La Liga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 03 Jun 2026 18:05:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg La Liga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Barca yabeba taji La Liga https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/barca-yabeba-taji-la-liga/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/barca-yabeba-taji-la-liga/#respond Tue, 12 May 2026 08:22:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14646 Barcelona, HispaniaBarcelona au Barca Jumapili Mei 10, 2026 wametwaa taji la La Liga msimu wa 2025-26 baada ya kuwachapa mahasimu wao Real Madrid mabao 2-0, ushindi wenye maana kubwa kwa Marcus Rashford aliyefunga bao la kwanza.Bao hilo la mpira wa adhabu limezidi kupaisha thamani ya Rashford ambaye ni kama amejifungulia njia katika kikosi cha timu […]

The post Barca yabeba taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Barcelona au Barca Jumapili Mei 10, 2026 wametwaa taji la La Liga msimu wa 2025-26 baada ya kuwachapa mahasimu wao Real Madrid mabao 2-0, ushindi wenye maana kubwa kwa Marcus Rashford aliyefunga bao la kwanza.
Bao hilo la mpira wa adhabu limezidi kupaisha thamani ya Rashford ambaye ni kama amejifungulia njia katika kikosi cha timu ya taifa ya England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.
Rashford pia amejifungulia njia katika klabu, uwezekano wa kupewa mkataba wa kudumu Barca ni mkubwa au kurudi Man United, timu yake iliyomtoa kwa mkopo baada ya kupitia kipindi kigumu.
Mpira wa adhabu uliopigwa na mshambuliaji huyo umbali wa mita 20 ulionekana kumtatiza kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois ambaye aliishia kuungalia ukiingia wavuni juu kwenye kona ya kushoto.
Kasi ya mashambulizi ya Barca iliendelea na majibu yake yakapatikana kwa bao la pili mfungaji akiwa ni Ferran Torres ambaye alishirikiana vizuri na Dani Olmo hadi kufunga bao hilo.
Barca waliokuwa wenyeji wa mechi hiyo maarufu El Clasico inayozihusisha timu hizo mahasimu wa soka la Hispania, ushindi wao umewawezessha kubeba taji hilo mara ya pili mfululizo.
Kwa upande mwingine wamezidi kuwaacha pagumu mahasimu wao Real Madrid msimu huu tangu kuachana na kocha wao Xabi Alonso hadi kutolewa katika michuano mbalimbali ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya, michuano inayotajwa kuwa ya hadhi yao.
Zaidi ya hilo hali tete imeendelea kujitokeza miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo kukiwa na abari kwamba wachezaji wamekuwa wakigombana wao kwa wao kila mmoja akijiona kuwa juu.
Matukio hayo yanaonekana kuongeza matatizo kwa kocha wa muda, Alvaro Arbeloa wakati mwenzake Hansi Flick akifurahia maisha katika kikosi cha Barca ambacho kimebeba taji kikiwa na mechi tatu mkononi.
Kinachoonekana Real Madrid ni kama vile timu imekuwa kubwa mno kwa Arbeloa, mastaa wamempanda kichwani na kuna kila dalili kwamba hatokuwa na timu hiyo msimu ujao.
Mmoja wa makocha ambaye jina lake limekuwa likitajwa kukabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo ni Jose Mourinho na kama hilo litafanikiwa basi kocha huyo maarufu Special One atakuwa anarudi katika timu hiyo kwa mara ya pili.

The post Barca yabeba taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/12/barca-yabeba-taji-la-liga/feed/ 0
Barca yatwaa taji La Liga https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/#respond Mon, 15 May 2023 09:21:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6171 Barcelona, HispaniaBarcelona hatimaye imetwaa taji la La Liga msimu wa 2022/23 kwa kishindo baada ya kuichapa Espanyol mabao 4-2 ikilitwaa taji hilo mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018-19.Barca imelibeba taji ikiwa na mechi nne mkononi, ina pointi 85 imewazidi mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi […]

The post Barca yatwaa taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Barcelona hatimaye imetwaa taji la La Liga msimu wa 2022/23 kwa kishindo baada ya kuichapa Espanyol mabao 4-2 ikilitwaa taji hilo mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018-19.
Barca imelibeba taji ikiwa na mechi nne mkononi, ina pointi 85 imewazidi mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 14 ambazo hawawezi kuzifikia kwa mechi zilizobaki.
Vinara hao waliutawala vyema mchezo kuanzia kipindi cha kwanza na kupata bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Roberto Lewandowski kabla Balde hajaongeza la pili dakika ya 20.
Lewandowski ambaye amekuwa na ukame wa mabao, aliongeza bao la tatu dakika ya 40 ambalo ni bao lake la 20 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Barca ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Dakika nane baada ya kuanza kipindi cha pili, Barca iliandika bao la nne lililofungwa kwa kichwa na Jules Kounde lakini Espanyol walipambana na kupata mabao mawili ya kufutia machozi yaliyofungwa na Javier Puado dakika ya 73 na Joselu katika dakika mbili za nyongeza.
Taji hilo linakuwa la kwanza kwa kocha Xavi ambaye wakati akiichezea Barca anajivunia rekodi ya kubeba taji la La Liga mara nane katika miaka 17 aliyotamba na timu hiyo.
Kwa nahodha Sergio Busquets taji hilo ambalo ni la tisa kwake limempa jambo la kujivunia wakati akiiaga timu hiyo, akihitimisha miaka yake 18 ya mafanikio ndani ya klabu hiyo kwani tayari ametangaza kustaafu baada ya msimu huu.
Kwa upande mwingine Barca kwa sasa inajiandaa kuufanyia marekebisho uwanja wake wa Nou Campo ingawa mashabiki watapata nafasi ya kulifurahia taji hilo kwenye uwanja huo kwenye mechi mbili zilizobaki dhidi ya Real Sociedad na Real Mallorca.
Maatokeo mechi nyingine za La Liga
Espanyol 2-4 Barcelona
Celta Vigo 1-2 Valencia
Elche 1-0 Atl Madrid
Real Valladolid 0-3 Sevilla

The post Barca yatwaa taji La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/15/barca-yatwaa-taji-la-liga/feed/ 0
Barca yamtaka bosi La Liga ajiuzulu https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/barca-yamtaka-bosi-la-liga-ajiuzulu/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/barca-yamtaka-bosi-la-liga-ajiuzulu/#respond Tue, 04 Apr 2023 09:42:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5678 Barcelona, HispaniaKlabu ya Barcelona ‘Barca’ imemtaka mtendaji mkuu wa Ligi Kuu Hispania au La Liga, Javier Tebas ajiuzulu kwa kutoa ushahidi wa uwongo kwa klabu hiyo kuhusu tuhuma za kutoa rushwa kwa mwamuzi.Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Tebas anadaiwa kuwasilisha ushahidi wa maandishi kwa waendesha mashitaka akiwataja marais wa zamani wa Barca katika […]

The post Barca yamtaka bosi La Liga ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Klabu ya Barcelona ‘Barca’ imemtaka mtendaji mkuu wa Ligi Kuu Hispania au La Liga, Javier Tebas ajiuzulu kwa kutoa ushahidi wa uwongo kwa klabu hiyo kuhusu tuhuma za kutoa rushwa kwa mwamuzi.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Tebas anadaiwa kuwasilisha ushahidi wa maandishi kwa waendesha mashitaka akiwataja marais wa zamani wa Barca katika kashfa hiyo.
Tebas amewahusisha marais hao na kashfa inayoiandama klabu hiyo ikidaiwa kumhonga makamu rais wa zamani wa kamati ya waamuzi Hispania kwa kinachodhaniwa kuwa ni kutaka upendeleo.
Habari za ndani hata hivyo zinadai kwamba ushahidi uliowasilishwa na Tebas dhidi ya marais hao, Sandro Rosell na Josep Maria Bartomeu hauhusiani na kashfa iliyopo.
Akijibu madai ya Barca kupitia akaunti ya Twitter, Tebas alisema kichwa cha habari cha nakala hiyo kilikosewa kwani hakumtuhumu yeyote kwa lolote na anamtuhumu mwandishi kwa madai ya upotoshaji.
Barca hata hivyo wametaka ufafanuzi wa kina kutoka kwa Tebas na kuelezea hasira zao na namna walivyochukizwa na jambo hilo wakimtaka Tebas ajiuzulu.

“Barcelona, kama alivyosema hivi karibuni rais Joan Laporta imejikuta katika mkakati maalum wa kuchafuliwa na vyombo vya habari kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni, Barca haikuwahi kununua mwamuzi,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.


“Si mara ya kwanza Rais wa La Liga amekuwa akitumia silaha yake ya vyombo vya habari kuichafua Barcelona lakini ukiacha upuuzi wake uliozoeleka hatukuwahi kufikiria angetaraji kuidhalilisha klabu yetu na ushahidi wa uwongo,” ilieleza taarifa ya Barca.
Baada ya waendesha mashitaka kuwasilisha tuhuma, mahakama nchini Hispania inachunguza malipo ya Euro 7 milioni ambayo Barca iliyafanya kwa rais wa zamani wa kamati ya waamuzi Hispania, Jose Maria Negreira kati ya mwaka 2001 na 2018.
Wakati ikidhaniwa kwamba malipo hayo yalitolewa ili klabu hiyo ipendelewe katika mechi zao, Barca imekana jambo hilo ikidai kwamba ilimlipa Negreira na kampuni yake ili awasaidie kupata taarifa ya ufundi kuhusu waamuzi na mwenendo wa mechi zao.

The post Barca yamtaka bosi La Liga ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/barca-yamtaka-bosi-la-liga-ajiuzulu/feed/ 0