Esperance - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 15 Mar 2026 13:56:19 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Esperance - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha mpya Esperance aipania Ahly https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/kocha-mpya-esperance-aipania-ahly/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/kocha-mpya-esperance-aipania-ahly/#respond Sun, 15 Mar 2026 13:56:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14428 Tunis, TunisiaKocha mkuu wa timu ya Esperance ya Tunisia, Patrice Beaumelle amesema timu yake itawakabili kwa nguvu zote Al Ahly katika mechi ya kwanza ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumapili Machi 15, 2026.Esperance waliokuwa kundi D na timu za Simba ya Tanzania, Stade Malien ya Mali na Petro Atletico ya Angola walifuzu […]

The post Kocha mpya Esperance aipania Ahly first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tunis, Tunisia
Kocha mkuu wa timu ya Esperance ya Tunisia, Patrice Beaumelle amesema timu yake itawakabili kwa nguvu zote Al Ahly katika mechi ya kwanza ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumapili Machi 15, 2026.
Esperance waliokuwa kundi D na timu za Simba ya Tanzania, Stade Malien ya Mali na Petro Atletico ya Angola walifuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo ingawa mwenendo wa timu haukuwa mzuri.
Kutokana na mwenendo wa timu kutokuwa mzuri, Maher Kanzari alitimuliwa na nafasi yake kupewa Beaumelle ambaye mtihani wake wa kwanza mkubwa utakuwa dhidi ya Ahly.
Katika Kundi D, mbali na Esperance, timu nyingine iliyofuzu robo fainali ni Stade Malien ambayo tayari imeanza vibaya mechi ya kwanza ya hatua hiyo kwa kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Esperance itakuwa mwenyeji katika mechi ya kwanza na Ahly katika dimba la Hammadi Agrebi kabla ya timu hizo kurudiana Jumamosi ijayo mjini Cairo.
Beaumelle alisisitiza Esperance lazima itumie fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza mbele ya mashabiki wake na matumaini yake ni kwamba mechi hiyo inaweza kuwapa faida wakati timu hizo zitakapokutana mara ya pili mjini Cairo.

“Tuna mechi ya nyumbani na ni lzima tucheze kwa nguvu zetu zote, katika mechi ya kwanza tunatakiwa kujitoa kwa kila kitu mbele ya mashabiki wetu ili tuweze kuwa na nafasi ya kucheza katika namna bora kadri iwezekanavyo katika mechi ya marudiano,” alisema Beaumelle.


Esperance itacheza mechi na Ahly ikiwa imetoka kurekodi ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Tunisia dhidi ya Future Marsa.
Katika mechi hiyo, Beaumelle alifanya mabadiliko ya haraka haraka kwa baadhi ya wachezaji muhimu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutotaka kuumiza wachezaji wake kabla ya mechi dhidi ya Ahly.

The post Kocha mpya Esperance aipania Ahly first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/kocha-mpya-esperance-aipania-ahly/feed/ 0
Mfaransa ndiye kocha mpya Esperance https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/kocha-mfaransa-akabidhiwa-esperance/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/kocha-mfaransa-akabidhiwa-esperance/#respond Sat, 07 Mar 2026 21:01:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14395 Tunis, TuniaKocha Patrice Beaumelle (pichani) mwenye asili ya Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Esperance ya Tunisia na amesaini mkataba utakaomfanya awe na timu hiyo hadi Juni, 2027.Beaumelle, 47, amekabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Maher Kanzari ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu baada ya timu hiyo kuwa na […]

The post Mfaransa ndiye kocha mpya Esperance first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tunis, Tunia
Kocha Patrice Beaumelle (pichani) mwenye asili ya Ufaransa ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Esperance ya Tunisia na amesaini mkataba utakaomfanya awe na timu hiyo hadi Juni, 2027.
Beaumelle, 47, amekabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Maher Kanzari ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu baada ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyoridhisha.
Miongoni mwa matokeo hayo ni kipigo cha bao 1-0 ambacho Esperance ilikipata kwa Stade Malien katika mechi ya mwisho hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ingawa timu hiyo imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mtihani wa kwanza mkubwa kwa kocha huyo ambaye amejiunga na timu hiyo na jopo la wasaidizi wake, utakuwa wiki ijayo ambapo Esperance itaumana na vigogo Al Ahly ya Misri katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Beaumelle ametua Esperance baada ya kuvunja mkataba wake na Shirikisho la Soka Angola alipokuwa akiinoa timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo alikuwa nayo kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka jana mwishoni nchini Morocco.
Kocha huyo si mgeni katika soka la Afrika, aliwahi kuwa mmoja wa wasaidizi wa kocha Mfaransa, Hervé Renard ambaye mwaka 2012 aliiongoza timu ya taifa ya Zambia maarufu Chipolopolo hadi kubeba taji la Afcon na wakawa tena pamoja mwaka 2015 na timu ya Ivory Coast iliyobeba taji hilo.
Kwa upande wa klabu, Beaumelle amejipatia mafanikio zaidi nchini Algeria wakati akiinoa Mouloudia Club d’Alger, timu aliyoiwezesha kubeba taji la Ligi Kuu Algeria msimu wa 2023-24 na kufika hatua ya fainali Kombe la Algeria msimu huo huo.

The post Mfaransa ndiye kocha mpya Esperance first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/kocha-mfaransa-akabidhiwa-esperance/feed/ 0
Esperance yatimua kocha https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/#respond Tue, 10 Feb 2026 18:48:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14335 Tunis, TunisiaKlabu ya Espérance ya Tunisia imemfuta kazi kocha Maher Kanzari (pichani) baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stade Malien katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mwishoni mwa wiki.Uamuzi wa klabu hiyo ulifikiwa jioni ya Jumapili Februari 8, 2026 sababu ikitajwa kuwa ni kiwango duni cha […]

The post Esperance yatimua kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tunis, Tunisia
Klabu ya Espérance ya Tunisia imemfuta kazi kocha Maher Kanzari (pichani) baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stade Malien katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mwishoni mwa wiki.
Uamuzi wa klabu hiyo ulifikiwa jioni ya Jumapili Februari 8, 2026 sababu ikitajwa kuwa ni kiwango duni cha timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Katika taarifa ya klabu hiyo ilielezwa kuwa Rais wa Esperance, Hamdi Meddeb ametangaza kuvunja mkataba wa klabu hiyo na kocha huyo mwenye asili ya Tunisia na benchi jipya la ufundi litatangazwa siku chache zijazo.
Kipigo dhidi ya Malien kimeiweka Esperance njia panda katika mbio za kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kupitia Kundi D wakati huu wakisubiri kucheza mechi yao ya mwisho.
Kanzari ambaye alikabidhiwa jukumu la kuinoa Esperance Machi mwaka jana akichukua nafasi ya Laurentiu Reghecampf kutoka Romania, amekuwa na wakati mgumu kutengeneza kikosi bora cha kutoa ushindani katika michuano ya klabu barani Afrika.
Wakati timu hiyo ikitajwa kuwa miongoni mwa timu bora Afrika, chini ya kocha Kanzari, baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakikosoa mambo kadhaa ikiwamo kushuka kwa mbinu na kutofurahishwa na staili ya uchezaji isiyotoa dalili za mafanikio.
Mabosi wa Esperance kwa sasa wana kibarua kigumu cha kufanya maamuzi wakati timu hiyo ikisubiri kuumana na Petro Atletico ya Angola mwishoni mwa wiki, mechi iliyobeba hatma ya timu hiyo kufuzu hadi robo fainali au kuishia hatua ya makundi.

The post Esperance yatimua kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/feed/ 0
Esperance yaiweka pagumu Simba https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/#respond Mon, 02 Feb 2026 08:59:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14311 Na mwandishi wetuMambo magumu kwa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Esperance ya Tunisia katika mechi iliyochezwa Jumapili Januari mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Matokeo hayo yanaifanya Simba kupoteza kwa kiasi kikubwa matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo […]

The post Esperance yaiweka pagumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mambo magumu kwa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Esperance ya Tunisia katika mechi iliyochezwa Jumapili Januari mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kupoteza kwa kiasi kikubwa matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
Simba hadi sasa inashikilia mkia katika kundi lake ikiwa na pointi moja, Esperance inashika nafasi ya pili na pointi zake sita na Petro Atlético ya tatu ikiwa na pointi tano wakati Stade Malien ndiye kinara wa kundi hilo akiwa na pointi nane.
Mazingira ya kundi hilo yanaonesha kuwa Simba ikishinda mechi mbili zilizobaki itafikisha pointi saba kwa hiyo ili iweze kusonga mbele itahitaji Esperance na Petro Atlético zipoteze mechi zao mbili zilizobaki au kila moja ipoteze moja na moja iishe kwa sare.
Kwa maana nyingine Simba si tu inatakiwa kushinda mechi zilizobaki bali ishinde kwa mabao mengi lakini pia ile dhana ya adui yako muombee njaa nayo pia imebeba hatma ya Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2025-26.
Kilichoifikisha Simba katika hali hiyo ni mechi yao na Esperance, mechi ambayo ilitoa matumaini ya timu hiyo kupata ushindi kabla ya mambo kuharibika na kujikuta wakitoa sare ya 2-2 huku Esperance wakikosa penalti.
Simba iliuanza mchezo huo vizuri na kuonesha kila dalili za kutoka uwanjani na pointi tatu baada ya kupata bao la kwanza dakika ya 39 lililofungwa na Shomari Kapombe.
Shamrashamra za mashabiki wa Simba baada ya bao hilo ziliongezeka kwa mara ya pili baada ya Yusuph Kagoma kuongeza bao la pili katika dakika za nyongeza kabla ya timu kwenda mapumziko.
Mambo yalianza kuiendea kombo Simba katika dakika ya 64 baada ya Aboubacar Diakité kuipatia Esperance bao la kwanza kabla Kouceila Boualia hajasawazisha dakika 15 baadaye na kuwaacha mashabiki wa Simba vichwa chini.
Kama hiyo haitoshi mashabiki hao waliingia unyonge tena katika dakika za nyongeza baada ya Esperance kupata penalti lakini Hamza Jelassi alishindwa kuitumia penalti hiyo kuipatia Esperance bao.
Katika mechi zijazo Simba itakuwa ugenini Angola kuumana na Petro de Luanda wakati Esperance itasafiri hadi Mali kuikabili Stade Malien.

The post Esperance yaiweka pagumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/feed/ 0
Esperance yailaza Simba 1-0 https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/#respond Sun, 25 Jan 2026 11:04:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14290 Na mwandishi wetuMambo si mazuri kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 na Esperance ya Tunisia katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumamosi Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi mjini Rades.Kwa matokeo hayo, Esperance wanashikilia usukani wa Kundi D wakiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi […]

The post Esperance yailaza Simba 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mambo si mazuri kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 na Esperance ya Tunisia katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumamosi Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi mjini Rades.
Kwa matokeo hayo, Esperance wanashikilia usukani wa Kundi D wakiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tatu wakati Simba ikiendelea kuburuza mkia katika kundi hilo ambalo pia lina timu za Stade Malien ya Mali na Petro De Luanda ya Angola.
Bao pekee lililowapa ushindi wenyeji Esperance lilipatikana katika dakika ya 21 mfungaji akiwa ni Jacques Diarra baada ya kuiwahi pasi ndefu na kumzidi kasi beki wa Simba, Shomari Kapombe kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Matokeo hayo pia yanazidi kufikisha matumaini ya Simba kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya klabu Afrika kwani hadi sasa timu hiyo imepoteza mechi zake zote tatu kati ya sita inazopaswa kucheza.
Kabla ya mechi ya Simba, mahasimu wao Yanga nao walikuwa ugenini Misri wakiumana na Al Ahly na Yanga kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-0.
Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano ya klabu Afrika, Jumapili hii Januari 25, 2026 wataingia katika viwanja tofauti kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam wakiwa wageni wa Nairobi United na Singida Black Stars watakuwa wenyeji wa AS Otoho ya Congo Brazzaville.

The post Esperance yailaza Simba 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/feed/ 0