Esperance - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 15 Feb 2026 11:14:03 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Esperance - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Esperance yatimua kocha https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/#respond Tue, 10 Feb 2026 18:48:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14335 Tunis, TunisiaKlabu ya Espérance ya Tunisia imemfuta kazi kocha Maher Kanzari (pichani) baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stade Malien katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mwishoni mwa wiki.Uamuzi wa klabu hiyo ulifikiwa jioni ya Jumapili Februari 8, 2026 sababu ikitajwa kuwa ni kiwango duni cha […]

The post Esperance yatimua kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tunis, Tunisia
Klabu ya Espérance ya Tunisia imemfuta kazi kocha Maher Kanzari (pichani) baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stade Malien katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mwishoni mwa wiki.
Uamuzi wa klabu hiyo ulifikiwa jioni ya Jumapili Februari 8, 2026 sababu ikitajwa kuwa ni kiwango duni cha timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Katika taarifa ya klabu hiyo ilielezwa kuwa Rais wa Esperance, Hamdi Meddeb ametangaza kuvunja mkataba wa klabu hiyo na kocha huyo mwenye asili ya Tunisia na benchi jipya la ufundi litatangazwa siku chache zijazo.
Kipigo dhidi ya Malien kimeiweka Esperance njia panda katika mbio za kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kupitia Kundi D wakati huu wakisubiri kucheza mechi yao ya mwisho.
Kanzari ambaye alikabidhiwa jukumu la kuinoa Esperance Machi mwaka jana akichukua nafasi ya Laurentiu Reghecampf kutoka Romania, amekuwa na wakati mgumu kutengeneza kikosi bora cha kutoa ushindani katika michuano ya klabu barani Afrika.
Wakati timu hiyo ikitajwa kuwa miongoni mwa timu bora Afrika, chini ya kocha Kanzari, baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakikosoa mambo kadhaa ikiwamo kushuka kwa mbinu na kutofurahishwa na staili ya uchezaji isiyotoa dalili za mafanikio.
Mabosi wa Esperance kwa sasa wana kibarua kigumu cha kufanya maamuzi wakati timu hiyo ikisubiri kuumana na Petro Atletico ya Angola mwishoni mwa wiki, mechi iliyobeba hatma ya timu hiyo kufuzu hadi robo fainali au kuishia hatua ya makundi.

The post Esperance yatimua kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/10/esperance-yatimua-kocha/feed/ 0
Esperance yaiweka pagumu Simba https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/#respond Mon, 02 Feb 2026 08:59:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14311 Na mwandishi wetuMambo magumu kwa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Esperance ya Tunisia katika mechi iliyochezwa Jumapili Januari mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Matokeo hayo yanaifanya Simba kupoteza kwa kiasi kikubwa matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo […]

The post Esperance yaiweka pagumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mambo magumu kwa Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Esperance ya Tunisia katika mechi iliyochezwa Jumapili Januari mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kupoteza kwa kiasi kikubwa matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
Simba hadi sasa inashikilia mkia katika kundi lake ikiwa na pointi moja, Esperance inashika nafasi ya pili na pointi zake sita na Petro Atlético ya tatu ikiwa na pointi tano wakati Stade Malien ndiye kinara wa kundi hilo akiwa na pointi nane.
Mazingira ya kundi hilo yanaonesha kuwa Simba ikishinda mechi mbili zilizobaki itafikisha pointi saba kwa hiyo ili iweze kusonga mbele itahitaji Esperance na Petro Atlético zipoteze mechi zao mbili zilizobaki au kila moja ipoteze moja na moja iishe kwa sare.
Kwa maana nyingine Simba si tu inatakiwa kushinda mechi zilizobaki bali ishinde kwa mabao mengi lakini pia ile dhana ya adui yako muombee njaa nayo pia imebeba hatma ya Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2025-26.
Kilichoifikisha Simba katika hali hiyo ni mechi yao na Esperance, mechi ambayo ilitoa matumaini ya timu hiyo kupata ushindi kabla ya mambo kuharibika na kujikuta wakitoa sare ya 2-2 huku Esperance wakikosa penalti.
Simba iliuanza mchezo huo vizuri na kuonesha kila dalili za kutoka uwanjani na pointi tatu baada ya kupata bao la kwanza dakika ya 39 lililofungwa na Shomari Kapombe.
Shamrashamra za mashabiki wa Simba baada ya bao hilo ziliongezeka kwa mara ya pili baada ya Yusuph Kagoma kuongeza bao la pili katika dakika za nyongeza kabla ya timu kwenda mapumziko.
Mambo yalianza kuiendea kombo Simba katika dakika ya 64 baada ya Aboubacar Diakité kuipatia Esperance bao la kwanza kabla Kouceila Boualia hajasawazisha dakika 15 baadaye na kuwaacha mashabiki wa Simba vichwa chini.
Kama hiyo haitoshi mashabiki hao waliingia unyonge tena katika dakika za nyongeza baada ya Esperance kupata penalti lakini Hamza Jelassi alishindwa kuitumia penalti hiyo kuipatia Esperance bao.
Katika mechi zijazo Simba itakuwa ugenini Angola kuumana na Petro de Luanda wakati Esperance itasafiri hadi Mali kuikabili Stade Malien.

The post Esperance yaiweka pagumu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/02/esperance-yaiweka-pagumu-simba/feed/ 0
Esperance yailaza Simba 1-0 https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/#respond Sun, 25 Jan 2026 11:04:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14290 Na mwandishi wetuMambo si mazuri kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 na Esperance ya Tunisia katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumamosi Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi mjini Rades.Kwa matokeo hayo, Esperance wanashikilia usukani wa Kundi D wakiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi […]

The post Esperance yailaza Simba 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mambo si mazuri kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 na Esperance ya Tunisia katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumamosi Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi mjini Rades.
Kwa matokeo hayo, Esperance wanashikilia usukani wa Kundi D wakiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tatu wakati Simba ikiendelea kuburuza mkia katika kundi hilo ambalo pia lina timu za Stade Malien ya Mali na Petro De Luanda ya Angola.
Bao pekee lililowapa ushindi wenyeji Esperance lilipatikana katika dakika ya 21 mfungaji akiwa ni Jacques Diarra baada ya kuiwahi pasi ndefu na kumzidi kasi beki wa Simba, Shomari Kapombe kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Matokeo hayo pia yanazidi kufikisha matumaini ya Simba kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya klabu Afrika kwani hadi sasa timu hiyo imepoteza mechi zake zote tatu kati ya sita inazopaswa kucheza.
Kabla ya mechi ya Simba, mahasimu wao Yanga nao walikuwa ugenini Misri wakiumana na Al Ahly na Yanga kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 2-0.
Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano ya klabu Afrika, Jumapili hii Januari 25, 2026 wataingia katika viwanja tofauti kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam wakiwa wageni wa Nairobi United na Singida Black Stars watakuwa wenyeji wa AS Otoho ya Congo Brazzaville.

The post Esperance yailaza Simba 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/25/esperance-yailaza-simba-1-0/feed/ 0