John Bocco - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 Sep 2023 11:39:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg John Bocco - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bocco kulipwa Sh 200 milioni https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/#respond Sat, 09 Sep 2023 11:39:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7703 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa timu ya Simba, John Bocco anatarajia kulipwa Sh Milioni 200 baada ya Mahakama Kuu Tanzania kuitaka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Princess Leisure kumlipa mchezaji huyo kiasi hicho cha fedha.Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba na mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatakiwa kulipwa kiasi hicho […]

The post Bocco kulipwa Sh 200 milioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa timu ya Simba, John Bocco anatarajia kulipwa Sh Milioni 200 baada ya Mahakama Kuu Tanzania kuitaka kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Princess Leisure kumlipa mchezaji huyo kiasi hicho cha fedha.
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba na mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kampuni hiyo kutumia picha zake katika matangazo yao.
Hukumu hiyo ilitolewa Agosti 31 na Jaji Irvin Mugeta iliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha licha ya kuwa katika madai ya awali, Bocco alitaka alipwe Sh bilioni 1 kama fidia ya kutumia picha hizo bila ya makubaliano.
Bocco aliyewakilishwa na mawakili Innocent Michael na Gadi Kabele, katika madai yake alidai kwamba kitendo cha kampuni hiyo kutumia picha yake kilimaanisha kwamba alivunja mkataba na klabu ya Simba ambayo ilijiandaa kumchukulia hatua za kinidhamu.
Mchezaji huyo pia alidai kwamba hakuwahi kuipa idhini kampuni hiyo kutumia picha yake na hawakuwa na makubaliano katika jambo hilo.
Jaji Mugeta wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alihitimisha kwa kuitaka kampuni hiyo kumlipa fidia mchezaji huyo.
Baadhi ya picha zilizotumika na kuonekana katika mtandao wa Instagram ni ile iliyokuwa na tangazo lililowakumbusha mashabiki kuhusu uhondo wa Ligi Kuu NBC.
Tangu kutolewa kwa hukumu hiyo na habari kusambaa kwenye vyanzo mbalimbali vya habari, imesababisha kuibuka kwa mjadala kuhusu hakimiliki na matumizi sahihi ya picha za wanamichezo na wasanii pale picha hizo zinapotumika kibiashara.

The post Bocco kulipwa Sh 200 milioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/09/bocco-kulipwa-sh-200-milioni/feed/ 0
Bocco awaangukia mashabiki https://www.greensports.co.tz/2023/02/22/bocco-awaangukia-mashabiki/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/22/bocco-awaangukia-mashabiki/#respond Wed, 22 Feb 2023 20:16:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5263 Na mwandishi wetuNahodha wa Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono kipindi hiki ambacho timu yao inapitia wakati mgumu wa kukosa matokeo.Simba haijapata ushindi katika michezo mitatu mfululizo, kati ya hiyo miwili ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC na Raja Casablanca kabla ya jana Jumanne kupata sare […]

The post Bocco awaangukia mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono kipindi hiki ambacho timu yao inapitia wakati mgumu wa kukosa matokeo.
Simba haijapata ushindi katika michezo mitatu mfululizo, kati ya hiyo miwili ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC na Raja Casablanca kabla ya jana Jumanne kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam kwenye Ligi Kuu NBC.
Bocco alikiri mambo kuwa magumu kwao lakini kingine kinachosababisha hilo ni uchovu uliotokana na kucheza mechi ngumu bila kupata muda wa kupumzika.

“Tunaomba mashabiki wetu watuvumilie, ni matokeo mabaya ambayo hatujayatarajia lakini hizi ni nyakati ambazo timu yoyote inaweza kuikuta lakini naamini yatapita na timu itarudi kwenye uwezo wake uliozoeleka,” alisema Bocco.


Mshambuliaji huyo ameeleza kuwa matokeo wanayoyapata hata yeye na wachezaji wenzake hawafurahishwi nayo lakini wanajitahidi kupambana kuepuka mwenendo huo mbaya kwenye mashindano yote.
Kuhusu ubingwa, nahodha huyo alisema bado wana nafasi ya kubeba taji hilo la ligi msimu huu ingawa wanalazimika kushinda mechi zao saba zilizobaki na kuwaombea mabaya watani zao Yanga kwenye mechi zilizosalia.

The post Bocco awaangukia mashabiki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/22/bocco-awaangukia-mashabiki/feed/ 0
Bocco awafagilia kina Baleke https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/bocco-awafagilia-kina-baleke/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/bocco-awafagilia-kina-baleke/#respond Thu, 26 Jan 2023 20:21:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4871 Na mwandishi wetuNahodha wa Simba, John Bocco amesema ana imani kubwa na wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni na timu hiyo kwamba watawasaidia kufikia malengo yao msimu huu.Kauli ya nahodha huyo inakuja kutokana na viwango vinavyooneshwa na wachezaji hao katika mechi za ligi ambazo wameshacheza hadi sasa.Katika dirisha la usajili la Januari lililofungwa hivi karibuni, Wekundu […]

The post Bocco awafagilia kina Baleke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Simba, John Bocco amesema ana imani kubwa na wachezaji wapya waliosajiliwa hivi karibuni na timu hiyo kwamba watawasaidia kufikia malengo yao msimu huu.
Kauli ya nahodha huyo inakuja kutokana na viwango vinavyooneshwa na wachezaji hao katika mechi za ligi ambazo wameshacheza hadi sasa.
Katika dirisha la usajili la Januari lililofungwa hivi karibuni, Wekundu hao waliwasajili wachezaji wanne ambao ni Saido Ntibazonkiza, Ismail Sawadogo, Jean Baleke na Mohammed Mussa.
Bocco ameeleza kuwa kwa muda mfupi tangu wachezaji hao wajiunge na timu hiyo wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chao ikiwemo kuwasaidia kuwapa ushindi katika baadhi ya mechi za ligi.

“Angalia Ntibazonkiza na Baleke wote wameshafunga mabao ambayo yameipa timu pointi tatu lakini Sawadogo alicheza vizuri kwenye mechi dhidi ya Dodoma Jiji, naamini uwepo wao utatusaidia kufikia malengo ambayo tumekusudia kuyafikia msimu huu,” alisema Bocco.


Mshambuliaji huyo anayeshika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye kikosi cha timu hiyo msimu huu ameeleza kuwa kasi waliyoanza nayo wachezaji hao inaendana na matarajio yao hasa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo lengo lao ni kufika nusu fainali.
Bocco alisema kitu cha msingi ni kuendelea kuwapa ushirikiano wachezaji hao ili waweze kuzowea mapema mazingira ya timu ikiwemo mifumo na hatimaye kutoa mchango mkubwa zaidi ya ule wanaoutoa hivi sasa.

The post Bocco awafagilia kina Baleke first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/26/bocco-awafagilia-kina-baleke/feed/ 0