Kompany - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 30 May 2024 05:58:17 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kompany - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kompany kocha mpya Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kompany-kocha-mpya-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kompany-kocha-mpya-bayern/#respond Thu, 30 May 2024 05:58:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11173 Munich, UjerumaniSasa ni rasmi, Bayern Munich hatimaye imemtangaza rasmi Vincent Kompany kuwa kocha mkuu mpya baada ya makubaliano na klabu ya Burnley ambayo kocha huyo alikuwa na mkataba nayo.Inadaiwa Kompany amesaini mkataba wa miaka miwili na Bayern imelazimika kuilipa Burnley Pauni 10 milioni na sasa ni rasmi Kompany anakuwa kocha mpya akichukua nafasi iliyoachwa na […]

The post Kompany kocha mpya Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Sasa ni rasmi, Bayern Munich hatimaye imemtangaza rasmi Vincent Kompany kuwa kocha mkuu mpya baada ya makubaliano na klabu ya Burnley ambayo kocha huyo alikuwa na mkataba nayo.
Inadaiwa Kompany amesaini mkataba wa miaka miwili na Bayern imelazimika kuilipa Burnley Pauni 10 milioni na sasa ni rasmi Kompany anakuwa kocha mpya akichukua nafasi iliyoachwa na Thomas Tuchel.
Kompany alijipatia umaarufu baada ya kuiwezesha Burnley kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu England (EPL) ingawa katika msimu huo huo wa kwanza EPL timu hiyo imeshuka daraja na msimu ujao wa 2024-25 itacheza ligi ya Championship.
Uteuzi wa Kompany umekuja baada ya mabosi Bayern kupitia wakati mgumu kumsaka mrithi wa Tuchel ambaye, Februari mwaka huu klabu hiyo ilitangaza kuachana naye baada ya msimu huu.

“Ninajiandaa kwa changamoto ya FC Bayern, ni heshima kubwa kuweza kufanya kazi katika klabu hii, FC Bayern ni taasisi katika soka la kimataifa,” alisema Kompany.


Naye mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Max Eberl alisema klabu yake ina furaha kubwa kumpata Kompany na wamefikia makubaliano haraka baada ya mazungumzo na kocha huyo kuonesha ni kwa kiasi gani amevutiwa na kazi ya kuinoa Bayern.
“Vincent Kampany ana njaa ya mafanikio na anawezesha kila kitu kufanikishwa, akiwa mchezaji tayari alionesha hulka za kiuongozi katika soka la kimataifa na anaendelea na hilo akiwa kocha,” alisema Eberl.
Kabla ya kumpata Kompany, Bayern walihusishwa na mipango ya kumchukua kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso na kocha wao wa zamani ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Ujerumani, Julian Nagelsmann, lakini wote walikataa.
Mwingine aliyetajwa kuwindwa na Bayern ni kocha wa zamani wa muda wa Man United, Ralf Rangnick ambaye pia aliamua kuendelea na kibarua chake cha kuinoa timu ya taifa ya Austria, hapo hapo kukawa na habari kwamba wangeendelea na Tuchel lakini pia haikuwezekana.

The post Kompany kocha mpya Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/kompany-kocha-mpya-bayern/feed/ 0
Kompany, Bayern mambo mazuri https://www.greensports.co.tz/2024/05/25/kompany-bayern-mambo-mazuri/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/25/kompany-bayern-mambo-mazuri/#respond Sat, 25 May 2024 20:23:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11117 Munich, UjerumaniKocha wa Burnley, Vincent Kompany inadaiwa amefikia makubaliano ya awali na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ili awe kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Thomas Tuchel aliyetimuliwa.Habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo aliyeipandisha Burnley Ligi Kuu England (EPL) msimu uliopita na kushuka nayo msimu huu, atasaini mkataba utakaofikia ukomo mwaka […]

The post Kompany, Bayern mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kocha wa Burnley, Vincent Kompany inadaiwa amefikia makubaliano ya awali na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ili awe kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Thomas Tuchel aliyetimuliwa.
Habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo aliyeipandisha Burnley Ligi Kuu England (EPL) msimu uliopita na kushuka nayo msimu huu, atasaini mkataba utakaofikia ukomo mwaka 2027.
Katika makubaliano hayo inadaiwa, Bayern watatakiwa kuwalipa Burnley zaidi ya Pauni milioni 10 kama malipo ya fidia kwa kuwa Kompany bado ana mkataba na Burnley.
Habari zaidi zinadai kwamba Kompany ambaye amepata nafasi hiyo baada ya makocha kadhaa kukataa ofa hiyo, akiwa Bayern hatokuwa pamoja na wasaidizi wake wote aliokuwa nao Burnley bali ataungana na baadhi yao.
Tangu Bayern itangaze kuachana na Tuchel, makocha kadhaa ambao wamekuwa wakitajwa kuwaniwa na timu hiyo wamekataa akiwamo Xabi Alonso wa Bayern Leverkusen.
Wengine waliokataa kuinoa timu hiyo ni Ralf Rangnick ambaye kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Austria na Julian Nagelsmann ambaye anainoa timu ya taifa ya Ujerumani.
Kompany, 38, beki wa zamani wa Man City na timu ya taifa ya Ubelgiji, inadaiwa pamoja na ubora wake katika kazi ya ukocha, pia anazungumza kwa ufasaha lugha ya Kijerumani.

The post Kompany, Bayern mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/25/kompany-bayern-mambo-mazuri/feed/ 0
Stori ya Kompany, Bayern yapamba moto https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/stori-ya-kompany-bayern-yapamba-moto/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/stori-ya-kompany-bayern-yapamba-moto/#respond Fri, 24 May 2024 05:59:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11099 Munich, UjerumaniKlabu za Bayern Munich ya Ujerumani na Burnley ya England inadaiwa zipo katika hatua za mwisho kufikia makubaliano ili kocha wa Burnley, Vincent Kompany asaini mkataba wa kuinoa Bayern Munich.Bayern, hivi karibuni iliachana na kocha Thomas Tuchel, hatimaye inadaiwa kumgeukia Kompany ambaye amewahi kuwa na klabu ya Hamburg pia ya Ujerumani kwa miaka miwili […]

The post Stori ya Kompany, Bayern yapamba moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu za Bayern Munich ya Ujerumani na Burnley ya England inadaiwa zipo katika hatua za mwisho kufikia makubaliano ili kocha wa Burnley, Vincent Kompany asaini mkataba wa kuinoa Bayern Munich.
Bayern, hivi karibuni iliachana na kocha Thomas Tuchel, hatimaye inadaiwa kumgeukia Kompany ambaye amewahi kuwa na klabu ya Hamburg pia ya Ujerumani kwa miaka miwili lakini pia ana uwezo wa kuzungumzia vizuri Kijerumani.
Hatua ya kumgeukia Kompany ambaye timu yake ya Burnley imeshuka daraja, imekuja baada ya makocha Xabi Alonso, Julian Nagelsmann na Ralf Rangnick kukataa ofa ya kuinoa timu hiyo na sasa akili imeelekezwa kwa Kompany.
Habari za ndani zinadai kwamba Bayern wanaamini kuwa Kompany, beki wa zamani wa Man City na timu ya taifa ya Ubelgiji, yuko tayari kwa kazi hiyo kama makubaliano yatafikiwa na Burnley.
Katika mpango huo, Bayern watapenda kuona Kompany anajiunga na timu hiyo ya mjini Munich pamoja na wasaidizi wake akiwamo mshambuliaji wa zamani wa Wales, Craig Bellamy.
Kompany alijiunga na Burnley mwaka 2022 akitokea Anderlecht ya Ubelgiji, katika msimu wake wa kwanza aliiwezesha Burnley kubeba taji la Championship ikikusanya pointi 101 na kufuzu kucheza Ligi Kuu England (EPL).
Timu hiyo hata hivyo katika msimu wa kwanza EPL imeshika nafasi ya 19 na kushuka daraja, hivyo msimu ujao wa 2024-25 itarudi katika Ligi ya Championship.
Kwa Kompany jina lake limeendelea kuwa juu licha ya Burnley kushuka, Pep Guardiola inadaiwa aliwahi kumtaja akimhusisha na kazi ya ukocha Man City, timu aliyoichezea kwa mafanikio kwa miaka 11, majira ya kiangazi msimu uliopita pia alihusishwa na timu za Tottenham na Chelsea.

The post Stori ya Kompany, Bayern yapamba moto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/stori-ya-kompany-bayern-yapamba-moto/feed/ 0
Kompany: Kiwango cha waamuzi EPL kimeshuka https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kompany-kiwango-cha-waamuzi-epl-kimeshuka/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kompany-kiwango-cha-waamuzi-epl-kimeshuka/#respond Tue, 02 Apr 2024 09:03:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10475 London, EnglandKocha wa Burnley, Vincent Kompany amesema kiwango cha waamuzi wa Ligi Kuu England (EPL) kimeshuka, hoja inayounga mkono shutuma ambazo waamuzi hao wamekuwa wakikutana nazo msimu huu.Waamuzi wa EPL hususan msimu huu wamejikuta wakibebeshwa lawama za mara kwa mara kutokana na maamuzi ya utata ambayo wamekuwa wakiyatoa katika baadhi ya mechi.Timu ya Burnley ilibaki […]

The post Kompany: Kiwango cha waamuzi EPL kimeshuka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Burnley, Vincent Kompany amesema kiwango cha waamuzi wa Ligi Kuu England (EPL) kimeshuka, hoja inayounga mkono shutuma ambazo waamuzi hao wamekuwa wakikutana nazo msimu huu.
Waamuzi wa EPL hususan msimu huu wamejikuta wakibebeshwa lawama za mara kwa mara kutokana na maamuzi ya utata ambayo wamekuwa wakiyatoa katika baadhi ya mechi.
Timu ya Burnley ilibaki na wachezaji 10 uwanjani katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Chelsea na baadaye Kompany kupewa kadi nyekundu kwa kulalamikia penalti iliyoonekana kuwa na utata.
Burnley ambayo inanyemelewa na janga la kushuka daraja, inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi hiyo zikiwa zimebaki mechi tisa na katika mechi hiyo na Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge ilitoka sare ya mabao 2-2.
“Hasira zimekuja kutokana na makosa yanayoendelea siku hadi siku na wakati wote yamekuwa yakizua mjadala,” alisema Kompany katika mkutano na waandishi wa habari.

“Madhara yake yanakuwa ni katika pointi na msimu wote, nafikiri mambo yote hayo yanakupa mawazo ya kuwa mwenye hasira lakini yakijitokeza tena nitajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili nikae kimya, nafikiri haitatokea tena msimu huu,” alisema Kompany.


Kompany alisema anaendelea kusema kile anachofikiri, ambacho hawezi kukiacha hivi hivi na analazimika kusema kwamba waamuzi kiwango chao hakijawa kizuri msimu huu na anasema hivyo katika namna ya kujenga.
Kocha huyo ambaye baadaye aliwaomba radhi waamuzi kwa kauli hiyo pia alikumbushia kauli yake ya mwaka jana aliposema kwamba EPL kuna waamuzi bora duniani lakini katika mtazamo wa kawaida tu hali hiyo haioni kwa mwaka huu.

The post Kompany: Kiwango cha waamuzi EPL kimeshuka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kompany-kiwango-cha-waamuzi-epl-kimeshuka/feed/ 0
Kompany asaini miaka 5 Burnley https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/kompany-asaini-miaka-5-burnley/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/kompany-asaini-miaka-5-burnley/#respond Mon, 08 May 2023 06:45:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6055 London, EnglandKlabu ya Burnley imemsainisha mkataba mpya wa miaka mitano kocha wake, Vincent Kompany ambaye sasa atakuwa na timu hiyo hadi mwaka 2028.Kompany ambaye ameirudisha timu hiyo kwenye Ligi Kuu England (EPL), amekuwa pia akidaiwa kutakiwa na klabu ya Chelsea iliyovutiwa na mafanikio aliyoyapata akiwa Burnley.Katika msimu wake wa kwanza na Burnley, Kompany, beki wa […]

The post Kompany asaini miaka 5 Burnley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Burnley imemsainisha mkataba mpya wa miaka mitano kocha wake, Vincent Kompany ambaye sasa atakuwa na timu hiyo hadi mwaka 2028.
Kompany ambaye ameirudisha timu hiyo kwenye Ligi Kuu England (EPL), amekuwa pia akidaiwa kutakiwa na klabu ya Chelsea iliyovutiwa na mafanikio aliyoyapata akiwa Burnley.
Katika msimu wake wa kwanza na Burnley, Kompany, beki wa zamani wa Man City, ameiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Championship akiwa na mechi kadhaa mkononi na sasa anajiandaa kuiongoza katika EPL kwa msimu wa 2023-24.

“Hakika tuna furaha, Vincent amesaini mkataba mpya, ni mtu sahihi anayefaa kwa namna ambavyo wote tunaona klabu ya soka ya Burnley inavyokwenda mbele,” alisema mwenyekiti wa klabu hiyo, Alan Pace.


“Ni kiongozi wa aina yake, ameweka malengo ya juu na anaipeleka klabu katika viwango ambavyo sote tunataka kuvifikia,” alisema.
Burnley leo Jumatatu itakuwa nyumbani kucheza mechi yake ya mwisho ya kumaliza msimu wa Champioship dhidi ya Cardiff City na baada ya mechi hiyo itakabidhiwa taji la ubingwa.

The post Kompany asaini miaka 5 Burnley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/kompany-asaini-miaka-5-burnley/feed/ 0