Ihefu FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 20 May 2024 17:52:28 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ihefu FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Maxime awatetea wachezaji Ihefu https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/maxime-awatetea-wachezaji-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/maxime-awatetea-wachezaji-ihefu/#respond Mon, 20 May 2024 17:52:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11040 Na mwandishi wetuKocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema hana cha kuwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB dhidi ya Yanga.Maxime alisema kwamba wachezaji hao walifanya kila alichowaagiza na kufanya mchezo huo kuwa mgumu akiamini hata mashabiki pia wamevutiwa na hilo.Ihefu ilipoteza mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja […]

The post Maxime awatetea wachezaji Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema hana cha kuwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB dhidi ya Yanga.
Maxime alisema kwamba wachezaji hao walifanya kila alichowaagiza na kufanya mchezo huo kuwa mgumu akiamini hata mashabiki pia wamevutiwa na hilo.
Ihefu ilipoteza mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kwa kufungwa bao 1-0 dakika ya 100 baada ya mechi hiyo iliyoisha kwa suluhu katika dakika 90 za awali kuongezwa dakika 30 za ziada.
“Nisemme tu ulikuwa mchezo mzuri, ukiwalaumu wachezaji utakuwa huwatendei haki, ni mchezo wa mpira tumepata nafasi sisi tena nzuri kuliko wao tumeshindwa kuzitumia, wao wamepata wametumia.
“Sina cha kuwadai wachezaji wangu, wamenipa kila nilichokuwa nakitaka lakini basi ni matokeo ya mchezo tu wenyewe, lakini nafikiri hata watazamaji wamefurahia mechi,” alisema Maxime.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye kikosi chake kitavaana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo amesema amefurahishwa na uvumilivu wa wachezaji wake kwa kupambana na timu nzuri kama Ihefu ingawa amekiri kutofurahishwa na uwanja waliochezea.
“Ulikuwa mchezo mgumu kwenye kipindi cha kwanza ambapo tulitengeneza nafasi kama nne na wao walifanya hivyo, kipindi cha pili nafikiri tulicheza sana mpira lakini walizuia vizuri na kutufanya tushindwe kufunga.
“Nikawaambia wachezaji wangu watulie wasipate preshA sababu kuna dakika 30 nyingine na nafikri Ihefu walishaanza kuchoka ikawa rahisi kidogo kwetu lakini kiukweli uwanja si rafiki kwa mchezo kama huu au wa fainali maana hata Ihefu sidhani kama walifurahia,” alisema Gamondi.

The post Maxime awatetea wachezaji Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/maxime-awatetea-wachezaji-ihefu/feed/ 0
Ni Yanga, Azam fainali CRDB https://www.greensports.co.tz/2024/05/19/ni-yanga-azam-fainali-crdb/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/19/ni-yanga-azam-fainali-crdb/#respond Sun, 19 May 2024 16:29:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11031 Na mwandishi wetu, ArushaHatimaye Yanga imefuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kuilaza Ihefu FC bao 1-0 katika mechi iliyopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.Kwa ushindi huo Yanga sasa itaumana na Azam FC katika mechi ya fainali itakayopigwa Juni 2 mjini Manyara, Azam imefuzu hatua hiyo baada […]

The post Ni Yanga, Azam fainali CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu, Arusha
Hatimaye Yanga imefuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kuilaza Ihefu FC bao 1-0 katika mechi iliyopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Kwa ushindi huo Yanga sasa itaumana na Azam FC katika mechi ya fainali itakayopigwa Juni 2 mjini Manyara, Azam imefuzu hatua hiyo baada ya kuilaza Coastal Union 3-0 katika nusu fainali nyingine iliyopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.
Bao pekee lililoipa ushindi Yanga leo lilifungwa na Stephanie Aziz Ki akiutumia mpira ulioanzia kwa Khalid Aucho ambaye alimuunganishia Pacome Zouzoua aliyepiga krosi ya chinichini na Ki kuunganisha moja kwa moja hadi wavuni.
Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata bao hilo kwani mechi hiyo ililazimika kuchezwa kwa dakika 120 baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika dakika 90 za kawaida na ndipo Yanga walipopata bao lao dakika ya 10 katika dakika 30 za nyongeza.
Kocha wa Ihefu, Mecky Maxime alisema mchezo ulikuwa mzuri na hana sababu yoyote ya kuwalaumu wachezaji wake kwa matokeo hayo kwani kufanya hivyo ni kuwakosea.
Kwa upande wake kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisema kwamba mechi ilikuwa ngumu na kuwapongeza Ihefu kwa namna walivyokaba vizuri lakini pia aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha ukomavu wa kisoka.
Katika hatua nyingine Gamondi pia alilalamikia hali ya uwanja kwa alichosema kwamba haukuwa mzuri kwa timu zote.
Naye kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya alitangazwa kuwa nyota wa mchezo huo na kukabidhiwa hundi ya Shs 500,000 ambazo zilitolewa na wadhamini wa michuano hiyo, Benki ya CRDB.
Mudathir alimshukuru Mungu kwa kupata tuzo hiyo na kuwapongeza wachezaji wenzake kwa ushirikiano pamoja na benchi la ufundi la timu yake.

The post Ni Yanga, Azam fainali CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/19/ni-yanga-azam-fainali-crdb/feed/ 0
Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/#respond Sat, 18 May 2024 17:11:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11013 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema anatambua wapinzani wao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB, Yanga wana wachezaji hatari lakini hata wao pia wana wachezaji wenye ubora mkubwa wa kuamua matokeo.Maxime ameyasema hayo leo Jumamosi kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo amesisitiza […]

The post Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema anatambua wapinzani wao katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB, Yanga wana wachezaji hatari lakini hata wao pia wana wachezaji wenye ubora mkubwa wa kuamua matokeo.
Maxime ameyasema hayo leo Jumamosi kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo amesisitiza kuwa anafahamu ushindi wao utatokana na umoja wakishirikiana kudhibiti, kukaba na kushambulia kwa pamoja kama timu.
“Kikubwa kwanza kwenye timu kuwa kitimu kimpira na sio walinzi peke yao ndio wafanye kazi ya kuzuia, yaani mnazuia kama timu na hiyo inakuwa pale mpira mnaponyang’anywa ndipo mara moja mnapoanza kufanya ulinzi.
“Japo tunafahamu Yanga ina wachezaji wazuri kama alivyosema mwalimu wao (Miguel Gamondi), wachezaji hatari ambao nafasi moja mbili wanakumaliza.
“Sasa Ihefu pia ina wachezaji bora na sasa hivi tupo kwenye muunganiko mzuri toafuti na mwanzo, sasa hivi timu imeshasimama kwa hiyo na sisi pia tunao watu ambao wanaweza kumaliza mechi.
“Kikubwa Yanga wanakimbia sana, sasa ili kwenda nao sawa lazima na wewe ubora wa kazi yako uwe mkubwa sana, kitu ambacho naamini tutakwenda kukifanya hiyo kesho,” alisema Maxime.

The post Maxime ajivunia ubora Ihefu akiivaa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/maxime-ajivunia-ubora-ihefu-akiivaa-yanga/feed/ 0
Simba yajiweka pagumu ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/04/14/simba-yajiweka-pagumu-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/14/simba-yajiweka-pagumu-ligi-kuu/#respond Sun, 14 Apr 2024 10:20:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10586 Na mwandishi wetuSimba imeendelea kujiweka pagumu katika mkakati wa kulibeba taji la Ligi Kuu NBC baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ihefu katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Liti mjini Singida.Katika mechi hiyo, Ihefu ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 41 mfungaji akiwa ni Duke Abuya ambaye aliyatumia […]

The post Simba yajiweka pagumu ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeendelea kujiweka pagumu katika mkakati wa kulibeba taji la Ligi Kuu NBC baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ihefu katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Liti mjini Singida.
Katika mechi hiyo, Ihefu ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 41 mfungaji akiwa ni Duke Abuya ambaye aliyatumia makosa ya kipa wa Simba Ally Salim kufunga bao hilo.
Simba walihaha kusawazisha bao hilo na juhudi zao kuzaa matunda dakika ya 71 kwa bao lililofungwa kwa penalti na Clatous Chama, penalti ambayo ilitolewa baada ya Kibu Dennis kuchezewa rafu.
Baada ya mechi hiyo kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola aliwalaumu wachezaji wake kwa kukosa umakini wakati kocha wa Ihefu, Mecky Maxime aliwapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri.
Simba ambayo hadi sasa imeshacheza mechi 20 za ligi hiyo inabaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 ikiwa imezidiwa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 katika mechi 21.
Mahasimu wa Simba, Yanga ndio wanaoshika usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 52 katika mechi 20 na Jumapili hii wanajitupa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kucheza mechi yao ya 21 ya ligi hiyo dhidi ya Singida Fountain Gate.

The post Simba yajiweka pagumu ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/14/simba-yajiweka-pagumu-ligi-kuu/feed/ 0
Maxime atatizwa ligi kusimama https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/maxime-atatizwa-ligi-kusimama/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/maxime-atatizwa-ligi-kusimama/#respond Thu, 21 Mar 2024 19:06:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10290 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema kusimama kwa Ligi Kuu NBC kunapunguza ari ya upambanaji wa timu yake katika mechi za ligi hiyo.Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, alisema wamekuwa na kiwango bora tangu kuanza kwa mzunguko wa pili jambo ambalo limewasaidia kupata matokeo chanya na kujiweka katika nafasi nzuri […]

The post Maxime atatizwa ligi kusimama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema kusimama kwa Ligi Kuu NBC kunapunguza ari ya upambanaji wa timu yake katika mechi za ligi hiyo.
Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, alisema wamekuwa na kiwango bora tangu kuanza kwa mzunguko wa pili jambo ambalo limewasaidia kupata matokeo chanya na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo lakini ghafla ligi imesimama.

“Nafahamu ni kalenda ya Fifa lakini hii wakati mwingine huwa inatuharibia, ligi itakapoendelea itatulazimu kucheza mechi tatu hadi nne ili kurudi kwenye kiwango chetu tulichokuwa nacho kabla ya ligi kusimama na si jambo zuri kwa kuwa msimu unaelekea ukingoni na ushindani umeongezeka,” alisema Maxime.


Kocha huyo alisema ili kuepuka hilo atajitahidi wapate mechi nyingi za kirafiki, kitu ambacho si rahisi sana kwa sababu timu nyingi hasa za Ligi ya Championship zipo kwenye mapambano ya kumaliza msimu.
Alisema utaratibu huo unaziumiza timu kubwa ambazo hazina wachezaji kwenye timu za taifa kwani kwa kipindi chote cha wiki mbili ambacho ligi imesimama, timu hizo zinaishia kufanya mazoezi ya wenyewe kwa wenyewe.

The post Maxime atatizwa ligi kusimama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/maxime-atatizwa-ligi-kusimama/feed/ 0
Yanga yaipiga Ihefu mkono https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/yanga-yaipiga-ihefu-mkono/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/yanga-yaipiga-ihefu-mkono/#respond Tue, 12 Mar 2024 05:46:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10140 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kudhihirisha ubabe wake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Ihefu FC mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja Azam Complex, Dar es Salaam.Kipigo hicho kimezima matumaini ya baadhi ya mashabiki waliodhani Ihefu ingeweza kuizuia kasi ya Yanga baada ya kuichapa mabao 2-1 katika mzunguko wa kwanza na safari […]

The post Yanga yaipiga Ihefu mkono first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kudhihirisha ubabe wake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Ihefu FC mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja Azam Complex, Dar es Salaam.
Kipigo hicho kimezima matumaini ya baadhi ya mashabiki waliodhani Ihefu ingeweza kuizuia kasi ya Yanga baada ya kuichapa mabao 2-1 katika mzunguko wa kwanza na safari hii imeonekana kuwa imara ikiongezewa nguvu na baadhi ya wachezaji waliokuwa Singida Fountain Gate.
Mambo hata hivyo yaligeuka kuwa kinyume na matarajio hayo, badala yake Ihefu ikajikuta ikipigwa mkono, kipigo ambacho pia Yanga imempa hasimu wake Simba katika mechi ya ligi mzunguko wa kwanza.
Yanga ilipata mabao yake mawili kabla ya timu hizo kwenda mapumziko yakifungwa na Pacome Zouazoua na Mudathir Yahya, wote wakitumia vizuri pasi kutoka kwa Stephanie Aziz Ki.
Aziz Ki baada ya kupika mabao hayo mawili aliifungia timu yake bao la tatu ambalo ni la 12 kwake kwenye ligi hiyo hivyo kufungana na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC ambaye pia amefunga mabao 12 hadi sasa.
Nyota ya Augustine Okrah nayo iling’ara katika mechi hiyo baada ya kuifungia timu yake bao la nne na kwa mara nyingine juhudi za Aziz Ki zilionekana alipotoa pasi iliyozaa bao hilo.
Karamu ya mabao ya Yanga ilihitimishwa na Maxi Nzengeli kwa kufunga bao la tano na la mwisho na kuifanya Yanga iongeze idadi ya timu ilizozifunga mabao matano ambapo mbali na Simba na Ihefu, timu nyingine zilizokutana na kipigo hicho nchini ni JKT Tanzania na KMC.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 49 katika michezo 18 huku ikiwa imetupia kambani mabao 47.

The post Yanga yaipiga Ihefu mkono first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/12/yanga-yaipiga-ihefu-mkono/feed/ 0
Sare yatibua hesabu za Maxime https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/sare-yatibua-hesabu-za-maxime/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/sare-yatibua-hesabu-za-maxime/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:20:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9954 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema matokeo ya sare ya kufunga bao 1-1 dhidi ya Mashujaa FC yamevuruga hesabu zao za kupanda nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.Maxime alisema mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Liti, Singida ulikuwa mgumu na kila timu ilipambana kutafuta ushindi lakini kujisahau kwa mabeki […]

The post Sare yatibua hesabu za Maxime first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema matokeo ya sare ya kufunga bao 1-1 dhidi ya Mashujaa FC yamevuruga hesabu zao za kupanda nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Maxime alisema mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Liti, Singida ulikuwa mgumu na kila timu ilipambana kutafuta ushindi lakini kujisahau kwa mabeki wake kuliwanufaisha wapinzani wao na kusawazisha bao hilo la mapema dakika ya 11 lililofungwa na Elvis Rupia.
“Sijafurahishwa na matokeo haya lakini hatuwezi kukata tamaa bado tuna mechi nyingi za kucheza nyumbani na ugenini, naamini tutapata matokeo mazuri yatakayotupandisha nafasi za juu,” alisema Maxime nahodha wa zamani wa Taifa Stars.
Naye kocha mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ alisema wakati wanaingia uwanjani kuikabili Ihefu walijua utakuwa mchezo mgumu hivyo walijipanga kuhakikisha wanapata ushindi au sare na anashukuru Mungu, moja ya malengo yao kufanikiwa.

“Ulikuwa mchezo muhimu kwetu sote Ihefu na sisi Mashujaa lakini tunashukuru kwa hiki kidogo tulichokipata, naamini itakuwa na maana kubwa kwetu katika harakati zetu za kujiondoa nafasi ya chini tuliyopo,” alisema Baresi.


Ihefu ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikikusanya pointi 20 katika mechi 18 wakati Mtibwa imebaki nafasi ya 15 wakiwa na idadi kama hiyo ya pointi.

The post Sare yatibua hesabu za Maxime first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/sare-yatibua-hesabu-za-maxime/feed/ 0
Maxime aahidi makubwa Ihefu https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/#respond Wed, 03 Jan 2024 17:42:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9140 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amewataka mabosi wa timu hiyo watarajie mambo makubwa kutokana na mifumo ya kisasa anayoipandikiza kwa wachezaji wake.Akizungumza leo Jumatano, kocha huyo alisema timu hiyo ina wachezaji wazuri isipokuwa kilichokuwa kinawasumbua kutopata matokeo mazuri ni mfululizo wa vipigo. “Kufungwa mfululizo kumevuruga saikolojia ya wachezaji, baada ya kukabidhiwa timu […]

The post Maxime aahidi makubwa Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amewataka mabosi wa timu hiyo watarajie mambo makubwa kutokana na mifumo ya kisasa anayoipandikiza kwa wachezaji wake.
Akizungumza leo Jumatano, kocha huyo alisema timu hiyo ina wachezaji wazuri isipokuwa kilichokuwa kinawasumbua kutopata matokeo mazuri ni mfululizo wa vipigo.

“Kufungwa mfululizo kumevuruga saikolojia ya wachezaji, baada ya kukabidhiwa timu kitu cha kwanza nilichoanza nacho ni kujenga saikolojia zao na kupandisha ari ya upambanaji ili waweze kufanya vizuri,” alisema Maxime.


Kocha huyo alisema mipango yake ni kuiondoa Ihefu nafasi ya 13 hivi sasa kwenye Ligi Kuu NBC na kuipandisha nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Alisema anatambua ugumu uliopo kwenye ligi ya msimu huu lakini anajivunia uwezo wa wachezaji wake pamoja na wasaidizi wake hakuna kitu kitashindikana.
Ihefu ambayo hadi sasa imeshatimua makocha wawili ambao ni Zuberi Katwila na Moses Basena, ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 13 katika michezo 14.

The post Maxime aahidi makubwa Ihefu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/03/maxime-aahidi-makubwa-ihefu/feed/ 0
Mchakato mrithi wa Basena wafika pazuri https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mchakato-mrithi-wa-basena-wafika-pazuri/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mchakato-mrithi-wa-basena-wafika-pazuri/#respond Mon, 11 Dec 2023 18:21:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8819 Na mwandishi wetuMchakato wa kumpata kocha mkuu mpya wa Ihefu FC atakayerithi mikoba ya Moses Basena (pichani) umefikia katika hatua nzuri na wanatarajia kumtambulisha kabla mzunguko wa kwanza haujamalizika.Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila alisema kwa sasa wanakamilisha baadhi ya taratibu ili wasaini mkataba na kuanza kazi kama ambavyo wamekusudia.“Ni kocha wa viwango ambaye tunaamini […]

The post Mchakato mrithi wa Basena wafika pazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mchakato wa kumpata kocha mkuu mpya wa Ihefu FC atakayerithi mikoba ya Moses Basena (pichani) umefikia katika hatua nzuri na wanatarajia kumtambulisha kabla mzunguko wa kwanza haujamalizika.
Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila alisema kwa sasa wanakamilisha baadhi ya taratibu ili wasaini mkataba na kuanza kazi kama ambavyo wamekusudia.
“Ni kocha wa viwango ambaye tunaamini atabadili mwenendo wa timu yetu na kutufikisha kule ambako tumekusudia kwa hiyo kupafika msimu huu ambako ni kumaliza kwenye nafasi nne za juu,” alisema Chalamila.
Kiongozi huyo alisema kingine kinachofanya wamlete kocha mpya kabla ya mzunguko wa pili ni kutaka kumpa nafasi ya kutoa mapendekezo yake kwenye usajili wa dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki hii.
Alisema kocha aliyepita Basena alishatoa mapendekezo yake kuhusu usajili wa dirisha dogo lakini wangependa kusikia na mapendekezo ya kocha wao mpya sababu yeye ndiye atakayekinoa kikosi hicho na kutimiza malengo ambayo wamempa.
Ihefu ambayo tayari imefukuza makocha wawili kabla ya mzunguko wa kwanza kumalizika msimu huu, inashika nafasi ya 13 ikiwa na idadi kama hiyo ya pointi na mechi walizocheza msimu huu.

The post Mchakato mrithi wa Basena wafika pazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/11/mchakato-mrithi-wa-basena-wafika-pazuri/feed/ 0
Basena awatisha Azam FC https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/basena-awatisha-azam-fc/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/basena-awatisha-azam-fc/#respond Fri, 03 Nov 2023 16:07:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8347 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Ihefu FC, Moses Basena amesema kuwa hawatarudia makosa ya mchezo uliopita yaliyosababisha wakapata sare na kuwaharibia hesabu zao.Ihefu wanashuka dimbani kesho Jumamosi kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.Vijana wa Basena wanaoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wanashuka kwenye […]

The post Basena awatisha Azam FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Moses Basena amesema kuwa hawatarudia makosa ya mchezo uliopita yaliyosababisha wakapata sare na kuwaharibia hesabu zao.
Ihefu wanashuka dimbani kesho Jumamosi kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu NBC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.
Vijana wa Basena wanaoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wanashuka kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya mabao 2-2 na Singida Fountain Gate wakati Azam inayoshika nafasi ya tatu ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa.

“Mchezo huu una maana kubwa kwetu, tunatakiwa kushinda ili kurejesha hali ya kujiamini kikosini baada ya morali yetu kushuka lakini tunarudi kurekebisha makosa yetu ili tukusanye pointi tatu kwenye mchezo ulio mbele yetu,” alisema Basena.


Kocha Msaidizi wa Azam, Bruno Ferry alisema baada ya kupata pointi tatu kwenye mchezo uliopita nguvu zao wanahamishia kwenye mechi ya Ihefu ingawa anaamini watakutana na upinzani mkubwa kwa kuwa watakuwa ugenini.
“Naamini utakuwa mchezo mgumu, wapinzani wetu wanapambana kupata matokeo lakini lengo letu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu ili tuendelee kusogea juu ya msimamo wa ligi,” alisema Ferry.

The post Basena awatisha Azam FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/03/basena-awatisha-azam-fc/feed/ 0