Greenwood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 02 Apr 2024 20:21:50 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Greenwood - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 La Liga wapotezea utata wa Bellingham, Greenwood https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/la-liga-wapotezea-utata-wa-bellingham-greenwood/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/la-liga-wapotezea-utata-wa-bellingham-greenwood/#respond Tue, 02 Apr 2024 20:21:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10487 Madrid, HispaniaUongozi wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ unadaiwa kuachana na uchunguzi kuhusu malalamiko ya klabu ya Getafe dhidi ya kauli anazodaiwa kutolewa mchezaji wao Mason Greenwood na Jude Bellingham wa Real Madrid.Nyota hao wote wa England inadaiwa waliingia katika utata na kutoleana kauli zisizopendeza wakati wa mechi baina ya timu zao iliyopigwa Februari Mosi […]

The post La Liga wapotezea utata wa Bellingham, Greenwood first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Uongozi wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ unadaiwa kuachana na uchunguzi kuhusu malalamiko ya klabu ya Getafe dhidi ya kauli anazodaiwa kutolewa mchezaji wao Mason Greenwood na Jude Bellingham wa Real Madrid.
Nyota hao wote wa England inadaiwa waliingia katika utata na kutoleana kauli zisizopendeza wakati wa mechi baina ya timu zao iliyopigwa Februari Mosi ambapo Bellingham anadaiwa kutoa kauli zenye utata kwa Greenwood.
Katika mechi hiyo ambayo iliisha kwa Real Madrid kutokana na ushindi wa mabao 2-0, Bellingham anadaiwa kumtolea Greenwood kauli zisizofaa wakati wachezaji hao wakiwania mpira na tukio hilo kuwa mjadala kwenye mitandao ya kijamii.


Habari zaidi zinadai kwamba maofisi wa La Liga waliomba msaada wa wataalam wa ‘kusoma midomo’ ili kujua msemaji alisema nini lakini uchunguzi wa sakata hilo haujakamilika huku kukiwa na habari kwamba umemalizwa kimya kimya.
Bellingham ambaye ndiye aliyemkaba Greenwood katika tukio na ndiye mtuhumiwa lakini zipo habari za vyanzo mbalimbali pia zinazodai kwamba Greenwood ameomba uchunguzi wa tukio hilo uachwe.

The post La Liga wapotezea utata wa Bellingham, Greenwood first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/la-liga-wapotezea-utata-wa-bellingham-greenwood/feed/ 0
Greenwood atua Getafe kwa mkopo https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/greenwood-atua-getafe-kwa-mkopo/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/greenwood-atua-getafe-kwa-mkopo/#respond Sat, 02 Sep 2023 20:12:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7652 Madrid, HispaniaMshambuliaji wa Manchester United anayeandamwa na kashfa ya udhalilishaji kijinsia, Mason Greenwood amejiunga kwa mkopo na klabu ya Getafe inayoshiriki Ligi Kuu Hispania au La Liga.Hatua hiyo imekuja baada ya mabosi wa Man United kutangaza kuwa mchezaji huyo angeondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano maalum baada ya uchunguzi uliofanywa na klabu hiyo kwa miezi […]

The post Greenwood atua Getafe kwa mkopo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa Manchester United anayeandamwa na kashfa ya udhalilishaji kijinsia, Mason Greenwood amejiunga kwa mkopo na klabu ya Getafe inayoshiriki Ligi Kuu Hispania au La Liga.
Hatua hiyo imekuja baada ya mabosi wa Man United kutangaza kuwa mchezaji huyo angeondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano maalum baada ya uchunguzi uliofanywa na klabu hiyo kwa miezi sita baada ya kufutiwa mashtaka ya kutaka kubaka na udhalilishaji kijinsia.
Greenwood, 21, mwezi Februari mwaka huu alifutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili lakini alijikuta katika wakati mgumu baada ya timu ya wanawake ya Man United na makundi ya wanaharakati kutishia kugoma na kuandamana iwapo mchezaji huyo angeruhusiwa kuichezea klabu hiyo.

“Hatua hiyo itamfanya Greenwood aanze kujenga upya maisha yake mapya ya soka nje ya klabu ya Manchester United. Klabu itaendelea kumpa sapoti Mason na familia yake katika kipindi hiki cha mpito,” ilieleza taarifa ya klabu ya Manchester United.


Getafe itakuwa ikilipa sehemu ndogo ya mshahara wa Greenwood ambaye bado ana mkataba na Man United unaofikia ukomo mwaka 2025.
Tangu ajiunge na Man United mwaka 2019 akiwa kijana wa miaka 17, Greenwood ameifungia timu hiyo mabao 35 katika mechi 129.
Greenwood hakuichezea Man United tangu Oktoba 2022 aliposhitakiwa kwa makosa ya kusudio la kubaka, ubabe na udhalilishaji kijinsia.
Mara baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani, makampuni ya Nike na Electronic Arts yalimfutia mchezaji huyo mikataba ya udhamini.

The post Greenwood atua Getafe kwa mkopo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/greenwood-atua-getafe-kwa-mkopo/feed/ 0
Greenwood njia panda Man United https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/greenwood-yuko-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/greenwood-yuko-njia-panda/#respond Thu, 17 Aug 2023 06:38:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7426 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imesema bado haijaamua lolote kuhusu kumrudisha kikosini mchezaji wake Mason Greenwood na kwamba jambo hilo linahitaji tafakuri ya kina kabla ya kufikia uamuzi.Msimamo huo unazidi kumuweka njia panda mshambuliaji huyo ambaye Februari mwaka huu alifutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili akituhumiwa kutaka kubaka pamoja na udhalilishaji wa kijinsia.Awali Man United walitarajia kutoa […]

The post Greenwood njia panda Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imesema bado haijaamua lolote kuhusu kumrudisha kikosini mchezaji wake Mason Greenwood na kwamba jambo hilo linahitaji tafakuri ya kina kabla ya kufikia uamuzi.
Msimamo huo unazidi kumuweka njia panda mshambuliaji huyo ambaye Februari mwaka huu alifutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili akituhumiwa kutaka kubaka pamoja na udhalilishaji wa kijinsia.
Awali Man United walitarajia kutoa uamuzi kuhusu Greenwood kabla ya Jumatatu iliyopita, siku ambayo timu hiyo ilicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2023-24 dhidi ya Wolves.
Jana Jumatano taarifa ya klabu hiyo ilieleza kuwa uchunguzi wa kutafuta ukweli kuhusu Greenwood tayari umekamilika na uamuzi wa mwisho upo mikononi mwa ofisa mtendaji mkuu Richard Arnold ambaye yuko katika hatua za mwisho.
Klabu ya Man United imekuwa ikiangalia zaidi suala la Greenwood kurudi katika kiwango kilicho bora lakini uzito wa mjadala unaoendelea kuhusu mchezaji huyo umeifanya klabu hiyo itulie na kuendelea kulifanyia tafakuri zaidi kabla ya kuamua kumrudisha kikosini au la.
Katika kulifanyia kazi sakata la mchezaji huyo, Man United imekusanya taarifa ambazo hazijulikani na wengi kutoka kwa watu waliohusika moja kwa moja au wenye uelewa wa jinsi tukio zima lilivyokuwa.
“Pia tuna jukumu kwa Mason kama waajiriwa wake, kama kijana mdogo ambaye amekuwa na klabu hii tangu akiwa na umri wa miaka saba,” ilieleza taarifa ya Man United.
“Tofauti na uvumi wa kwenye vyombo vya habari, hakuna uamuzi wowote uliofikiwa na sasa suala hilo lipo katika uchunguzi wa kina, uamuzi utakapofikiwa tutatangaza na kutoa ufafanuzi kwa wahusika wa ndani ya klabu na wadau wengine,” ilifafanua taarifa hiyo.
Miongoni mwa wadau ambao inadaiwa watahusika katika mashauriano kabla ya kufanya uamuzi wowote ni pamoja na mabosi wa timu ya wanawake ya Man United.

The post Greenwood njia panda Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/17/greenwood-yuko-njia-panda/feed/ 0