DRC Congo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 Apr 2026 18:12:52 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg DRC Congo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/#respond Wed, 01 Apr 2026 18:12:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14513 Jalisco, MexicoTimu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ‘DR Congo’ imefuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Jamaica na hivyo kurudi katika fainali hizo walizoshiriki mara ya mwisho miaka 52 iliyopita.DR Congo ilipambana na Jamaica katika mechi hiyo ya play-off iliyochezwa Jumanne Machi 31, […]

The post DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Jalisco, Mexico
Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ‘DR Congo’ imefuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Jamaica na hivyo kurudi katika fainali hizo walizoshiriki mara ya mwisho miaka 52 iliyopita.
DR Congo ilipambana na Jamaica katika mechi hiyo ya play-off iliyochezwa Jumanne Machi 31, 2026 kwenye dimba la Akron nchini Mexico na kumalizika kwa sare ya bila kufungana katika dakika 90 kabla ya beki Axel Tuanzebe kufunga bao pekee katika dakika za nyongeza.
Ushindi huo umelihakikishia taifa hilo kushiriki fainali hizo zitakazoanza Juni 11, 2026 katika nchi za Canada, Mexico na Marekani na hivyo kujikumbusha walipofuzu mara ya mwisho mwaka 1974 wakati nchi hiyo ikiitwa Zaire chini ya Rais Mobutu Seseseko.
Mechi ya DR Congo ‘The Leopards’ na Jamaica ‘The Reggae Boyz’ kwa kipindi kirefu ilionesha kuwa na nguvu sawa kwa kila timu kutengeneza mashambulizi na umakini katika kujihami.
Hatimaye DR Congo walinufaika na shambulizi walilolifanya katika dakika ya 100 ambapo Tuanzebe aliruka juu kuuwahi mpira wa kona na kuujaza wavuni kwa kichwa hali iliyoamsha shangwe kwa mashabiki wake.
Kwa kufuzu huko, DR Congo inaingia katika fainali hizo ikiwa Kundi K ambalo pia lina timu za Colombia, Ureno na Uzbekistan.
DR Congo inaungana na timu nyingine tisa za Afrika kushiriki michuano hiyo na hivyo kufanya idadi ya timu za Afrika katika fainali za mwaka huu kuwa 10.
Timu nyingine za Afrika zilizofuzu kushiriki fainali hizo ni Misri, Algeria, Afrika Kusini, Senegal, Cape Verde, Morocco, Ghana, Tunisia na Ivory Coast.
Italia yakwama tena
Wakati mashabiki DR Congo wakishangilia kurudi kwenye fainali hizo baada ya miaka 52, nchini Italia ni huzuni baada ya timu hiyo mabingwa mara nne wa Kombe la Dunia kushindwa kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo.
Italia ilishindwa kufuzu katika fainali hizo mwaka 2018 nchini Ufaransa na baada ya hapo ikashindwa kwa mara nyingine kufuzu katika fainali za Qatar mwaka 2022.
Kilichoiangusha Italia hadi kukosa fainali za 2026 ni mikwaju ya penalti katika mechi yao ya play-off dhidi ya Bosnia-Herzegovina iliyochezwa Jumanne Machi 31, 2026 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida na 30 za nyongeza.
Italia chini ya kocha Gennaro Gattuso, kiungo aliyekuwa na timu ya Italia iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, ilishindwa kuonesha umahiri kwenye penalti baada ya kulala kwa penalti 4-1.
Bosnia-Herzegovina chini ya nahodha wake mkongwe Edin Dzeko, 40, kama DR Congo nayo inafuzu kwa mara ya pili katika historia ya nchi hiyo na imepangwa Kundi B na timu za Uswisi, Canada na Qatar.

The post DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/feed/ 0
Mayele, Inonga waitwa timu ya Taifa https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/mayele-inonga-waitwa-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/mayele-inonga-waitwa-timu-ya-taifa/#respond Tue, 28 Feb 2023 13:15:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5336 Na mwandishi wetuKocha wa timu ya Taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre leo Jumanne ameita kikosi cha timu hiyo na kuwajumuisha wachezaji wanaokipiga Tanzania, Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba.Desbare raia wa Ufaransa amekiita kikosi hicho cha wachezaji 42 huku Mayele na Inonga wakiwa ni wachezaji pekee wa DR Congo wanaocheza Ligi […]

The post Mayele, Inonga waitwa timu ya Taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya Taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre leo Jumanne ameita kikosi cha timu hiyo na kuwajumuisha wachezaji wanaokipiga Tanzania, Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba.
Desbare raia wa Ufaransa amekiita kikosi hicho cha wachezaji 42 huku Mayele na Inonga wakiwa ni wachezaji pekee wa DR Congo wanaocheza Ligi Kuu NBC kuitwa na kocha huyo.
DR Congo imeita kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili za kufuzu michuano ya Mataifa Afrika (Afcon 2024) dhidi ya Mauritania zitakazopigwa Machi 24 na marudiano Machi 29, mwaka huu.
Kuitwa kwa wachezaji hao ambao wamekuwa wakionesha viwango bora tangu watue nchini kumekuja wakati ambao wachezaji hao wametoka kuzisaidia timu zao kupata pointi kwenye mechi za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi iliyopita.
Inonga alifunga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda na kuipa Simba pointi tatu za kwanza msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya awali kufungwa bao 1-0 na Horoya ya Guinea na kisha kuchapwa mabao 3-0 na Raja Casablanca ya Morocco.
Mayele ambaye anaitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho tangu atue Yanga misimu miwili iliyopita, alifunga bao kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Real Bamako ya Mali na kuifanya Yanga iondoke na pointi moja ugenini.
DR Congo imeita makipa watano, mabeki 13, viungo 16 na washambuliaji wanane wakitazamiwa kupunguzwa kabla ya kufikia maandalizi ya mwisho mwisho dhidi ya mechi na Mauritania.

The post Mayele, Inonga waitwa timu ya Taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/28/mayele-inonga-waitwa-timu-ya-taifa/feed/ 0