Ihefu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Mar 2023 11:23:07 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ihefu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ihefu mguu sawa kuivaa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/#respond Sun, 19 Mar 2023 11:22:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5530 Na mwandishi wetuTimu ya Ihefu imeeleza kuwa inajipanga vilivyo kuhakikisha inavaana na Simba kwenye mechi mbili mfululizo za michuano tofauti na kuibukia kidedea dhidi ya Wekundu hao.Ihefu ambayo ilikuwa na mapumziko ya siku tano, imerejea mazoezini jana kuanza rasmi mawindo yao hayo ya mechi ya robo fainali ya Kombe la FA na ile ya ligi, […]

The post Ihefu mguu sawa kuivaa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Ihefu imeeleza kuwa inajipanga vilivyo kuhakikisha inavaana na Simba kwenye mechi mbili mfululizo za michuano tofauti na kuibukia kidedea dhidi ya Wekundu hao.
Ihefu ambayo ilikuwa na mapumziko ya siku tano, imerejea mazoezini jana kuanza rasmi mawindo yao hayo ya mechi ya robo fainali ya Kombe la FA na ile ya ligi, zote dhidi ya Simba zinazotarajiwa kupigwa Aprili, mwaka huu.
Kocha Msaidizi wa Ihefu, Zuberi Katwila ameiambia GreenSports kuwa wanafahamu kibarua hicho dhidi ya Wekundu hao na kwa kuwa ni mechi mbili zenye hadhi tofauti basi wanafahamu tofauti ya namna ya kujipanga nazo ili zote wapate matokeo.
“Tuko kwenye kujiandaa dhidi ya Simba, ni mechi mbili tofauti, hivyo maandalizi ya Kombe la FA yatakuwa ni ya dakika 90 na ligi yatakuwa namna ya kutafuta pointi, yaani tunajipanga kwa namna mechi husika inavyotaka na lengo ni kupata ushindi mechi zote.

“Lengo letu ni kuvuka kwanza hapa tulipo kwa maana ya kusonga nusu fainali ya Kombe la FA, tutakayekutana naye mbele naye tutajua namna ya kufanya, ni hatua moja baada ya nyingine na tunajipanga kwa ajili ya kufanya vizuri,” alisema Katwila.


Licha ya kuteka hisia za wengi kwa timu hizo kukutana mara mbili mfululizo kwenye michuano tofauti lakini pia kiwango ilichonacho Ihefu hivi karibuni kimekuwa gumzo zaidi.
Ihefu ambayo ilianza vibaya ligi, imeshinda mechi nne na sare moja katika mechi zake tano zilizopita huku pia ikisifika kuwaadhibu vigogo kila wanapokuwa uwanja wao wa nyumbani.
Iliichapa Azam bao 1-0 kwenye mechi ya mwisho na ndiyo timu pekee iliyoifunga Yanga msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-1.

The post Ihefu mguu sawa kuivaa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/19/ihefu-mguu-sawa-kuivaa-simba/feed/ 0
Simba wanaijua vizuri Ihefu https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/simba-wanaijua-vizuri-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/simba-wanaijua-vizuri-ihefu/#respond Fri, 17 Mar 2023 19:35:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5520 Na mwandishi wetuTimu ya Simba imeeleza kutambua ugumu uliopo kupambana na Ihefu kwenye michezo miwili ya karibuni lakini imeeleza kuwa watajipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kusonga mbele.Simba itavaana na Ihefu itakayokuwa kwao kwenye mchezo ujao wa ligi lakini pia juzi imepangwa kucheza nayo kwenye robo fainali ya Kombe la FA (ASFC).Ofisa Habari wa Simba, […]

The post Simba wanaijua vizuri Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Simba imeeleza kutambua ugumu uliopo kupambana na Ihefu kwenye michezo miwili ya karibuni lakini imeeleza kuwa watajipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kusonga mbele.
Simba itavaana na Ihefu itakayokuwa kwao kwenye mchezo ujao wa ligi lakini pia juzi imepangwa kucheza nayo kwenye robo fainali ya Kombe la FA (ASFC).
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa wanafahamu namna gani mambo yalivyo magumu mbele ya Ihefu lakini wanasuka mipango ya kuhakikisha wanapata ushindi kwenye Kombe la FA na kusonga mbele kulekea kuchukua ubingwa huo.
“Tunakutana mara mbili sasa, kwenye Kombe la FA pia mechi itakuwa ngumu kutokana na uimara walionao Ihefu sasa, usajili walioufanya ni mzuri lakini inafahamika sisi tunataka ushindi, lengo letu kuchukua ubingwa huu.
“Hivyo lazima tupambane, lazima tuwe na mikakati juu ya hili kuhakikisha tunashinda hapa na tunasonga mbele kuelekea kutwaa ubingwa huu, hakika tunauhitaji ubingwa wa FA na Ihefu ni miongoni mwa timu unazokutana nazo kwenye hatua kama hii hivyo tutapambana zaidi,” alisema Ally.
Katika droo hiyo, mshindi wa Simba na Ihefu atakutana na mshindi wa Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC. Kwenye robo nyingine itazikutanisha Yanga dhidi ya Geita Gold na mshindi atapepetana na mshindi wa mechi ya Singida Big Stars dhidi ya Mbeya City.
Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo itapigwa Uwanja wa Nangwanda, Mtwara wakati nusu fainali ya pili itachezwa Uwanja wa Liti, Singida na fainali itakuwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

The post Simba wanaijua vizuri Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/17/simba-wanaijua-vizuri-ihefu/feed/ 0
Usajili waipa jeuri Ihefu https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/usajili-waipa-jeuri-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/usajili-waipa-jeuri-ihefu/#respond Fri, 05 Aug 2022 14:19:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2220 Na mwandishi wetuMchanganyiko wa usajili wa wachezaji wa kigeni na wa ndani uliofanywa na timu ya Ihefu umeipa jeuri timu hiyo kiasi cha kujinasibu kuwa wachezaji hao watawabeba mno msimu ujao wa 2022/23 na kuonesha umahiri wao dhidi ya timu za Ligi Kuu ya NBC Bara.Ihefu imepanda daraja kushiriki ligi hiyo baada ya kufanya hivyo […]

The post Usajili waipa jeuri Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mchanganyiko wa usajili wa wachezaji wa kigeni na wa ndani uliofanywa na timu ya Ihefu umeipa jeuri timu hiyo kiasi cha kujinasibu kuwa wachezaji hao watawabeba mno msimu ujao wa 2022/23 na kuonesha umahiri wao dhidi ya timu za Ligi Kuu ya NBC Bara.
Ihefu imepanda daraja kushiriki ligi hiyo baada ya kufanya hivyo pia msimu wa 2020/21 lakini ilishuka mwisho wa msimu huo baada ya kufanya vibaya na sasa imerejea upya.
Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuberi Katwila amesema wanaamini usajili huo utawasaidia kwa kuwa ni wachezaji wenye viwango vizuri na uzoefu mkubwa katika ligi kutokana na ushindani waliounyesha huko walikopita.
Mpaka sasa timu hiyo ambao ni mabingwa wa Championship wamewasajili wachezaji Obrey Chirwa aliyekuwa Namungo, Nicolas Wadada na Never Tigere waliokuwa Azam, Said Makapu (Polisi Tanzania), Peter Mwalyanzi (Kagera Sugar), Juma Nyosso (Geita Gold) na wengine.
“Usajili huu si tu kwamba ni mkubwa ila ni wa wachezaji ambao wanafahamika na utatusaidia kutokana na uzoefu walionao na pia viwango walivyonavyo kuelekea kwenye ushindani mkali wa msimu ujao wa ligi maana kila timu imesajili vizuri.
“Na imefanyika hivyo baada ya tathmini yenye lengo la kutaka kufanya vizuri zaidi msimu ujao tofauti na wakati ule tulipopanda tukashuka, tunahitaji kusalia mwisho wa msimu na kama kutakuwa na mengine hiyo ni faida ya ziada kwetu,” alisema Katwila.

The post Usajili waipa jeuri Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/usajili-waipa-jeuri-ihefu/feed/ 0
Tshishimbi atamba kuibeba Ihefu FC https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/tshishimbi-atamba-kuibeba-ihefu-fc/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/tshishimbi-atamba-kuibeba-ihefu-fc/#respond Wed, 27 Jul 2022 16:40:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=1994 Na mwandishi wetuKiungo mpya wa Ihefu FC, Papy Tshishimbi ameahidi kufanya mambo makubwa msimu ujao ikiwemo kuipa timu hiyo moja ya nafasi za juu kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.Mchezaji huyo aliyewahi kutamba akiwa na mabingwa watetezi Yanga, ameeleza kuwa pamoja na ugumu uliopo lakini haoni kikwazo kitakachomzuia kutamba kutokana na uzoefu aliokuwa nao […]

The post Tshishimbi atamba kuibeba Ihefu FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa Ihefu FC, Papy Tshishimbi ameahidi kufanya mambo makubwa msimu ujao ikiwemo kuipa timu hiyo moja ya nafasi za juu kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.
Mchezaji huyo aliyewahi kutamba akiwa na mabingwa watetezi Yanga, ameeleza kuwa pamoja na ugumu uliopo lakini haoni kikwazo kitakachomzuia kutamba kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye ligi hiyo.
“Najua kwamba ligi ya Tanzania kuanzia msimu uliopita imekuwa na ushindani mkubwa lakini kwangu nimejipanga kuhakikisha napambana nao na kuisaidia timu yangu mpya kufanya vizuri ikiwemo kumaliza nafasi mbili za juu,” alisema Tshisimbi.
Kiungo huyo raia wa DR Congo amefafanua kuwa ameamua kurudi kucheza Tanzania kutokana na ubora wa ligi iliyokuwa nayo ikilinganisha na ya kwao Congo lakini pia ni ligi ambayo inalipa vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema anaamini Ihefu ni timu sahihi ambayo itarudisha jina lake na kumfanya awe bora kama ilivyokuwa wakati anatua kwa mara ya kwanza Yanga mwaka 2018 akitokea Mbabane Swallows ya Botswana.
Tshishimbi amejiunga na Ihefu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Kitayose FC ya Tabora inayoshiriki Ligi ya Championship.

The post Tshishimbi atamba kuibeba Ihefu FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/tshishimbi-atamba-kuibeba-ihefu-fc/feed/ 0