inonga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 25 Jun 2024 06:37:10 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg inonga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Inonga naye aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/inonga-naye-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/inonga-naye-aachwa-simba/#respond Tue, 25 Jun 2024 06:37:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11418 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imetangaza kuachana na beki wake wa kati, Henock Inonga Bacca baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo.Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo iliweka wazi uamuzi huo na kumtakia kila la heri beki huyo ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya DR Congo.Inonga anakuwa […]

The post Inonga naye aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imetangaza kuachana na beki wake wa kati, Henock Inonga Bacca baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo.
Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo iliweka wazi uamuzi huo na kumtakia kila la heri beki huyo ambaye pia ni beki wa timu ya taifa ya DR Congo.
Inonga anakuwa mchezaji mwingine kuachwa na uongozi wa Simba katika siku za hivi karibuni baada ya kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye ni raia wa Burundi.
Inonga atakumbukwa kwa namna ambavyo ametoa mchango mkubwa kwa timu hiyo hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali mara tatu.
Uamuzi huo ni katika mikakati ya uongozi wa Simba kukisuka upya kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa 2024-25 baada ya kutoridhishwa kwa ujumla na mwenendo wa timu yao katika msimu wa 2023-24.
Simba imemaliza msimu wa 2023-24 ikiwa nafasi ya tatu katika Ligi Kuu NBC pamoja na kufikia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa inajiandaa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao wa 2024-25.

The post Inonga naye aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/inonga-naye-aachwa-simba/feed/ 0
Majeruhi Inonga aitwa timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/majeruhi-inonga-aitwa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/majeruhi-inonga-aitwa-timu-ya-taifa/#respond Wed, 04 Oct 2023 20:19:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7952 Na mwandishi wetuBeki wa Simba, Henock Inonga ambaye kwa sasa ni majeruhi, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kinachojiandaa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya New Zealand na Angola.Inonga amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 26 kinachoundwa na kundi kubwa la nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika lakini […]

The post Majeruhi Inonga aitwa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki wa Simba, Henock Inonga ambaye kwa sasa ni majeruhi, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kinachojiandaa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya New Zealand na Angola.
Inonga amejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 26 kinachoundwa na kundi kubwa la nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika lakini imestaajabisha kuona kocha wa timu hiyo, Sebastien Desabre akiwatema nyota wa Brentford ya England, Yoane Wissa na Jordan Ikoko wa Pafos ya Cyprus.
Inonga alipata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union wiki mbili zilizopita na kushindwa kuitumikia timu hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Wachezaji wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni makipa Lionel Mpasi, Dimitry Bertaud na Baggio Siadi wakati mabeki ni Brian Bayeye, Gedeon Kalulu, Dylan Batubinska, Inonga, Chancel Mbemba, Arthur Masuaku, Rocky Bushiri na Joris Kayembe.
Eneo la kiungo, kuna Aaron Tshibola, Edo Kayembe, Samuel Moutousammy, Elia Meschack, Joel Kakuta, William Balikwisha, Theo Bongonda, Charles Pickel na Grady Diangana.
Na Washambuliaji walioitwa ni Fiston Mayele, Bakambu, Jackson Muleka, Ben Malango, Silas Katompa na Simon Banza.

The post Majeruhi Inonga aitwa timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/04/majeruhi-inonga-aitwa-timu-ya-taifa/feed/ 0
Inonga kuwakosa Dynamos https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/inonga-kuwakosa-dynamos/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/inonga-kuwakosa-dynamos/#respond Wed, 27 Sep 2023 19:37:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7875 Na mwandishi wetuMeneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally ameeleza kuwa beki wao wa kati, Henock Inonga ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Oktoba Mosi, mwaka huu.Ameeleza kuwa Inonga ataendelea kusalia nje ya uwanja kwa takriban siku 10 zaidi akiuguza […]

The post Inonga kuwakosa Dynamos first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally ameeleza kuwa beki wao wa kati, Henock Inonga ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Oktoba Mosi, mwaka huu.
Ameeleza kuwa Inonga ataendelea kusalia nje ya uwanja kwa takriban siku 10 zaidi akiuguza jeraha lake la mguu wa kulia alilolipata kwenye mchezo wao dhidi ya Coastal Union uliopigwa wiki iliyopita.
Wengine wataokosa mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kipa Aishi Manula anayetarajia kurejea dimbani Oktoba, mwaka huu na Aubin Kramo anayeendelea kupatiwa matibabu.

“Tunafahamu mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, wote mliona namna walivyotusumbua lakini wanakuja nyumbani Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama na hicho ndicho watakutana nacho,” alisema Ally.


Alisema anaamini wataingia hatua ya makundi na hilo ni jambo la kawaida kwao, kwani wameshaingia zaidi ya mara tatu na kuishia hatua ya robo fainali kwenye miaka mitano iliyopita.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, Dynamos inatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi majira ya saa 12 jioni huku waamuzi wa mtanange huo wakitarajiwa kutua nchini Septemba 30, mwaka huu.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya mabao 2-2.

The post Inonga kuwakosa Dynamos first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/inonga-kuwakosa-dynamos/feed/ 0
Aliyemuumiza Inonga aomba radhi https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/aliyemuumiza-inonga-aomba-radhi/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/aliyemuumiza-inonga-aomba-radhi/#respond Sat, 23 Sep 2023 13:17:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7832 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Coastal Union, Hija Ugando ameomba radhi kwa kitendo cha kumchezea vibaya beki wa kati wa Simba SC, Henock Inonga kwenye mechi iliyopigwa Alhamisi hii Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Katika tukio hilo lililotokea dakika ya 19 ya mchezo huo ulioisha kwa Simba kushinda mabao 3-0, Ugando alipewa kadi nyekundu na Inonga […]

The post Aliyemuumiza Inonga aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Coastal Union, Hija Ugando ameomba radhi kwa kitendo cha kumchezea vibaya beki wa kati wa Simba SC, Henock Inonga kwenye mechi iliyopigwa Alhamisi hii Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika tukio hilo lililotokea dakika ya 19 ya mchezo huo ulioisha kwa Simba kushinda mabao 3-0, Ugando alipewa kadi nyekundu na Inonga kukimbizwa hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata.
“Natanguliza samahani sababu kila muungwana anapovuliwa nguo huchutama, binafsi sikutegemea wala sikuwahi kufanya kitendo hicho kabla. Imeniumiza na kunisikitisha sana, naomba radhi sababu mimi si muumini wa kufanya vitendo vibaya uwanjani,” alisema Ugando.
Pia imeelezwa kuwa beki huyo amesharuhusiwa kutoka hospitali kwani amepatwa na kidonda ambacho ameshonwa nyuzi 13 tofauti na ilivyodhaniwa kuwa amevunjika.

“Inonga hajavunjika, amepata kidonda pale ambapo alikanyagwa na ameshapatiwa matibabu kutoka Hospitali ya Temeke na sasa ameruhusiwa kurejea kwake, anaendelea kuuguza kidonda na tunashukuru Mungu kuona hajavunjika,” alisema Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally.


Ofisa huyo alifafanua kuwa Inonga atakaa nje kwa wiki chache kabla ya kuruhusiwa kuanza mazoezi na wenzake ikitegemeana na maendeleo ya kidonda hicho.

The post Aliyemuumiza Inonga aomba radhi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/23/aliyemuumiza-inonga-aomba-radhi/feed/ 0
Inonga arejea kikosini Simba https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/inonga-arejea-kikosini-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/inonga-arejea-kikosini-simba/#respond Fri, 01 Sep 2023 20:34:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7640 Na mwandishi wetuWachezaji wa Simba wa kimataifa Henock Inonga na Aubin Kramo waliokuwa majeruhi wamerejea kwenye kikosi hicho tayari kwa mashindano yaliyoko mbele yao.Inonga aliumia katika michuano ya Ngao ya Jamii mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Big Stars na kukosa mchezo wa fainali dhidi ya Yanga na michezo miwili ya Ligi Kuu NBC.Kramo […]

The post Inonga arejea kikosini Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji wa Simba wa kimataifa Henock Inonga na Aubin Kramo waliokuwa majeruhi wamerejea kwenye kikosi hicho tayari kwa mashindano yaliyoko mbele yao.
Inonga aliumia katika michuano ya Ngao ya Jamii mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Big Stars na kukosa mchezo wa fainali dhidi ya Yanga na michezo miwili ya Ligi Kuu NBC.
Kramo ambaye hakuwahi kupata nafasi ya kuitumikia Simba tangu kusajiliwa kwake msimu huu ambapo awali ilielezwa anasumbuliwa na kuumwa mara kwa mara, sasa mambo yanakwenda vizuri.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alithibitisha kurejea kwa wachezaji hao na tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mashindano yote yaliyoko mbele yao.
“Wachezaji wetu wote majeruhi wamepona, Inonga alipewa wiki mbili za mapumziko na Kramo alipewa wiki moja baada ya majeraha aliyoyapata, sasa wameshapona na wamerejea kikosini,” alisema.
Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaochezwa ugenini Zambia Septemba 16, mwaka huu hivyo kurejea kwa wachezaji hao kunarejesha matumaini ya timu hiyo kuelekea katika mechi hizo.

The post Inonga arejea kikosini Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/inonga-arejea-kikosini-simba/feed/ 0
Inonga nje wiki mbili https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/inonga-nje-wiki-mbili/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/inonga-nje-wiki-mbili/#respond Wed, 16 Aug 2023 18:55:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7416 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imesema kuwa beki wa kati wa timu hiyo, Henock Inonga atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili sawa na siku 14 akiuguza jeraha lake la bega.Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo alifafanua kuwa mchezaji huyo hajapata majeraha makubwa kama ilivyodhaniwa baada ya kuumia kwenye mechi ya Ngao […]

The post Inonga nje wiki mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imesema kuwa beki wa kati wa timu hiyo, Henock Inonga atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili sawa na siku 14 akiuguza jeraha lake la bega.
Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo alifafanua kuwa mchezaji huyo hajapata majeraha makubwa kama ilivyodhaniwa baada ya kuumia kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate iliyopigwa wiki iliyopita, hivyo atakaa nje kwa muda huo kisha atarejea kazini.
“Kulingana na vipimo baada ya kumchunguza zaidi, imeonekana Inonga hajapata madhara makubwa kama ambavyo pengine ilihisiwa, hivyo atakaa nje akiuguza jeraha hilo ili kuwa kamili kabisa kabla ya kurejea uwanjani rasmi,” alisema Kagabo.
Inonga aliumia kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kukosekana kwenye mechi ya fainali ya Ngao ambapo Simba walishinda kwa matuta 3-1 baada ya suluhu ya dakika 90 za kawaida.
Beki huyo ataukosa pia mchezo wa awali wa Ligi Kuu NBC wa kesho ambapo Simba itaanza ligi kwa kuumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro kuanzia saa 10 jioni.

The post Inonga nje wiki mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/16/inonga-nje-wiki-mbili/feed/ 0
Mayele, Inonga waitwa DR Congo https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/#respond Tue, 30 May 2023 19:44:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6382 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre ameita kikosi chake akiwajumuisha Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba kwa ajili ya kuivaa Gabon katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023.Mayele anaitwa kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kiwango anachoendelea kukionesha kwenye michuano inayoshiriki Yanga […]

The post Mayele, Inonga waitwa DR Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre ameita kikosi chake akiwajumuisha Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba kwa ajili ya kuivaa Gabon katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023.
Mayele anaitwa kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kiwango anachoendelea kukionesha kwenye michuano inayoshiriki Yanga ikiwemo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambako mchezaji huyo anaongoza kwa mabao saba.


Na licha ya Simba kushindwa kutwaa taji lolote msimu huu lakini kiwango cha Inonga kimeendelea kung’ara na kumshawishi Desbare kumwita kwenye kikosi hicho chenye wachezaji 27.
Kabla ya kuivaa Gabon Juni 18, DR Congo itacheza na Uganda mechi ya kirafiki itakayopigwa Juni 14, mwaka huu mjini Douala, Cameroon.
Congo inahitaji ushindi dhidi ya Gabon ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya Kundi I ambako inaburuza mkia kwa pointi nne baada ya mechi nne ikiwa imeshinda mchezo mmoja, sare moja na kufungwa mara mbili.
Pia, Congo ikiwa ugenini Uwanja wa Franceville, mjini Franceville itahitaji ushindi kulipa kisasi kwa Gabon iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi iliyopita iliyopigwa Uwanja wa Martyrs, Kinshasa, DR Congo.
Mara ya mwisho, Chui hao kushiriki michuano ya Afcon ilikuwa mwaka 2019 walipopangwa kundi moja na Misri, Zimbabwe na Uganda ambapo Desabre ndiye aliyekuwa kocha wao wakati huo.

The post Mayele, Inonga waitwa DR Congo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mayele-inonga-waitwa-dr-congo/feed/ 0
Manula, Inonga wapo fiti https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/#respond Tue, 11 Apr 2023 12:21:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5756 Na mwandishi wetuRipoti ya matibabu ya wachezaji wa Simba, kipa Aishi Manula (pichani) na beki Henock Inonga imeondoa hofu kuhusu kuumia kwa wachezaji hao ikieleza kuwa wanaendelea vizuri, watajiunga na wenzao mazoezini.Wachezaji hao walishindwa kumaliza dakika 90 katika mechi ya robo fainali Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu ambapo Simba ilishinda kwa mabao 5-1 […]

The post Manula, Inonga wapo fiti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ripoti ya matibabu ya wachezaji wa Simba, kipa Aishi Manula (pichani) na beki Henock Inonga imeondoa hofu kuhusu kuumia kwa wachezaji hao ikieleza kuwa wanaendelea vizuri, watajiunga na wenzao mazoezini.
Wachezaji hao walishindwa kumaliza dakika 90 katika mechi ya robo fainali Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu ambapo Simba ilishinda kwa mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Daktari mkuu wa Simba, Edwin Kagoba alisema kuwa wachezaji hao waliumia lakini baada ya kuwapeleka hospitali na kuwafanyia vipimo wamebaini maumivu waliyopata ni ya kawaida.

“Siku ya pili baada ya mchezo tuliwapeleka Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi na majibu yalipotoka juzi, yamebaini wana maumivu ya kawaida, tumewapa mapumziko ya siku tatu, timu itakaporudi kutoka Mbeya wataungana na wenzao kuendelea na mazoezi,” alisema Kagoba.


Taarifa hiyo imerudisha furaha na tabasamu kwa benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiyo hasa ukizingatia mchango wa wachezaji hao kwenye kikosi cha Simba na ugumu wa mashindano yanayowakabili kwa sasa.
Simba ipo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa watetezi Wydad Casablanca.
Kwenye Ligi Kuu NBC inaendelea kupambana, ipo nafasi ya pili ikipambana kurudisha taji hilo ambalo walilibeba kwa misimu minne mfulululizo kabla ya msimu uliopita kuporwa na mahasimu wao Yanga.
Simba pia wapo hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA wakitarajia kuumana na Azam FC ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye robo fainali iliyopigwa Azam Complex.

The post Manula, Inonga wapo fiti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/11/manula-inonga-wapo-fiti/feed/ 0
Tumpongeze Inonga wa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/tumpongeze-inonga-wa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/tumpongeze-inonga-wa-simba/#respond Sun, 05 Mar 2023 16:23:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5405 Na Hassan KinguHaishangazi beki Henock Inonga Baka wa Simba kuibuka kinara wa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki kwa mwezi Februari, tuzo inayodhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile.Tuzo hiyo inayoandamana na kitita cha Sh milioni 2 ni ishara ya kutambua mchango wa mchezaji hapo hapo ikionyesha thamani ya mchezaji huyo kwenye timu ya Simba.Kwa […]

The post Tumpongeze Inonga wa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Haishangazi beki Henock Inonga Baka wa Simba kuibuka kinara wa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki kwa mwezi Februari, tuzo inayodhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile.
Tuzo hiyo inayoandamana na kitita cha Sh milioni 2 ni ishara ya kutambua mchango wa mchezaji hapo hapo ikionyesha thamani ya mchezaji huyo kwenye timu ya Simba.
Kwa Inonga tuzo hiyo kakabidhiwa mtu sahihi kwa mwezi Februari, na jambo zuri ni kwamba ameendelea kuonyesha ubora wake hadi sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo. Anahitaji pongezi kwa hilo.
Na kama kuna sehemu ndani ya kikosi cha Simba yenye suluhisho sahihi, la kudumu na la muda mrefu basi sehemu hiyo ni nafasi ya beki wa kati anayocheza Inonga.
Hajaanza mwezi Februari au Machi mwaka huu, tangu atue Simba misimu miwili iliyopita akitokea DC Motema Pembe ya kwao DR Congo, Inonga amekuwa akionesha kiwango kikubwa na kuwa mhimili wa nafasi ya ulinzi Simba.
Inonga ambaye mashabiki wa Simba wamempachika jina la Varane akifananishwa kiuchezaji na beki wa zamani wa Real Madrid ambaye kwa sasa anaitumikia Man United.
Inonga alianza kujizolea umaarufu baada ya kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kwenye mechi mbili za Dar Derby katika msimu wake wa kwanza akiwa Simba.
Mapema alionesha ukomavu, akili na ujasiri wa hali ya juu na kuaminiwa na Wanasimba kutokana na kipaji alichonacho.
Ufanisi wa kazi za Inonga uwanjani umeendelea kuiweka salama Simba hata baada ya msimu uliopita kuondoka kwa beki aliyekuwa tegemeo, Paschal Wawa au kupungua kwa kasi ya Erasto Nyoni.
Awali ilionekana Joash Onyango anapaswa kutafutiwa mtu wa kusaidiana naye kutokana na kazi zake nzito uwanjani lakini ujio wa Inonga umebadili taswira na sasa yeye ndiye anayetafutiwa mtu wa kumsaidia kazi zake zinazotumia akili mno.
Ingawa Mohamed Ouattara aliyesajiliwa Simba msimu huu alitua kumpa changamoto Inonga lakini uimara wake umeendelea kumbakisha kikosi cha kwanza.
Licha ya Inonga kukaba kwa akili, kupiga ‘tackling’ za kupendeza dhidi ya wapinzani lakini pia anaburudisha na kusisimua mioyo ya mashabiki anapofanya ufundi wa kufinya, kupiga chenga akiwa eneo lake la ulinzi bila wasiwasi na mambo yakaenda sawa.
Kwa kifupi bado anaweza kukuburudisha kwa kucheza kama ‘mtu wa mwisho’ na hiyo ni kutokana na faida nyingine aliyonayo ya kumudu kucheza kama kiungo mkabaji. Inonga ana faida lukuki mno!
Simba ilifanya jambo la kupongezwa baada ya Desemba, mwaka jana kutangaza kumuongezea mkataba mchezaji huyo mpaka mwaka 2025. Maana yake wameridhishwa na ulinzi unaofanywa na beki huyo na wanafurahi usalama wa lango lao likiwa chini yake.
Msimu huu Inonga ameendelea kuonesha ubora wake hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya wikiendi iliyopita kuifungia Simba bao pekee ikiwa ugenini Uganda dhidi ya Vipers na kuipa ushindi na bao la kwanza tangu kuanza kwa michuano hiyo msimu huu.
Ndio maana haikushangaza kumuona akiingia kwenye kikosi bora cha wiki ya tatu ya michuano hiyo pamoja na wakali wengine kama Raed Bouchniba na Mohamed Hammouda wa Esperance, Makabi Lilepo (Al Hilal), Lema Mabidi (AS Vita), Jamal Harkass (Raja), kipa wa Mamelodi Sundowns, Ronwen Williams.
Hii si mara ya kwanza Inonga kuiokoa Simba, mfano msimu huu wakati jahazi linazama dhidi ya Kagera Sugar, beki huyo aliifungia bao timu hiyo na kulazimisha sare ya ugenini ya bao 1-1.
Usisahau msimu uliopita ambao ndio ulikuwa msimu wa kwanza kwa Inonga, aliibuka beki bora wa msimu wa Ligi Kuu NBC.
Pia, msimu huo mwezi Aprili alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Simba, kitu ambacho amekirudia msimu huu kwa juzi kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari!
Ikumbukwe tuzo hiyo kwa msimu hutolewa takriban mara nane pekee kulingana na muda ambao ligi inachezwa, hivyo ndani ya kikosi cha wachezaji 30 kuibuka mchezaji bora wa mwezi kila msimu angalau mara moja tena kwa beki, si jambo rahisi.
Inonga haimbwi sana kama Clatous Chama au ilivyokuwa kwa Luis Miquissone au Meddie Kagere lakini umuhimu wake ni mkubwa na kila kukicha anazidi kulidhihirisha hilo kwa namba anazoandika kila msimu.
Kocha wa timu ya taifa ya DR Congo, Sebastien Desabre anaufahamu ubora wa Inonga, licha ya kuwa na machaguo mengi ya mabeki lakini amemjumuisha pia beki huyo wa zamani wa FC Renaissance kwenye kikosi chake. Anatambua dhahabu inayopatikana miguuni mwa Inonga.
Itoshe kusema kwamba Inonga ni msaada mkubwa Simba, ni beki mnyumbulifu mwenye akili, anamudu kucheza nafasi zaidi ya moja na kuna wakati anacheza rafu inapobidi ili kuitetea Simba.
Simba itambue zaidi thamani yake sasa na ifahamu mapema mipango yao ya baadaye kuhusu beki huyo maana kwa timu zilizoendelea kwa mtu mwenye msaada kama huyu anapaswa kulindwa kwa vifungu vingi vyenye faida kwa Simba na mchezaji hapo baadaye.
Sifa moja kubwa ya Inonga ni ukweli kwamba kipaji chake kimeendelea kuwa hivyo hivyo kwa wakati wote, hajatetereka au kuporomoka, zaidi ameendelea kuwa mtu muhimu katika kikosi cha Simba. Tumpongeze kwa hilo.
Ndio kwanza anamalizia msimu wake wa pili tangu atue Simba japokuwa bado ana mkataba mrefu lakini lulu kama hii haipaswi kupita tu Simba ikafanya kazi zake kisha ikaondoka kwa urahisi. Ni aidha pesa ndefu au huduma ya mrefu iliyotukuka!

The post Tumpongeze Inonga wa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/05/tumpongeze-inonga-wa-simba/feed/ 0
Mayele, Inonga wang’ara Afrika https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mayele-inonga-wangara-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mayele-inonga-wangara-afrika/#respond Wed, 01 Mar 2023 12:34:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5354 Na mwandishi wetuBeki wa Simba, Henock Inonga na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ni kati ya wachezaji 11 bora wa kikosi cha wiki kwa mechi za tatu za makundi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.Kikosi hicho kimetajwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kikiwa na mchezaji pekee kutoka Simba na Tanzania kwa […]

The post Mayele, Inonga wang’ara Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki wa Simba, Henock Inonga na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ni kati ya wachezaji 11 bora wa kikosi cha wiki kwa mechi za tatu za makundi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kikosi hicho kimetajwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kikiwa na mchezaji pekee kutoka Simba na Tanzania kwa ujumla wakati Esperance ya Tunisia ikitoa wachezaji wanne katika kikosi hicho.
Inonga amejumuishwa kutokana na kiwango alichoonesha katika mechi yao ya tatu dhidi ya Vipers ambapo alifunga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 na kuiandikia Simba ushindi wa kwanza katika kundi lake.
Katika mechi mbili za awali, Wekundu hao walifungwa bao 1-0 na Horoya ya Guinea kabla ya kubugizwa mabao 3-0 na Raja Casablanca ya Morocco.
Wachezaji wa Esperance waliotajwa ni beki Raed Bouchniba, viungo Ghalyene Chaaeli, Mohamed Romdhane na mshambuliaji Mohamed Hammouda. Wengine ni mshambuliaji wa Al Hilal, Makabi Lilepo, Lema Mabidi (AS Vita), Mustafa Karshoum (Al-Merreikh), Roger Ahlolou na Jamal Harkass (Raja) na kipa wa Mamelodi Sundowns, Ronwen Williams.
Kwa upande wa Mayele naye ametajwa kwenye kikosi bora cha mechi za tatu za Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika kikosi hicho, Asec Mimosas imetoa wachezaji wawili, Kouassi Attohoula na Aubin Kouame kama AS FAR ilivyowakilishwa na Hamza Igamane na Reda Slim, US Monastir nayo imetoa wawili; Ousmane Ouattara na kipa Bechir Said.
Wengine ni Ngweni Ndasi wa Rivers United, Zineddine Belaid wa USMA, Abdallah El-Said wa Pyramids na Emmanuel Lonota wa FC Lupopo.
Mayele ameingia kwenye kikosi hicho kutokana na ufundi aliouonesha kwenye mechi yao dhidi ya Real Bamako ambapo alifunga bao kwenye sare ya 1-1 katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Bamako nchini Mali.
Mafanikio ya Mayele na Inonga pia yameonekana nchini mwao baada ya kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo wakiwa wachezaji pekee wa nchi hiyo wanaocheza soka Tanznaia kuitwa katika kikosi hicho.

The post Mayele, Inonga wang’ara Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mayele-inonga-wangara-afrika/feed/ 0