Kamungo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 10 Oct 2023 19:15:50 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kamungo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kamungo aitwa timu ya taifa Marekani https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/kamungo-aitwa-timu-ya-taifa-marekani/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/kamungo-aitwa-timu-ya-taifa-marekani/#respond Tue, 10 Oct 2023 19:15:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8040 Na mwandishi wetuRasmi mshambuliaji wa FC Dallas ya Ligi Kuu Marekani, Benard Kamungo (pichani akiwa na Lionel Messi) amejumuishwa juzi kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Marekani kwa vijana chini ya miaka 23.Kamungo, 21 ambaye ni mzaliwa wa Kasulu, Kigoma ametajwa kwenye kikosi hicho cha awali kinachotarajia kushiriki Michezo ya […]

The post Kamungo aitwa timu ya taifa Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rasmi mshambuliaji wa FC Dallas ya Ligi Kuu Marekani, Benard Kamungo (pichani akiwa na Lionel Messi) amejumuishwa juzi kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Marekani kwa vijana chini ya miaka 23.
Kamungo, 21 ambaye ni mzaliwa wa Kasulu, Kigoma ametajwa kwenye kikosi hicho cha awali kinachotarajia kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa, mwakani.
Hiyo imekuja miezi michache tangu mchezaji huyo alipoitwa Juni, mwaka huu kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Algeria lakini alishindwa kutokana na sababu mbalimbali huku mwenyewe akieleza yuko tayari kuitumikia Tanzania kama mambo yatakaa sawa mapema.
Kamungo ambaye anafanya vizuri kwa sasa kwenye mechi za Ligi ya Marekani, aliondoka Kambi ya Nyarugusu, Kigoma na kuhamia Texas mwaka 2016 na familia yake kupitia Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC) kabla ya kujiunga na North Texas mwaka 2021 kisha kutua Dallas mwaka jana.
Akiwa katika mazoezi na kikosi hicho kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Japan na Mexico, Kamungo anapaswa kuonesha uwezo wa juu ili kupata nafasi katika orodha ya mwisho ya kikosi kitakachoiwakilisha Marekani kwenye Michezo ya Olimpiki.

The post Kamungo aitwa timu ya taifa Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/kamungo-aitwa-timu-ya-taifa-marekani/feed/ 0
Kamungo aitamani Taifa Stars https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/kamungo-aitamani-taifa-stars/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/kamungo-aitamani-taifa-stars/#respond Tue, 08 Aug 2023 15:10:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7283 Na mwandishi wetuNyota wa Dallas FC ya Marekani, Bernard Kamungo amesema yuko tayari kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars huku akionesha furaha yake kwa kuifunga timu ya Inter Miami, ambayo Lionel Messi ni nahodha wake.Winga huyo alisema hayo baada ya kugeuka gumzo kufuatia bao alilofunga na kiwango alichoonesha usiku wa kuamkia jana katika […]

The post Kamungo aitamani Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nyota wa Dallas FC ya Marekani, Bernard Kamungo amesema yuko tayari kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars huku akionesha furaha yake kwa kuifunga timu ya Inter Miami, ambayo Lionel Messi ni nahodha wake.
Winga huyo alisema hayo baada ya kugeuka gumzo kufuatia bao alilofunga na kiwango alichoonesha usiku wa kuamkia jana katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Ligi dhidi ya Inter Miami.
Kamungo (pchani juu akiwa na Messi) aliyefunga bao la pili na kuipa Dallas uongozi wa mabao 2-1 hadi mapumziko.
Kamungo pia alielezea furaha yake kwa kufunga mbele ya Messi, nahodha wa Argentina ambaye naye alifunga mabao mawili katika sare ya mabao 4-4 ya dakika 90 za awali kabla ya Dallas kutolewa kwa matuta 5-3.

“Yaani sijui hata niseme vipi kwa sababu pia sikuwahi kufunga bao mbele ya Imani (kaka yake aliyekuwa uwanjani, Uwanja wa Toyota), ilikuwa mara ya kwanza kufunga mbele yake na ilikuwa nimefunga dhidi ya Messi, ni kitu kikubwa,” alisema.


“Timu ya taifa niliitwa mara ya mwisho (dhidi ya Niger) lakini moja ya sababu ya kutoonekana na wengi wanajiuliza ilikuwaje, ilikuwa ni masuala ya pasi ya kusafiria, pasi ilichelewa kidogo ndio maana ikashindikana ila naamini kama kila kitu kitakwenda sawa, mwezi ujao mechi ya Algeria nitakuwepo, ikitegemea na taifa litakavyoamua lakini mimi niko tayari kuitumikia Tanzania,” alisema Kamungo.
Kamungo, 21 anayetajwa kutoka kambi ya wakimbizi Kigoma kabla ya kutimkia Marekani mwaka 2017, alianza soka lake la kulipwa katika klabu ya North Texas inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu Marekani kabla ya kujiunga na Dallas Agosti mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu.

The post Kamungo aitamani Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/08/kamungo-aitamani-taifa-stars/feed/ 0