Kally Ongala - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 15 Jun 2023 15:12:43 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kally Ongala - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Azam yaachana na Kally Ongala https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/azam-yaachana-na-kally-ongala/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/azam-yaachana-na-kally-ongala/#respond Thu, 15 Jun 2023 15:12:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6609 Na mwandishi wetuTimu ya Azam FC imetangaza kuachana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Kali Ongala baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa msimu mmoja.Ongala aliyeanza kazi katika timu hiyo mwanzoni mwa msimu msimu kama kocha wa washambuliaji, baadaye alikaimu nafasi za kocha mkuu huku akiendelea na majukumu yake kabla ya jana kuelezwa ameachana na […]

The post Azam yaachana na Kally Ongala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam FC imetangaza kuachana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Kali Ongala baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa msimu mmoja.
Ongala aliyeanza kazi katika timu hiyo mwanzoni mwa msimu msimu kama kocha wa washambuliaji, baadaye alikaimu nafasi za kocha mkuu huku akiendelea na majukumu yake kabla ya jana kuelezwa ameachana na timu hiyo.
Azam imeeleza hayo leo Alhamisi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikieleza kumshukuru kwa muda wote aliokuwa nao huku ikimtakia heri katika majukumu yake mapya.
Timu hiyo yenye maskani yake Chamazi, Dar es Salaam pia ilitangaza kuachana na wachezaji wawili, mshambuliaji Ismail Aziz ‘Kader’ na kiungo Clephas Mkandala aliyedumu kwa msimu mmoja katika kikosi hicho.
Kader aliyejiunga na timu hiyo tangu msimu wa 2020-21 akitokea Prisons amekuwa akikosa nafasi kutokana na ubora wa wachezaji wanaocheza nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Mkandala aliyejiunga na kikosi hicho akitokea Dodoma Jiji.
Huo umekuwa mwendelezo wa Azam kuisafisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao baada ya juzi pia kuweka wazi kuachana na mchezaji wake mkongwe, Bruce Kangwa aliyedumu kwa miaka saba.
Wengine waliotangazwa kuachana na timu hiyo mpaka sasa ni Rodgers Kola, Kenneth Muguna na aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Dani Cadena.

The post Azam yaachana na Kally Ongala first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/15/azam-yaachana-na-kally-ongala/feed/ 0
Kally ataja siri ya ushindi Azam https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/#respond Tue, 04 Apr 2023 19:02:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5685 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ni wachezaji wake kuutawala mchezo na kufuata vyema maelekezo aliyowapa .Azam jana iliungana na Singida Big Stars kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA (ASFC), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 kwenye Uwanja wa […]

The post Kally ataja siri ya ushindi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema siri ya ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ni wachezaji wake kuutawala mchezo na kufuata vyema maelekezo aliyowapa .
Azam jana iliungana na Singida Big Stars kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA (ASFC), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kocha huyo alikiri kuwa timu yake haikucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini nidhamu iliyooneshwa na wachezaji wake na ushindi walioupata imemfanya ajisikie furaha.

“Tulicheza pungufu kwa dakika 70 lakini nawapongeza wachezaji wangu kwa kuwaheshimu Mtibwa na kucheza kwa nidhamu muda wote wa dakika 90, naamini pamoja na kuwa pungufu lakini tulistahili kushinda,” alisema Kally.


Kocha huyo ameeleza kuwa baada ya ushindi huo wanarudi kwenye uwanja wa mazoezi kuangalia mapungufu yao ili kuyarekebisha na kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao lengo likiwa ni kufanya vizuri na kusonga hatua inayofuata.
Alisema anatambua kuwa hatua inayofuata itakuwa ngumu zaidi lakini dhamira yao msimu huu ni kuwa mabingwa wa Kombe la FA hivyo watajipanga vizuri na kurekebisha mapungufu yao ili kushinda mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameeleza kuwa kipigo walichokipata kutoka kwa wapinzani wao kimetokana na makosa ambayo waliyafanya ikiwemo kushindwa kutumia faida ya wapinzani wao kuwa pungufu uwanjani.
“Tumepoteza mchezo kwa uzembe wetu wenyewe, tulifanya makosa wenzetu wameyatumia, lakini hata sisi tulitengeneza nafasi tukashindwa kuzitumia kitu ambacho kimetugharimu na kujikuta tunatolewa kwenye mashindano,” alisema Mayanga.
Kocha huyo ameeleza kuwa wamekubali matokeo na wanarudi kujipanga kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya mwaka ujao .

The post Kally ataja siri ya ushindi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/04/kally-ataja-siri-ya-ushindi-azam/feed/ 0