KMC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 25 Feb 2025 18:53:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg KMC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaigaragaza KMC 6-1 https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/yanga-yaigaragaza-kmc-6-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/yanga-yaigaragaza-kmc-6-1/#respond Sat, 15 Feb 2025 11:58:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13017 Na mwandishi wetuYanga imekamata usukani wa Ligi Kuu NBC kwa kishindo baada ya kuigaragaza KMC mabao 6-1 huku kiungo Stephane Aziz Ki akifunga mabao matatu (hat trick) peke yake.Ushindi huo uliopatikana Ijumaa hii, Februari 14, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam unaifanya Yanga kujikita kileleni mwa ligi hiyo kwa fikisha pointi 49.Yanga […]

The post Yanga yaigaragaza KMC 6-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imekamata usukani wa Ligi Kuu NBC kwa kishindo baada ya kuigaragaza KMC mabao 6-1 huku kiungo Stephane Aziz Ki akifunga mabao matatu (hat trick) peke yake.
Ushindi huo uliopatikana Ijumaa hii, Februari 14, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam unaifanya Yanga kujikita kileleni mwa ligi hiyo kwa fikisha pointi 49.
Yanga imekusanya idadi hiyo ya pointi katika mechi 19 na kuwazidi mahasimu wao Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili ingawa Yanga imecheza mechi 19 na Simba 18.
Karamu ya mabao ya Yanga katika mechi hiyo ilianza kuandikwa katika dakika ya 11 kwa bao la Prince Dube akiiitumia vizuri pasi ya Maxi Nzengeli.
Dakika saba baadaye, KMC waliumizwa kwa mara nyingine baada ya Aziz Ki kuifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa baada ya Clement Mzize kuangushwa ndani ya eneo la 18.
Hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao mawili na muda mchache baada ya kuanza kipindi cha pili, Aziz Ki ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo aliiongezea Yanga bao la tatu kwa shuti kali.
Mabao matatu ya Yanga hayakuwafanya KMC kukata tamaa ambapo dakika ya 52 walipata bao mfungaji akiwa ni Remdatus Mussa aliyefumua shuti lililomshinda kipa, Djigui Diarra.
Mambo hata hivyo yaliwaharibikia tena KMC dakika sita baadaye kwa Yanga kupata bao la nne lililofungwa tena kwa penalti na Aziz Ki, penalti iliyotolewa baada ya Dube kuangushwa ndani ya eneo la 18.
Yanga waliendelea kutawala mchezo na kuwanyanyasa wenyeji KMC kwa kuandika mabao mengine mawili yaliyofungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 90 na Israel Mwenda katika dakika tano za nyongeza.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Ken Gold na Tabora United zilitoka sare ya bao 1-1, Tanzania Prisons ililala kwa bao 1-0 mbele ya Namungo na Kagera Sugar iliilaza Fountain Gate 3-0.

The post Yanga yaigaragaza KMC 6-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/yanga-yaigaragaza-kmc-6-1/feed/ 0
Mwaigaga sasa mali ya KMC https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mwaigaga-sasa-mali-ya-kmc/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mwaigaga-sasa-mali-ya-kmc/#respond Thu, 04 Jul 2024 06:01:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11502 Na mwandishi wetuKlabu ya KMC imethibitisha kwa kumtangaza Oscar Paul Mwaigaga (pichani) kama mchezaji wao mpya ambaye wamemnasa kutoka klabu ya Kakamega Home Boys ya Kenya.Oscar raia wa Tanzania anayemudu nafasi ya kiungo wa kati, alijiunga na Kakamega msimu uliopita akitokea Tanzania Prisons aliyoachana nayo baada ya kumaliza mkataba.KMC ambayo imemtambulisha Mwaigaga Jumatano hii kupitia […]

The post Mwaigaga sasa mali ya KMC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya KMC imethibitisha kwa kumtangaza Oscar Paul Mwaigaga (pichani) kama mchezaji wao mpya ambaye wamemnasa kutoka klabu ya Kakamega Home Boys ya Kenya.
Oscar raia wa Tanzania anayemudu nafasi ya kiungo wa kati, alijiunga na Kakamega msimu uliopita akitokea Tanzania Prisons aliyoachana nayo baada ya kumaliza mkataba.
KMC ambayo imemtambulisha Mwaigaga Jumatano hii kupitia majukwaa yake mitandaoni, imeelezwa kumjumuisha nyota huyo kutokana na kiwango alichokionesha Kakamega.
Mei, mwaka huu Mwaigaga alikuwa ni sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyoenda Saudi Arabia kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Sudan.
Klabu hiyo ya Kinondoni pia imeripotiwa kuwa kwenye vita kali ya kuwania saini ya kipa wa Vipers ya Uganda, Fabien Mutombola kipa wa Burundi ambaye pia anawindwa na KCCA ya Uganda na AFC Leopards ya nchini Kenya.

The post Mwaigaga sasa mali ya KMC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mwaigaga-sasa-mali-ya-kmc/feed/ 0
KMC yaisaka nafasi ya nne kupitia Simba https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/kmc-yaisaka-nafasi-ya-nne-kupitia-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/kmc-yaisaka-nafasi-ya-nne-kupitia-simba/#respond Fri, 24 May 2024 18:55:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11104 Na mwandishi wetuKocha msaidizi wa KMC, John Matambala (pichani) amesema wamejiandaa takriban wiki nzima kwa ajili ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi yao ya kesho Jumamosi dhidi ya Simba ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza kwenye nne bora.Matambala ameeleza hayo leo Ijumaa kuelekea mchezo wao huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha […]

The post KMC yaisaka nafasi ya nne kupitia Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha msaidizi wa KMC, John Matambala (pichani) amesema wamejiandaa takriban wiki nzima kwa ajili ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi yao ya kesho Jumamosi dhidi ya Simba ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza kwenye nne bora.
Matambala ameeleza hayo leo Ijumaa kuelekea mchezo wao huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha akisisitiza kuwa licha ya kubadilishwa kwa uwanja huo dakika za mwisho lakini haijabadili chochote katika azma ya kutafuta matokeo katika mechi hiyo.
“Tumesafiri salama kufika hapa Arusha, maandalizi yako salama na tuko tayari na mchezo wetu wa Simba, maandalizi tumeyafanya zaidi ya wiki nzima sasa, tumepata taarifa ya ghafla kubadilishiwa uwanja na sisi KMC kama wanajeshi baada ya taarifa hiyo tukajipanga haraka tukaja Arusha.

“Mechi ya kwanza na Simba iliisha kwa sare kutokana na kila mmoja kuwa bora upande wake, lakini kiujumla KMC tunauhitaji zaidi mchezo wa kesho kupata pointi maana tunahitaji kupanda juu zaidi, lengo letu ni kumaliza kwenye nne bora, tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini tumejipanga kupambana na Simba,” alisema Matambala.


Naye, kaimu kocha mkuu Simba, Juma Mgunda alisema: “Maandalizi yamekamilika na tumekuja hapa Arusha kutimiza kile tulichokiandaa, hivyo kesho tuko tayari kwa maana ya maandalizi tuliyofanya kwa ajili ya mechi hii muhimu, naamini mechi itakuwa ngumu na ushindani kutokana na mahitaji.
“Sisi tuna mahitaji yetu na wapinzani wana yao, lakini kwa kanuni ya mchezo wa kiungwana lazima umuheshimu mpinzani wako, hivyo tunamheshimu mpinzani wetu lakini niseme maandalizi yote ya kucheza mechi ngumu nzito ya kesho yamekamilika.”
Simba inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi 63 sawa na Azam inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga inahitaji kumaliza ya pili ili kuiwakilisha nchi msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
KMC inayoshika nafasi ya tano kwa pointi 36 ikijiwinda kuipita Coastal Union inayomiliki nafasi ya nne kwa pointi 41 huku ikisalia mechi na mechi mbili kabla ya ligi kumalizika.

The post KMC yaisaka nafasi ya nne kupitia Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/kmc-yaisaka-nafasi-ya-nne-kupitia-simba/feed/ 0
Waziri Jr ataja siri ya mabao yake https://www.greensports.co.tz/2024/03/22/waziri-jr-ataja-siri-ya-mabao-yake/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/22/waziri-jr-ataja-siri-ya-mabao-yake/#respond Fri, 22 Mar 2024 05:37:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10303 Na mwandishi wetuKinara wa mabao kwenye kikosi cha KMC, Wazir Junior amesema siri ya ubora alionao msimu huu ni kutokana na kumsikiliza kwa umakini kocha wake Abdulhamid Moallin.Mshambuliaji huyo ambaye alifunga ‘hat-trick’ timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tabora United na kufikisha jumla ya mabao 11 msimu huu akiwa na Watoza […]

The post Waziri Jr ataja siri ya mabao yake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao kwenye kikosi cha KMC, Wazir Junior amesema siri ya ubora alionao msimu huu ni kutokana na kumsikiliza kwa umakini kocha wake Abdulhamid Moallin.
Mshambuliaji huyo ambaye alifunga ‘hat-trick’ timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tabora United na kufikisha jumla ya mabao 11 msimu huu akiwa na Watoza Ushuru hao wa Manispaa ya Kinondoni.
Waziri Jr ambaye pia ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga alisema amekuwa akifuata kikamilifu mbinu anazopewa na kocha wake na anashukuru Mungu mambo yake yanakwenda vizuri msimu huu.
“Namshukuru kocha Moallin mbinu zake ndio zinanifanya nionekane bora leo lakini ni vyema watu wakajua siri ya ubora nilionao msimu huu unatokana na kusikiliza kwa umakini maelekezo ya kocha na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzangu,” alisema Wazir.
Alisema pamoja na kufikisha mabao ambayo yamemfanya kupnda juu kwenye orodha ya wafungaji, bado hajafikiria kubeba tuzo ya mfungaji bora kutokana na wapinzani anaoshindana nao Feisal Salum wa Azam FC na Stephane Aziz Ki wa Yanga.
Waziri Jr, maarufu kwa jina la King of CCM Kirumba, tangu ajiunge na KMC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Dodoma Jiji amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho.
Mabao ya mshambuliaji huyo yameipandisha timu hiyo kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiwa sasa inapambana kupata nafasi ya kushiriki msimu ujao michuano ya klabu Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

The post Waziri Jr ataja siri ya mabao yake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/22/waziri-jr-ataja-siri-ya-mabao-yake/feed/ 0
Awesu ataka ushindi mechi zilizobaki https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/awesu-ataka-ushindi-mechi-zilizobaki/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/awesu-ataka-ushindi-mechi-zilizobaki/#respond Thu, 21 Mar 2024 19:09:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10292 Na mwandishi wetuNahodha wa timu ya KMC, Awesu Awesu amesema watapambana kuhakikisha wanashinda mechi zao tisa zilizobaki ili kumaliza msimu ndani ya nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu NBC.Alisema kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wamewazidi kete Coastal Union waliowazidi kwa pointi mbili na Tanzania Prisons waliofungana nao kwa pointi.Awesu ambaye yupo kwenye kiwango bora […]

The post Awesu ataka ushindi mechi zilizobaki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa timu ya KMC, Awesu Awesu amesema watapambana kuhakikisha wanashinda mechi zao tisa zilizobaki ili kumaliza msimu ndani ya nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu NBC.
Alisema kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wamewazidi kete Coastal Union waliowazidi kwa pointi mbili na Tanzania Prisons waliofungana nao kwa pointi.
Awesu ambaye yupo kwenye kiwango bora kwa sasa alisema lengo lao kubwa ni kushiriki michuano ya kimataifa kama walivyowahi kufanya katika misimu mitatu nyuma.
“Tumekuwa na msimu bora sana, itapendeza kama tutamaliza ndani ya nne bora ingawa najua vita ni kali lakini tutapambana kwa ajili ya kutimiza lengo letu,” alisema Awesu.
Kiungo huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ alisema mbali na kutaka kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao lakini anaamini timu hiyo itafanya usajili mkubwa zaidi ili msimu ujao wawe miongoni mwa timu zinazowania ubingwa wa ligi kuu.
Alisema anajivunia ubora wa kikosi chao pamoja na uwezo mkubwa alionao chini ya kocha wao, Abdulhamid Moallin ambaye anaonekana kuibadili timu hiyo kwa kiasi kikubwa.
KMC inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 28 sawa na Prisons inayoshika nafasi ya tano huku Coastal iking’ang’ania nafasi ya nne kwa pointi zake 30 baada ya kila timu kushuka dimbani mara 21.

The post Awesu ataka ushindi mechi zilizobaki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/awesu-ataka-ushindi-mechi-zilizobaki/feed/ 0
Bao lampa mzuka Chilunda https://www.greensports.co.tz/2024/02/29/bao-lampa-mzuka-chilunda/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/29/bao-lampa-mzuka-chilunda/#respond Thu, 29 Feb 2024 07:14:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9925 Na mwandishi wetuBaada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya KMC, mshambuliaji Shaban Chilunda amesema bao hilo litamuongezea ari ya kuendelea kupambana na kufunga mechi zijazo.Chilunda ambaye alifunga bao hilo kwenye sare ya 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, alisema kwamba bao hilo limefufua pia matumaini ya kuendelea kung’ara akiwa na uzi wa […]

The post Bao lampa mzuka Chilunda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya KMC, mshambuliaji Shaban Chilunda amesema bao hilo litamuongezea ari ya kuendelea kupambana na kufunga mechi zijazo.
Chilunda ambaye alifunga bao hilo kwenye sare ya 1-1 dhidi ya JKT Tanzania, alisema kwamba bao hilo limefufua pia matumaini ya kuendelea kung’ara akiwa na uzi wa KMC msimu huu.
“Naamini kocha ataendelea kunipa nafasi ili niendeleze hiki ambacho nimekianza, kwa muda mrefu nilikuwa nalisaka bao hili na najisikia furaha kulipata sababu litaniongezea ari ya kujiamini,” alisema Chilunda.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa CD Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania, alisema kwa sapoti anayoipata akiwa na timu hiyo anaamini atarudi kwenye kiwango chake na kuisaidia timu hiyo kufikia malengo.
Chilunda ni miongoni mwa wachezaji walioibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha Akademi ya Azam FC na kupandishwa timu ya wakubwa na baadaye kuuzwa Tenerife kabla ya kutua Simba na sasa KMC.

The post Bao lampa mzuka Chilunda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/29/bao-lampa-mzuka-chilunda/feed/ 0
Kipa KMC aomba radhi https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/kipa-kmc-aomba-radhi/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/kipa-kmc-aomba-radhi/#respond Mon, 19 Feb 2024 07:12:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9803 Na mwandishi wetuKipa namba moja wa KMC, Wilbol Maseke amewaomba radhi mashabiki kwa kitendo cha kumrushia ngumi mchezaji mwenzake, Ibrahim Mao kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.Tukio hilo lilitokea baada ya KMC kufungwa bao la kwanza dakika za mapema kutokana na makosa ya Maseke […]

The post Kipa KMC aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa namba moja wa KMC, Wilbol Maseke amewaomba radhi mashabiki kwa kitendo cha kumrushia ngumi mchezaji mwenzake, Ibrahim Mao kwenye mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Tukio hilo lilitokea baada ya KMC kufungwa bao la kwanza dakika za mapema kutokana na makosa ya Maseke na kumfanya aendelee kufanya makosa mengi ndipo Ibrahim Mao akaenda kumshauri atulie na kusababisha ugomvi huo.
Dakika ya 46, KMC ilifanya mabadiliko ya kipa kwa kumtoa Maseke na nafasi yake ikachukuliwa na Denis Richard katika mchezo huo ulioisha kwa Yanga kutoka uwanjani na ushindi wa mabao 3-0.
Maseke ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuomba radhi kwa kilichotokea kuwa si cha kimichezo baada ya mchezo huo.
“Poleni mashabiki zangu na wanaopenda kazi ninayofanya nikiwa uwanjani, niombe radhi kwa kitendo kilichojitokeza mimi kugombana na mwenzangu.

“Haikuwa kusudio langu, pia baada ya hapo ukweli ni kwamba sikuendelea na ugomvi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo bali yale ni maamuzi ya mwalimu kunitoa na nimeheshimu hilo,” alisema Maseke.


Maseke aliongeza kuwa ana mengi ya kusema ambayo huwa yanaendelea nje ya uwanja ambayo yalisababisha kuharibu saikolojia yake lakini akaomba wamsamehe kwa kilichotokea.

The post Kipa KMC aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/kipa-kmc-aomba-radhi/feed/ 0
KMC hoi, Yanga yainyuka 3-0 https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/kmc-hoi-yanga-yainyuka-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/kmc-hoi-yanga-yainyuka-3-0/#respond Sat, 17 Feb 2024 19:26:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9788 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka KMC mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi 43 katika mechi 16 na kuwaacha mahasimu wake Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti […]

The post KMC hoi, Yanga yainyuka 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka KMC mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi 43 katika mechi 16 na kuwaacha mahasimu wake Simba wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi saba ingawa Simba imecheza mechi 15.
Yanga iliandika bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo lililofungwa na Mudathir Yahya baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la KMC.
Mpira uliozaa bao hilo ulitokana na kosa la kipa wa KMC, Wilbol Maseke aliyejichanganya wakati wa kuokoa na mpira ambao aliupiga vibaya na kumkuta Pacome Zouazoua na hatimaye KMC wakajikuta wakiadhibiwa mapema.
Bao hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza kabla ya Mudathir kuandika bao la pili katika dakika ya 53 safari hii akiitumia pasi ya Nickson Kibabage.
Dakika sita baada ya kupika bao hilo, Kibabage kwa mara nyingine, alimuunganishia pasi, Pacome ambaye aliifungia Yanga bao la tatu na la mwisho kwa timu hiyo.
Yanga katika mechi hiyo ilimtumia mshambuliaji wake mpya Joseph Guede ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Clement Mzize lakini hakuweza kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo baada ya kutoka uwanjani bila ya bao.
Matokeo hayo yanakuwa ni kipigo kingine kikubwa kwa KMC ambao katika mechi ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga, walikubali kichapo cha mabao 5-0.
Katika hali ya kushangaza kipa wa KMC, Maseke alijikuta akipambana na beki wake, Ibrahim Elias kabla ya wawili hao kuamuliwa na wenzao ingawa mwamuzi wa mechi hiyo, Omar Mdoe naye alionekana kuwashangaza baadhi ya mashabiki kwa kutotoa adhabu yoyote kwa wachezaji hao.
Baada ya ushindi huo Yanga sasa inajiandaa kuumana na CR Belouizdad ya Algeria katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

The post KMC hoi, Yanga yainyuka 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/kmc-hoi-yanga-yainyuka-3-0/feed/ 0
Yanga yaifuata KMC Morogoro https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/yanga-yaifuata-kmc-morogoro/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/yanga-yaifuata-kmc-morogoro/#respond Thu, 15 Feb 2024 19:55:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9746 Na mwandishi wetuMsafara wa Yanga uliojumuisha wachezaji 25 na viongozi 11 wa benchi la ufundi upo Morogoro kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC dhidi ya KMC utakaochezwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri.Yanga iliyomaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kukusanya pointi 40 […]

The post Yanga yaifuata KMC Morogoro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Msafara wa Yanga uliojumuisha wachezaji 25 na viongozi 11 wa benchi la ufundi upo Morogoro kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu NBC dhidi ya KMC utakaochezwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Yanga iliyomaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kukusanya pointi 40 katika michezo 15, imedhamiria kushinda mchezo huo dhidi ya KMC ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo.
“Ni mchezo mgumu sana, KMC ni kati ya timu zilizofanya vizuri kwenye mzunguko wa kwanza ndio maana ipo nafasi ya nne, kwa kulijua hilo ndio maana tumekuja na wachezaji wetu wote kuhakikisha ushindi unapatikana,” alisema meneja wa Yanga, Walter Harrison.
Meneja huyo alisema mbali na kutaka ushindi lakini wamepanga kuutumia mchezo huo kama maandalizi ya kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad.
Alisema wachezaji wao wote wakiwemo Abubakar Salum ‘Sure Boy’ na Mahtlas Makudubela ‘Skudu’ wapo fiti na wamejumuishwa kwenye msafara huo na kazi inabaki kwa benchi lao la ufundi kama watahitaji kuwatumia au kuendelea kuwapumzisha.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, timu hiyo ya Jangwani iliibugiza KMC mabao 5-0.

The post Yanga yaifuata KMC Morogoro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/yanga-yaifuata-kmc-morogoro/feed/ 0
Waziri Jr: Kocha ameniamini https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/waziri-jr-kocha-ameniamini/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/waziri-jr-kocha-ameniamini/#respond Sun, 24 Dec 2023 12:50:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9005 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa KMC, Waziri Junior aliyefunga mabao yote mawili kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba jana Jumamosi amesema siri kubwa ya kiwango chake ni kuaminiwa na kocha wao Abdiamin Moallin.Waziri alifunga bao la kuongoza dakika ya 31 kabla ya kufunga bao la kuchomoa dakika ya 88 na kuipa KMC pointi moja […]

The post Waziri Jr: Kocha ameniamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa KMC, Waziri Junior aliyefunga mabao yote mawili kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba jana Jumamosi amesema siri kubwa ya kiwango chake ni kuaminiwa na kocha wao Abdiamin Moallin.
Waziri alifunga bao la kuongoza dakika ya 31 kabla ya kufunga bao la kuchomoa dakika ya 88 na kuipa KMC pointi moja kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
“Unajua kikubwa ni kuwa makini na kazi uwanjani lakini pia kocha amekuwa akinipa mbinu mbalimbali ikiwemo ya kwenye mchezo wa Simba ya kukimbia nyuma ya migongo ya mabeki wa kati na imeonekana nikapata mabao mawili.

“Niseme tu kila kitu ni kocha kwenye kuimarika kwangu msimu huu, maana mwalimu anapokupa nafasi na kukuamnini, unaendelea kupambana, hata ukikosea anakueleza na kukupa nafasi, kwa hiyo siri kubwa ni mwalimu,” alisema Waziri mchezaji wa zamani wa Yanga.


Katika mechi dhidi ya Simba, mabao ya Simba yalifungwa na Saido Ntibazonkiza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 57 na Jean Baleke Baleke kwa kichwa dakika mbili baadaye akimalizia mpira uliopigwa na Shomary Kapombe.

The post Waziri Jr: Kocha ameniamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/waziri-jr-kocha-ameniamini/feed/ 0