Gundogan - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 22 Jun 2023 14:44:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Gundogan - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Gundogan asajiliwa Barca https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/#respond Thu, 22 Jun 2023 14:44:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6678 Manchester, EnglandKlabu ya Barcelona imefikia makubaliano na Manchester City ya kumsajili kiungo Ilkay Gundogan akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake wa sasa kufikia ukomo Juni 30 mwaka huu.Gundogan, nyota wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na Barca ambao una kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kuongeza mwaka wa tatu.Hadi […]

The post Gundogan asajiliwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na Manchester City ya kumsajili kiungo Ilkay Gundogan akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake wa sasa kufikia ukomo Juni 30 mwaka huu.
Gundogan, nyota wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na Barca ambao una kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kuongeza mwaka wa tatu.
Hadi kukubali kujiunga na Barca, Gundogan amekataa ofa ya kuendelea kuichezea Man City akiwa tayari ameichezea timu hiyo kwa miaka saba, lakini pia amekataa ofa ya Arsenal na klabu za Saudi Arabia.
Machi mwaka huu zilikuwapo habari kwamba Barca ilianza mchakato wa kumsajili mchezaji huyo ikidaiwa kwamba kutokana na kanuni za matumizi ya fedha kuwabana, klabu hiyo imeamua kukimbilia kwa mchezaji huyo ili kumsajili akiwa huru.
Kwa upande wa Man City kulikuwa na ugumu kumruhusu kiungo huyo kuondoka ingawa ilichotaka ni kumpa mkataba wa mwaka mmoja lakini mwenyewe akaamua kuichagua Barca licha ya kocha wa Man City, Pep Guardiola kuonesha nia ya kumbakisha katika timu hiyo.
Kocha wa Barca, Xavi ndiye aliyeongoza mpango wa kumsajili Gundogan ili kuiimarisha timu hiyo hasa baada ya kumkosa Lionel Messi ambaye amejiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani.

The post Gundogan asajiliwa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/gundogan-asajiliwa-barca/feed/ 0
Timu nne zamtaka Gundogan https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/timu-nne-zamtaka-gundogan/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/timu-nne-zamtaka-gundogan/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:24:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6485 London, EnglandNahodha wa Man City, Ilkay Gundogan huenda akaihama timu hiyo baada ya kutakiwa na timu nne tofuati ingawa kocha Pep Guardiola anaamini msimu ujao atakuwa na mchezaji huyo Man City.Gundogan (pichani) ambaye ana umri wa miaka 32 huenda akarudi Borussia Dortmund ambayo imeonesha nia ya kumtaka hasa baada ya Barcelona ambayo pia inamtaka kukwamishwa […]

The post Timu nne zamtaka Gundogan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Nahodha wa Man City, Ilkay Gundogan huenda akaihama timu hiyo baada ya kutakiwa na timu nne tofuati ingawa kocha Pep Guardiola anaamini msimu ujao atakuwa na mchezaji huyo Man City.
Gundogan (pichani) ambaye ana umri wa miaka 32 huenda akarudi Borussia Dortmund ambayo imeonesha nia ya kumtaka hasa baada ya Barcelona ambayo pia inamtaka kukwamishwa na suala la mshahara wa mchezaji huyo.
Ukiachana na klabu hizo mbili ambazo kila moja inamchungulia mwenzake, Arsenal nayo ipo tayari kumpa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili na marupurupu ya maana hapo hapo kukiwa na habari kwamba kuna klabu ya Saudi Arabia nayo inamtaka.
Gundogan anaonekana kutaka mkataba mrefu katika klabu hizo jambo ambalo linazifanya zote zisite kutokana na umri wake hapo hapo zikiwa zinaviziana katika kupanda dau.
Wakati yote hayo yakiendelea, Pep anaamini mchezaji huyo ataongeza mkataba Man City na kwamba timu hiyo itapenda kuendelea kuwa naye msimu ujao kutokana na umuhimu wake.
Pep anaamini kuwa mbali na umuhimu wa Gundogan uwanjani lakini pia mchezaji huyo ni kiongozi mzuri kwenye timu ambaye anasikilizwa na wachezaji wenzake na kwa hilo Pep hatopenda kuona akiondoka.

The post Timu nne zamtaka Gundogan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/timu-nne-zamtaka-gundogan/feed/ 0