Diao - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 07 Sep 2023 19:06:17 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Diao - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha Azam amtetea Diao https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/kocha-azam-amtetea-diao/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/kocha-azam-amtetea-diao/#respond Thu, 07 Sep 2023 19:06:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7684 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema mshambuliaji wake, Alassane Diao (pichani kushoto) anahitaji muda ili kuwa katika kiwango chake.Akizungumza Dar es Salaam leo Alhamisi, kocha huyo alisema Diao anahitaji muda kuzoea mazingira lakini pia, anahitaji kupewa nafasi ili kuonesha kile alichonacho.“Diao anahitaji muda kwa sababu hata wachezaji wenzake hawafahamu uchezaji wake, […]

The post Kocha Azam amtetea Diao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema mshambuliaji wake, Alassane Diao (pichani kushoto) anahitaji muda ili kuwa katika kiwango chake.
Akizungumza Dar es Salaam leo Alhamisi, kocha huyo alisema Diao anahitaji muda kuzoea mazingira lakini pia, anahitaji kupewa nafasi ili kuonesha kile alichonacho.
“Diao anahitaji muda kwa sababu hata wachezaji wenzake hawafahamu uchezaji wake, hawamuelewi vizuri, naamini muda si mrefu watamuelewa na kutupa kile tunakichotarajia kutoka kwake,” alisema.
Mchezaji huyo aliyetokea klabu ya US Goree ya Senegal hajaonesha ubora unaotarajiwa na wengi kama ilivyoelezwa wakati akisajiliwa na Azam huku akiwa amepewa dakika chache uwanjani katika mechi za hivi karibuni za Azam.
Katika mechi mbili za Ligi Kuu NBC, Kombe la Shirikisho Afrika na za Ngao ya Jamii, mchezaji huyo hakupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza, aliishia kwenye benchi la timu hiyo.

The post Kocha Azam amtetea Diao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/kocha-azam-amtetea-diao/feed/ 0
Azam FC: Diao mchezaji wetu halali https://www.greensports.co.tz/2023/07/08/azam-fc-diao-mchezaji-wetu-halali/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/08/azam-fc-diao-mchezaji-wetu-halali/#respond Sat, 08 Jul 2023 20:02:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6871 Na mwandishi wetuKlabu ya Azam FC, imeeleza kuwa mshambuliaji Msenegali, Alassane Diao waliyemsajili kutoka US Goree walimchukua akiwa huru na hakuwa na mkataba na klabu ya Goree kama inavyoelezwa.Azam imeeleza hayo baada ya Goree juzi kutoa taarifa kwa umma kuwa Diao ni mchezaji wao halali na amesajiliwa akiwa na mkataba na timu hiyo, hivyo wanajipanga […]

The post Azam FC: Diao mchezaji wetu halali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC, imeeleza kuwa mshambuliaji Msenegali, Alassane Diao waliyemsajili kutoka US Goree walimchukua akiwa huru na hakuwa na mkataba na klabu ya Goree kama inavyoelezwa.
Azam imeeleza hayo baada ya Goree juzi kutoa taarifa kwa umma kuwa Diao ni mchezaji wao halali na amesajiliwa akiwa na mkataba na timu hiyo, hivyo wanajipanga kuchukua hatua stahiki.
Ofisa Habari wa Azam, Zakaria Thabit (pichani juu) amezungumza na GreenSports na kusema kwanza wao hawana taarifa rasmi za malalamiko hayo zaidi ya kuona mitandaoni lakini wana nyaraka zote sahihi zinazoonesha mchezaji huyo alikuwa huru wakati wanamsajili.
“Kama kweli wana mkataba naye walete malalamiko rasmi kwetu, pili tulishawasiliana na kambi ya mchezaji na kuthibitisha juu ya kumalizika kwa makataba wake. Isipokuwa mkanganyiko uliopo umetokana na kusogezwa mbele kwa msimu wa ligi ya Senegal.

“Kilichotokea ni ligi yao kusogezwa mbele na kufanya mkataba wa Diao kumalizika kabla ya ligi kuisha, wao walipaswa wamwombe mchezaji amalizie ligi wakati huu lakini wanasema ni mchezaji wao halali wakati kimsingi amemaliza mkataba,” alisema Zakaria.


Ligi Kuu ya Senegal maarufu Ligue 1 inayoshirikisha timu 14 mpaka sasa imecheza mechi 23 zikiwa zimesalia mechi tatu kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la ligi hiyo msimu huu.

The post Azam FC: Diao mchezaji wetu halali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/08/azam-fc-diao-mchezaji-wetu-halali/feed/ 0
Diao kuiingiza matatani Azam FC? https://www.greensports.co.tz/2023/07/07/diao-kuiingiza-matatani-azam-fc/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/07/diao-kuiingiza-matatani-azam-fc/#respond Fri, 07 Jul 2023 20:18:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6864 Na mwandishi wetuSiku chache baada ya Azam FC kumtangaza mshambuliaji Alassane Diao, klabu ya US Goree ya Senegal aliyotokea mchezaji huyo imeeleza kusikitishwa na Azam kumsajili Diao wakati wao wana mkataba naye.Goree imeeleza hayo kupitia taarifa waliyoweka juzi kwenye mtandao wao wamedai kuwa kutokana na hayo wamedhamiria kufuata sheria za uhamisho zilizowekwa na Shirikisho la […]

The post Diao kuiingiza matatani Azam FC? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku chache baada ya Azam FC kumtangaza mshambuliaji Alassane Diao, klabu ya US Goree ya Senegal aliyotokea mchezaji huyo imeeleza kusikitishwa na Azam kumsajili Diao wakati wao wana mkataba naye.
Goree imeeleza hayo kupitia taarifa waliyoweka juzi kwenye mtandao wao wamedai kuwa kutokana na hayo wamedhamiria kufuata sheria za uhamisho zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Katika hilo, klabu ya US Goree imedhamiria kuhakikisha maslahi ya klabu na wachezaji wake chini ya mkataba yanazingatiwa.
“Kupitia mitandao ya kijamii, Union Sportive Goreenne imebaini utiaji saini wa mkataba wa miaka miwili kati ya mchezaji wetu Alassane Diao na klabu ya Azam FC ya Tanzania.
“Diao bado ana mkataba na US Goree, na hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanzishwa na klabu ya Azam FC katika mwelekeo wa kumwachilia mchezaji huyo hivyo hawezi kufuzu kucheza katika klabu nyingine Senegal au kimataifa kabla ya mwisho wa mkataba wake wa sasa.
“Kwa kuheshimu taratibu zinazosimamia soka, US Gorée inasisitiza dhamira yake ya kufuata sheria za uhamisho zilizowekwa na Fifa na kuhakikisha maslahi ya klabu na wachezaji wake walio chini ya mkataba,” ilieleza taarifa hiyo iliyowekwa juzi na uongozi wa Goree.
GreenSports ilifanya juhudi za kumtafuta Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ kuhusiana na sakata la mchezaji huyo raia wa Senegal lakini simu yake muda wote ilikuwa ikitumika.
Hata alipotafutwa Ofisa Habari wa Azam, Zakaria Thabiti ili atoe ufafanuzi wa jambo hilo naye simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa.

The post Diao kuiingiza matatani Azam FC? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/07/diao-kuiingiza-matatani-azam-fc/feed/ 0