Karia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 08 Apr 2025 13:01:58 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Karia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Karia awaahidi ushirikiano MREFA https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/karia-awaahidi-ushirikiano-mrefa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/karia-awaahidi-ushirikiano-mrefa/#respond Sun, 06 Apr 2025 18:54:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13220 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ameahidi kuwapa ushirikiano viongozi wapya wa kamati ya utendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA).Hayo yamo katika taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumapili Aprili 6, 2025 na kusainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Clliford Ndimbo.Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo […]

The post Karia awaahidi ushirikiano MREFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ameahidi kuwapa ushirikiano viongozi wapya wa kamati ya utendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA).
Hayo yamo katika taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumapili Aprili 6, 2025 na kusainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Clliford Ndimbo.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika leo jijini Mbeya ni Elias Mwanjala aliyeshinda nafasi ya uenyekiti na Emmanuel Jacob aliyeibuka kidedea nafasi ya makamu mwenyekiti.
Wengine waliochaguliwa ni Geoofrey Mkumbwa aliyeshinda nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Elisia Mwaipopo na Mohamed Mashango ambao wameshinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.
Karia mbali na kuahidi kuipa ushirikiano kamati hiyo mpya, pia aliwataka wajumbe waliochaguliwa kuhakikisha wanasimamia maendeleo ya mpira wa miguu mkoani Mbeya.

The post Karia awaahidi ushirikiano MREFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/06/karia-awaahidi-ushirikiano-mrefa/feed/ 0
Karia awapongeza viongozi wapya Iringa https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/#respond Tue, 01 Apr 2025 10:52:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13172 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amewapongeza viongozi wapya wa Chama cha Soka Iringa (IRFA) walioachaguliwa hivi karibuni katika mkutano mkuu wa uchaguzi.Katika taarifa iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imewataja viongozi hao kuwa ni Cyprian Kuyava aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti na Joel Musiba (makamu mwenyekiti).Wengine ni […]

The post Karia awapongeza viongozi wapya Iringa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amewapongeza viongozi wapya wa Chama cha Soka Iringa (IRFA) walioachaguliwa hivi karibuni katika mkutano mkuu wa uchaguzi.
Katika taarifa iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imewataja viongozi hao kuwa ni Cyprian Kuyava aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti na Joel Musiba (makamu mwenyekiti).
Wengine ni Abousufian Sillia (mjumbe wa mkutano mkuu), Davis Wapalila, Rehema Mhehe na Victoria Mwenda ambao wamechaguliwa katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji.
Karia amewataka viongozi hao kusimamia maendeleo ya soka mkoani Iringa akiwataka kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa maslahi ya soka la Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Wakati huo huo, TFF imeufungulia Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambao sasa utaruhusiwa kutumiwa kwa ajili ya mechi za ligi baada ya kufanya marekebisho kama ilivyotakiwa kikanuni na sheria za soka.
Uwanja huo ulifungiwa kutokana na miundombinu yake kutokidhi matakwa ya kanuni lakini baada ya kukaguliwa imebainika kuwa marekebisho yaliyofanywa yamekidhi vigezo.
TFF imewasisitiza viongozi wa klabu kuhakikisha wanaboresha mazingira ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja hivyo ili kukidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni.

The post Karia awapongeza viongozi wapya Iringa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/karia-awapongeza-viongozi-wapya-iringa/feed/ 0
Karia awapongeza mabosi wa soka Mara https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/karia-awapongeza-mabosi-wa-soka-mara/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/karia-awapongeza-mabosi-wa-soka-mara/#respond Sun, 02 Mar 2025 09:06:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13070 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameipongeza kamati mpya ya utendaji Chama cha Soka Mara (FAM) iliyochaguliwa kwenye kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni mkoani Mara.Viongozi wapya waliochaguliwa ni Mussa Nyamandege ambaye ameshinda nafasi ya mwenyekiti na Harub Salum ambaye ameshinda nafasi ya makamu mwenyekiti.Wengine waliochaguliwa kupitia uchaguzi […]

The post Karia awapongeza mabosi wa soka Mara first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameipongeza kamati mpya ya utendaji Chama cha Soka Mara (FAM) iliyochaguliwa kwenye kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni mkoani Mara.
Viongozi wapya waliochaguliwa ni Mussa Nyamandege ambaye ameshinda nafasi ya mwenyekiti na Harub Salum ambaye ameshinda nafasi ya makamu mwenyekiti.
Wengine waliochaguliwa kupitia uchaguzi huo na nafasi zao kwenye mabano ni Augustine Mgendi (mjumbe mkutano mkuu TFF) na Hollo CHarles na Paschal Chiganga (wajumbe wa kamati ya utendaji).
Karia ameahidi kuwapa ushirikiano viongozi hao wapya wa FAM na kuwataka wasimamie maendeleo ya mpira wa miguu mkoani Mara.
Wakati huo huo TFF wameufungia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora baada ya kubainika kuwa haukikidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa hii ilieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini kuwa uwanja huo haukidhi matakwa kama ilivyoanishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.
Kutokana na uamuzi huo, timu zote zinazotumia uwanja huo kwa mechi zao za ligi kama uwanja wa nyumbani zitalazimika kutafuta uwanja mwingine kama kanuni zinavyoelekeza.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, uamuzi huo utabaki hivyo hadi uwanja huo utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.
TFF kupitia taarifa hiyo pia imeendelea kuzikumbusha klabu umuhimu wa kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.

The post Karia awapongeza mabosi wa soka Mara first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/karia-awapongeza-mabosi-wa-soka-mara/feed/ 0
Karia awapa pole, Dom Jiji https://www.greensports.co.tz/2025/02/10/karia-awapo-pole-dom-jiji/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/10/karia-awapo-pole-dom-jiji/#respond Mon, 10 Feb 2025 18:23:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12999 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ametuma salamu za pole kwa timu ya Dodoma Jiji baada ya kikosi cha timu hiyo kupata ajali ya gari, leo Jumatatu, Februari 10, 2025.Msafara wa timu hiyo ulipata ajali majira ya saa nne asubuhi eneo la Nangulukuru mkoani Lindi wakati wakitokea Ruangwa kwenye mechi […]

The post Karia awapa pole, Dom Jiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Walace Karia ametuma salamu za pole kwa timu ya Dodoma Jiji baada ya kikosi cha timu hiyo kupata ajali ya gari, leo Jumatatu, Februari 10, 2025.
Msafara wa timu hiyo ulipata ajali majira ya saa nne asubuhi eneo la Nangulukuru mkoani Lindi wakati wakitokea Ruangwa kwenye mechi yao ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa.
Katika salamu hizo zilizotolewa kupitia taarifa ya TFF iliyosainiwa na ofisa habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo, Karia amewatakia heri majeruhi wote wapone na kurejea katika majukumu yao kama kawaida.
Katika ajali hiyo hakuna taarifa yoyote ya kifo iliyotangazwa zaidi ya majeruhi ambao nao inadaiwa hawako katika hali mbaya sana.

The post Karia awapa pole, Dom Jiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/10/karia-awapo-pole-dom-jiji/feed/ 0
Karia ampongeza bosi ARFA https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/karia-ampongeza-mwenyekiti-arfa/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/karia-ampongeza-mwenyekiti-arfa/#respond Sat, 24 Aug 2024 21:11:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11806 Na mwandishi wetuRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Soka Arusha (ARFA). Zakayo Mjema (pichani) kwa kuchaguliwa tena kukiongoza chama hicho.Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumamosi na kusainiwa na ofisa habari wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo ilimnukuu kiongozi huyo wa TFF akisema kuwa ushindi wa Mjema unaonesha imani […]

The post Karia ampongeza bosi ARFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walace Karia amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Soka Arusha (ARFA). Zakayo Mjema (pichani) kwa kuchaguliwa tena kukiongoza chama hicho.
Taarifa ya TFF iliyopatikana leo Jumamosi na kusainiwa na ofisa habari wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo ilimnukuu kiongozi huyo wa TFF akisema kuwa ushindi wa Mjema unaonesha imani ya wajumbe kwake.
Karia alimtaka Mjema ambaye ameshinda katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi wilayani Longido, kuendelea kusimamia vizuri maendeleo ya mpira wa miguu katika mkoa wa Arusha.
Viongozi wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni James Rugangira aliyeshinda nafasi ya makamu mwenyekiti na Joseph Obedi ambaye ameshinda nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa TFF.
Walioshinda nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ni Athanas Sarwat, Siza Masaka, Hawa Msangi na Engineer Owden ambao wote kwa pamoja wataiongoza ARFA kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

The post Karia ampongeza bosi ARFA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/karia-ampongeza-mwenyekiti-arfa/feed/ 0
Karia apongeza mechi za hisani https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/karia-apongeza-mechi-za-hisani/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/karia-apongeza-mechi-za-hisani/#respond Tue, 25 Jun 2024 19:21:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11431 Na mwandishi wetuLicha ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kufurahishwa na mechi za hisani kwa jamii lakini amewataka wadau na wadhamini mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono juhudi hizo.Karia amezungumza hayo baada ya juzi kushuhudia mchezo wa hisani wa Wape Tabasamu uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo Team Job iliyokuwa ikiundwa […]

The post Karia apongeza mechi za hisani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Licha ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kufurahishwa na mechi za hisani kwa jamii lakini amewataka wadau na wadhamini mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono juhudi hizo.
Karia amezungumza hayo baada ya juzi kushuhudia mchezo wa hisani wa Wape Tabasamu uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo Team Job iliyokuwa ikiundwa na Dickson Job iliibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Team Kibwana ya Kibwana Shomari.
“Malengo ambayo yanatakiwa ule mchezo yalifikia maana uwanja ulijaa na wengine wakachangia ambao hawakuja uwanjani, lakini malengo yamefikiwa na niwapongeze wachezaji hawa wamekusanyika kuja kusapoti jambo ambalo ni la jamii.
“Ni kitu kikubwa hicho maana wametumia muda wao wa mapumziko kusapoti jamii kuliko ambavyo kila mmoja angeenda kivyake lakini wameamua kuja kuchangia jamii na walioanzisha hili wazo ni jema na tuwaombee na liende kufanya makubwa walikodhamiria kupeleka,” alisema Karia na kuongeza:
“Kwa hiyo wanachofanya ni jambo jema zaidi, na taasisi mbalimbali ziwadhamini kwenye mikoa mingine waweze kwenda na kurejesha kwa jamii kwa pamoja, kwa hiyo wakati mwingine watu wawadhamini ili wafanye bora zaidi hili jambo kwa jamii.”
Karia pia aliwapongeza wachezaji wengine walioshirikiana kwenye kipindi hiki cha mapumziko kucheza mechi hizo kama vile walivyofanya Feisal Salum na Abdulaziz Makame kule Zanzibar au Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya walipokuwa Mbeya.

The post Karia apongeza mechi za hisani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/karia-apongeza-mechi-za-hisani/feed/ 0
Ligi Kuu NBC kutumia VAR https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/#respond Sun, 17 Dec 2023 16:53:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8903 Na mwandishi wetuImebainika kuwa muda mfupi ujao baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC zitaanza kuamuliwa kwa usaidiziwa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR).Hayo yameelezwa lumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia akifafanua kuwa huo ni uamuzi waShirikisho la Soka Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi yaviwanja.Karia akizungumza kwenye […]

The post Ligi Kuu NBC kutumia VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imebainika kuwa muda mfupi ujao baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC zitaanza kuamuliwa kwa usaidizi
wa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR).
Hayo yameelezwa lumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia akifafanua kuwa huo ni uamuzi waShirikisho la Soka Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi yaviwanja.
Karia akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa TFF unaofanyika Iringa, alisema: “Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni mwendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalamu wameingia jana (juzi) kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye ubora.”
Karia alisema kuwa wanaangalia pia uwezekano wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mchezo wa soka unaendelea kupata mafanikio zaidi nchini.
TFF imeanza mkutano wake huo wa mwaka baada ya kutanguliwa na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika juzi katika Hotel ya Hans Poppe kunakoendelea pia mkutano huo.

The post Ligi Kuu NBC kutumia VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/feed/ 0