Julio - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 13 Mar 2024 18:49:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Julio - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Julio akabidhiwa mikoba Singida https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/julio-akabidhiwa-mikoba-singida/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/julio-akabidhiwa-mikoba-singida/#respond Wed, 13 Mar 2024 18:49:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10174 Na mwandishi wetuKlabu ya Singida Fountain Gate FC leo Jumatano imemtambulisha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, John Kadutu alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho kilipokuwa chini ya Thabo Senong na msaidizi wake, Nizar Khalfan.“Tumempa mkataba wa muda […]

The post Julio akabidhiwa mikoba Singida first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Singida Fountain Gate FC leo Jumatano imemtambulisha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, John Kadutu alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho kilipokuwa chini ya Thabo Senong na msaidizi wake, Nizar Khalfan.
“Tumempa mkataba wa muda mfupi Julio hadi mwisho wa msimu huu ili kuangalia mwenendo wa timu katika mechi 10 zilizobaki kabla ya msimu kumalizika baada ya hapo kama tutafanikiwa kubaki lgi kuu tutampa mkataba mrefu pamoja na kufanya usajili wa nguvu kuimarisha kikosi chetu,” alisema Kadutu.
Kiongozi huyo alisema mbali ya Julio, pia imembakisha Ngawina Ngawina katika nafasi ya kocha msaidizi na pia wamemchukua Ally Mustapha ‘Bartherz’ kuwa kocha wao wa makipa.
Kadutu alisema wana imani kubwa na Julio kutokana na uzoefu wake kwenye Ligi Kuu NBC na kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya waliyokuwa wakiyapata tangu mwanzo wa mwaka huu.
Kiongozi huyo alisema kwamba wanaamini mchezo ujao dhidi ya Namungo FC watapata ushindi wao wa kwanza.
Singida FG ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 21 katika mechi zake 20 ilizoshuka dimbani mpaka sasa.

The post Julio akabidhiwa mikoba Singida first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/julio-akabidhiwa-mikoba-singida/feed/ 0
Julio ajipa matumaini KMC https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/julio-ajipa-matumaini-kmc/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/julio-ajipa-matumaini-kmc/#respond Wed, 14 Jun 2023 14:03:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6592 Na mwandishi wetuLicha ya KMC kulala kwa mabao 2-1 mbele ya Mbeya City jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema bado wana imani ya kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano.KMC ilipokea kipigo hicho kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuwania kutoshuka daraja na kuendelea kushiriki Ligi Kuu NBC msimu ujao. Mechi […]

The post Julio ajipa matumaini KMC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Licha ya KMC kulala kwa mabao 2-1 mbele ya Mbeya City jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema bado wana imani ya kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano.
KMC ilipokea kipigo hicho kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuwania kutoshuka daraja na kuendelea kushiriki Ligi Kuu NBC msimu ujao. Mechi ya marudiano itapigwa Dar es Salaam Juni 16, mwaka huu.
Julio alisema anawapongeza vijana wake kwa kupambana kutafuta ushindi lakini walifungwa na kwa matokeo hayo yanampa matumaini ya kupata ushindi kwenye mchezo wa pili na kusalia ligi kuu.

“Mechi hizi ni ngumu sababu wote tunataka kujinusuru na kusalia ligi kuu, nimekubali tumefungwa na goli moja tulilolipata tutalitumia vizuri kutafuta faida kubwa tukiwa nyumbani. Vijana wamepambana, wameonesha kuna jambo wanalitafuta na sasa tunakwenda kujipanga vizuri nyumbani,” alisema Julio.


Naye Kocha Mkuu wa Mbeya City, Abdallah Mubiru alisema: “Tulikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi lakini imeshindikana, kikubwa tumepata ushindi na sasa tunajipanga kuhakikisha tunaulinda ushindi wetu na kutafuta matokeo mazuri zaidi.”

The post Julio ajipa matumaini KMC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/14/julio-ajipa-matumaini-kmc/feed/ 0
Julio: Hatuna cha kuogopa https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/julio-hatuna-cha-kuogopa/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/julio-hatuna-cha-kuogopa/#respond Sat, 13 May 2023 20:20:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6153 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa KMC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema hawaihofii timu yoyote na watahakikisha mechi mbili zilizosalia wanazitumia sawasawa kusalia Ligi Kuu NBC msimu ujao.Julio ameyasema hayo baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars na kufikisha pointi 29 zilizowatoa nafasi ya 14 mpaka ya 12.Hiyo ni mechi […]

The post Julio: Hatuna cha kuogopa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa KMC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema hawaihofii timu yoyote na watahakikisha mechi mbili zilizosalia wanazitumia sawasawa kusalia Ligi Kuu NBC msimu ujao.
Julio ameyasema hayo baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars na kufikisha pointi 29 zilizowatoa nafasi ya 14 mpaka ya 12.
Hiyo ni mechi ya pili kwa Julio tangu akabidhiwe timu hiyo wiki nne zilizopita akirithi mikoba ya Thierry Hitimana, mechi ya kwanza alipoteza dhidi ya Dodoma Jiji kwa bao 1-0 kabla ya kuifunga Singida Big kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
“Nimewaeleza kwamba haijaisha mpaka iishe, tulifungwa na Dodoma, tumeshinda na Singida, bado tuna mechi mbili mkononi dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons ambao wapo kama sisi, kwa hiyo tutahakikisha tunapambana tuone nani aliyejipanga vizuri na kupata ushindi.

“Hatuna mtu wa kumuogopa, huu ni mpira na kwenye mpira kikubwa ni kujipanga na kushindana, wapo kwao na sisi tutatoka kwetu kwenda kushindana, atakayekuwa na bahati ambaye naamini ni mimi tutashinda mechi,” alisema Julio.


Mbeya City iliyo nafasi ya 14 na pointi 27 inapambana isishuke daraja ikiwa imebakiza mechi tatu kama Prisons wanaoshika nafasi ya tisa kwa pointi 31 lakini wakihitaji ushindi waepuke kwenda chini na kucheza mechi za mtoano kuwania kusalia kwenye ligi msimu ujao.

The post Julio: Hatuna cha kuogopa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/julio-hatuna-cha-kuogopa/feed/ 0
Mechi tatu kuibakisha KMC ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/mechi-tatu-kuibakisha-kmc-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/mechi-tatu-kuibakisha-kmc-ligi-kuu/#respond Fri, 28 Apr 2023 18:46:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5967 Na mwandishi wetuTimu ya KMC imesema bado ina matumaini ya kubaki kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao huku ikipigia hesabu mechi tatu walizobakiza kuwa watapambana kufa au kupona.Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema licha ya kufanya vibaya katika mechi zilizopita hawapaswi kukata tamaa hadi mechi ya mwisho.Alisema […]

The post Mechi tatu kuibakisha KMC ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya KMC imesema bado ina matumaini ya kubaki kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao huku ikipigia hesabu mechi tatu walizobakiza kuwa watapambana kufa au kupona.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema licha ya kufanya vibaya katika mechi zilizopita hawapaswi kukata tamaa hadi mechi ya mwisho.
Alisema wana imani kwa maandalizi mazuri ya kikosi chao kuelekea katika mechi tatu za lama salama watashinda na kujiweka mazingira mazuri ya kubaki salama.
“Tunajua tuko katika nafasi ambayo si nzuri lakini bado hatujapoteza matumaini, tunasema haijaisha mpaka mechi ya mwisho,” alisema na kuongeza kuwa timu imejipanga kupambana.
KMC inashika nafasi ya 14 kwa pointi 26 baada ya kucheza michezo 27, kushinda sita, sare nane na kupoteza michezo 13.
Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hiyo, wameshinda mmoja na kupoteza michezo minne huku ikiwa imebakiza mechi dhidi ya Singida Big Stars, Tanzania Prisons na Mbeya City kabla ya kufungwa pazia la ligi msimu huu.
Mwenendo mbaya wa timu hiyo ulimwondosha aliyekuwa kocha wao, Thiery Hitimana na kikosi hicho kukabidhiwa Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye ana kazi ya kuhakikisha timu hiyo inabaki salama.

The post Mechi tatu kuibakisha KMC ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/28/mechi-tatu-kuibakisha-kmc-ligi-kuu/feed/ 0
Julio azipa tano Yanga, Simba https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/julio-azipa-tano-yanga-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/julio-azipa-tano-yanga-simba/#respond Wed, 26 Apr 2023 14:37:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5933 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa KMC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amezipongeza timu za Simba na Yanga kwa hatua walizofika kwenye michuano ya klabu Afrika.Timu hizo zimeonesha kiwango kikubwa kwenye mechi za robo fainali za michuano wanayoshiriki zikiwa tayari zimeshinda mechi zao kwanza za hatua hiyo kabla ya za marudiano zitakazopigwa Ijumaa na Jumapili hii.Simba ikiwa nyumbani […]

The post Julio azipa tano Yanga, Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa KMC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amezipongeza timu za Simba na Yanga kwa hatua walizofika kwenye michuano ya klabu Afrika.
Timu hizo zimeonesha kiwango kikubwa kwenye mechi za robo fainali za michuano wanayoshiriki zikiwa tayari zimeshinda mechi zao kwanza za hatua hiyo kabla ya za marudiano zitakazopigwa Ijumaa na Jumapili hii.
Simba ikiwa nyumbani iliwachapa bao 1-0 mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ugenini kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Julio alisema timu zote zimefanya kazi kubwa, Simba wameshinda nyumbani lakini Yanga wao wamepata ushindi ugenini ambako mara ya kwanza walipoteza, kama kocha alishangilia ushindi kwa sababu ya Utanzania wake.
“Watu walishangaa kwa nini nilishangilia, mimi nilikuwa namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Philip Mpango lakini pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao kwa pamoja wametoa sapoti kubwa kwenye michezo,” alisema Julio.

“Naamini Simba wataenda kufanya kama ilivyotokea kwa Zamalek ambapo walishinda 1-0 nyumbani lakini wakapoteza 1-0 Misri tukawatoa kwa penalti baada ya kipa Juma Kaseja kuokoa penalti mbili zilizoivusha timu hatua inayofuata,” alisema Julio.


Alisema anampongeza mwekezaji wa Simba Mohamed Dewji kwa kazi kubwa aliyoifanya hata kama kuna mapungufu ya kibinadamu kwani kwenye ubora wa Simba amechangia kiasi kikubwa kufika pale ilipo.
“Lakini pia nimpongeze Ghalib Mohamed na Rais wa Yanga, Hersi Said wamefanya kazi kubwa kuitoa Yanga ilikokuwa kwa kufanya usajili bora na kuitengeneza timu ya ushindani ambayo inawafurahisha Watanzania wote hadi Rais Samia,” alisema Julio.
Simba itacheza keshokutwa Ijumaa dhidi ya Wydad kwenye Uwanja wa Mohamed V, jijini Casablanca wakati Yanga itakuwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumapili hii kuvaana na Rivers.

The post Julio azipa tano Yanga, Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/26/julio-azipa-tano-yanga-simba/feed/ 0