliaji huyo wa Barca na nafasi hiyo kumpa Piotr Zielinski.
“Kocha amemuarifu Robert Lewandowski, timu yote na maofisa wa timu hiyo kuhusu uamuzi alioifikia,” ilieleza taarifa ya Shirikisho la Soka Poland.
Dakika zipatazo 40 baada ya tangazo hilo, Lewandowski alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kwamba anaacha kuichezea timu hiyo kama itaendelea kuwa chini ya Probierz.
“Kwa kuzingatia mazingira na kukosekana kuaminiwa na kocha wa timu ya Poland, nimeamua kujiweka kando katika kuichezea timu ya taifa ya Poland kama kocha wa timu ataendelea kuwa huyo huyo,” alisema Lewandowski.
Lewandowski licha ya kutoa msimamo huo lakini pia alisisitiza kwamba anaamini atapata nafrasi ya kuichezea timu hiyo kwa mara nyingine kwa ajili ya mashabiki bora duniani.
Lewandowski alisema kwamba aliarifiwa uamuzi wa kuvuliwa unahodha usiku kwa njia ya simu wakati akiwaandaa watoto wake kwenda kulala.

“Nilipata taarifa ya simu kutoka kwa kocha MichaƂ Probierz kwamba ameamua kunivua unahodha, sikuwa nimejiandaa kwa namna yoyote, nilikuwa katika kuwaandaa watoto kwa ajili ya kulala,” alisema.


Alisema kwamba hakuwa hata na muda wa kuiarifu familia yake au kuzungumza na mtu yeyote kuhusu unahodha wake kwa sababu muda mfupi baadaye taarifa ilionekana kupitia mtandao.
Lewandoski, 36, alifafanua kuwa licha ya kukutana na Probierz baada ya mechi ya Ijumaa lakini hakuonesha dalili zozote kwamba alikuwa na mpango wa kumvua unahodha.

The post Lewandowski adai amesalitiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/10/lewandowski-adai-amesalitiwa/feed/ 0
Lewandoski kuwakosa Uholanzi Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/lewandoski-kuwakosa-uholanzi-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/lewandoski-kuwakosa-uholanzi-euro-2024/#respond Wed, 12 Jun 2024 06:25:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11299 Warsaw, PolandMshambuliaji wa timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski ataikosa mechi ya kwanza ya timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Ulaya (Euro 2024) dhidi ya Uholanzi baada ya kuumia misuli.Lewandowski ambaye pia ni mshambuliaji wa Barcelona, aliumia juzi Jumatatu wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Uturuki ambayo Poland ilitoka na ushindi wa […]

The post Lewandoski kuwakosa Uholanzi Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Warsaw, Poland
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski ataikosa mechi ya kwanza ya timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Ulaya (Euro 2024) dhidi ya Uholanzi baada ya kuumia misuli.
Lewandowski ambaye pia ni mshambuliaji wa Barcelona, aliumia juzi Jumatatu wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Uturuki ambayo Poland ilitoka na ushindi wa mabao 2-1.
Poland itaumana na Uholanzi Jumapili ijayo, mechi ambayo itakuwa ya kwanza kwa timu hizo kwenye fainali za Euro 2024 zitakazoanza rasmi keshokutwa Ijumaa nchini Ujerumani.
Matarajio ya awali ni kwamba Lewandowski angecheza mechi na Uholanzi lakini aliumia dakika ya 33 katika mechi na Uturuki, mechi ambayo ni ya mwisho ya kujipima nguvu kwa timu hizo kabla ya kuanza rasmi kwa fainali za Euro 2024.
Baada ya mechi na Uholanzi, Poland itacheza mechi yake ya pili dhidi ya Austria hapo Juni 21 kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi D dhidi ya Ufaransa, mechi itakayopigwa Juni 25.

“Lewandowski amepata tatizo la misuli, ni tatizo ambalo litamfanya asiwemo kwenye mechi ya kwanza ya fainali hizi,” ilieleza taarifa ya Poland.


Wachezaji wengine wa Poland walioumia katika mechi hiyo ni beki Pawel Dawidowicz na mshambuliaji Karol Swiderski ambao baadaye ilielezwa kwamba watakuwa vizuri mapema.

The post Lewandoski kuwakosa Uholanzi Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/12/lewandoski-kuwakosa-uholanzi-euro-2024/feed/ 0
Lewandoski: Hatuiogopi Madrid yenye Mbappe https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/lewandoski-hatuiogopi-madrid-yenye-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/lewandoski-hatuiogopi-madrid-yenye-mbappe/#respond Fri, 24 May 2024 06:03:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11101 Barcelona, HispaniaMshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski amesema kwamba timu yao haina hofu yoyote juu ya ujio wa Kylian Mbappe anayejiunga na mahasimu wao, Real Madrid.Msimu huu Real Madrid imekuwa tishio katika Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, ndiyo inayoshika usukani ikiizidi Barca inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 12 na wikiendi hii itacheza mechi […]

The post Lewandoski: Hatuiogopi Madrid yenye Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski amesema kwamba timu yao haina hofu yoyote juu ya ujio wa Kylian Mbappe anayejiunga na mahasimu wao, Real Madrid.
Msimu huu Real Madrid imekuwa tishio katika Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, ndiyo inayoshika usukani ikiizidi Barca inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 12 na wikiendi hii itacheza mechi yake ya mwisho ya La Liga ikiwa tayari imeshalibeba taji hilo.
Real Madrid pia Juni Mosi itaumana na Borussia Dortmund katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati ikiwa katika mafanikio hayo, klabu hiyo inadaiwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji tishio duniani, Kylian Mbappe ambaye tayari ameshaaga katika timu yake ya sasa ya PSG.
“Kuogopa? Hapana. Ni kweli kwamba Mbappe ni mchezaji wa kipekee na kama atajiunga na Real Madrid, timu hiyo pamoja na mchezaji huyo wote watakuwa imara.

“Hata hivyo kwa mtazamo wetu ni kwamba haijalishi wachezaji ni wazuri kiasi gani, kama sisi tutakuwa pamoja kitimu, tukafanya kazi pamoja na kuwa na mtazamo sahihi, tunaweza kuwashinda, tunaweza kupambana nao,” alisema Lewandowski.


Lewandowski, 35, alijiunga na Barca Julai, 2022 na katika msimu wake wa kwanza aliisaidia timu hiyo kubeba taji la La Liga akiwa amefunga mabao 23.
Msimu huu hata hivyo umekuwa mgumu kwa timu hiyo pamoja na mshambuliaji huyo ingawa pamoja na hali hiyo ameweza kufunga mabao 18 ya ligi na kushika nafasi ya nne kwa kufunga mabao mengi.

The post Lewandoski: Hatuiogopi Madrid yenye Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/lewandoski-hatuiogopi-madrid-yenye-mbappe/feed/ 0
Lewandowski atakiwa Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/lewandowski-atakiwa-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/lewandowski-atakiwa-saudi-arabia/#respond Mon, 02 Oct 2023 06:48:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7913 Barcelona, HispaniaMshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski yumo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kwenda kucheza soka katika ligi ya Saudi Arabia.Saudi Arabia ipo katika mkakati mzito wa kuiboresha ligi yao pamoja na soka la nchini humo kwa kusajili kwa pesa nyingi wanasoka mastaa wanaotamba hasa barani Ulaya na chanzo kimoja […]

The post Lewandowski atakiwa Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski yumo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kwenda kucheza soka katika ligi ya Saudi Arabia.
Saudi Arabia ipo katika mkakati mzito wa kuiboresha ligi yao pamoja na soka la nchini humo kwa kusajili kwa pesa nyingi wanasoka mastaa wanaotamba hasa barani Ulaya na chanzo kimoja cha habaru kimedokeza kuwa mchezaji huyo naye anawindwa Saudi Arabia.
Chanzo hicho hata hivyo haikuweka wazi jina la klabu inayomuwinda mshambuliaji huyo lakini inaeleweka kwamba ni moja ya klabu mbili mahasimu katika jiji la Riyadh za Al Nassr ni Al Hilal.
Lewandowski mwenye miaka 35 sasa, alijiunga na Barca Julai mwaka jana akitokea Bayern Munich, klabu ambayo kwa kiasi kikubwa imebeba historia ya mafanikio yake kwenye soka barani Ulaya.
Akiwa Bayern, Lewandowski aliweka rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji na tuzo mbalimbali zikiwamo za mfungaji bora kwa miaka minane.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Poland, licha ya mafanikio hayo, aliamua kuondoka Bayern na kwenda Barca kwa alichodai kwamba anataka changamoto mpya na sasa swali linabaki je atakuwa tayari kwa changamoto nyingine mpya ya Saudi Arabia.
Miongoni mwa wachezaji mastaa wa Ulaya ambao wametimkia Saudi Arabia ni Cristiano Ronaldo, Neymar, N’Golo Kante, Eduardo Mendy, Karim Benzema na wengineo.

The post Lewandowski atakiwa Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/lewandowski-atakiwa-saudi-arabia/feed/ 0
Lewandowski kuikosa El Clasico https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/lewandowski-kuikosa-el-clasico/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/lewandowski-kuikosa-el-clasico/#respond Tue, 28 Feb 2023 09:20:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5333 Barcelona, HispaniaMshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski ataikosa mechi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid maarufu El-Clasico itakayopigwa keshokutwa Alhamisi baada ya kuumia mguu katika mechi na Almeira.Lewandowski, mshambuliaji tegemeo wa Barca kukosekana kwake katika mechi hiyo kunaiongezea majanga timu yake ambayo katika mechi hiyo ya La Liga dhidi ya Almeira ililala kwa bao 1-0.Matokeo hayo […]

The post Lewandowski kuikosa El Clasico first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Robert Lewandowski ataikosa mechi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid maarufu El-Clasico itakayopigwa keshokutwa Alhamisi baada ya kuumia mguu katika mechi na Almeira.
Lewandowski, mshambuliaji tegemeo wa Barca kukosekana kwake katika mechi hiyo kunaiongezea majanga timu yake ambayo katika mechi hiyo ya La Liga dhidi ya Almeira ililala kwa bao 1-0.
Matokeo hayo ya kushtusha yameifanya Barca inayoshika usukani katika La Liga kushindwa kuongeza tofauti ya pointi kufikia 10 dhidi ya Real Madrid inayoshika nafasi ya pili.
Mechi hiyo ya wababe wa Hispania itakayopigwa Alhamisi ni ya nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme maarufu Copa del Rey na huenda Lewandowski tena akaikosa mechi ya La Liga dhidi ya Valencia wikiendi ijayo.
Baada ya hapo, Barca itaumana kwa mara nyingine na Real Madrid katika mechi ya La Liga ambayo itapigwa Machi 19 kwenye dimba la Nou Camp, mechi ambayo huenda Lewandowski akawa fiti kwa ajili ya kucheza.
Taarifa ya Barca kuhusu Lewandowski ilieleza kwa kifupi, “Robert Lewandowski amepata matatizo ya misuli ya mguu wa kushoto, mchezaji huyo kutoka Poland hatokuwa uwanjani hadi tatizo litakapoisha.”
Awali Lewandowski alipewa adhabu na kukosa mechi tatu za mwezi Januari na Barca ikawa katika wakati mgumu kwa kumkosa mtu sahihi wa kuziba pengo lake baada ya kuwaruhusu Pierre-Emerick Aubameyang na Memphis Depay waihame klabu hiyo.
Timu hiyo pia inawakosa Pedri na Ousmane Dembele ambao ni majeruhi, Dembele alicheza mara ya mwisho Januari mwishoni dhidi ya Girona wakati Pedri amekuwa nje tangu aumie Februari 16 katika mechi dhidi ya Man United.
Barca pia itamkosa Gavi katika mechi na Valencia kwa kuwa mchezaji huyo atakuwa akitumikia adhabu ya kukosa mechi moja kama ilivyo kwa kocha Xavi.

The post Lewandowski kuikosa El Clasico first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/lewandowski-kuikosa-el-clasico/feed/ 0
Lewandowski, Bayern wazika tofauti https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/#respond Tue, 02 Aug 2022 19:16:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2103 Munich, UjerumaniMshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski hatimaye leo amekutana na kuagana rasmi na wachezaji na maofisa wa klabu yake ya zamani ya Bayern Munich na hivyo kuzika hali ya utata uliotokana na kuondoka kwake.Lewandowski ambaye akiwa Bayern amejiwekea rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji mbalimbali zikiwamo tuzo […]

The post Lewandowski, Bayern wazika tofauti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski hatimaye leo amekutana na kuagana rasmi na wachezaji na maofisa wa klabu yake ya zamani ya Bayern Munich na hivyo kuzika hali ya utata uliotokana na kuondoka kwake.
Lewandowski ambaye akiwa Bayern amejiwekea rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji mbalimbali zikiwamo tuzo za mfungaji bora kwa miaka minane, amejiunga na Barca mwezi uliopita kwa ada inayofikia Euro milioni 45, uhamisho ambao aliulazimisha baada ya Bayern kuonekana kuwa wagumu na hivyo kuibua sintofahamu kati yake na klabu hiyo.
Tangu kuondoka Bayern, Lewandowski ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Poland, alijikuta katika hali ya kushutumiana na mabosi wake wa zamani huku mchezaji huyo akidai kwamba uhamisho wake ulijaa siasa nyingi kutoka Bayern ambao aliwashutumu kwa kujaribu kutafuta hoja ili wamuuze.
Bayern nao kwa upande wao walisema kwamba hali hiyo ilisababishwa na mchezaji huyo ambaye alikuwa akisisitiza kutaka kuhama licha ya kwamba alikuwa na mkataba ambao ulikuwa unafikia ukomo mwaka 2023.
“Kwa sasa kila kitu kiko vizuri, nimekutana na kila mtu na kuwashukuru, sitosahau nilichokipata hapa na uzoefu nilioupata, hilo ni jambo muhimu sana kwangu, wiki iliyopita kidogo kulikuwa na hali ya utata lakini kuna wakati haya ni mambo yanayotokea kwenye soka,” alisema Lewandowski katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Sky.
Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic alizungumza na Lewandowski kwa muda mfupi ambao mchezaji huyo alifika katika klabu hiyo na wameyaweka mambo sawa na hatimaye kuondoa utata uliojitokeza.
“Robert alikuja ofisini kwangu kuniaga na tumezungumza kwa dakika 15, nilimueleza kila kitu na tumeyaweka mambo sawa, Robert amefanya mambo makubwa hapa Bayern na hilo litabaki kuwa hivyo, naye pia anajua kwamba kwa nini anatakiwa kuishukuru Bayern,” alisema Salihamidzic.

The post Lewandowski, Bayern wazika tofauti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/feed/ 0
Lewandowski: Bayern waongo https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/#respond Sat, 30 Jul 2022 12:05:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2047 Barcelona, HispaniaMshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Bayern Munich ameishutumu klabu yake ya zamani kwa kusema uwongo kuhusu kuondoka kwake kwa lengo la kuwatuliza mashabiki.Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Lewandowski aliulizwa sababu hasa iliyomfanya aihame Bayern kuwa ni uvumi ulioenea kwamba timu hiyo ilipanga kumsajili […]

The post Lewandowski: Bayern waongo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Bayern Munich ameishutumu klabu yake ya zamani kwa kusema uwongo kuhusu kuondoka kwake kwa lengo la kuwatuliza mashabiki.
Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Lewandowski aliulizwa sababu hasa iliyomfanya aihame Bayern kuwa ni uvumi ulioenea kwamba timu hiyo ilipanga kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ambaye hata hivyo baadaye alijiunga na Man City.
“Hapana, hakuna uhusiano wowote na usajili wa Erling, mimi ni mtu ambaye hata kama jambo fulani si zuri kwangu ukweli unabaki kuwa muhimu, sitaki kuzungumzia nini hasa kilichotokea lakini kama sababu ya kuhama ni Erling, hiyo hapana, mimi sikuona tatizo lolote kama yeye angejiunga na Bayern Munich.
“Lakini kuna aina ya watu ambao hawasemi ukweli kuhusu mimi, wanasema vitu tofauti, lakini kwangu wakati wote ni muhimu kuwa wazi, kusema ukweli na labda kwa baadhi ya watu wachache hilo lilikuwa tatizo, ni sawa lakini mwisho wa siku niliona ni wakati sahihi kwa mimi kuondoka Bayern Munich na kujiunga na Barcelona,” alisema.
“Nilikuwa na uhusiano mzuri na wachezaji wenzangu, maofisa, kocha na haya yote ni mambo ambayo nitayakosa kwa sababu nilikuwa na wakati mzuri pale na hatukuwa marafiki uwanjani tu bali ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini hatimaye ukurasa umefungwa na nafungua ukurasa mpya wa maisha yangu.”
“Kwa hiyo najiona niko katika msimamo sahihi, mahali sahihi lakini yote ambayo yalijitokeza mwishoni, wiki chache kabla sijaondoka Bayern Munich ni siasa nyingi, klabu ilikuwa inajaribu kutafuta hoja ya kwanini wanaweza kuniuza mimi katika klabu nyingine, kwa sababu hapo kabla labda kulikuwa na ugumu kulieleza hilo kwa mashabiki, na lazima nikubali kwamba kuna uwongo mwingi umesemwa kuhusu mimi, lakini yote kwa yote bado najua ukweli kwamba mashabiki hata katika wakati huu bado wananiunga mkono.
Lewandowski ameondoka Bayern baada ya kuichezea timu hiyo kwa mafanikio kwa miaka minane akifunga mabao 344 katika mechi 375, awali klabu yake ilikuwa ikipata tabu kumruhusu aondoke licha ya mwenyewe kusisitiza azma yake ya kutaka changamoto mpya kwingineko Ulaya.

The post Lewandowski: Bayern waongo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/feed/ 0