Ibrahim Bacca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 10 May 2024 07:47:28 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ibrahim Bacca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bacca akiri Kagera wagumu https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/bacca-akiri-kagera-wagumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/bacca-akiri-kagera-wagumu/#respond Fri, 10 May 2024 07:47:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10910 Na mwandishi wetuBeki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca amesema mchezo wao wa jana Jumatano dhidi ya Kagera Sugar ulikuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuziba njia zao zote lakini mbinu za kocha wao, Miguel Gamondi ziliwatoa kwenye mtego huo na kuibuka na pointi tatu.Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es […]

The post Bacca akiri Kagera wagumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca amesema mchezo wao wa jana Jumatano dhidi ya Kagera Sugar ulikuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuziba njia zao zote lakini mbinu za kocha wao, Miguel Gamondi ziliwatoa kwenye mtego huo na kuibuka na pointi tatu.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Yanga ililazimika kusubiri mpaka dakika ya 82 kupata bao kupitia kwa Mudathir Yahya na kuendelea kujikita kileleni kwa pointi 68 kwa mechi 26.
“Nadhani ulikuwa mchezo mzuri, na walishtukia Kagera na kuziba njia zote, sehemu zote tunazopitia na wakawa wakakamavu kuanzia mwanzo nadhani mpaka dakika za mwisho lakini kwa ukubwa wetu na maono yake mwalimu alibadili vitu kidogo tukapata ushindi, Muda alitumia vizuri ile nafasi tuliyoipata,” alisema Bacca.
Beki huyo pia alisema kuwa licha ya kuuona kidogo mwanga wa ubingwa kwa mara nyingine msimu huu lakini anaamini bado wanahitaji kuongeza nguvu na umakini katika mechi zao zilizosalia ambazo nyingi watacheza ugenini dhidi ya timu zinazopigania vitu tofauti katika ligi hiyo.
Yanga imebakisha michezo minne kufunga rasmi pazia la ligi kwa kuumana na Mtibwa Sugar Mei 13 na Dodoma Jiji Mei 22, mechi zote mbili zikiwa ugenini kabla ya kurejea nyumbani kuvaana na Tabora United Mei 25 na Tanzania Prisons Mei 28, mwaka huu.

The post Bacca akiri Kagera wagumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/bacca-akiri-kagera-wagumu/feed/ 0
Adam Adam akiri Bacca msumbufu https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/adam-adam-akiri-bacca-msumbufu/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/adam-adam-akiri-bacca-msumbufu/#respond Tue, 30 Jan 2024 18:56:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9510 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Mashujaa FC, Adam Adam amesema beki pekee anayemsumbua kwenye Ligi Kuu NBC ni Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (pichani) wa Yanga.Akizungumza na GreenSports, kinara huyo wa mabao msimu huu kwenye kikosi cha Mashujaa alisema beki huyo ni miongoni mwa mabeki wachache wenye uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake na kuipa mafanikio timu yake.“Ukweli […]

The post Adam Adam akiri Bacca msumbufu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Adam Adam amesema beki pekee anayemsumbua kwenye Ligi Kuu NBC ni Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (pichani) wa Yanga.
Akizungumza na GreenSports, kinara huyo wa mabao msimu huu kwenye kikosi cha Mashujaa alisema beki huyo ni miongoni mwa mabeki wachache wenye uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake na kuipa mafanikio timu yake.
“Ukweli kwangu Bacca ndiye beki bora kwenye ligi ligi yetu, ana uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake, maana ameonesha hilo akiwa na timu yake ya Yanga lakini hata timu ya taifa kule kwenye fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast,” alisema Adam..
Alisema amekutana na mabeki wengi wenye majina makubwa nchini akiwemo mkongwe Kelvin Yondani, Bakari Mwamnyeto na Juma Nyosso lakini Bacca ameonesha utofauti mkubwa kutokana na uchezaji wake.
Mshambuliaji huyo amewashauri viongozi kutoa kipaumbele kwa wachezaji wazawa kama ilivyofanya Yanga kwa Bacca kwani kama wakituliza akili wanaweza kupata wachezaji wengi wenye vipaji kuliko kutumia pesa nyingi kwenda nje ya nchi.

The post Adam Adam akiri Bacca msumbufu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/30/adam-adam-akiri-bacca-msumbufu/feed/ 0
Bacca aongezewa miaka miwili Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/bacca-aongezewa-miaka-miwili-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/bacca-aongezewa-miaka-miwili-yanga/#respond Wed, 29 Nov 2023 18:57:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8675 Na mwandishi wetuBeki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca ameongezewa mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2027.Mchezaji huyo alijiunga na Yanga Januari mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar baada ya kuonesha kiwango bora kunako klabu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.Tangu kutua Yanga, Bacca amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi […]

The post Bacca aongezewa miaka miwili Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca ameongezewa mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2027.
Mchezaji huyo alijiunga na Yanga Januari mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar baada ya kuonesha kiwango bora kunako klabu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.
Tangu kutua Yanga, Bacca amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha kiwango bora tangu msimu uliopita, akiisaidia timu hiyo kubeba mataji ya Ligi Kuu NBC, Kombe la FA na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kupitia mtandao wake, Yanga leo Jumatano imebainisha kumalizana na mchezaji huyo kwa kuandika: “Bacca ataendelea kusalia Yanga hadi 2027.”
Kuelekea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly wikiendi hii, Bacca ndiye mchezaji aliyechaguliwa kuwa ataenziwa yaani itakuwa siku yake maalum kuthamini kazi yake na mchango anaouonesha katika klabu hiyo.
Tayari baadhi ya wachezaji kama Stephane Aziz Ki na Max Nzengeli waliwahi kuenziwa ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo wachezaji na kuthamini mchango wao.

The post Bacca aongezewa miaka miwili Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/29/bacca-aongezewa-miaka-miwili-yanga/feed/ 0