Dembele - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 18 Dec 2025 20:29:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Dembele - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Dembele atwaa tuzo ya Fifa https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/dembele-atwaa-tuzo-ya-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/dembele-atwaa-tuzo-ya-fifa/#respond Wed, 17 Dec 2025 12:52:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14192 Doha, QatarMshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa kwa upande wa wanaume katika tukio lililofanyika usiku wa Jumanne, Desemba 16, 2025 mjini Doha, Qatar.Hiyo ni tuzo ya pili kubwa kwa Dembele katika kipindi kisichozidi miezi minne, baada ya mchezaji huyo kushinda tuzo ya […]

The post Dembele atwaa tuzo ya Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Doha, Qatar
Mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa kwa upande wa wanaume katika tukio lililofanyika usiku wa Jumanne, Desemba 16, 2025 mjini Doha, Qatar.
Hiyo ni tuzo ya pili kubwa kwa Dembele katika kipindi kisichozidi miezi minne, baada ya mchezaji huyo kushinda tuzo ya Ballon d’Or Septemba mwaka huu.
Mafanikio ya Dembele hadi kubeba tuzo hizo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na alivyoisaidia PSG kushinda mataji manne katika msimu uliopita wa 2024-25 akiwa amehusika katika mabao 51 kwenye mechi 53 za PSG.
Katika mataji hayo limo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambalo PSG ililibeba kwa mara ya kwanza baada ya kuhaha kwa misimu kadhaa ikiwamo licha ya kuwa na kikosi kilichosheheni mastaa wakiwamo Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe.
Dembele, 28, ambaye aliwahi kuichezea Borussia Dortmud kabla ya kujiunga na PSG mwaka 2023 akitokea Barca, mwaka 2023, atika tuzo hiyo ya Fifa aliwashinda Lamine Yamal wa Barca na Mbappe wa Real Madrid.
Katika makabidhiano ya tuzo hiyo, Dembele alishiriki katika hafla hiyo ambayo itafuatiwa na mechi ya taji la mabara ambapo PSG itaumana na Flamengo ya Brazil siku ya Jumatano.
Tuzo hiyo ya Fifa ambayo inahusisha matukio yaliyoanzia Agosti 2024 hadi Agosti 2025, mshindi hupatikana kwa njia ya kura ambazo zinapigwa na makocha wa timu za taifa, manahodha, waandishi wa habari na mashabiki.
Bonmati kinara wa wanawake
Naye kiungo wa timu ya wanawake ya Barcelona, Aitana Bonmati (pichani chini) ametwaa tuzo kama ya Dembele kwenye soka la wanawake hii ikiwa ni mara yake ya tatu kubeba tuzo hiyo, wakati kocha wa timu ya wanawake ya England, Sarina Wiegman akibeba tuzo ya kocha bora kwa mara ya tano.

Bonmati, 27, pia alikuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania iliyoshika nafasi ya pili katika fainali za wanawake za Euro 2025 ambazo England ilibeba taji.
Mafanikio ya Bonmati kwa kiasi kikubwa yamebebwa na mataji matatu aliyoisaidia timu ya wanawake ya Barcelona kuyabeba akifunga mabao 12 lakini pia timu hiyo ilishika nafasi ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa na timu ya wanawake ya Arsenal.
Wakati huo huo kocha wa PSG, Luis Enrique, 55, ametwaa tuzo ya kocha wa mwaka baada ya kuiwezesha kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiweka rekodi kwa kuziangusha Liverpool, Arsenal na Inter Milan.
Enrique ambaye amekuwa kocha wa PSG tangu mwaka 2023 akitokea Barca, katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo amewashinda, Arne Slot wa Liverpool na Hansi Flick wa Barca.
Enrique hata hivyo hakuweza kushiriki katika hafla hiyo mjini Doha na badala yake kocha msaidizi wa PSG, Rafel Pol Cabanellas aliipokea tuzo hiyo kwa niaba yake.
Wachezaji 11 bora pia wametajwa katika timu bora ya mwaka, majina na klabu wanaoztoka katika mabano ni kama ifuatavyo: Gianluigi Donnarumma (PSG/Man City), Achraf Hakimi (PSG), Willian Pacho (PSG), Virgil van Dijk (Liverpool), Nuno Mendes (PSG), Cole Palmer (Chelsea), Jude Bellingham (Real Madrid), Vitinha (PSG), Pedri (Barca), Lamine Yamal (Barca) na Dembele (PSG).

The post Dembele atwaa tuzo ya Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/17/dembele-atwaa-tuzo-ya-fifa/feed/ 0
Dembele abeba Ballon d’Or https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/dembele-abeba-ballon-dor/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/dembele-abeba-ballon-dor/#respond Tue, 23 Sep 2025 19:40:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13939 Paris, UfaransaWinga wa PSG, Ousmane Dembele ameshinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2025 na kuwa mchezaji wa kwanza wa PSG kubeba tuzo hiyo akiwabwaga Mohamed Salah wa Liverpool na Lamine Yamal wa Barcelona.Dembele ambaye alitwaa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika usiku wa Jumatatu hii Septemba 22, 2025 jijini Paris, pia anakuwa mchezaji wa kwanza […]

The post Dembele abeba Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Winga wa PSG, Ousmane Dembele ameshinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2025 na kuwa mchezaji wa kwanza wa PSG kubeba tuzo hiyo akiwabwaga Mohamed Salah wa Liverpool na Lamine Yamal wa Barcelona.
Dembele ambaye alitwaa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika usiku wa Jumatatu hii Septemba 22, 2025 jijini Paris, pia anakuwa mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kubeba tuzo hiyo baada ya Karim Benzema kufanya hivyo mwaka 2018.
Kwa ushindi huo Dembele pia anakuwa mshindi wa 34 akiwa ameibeba tuzo hiyo kutoka kwa Rodri wa Man City ambaye aliibuka kinara mwaka 2024.
Baada ya kuandamwa na janga la kuwa majeruhi na kuonkeana kama ameanza kupoteza kiwango, mambo yalianza kumnyookea Dembele katika msimu uliopita, alicheza mechi 49 za PSG katika mashindano yote na kufunga mabao 33 huku akitoa asisti 15.
Katika msimu huo Dembele pia alimaliza Ligi Kuu Ufaransa maarufu Ligi 1 akiwa mfungaji bora mwenye mabao 21 katika mechi 29 za ligi hiyo.
Kubwa zaidi kwa Dembele hayakuwa mabao aliyofunga bali ubora wakati katika kutengeneza mashambulizi na kuwa mbunifu katika kila mechi aliyozocheza.
Kwa upande wa mataji, mchango wa Dembele haukujificha kwani PSG ilifanikiwa kubeba taji la Ligi 1, taji la Ufaransa na Ligi ya Mabingwa Ulaya walilolibeba kibabe kwa kuinyuka Inter Milan ya Italia mabao 5-0 katika mechi ya fainali.
Katika mechi hiyo ya fainali Dembele alitoa asisti mbili zilizozaa mabao ya Khvicha Kvaratskhelia na Desire Doue na hivyo kuwa mchezaji wa kwanza baada ya Marcelo kutoa asisti mbili kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika kipindi chote cha kulisaka taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mchango wa Dembele ulikuwa wazi kwa kutoa asisti sita na kufunga mabao manane lakini anakumbukwa zaidi kwa bao lake lililoizamisha Liverpool na kwa bao la ushindi dhidi ya Arsenal katika mechi ya nusu fainali.
Dembele pia anakumbukwa kwa kufunga mabao matatu katika mechi moja (hat trick) kwa mechi mbili mfululizo, alianza katika mechi dhidi ya VfB Stuttgart kwenye Ligi ya Mabingwa na siku chache baadaye dhidi ya Brest katika mechi ya Ligi 1.

The post Dembele abeba Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/23/dembele-abeba-ballon-dor/feed/ 0
Dembele yuko fiti, aisubiri Arsenal https://www.greensports.co.tz/2025/05/06/dembele-yuko-fiti-aisubiri-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/06/dembele-yuko-fiti-aisubiri-arsenal/#respond Tue, 06 May 2025 20:00:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13416 Paris, UfaransaMshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembele yuko fiti kwa ajili ya mechi ya kesho Jumatano Mei 7, 2025 dhidi ya Arsenal baada ya kupona matatizo ya misuli yaliyokuwa yakimkabili.Awali, Dembele ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ufaransa alikuwa katika hatihati ya kucheza mechi hiyo ya nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya […]

The post Dembele yuko fiti, aisubiri Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Paris, Ufaransa
Mshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembele yuko fiti kwa ajili ya mechi ya kesho Jumatano Mei 7, 2025 dhidi ya Arsenal baada ya kupona matatizo ya misuli yaliyokuwa yakimkabili.
Awali, Dembele ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ufaransa alikuwa katika hatihati ya kucheza mechi hiyo ya nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kumaliza mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Emirates.
Dembele ambaye ndiye aliyefunga bao pekee na la ushindi katika mechi ya kwanza, alikosa mechi ya Ligi 1 ya PSG na Strasbourg wikiendi iliyopita lakini jana Jumatatu alianza mazoezi.

“Amekuwa akifanya mazoezi nasi kwa siku mbili zilizopita, mlimuona Jumanne (leo) ameshiriki ratiba ya kawaida ya mazoezi na atakuwa uwanjani kwa ajili ya mechi ya Jumatano,” alisema kocha wa PSG, Luis Enrique.


Dembele ambaye alijiunga na PSG mwaka 2023 akitokea Barcelona, kwa sasa ndiye mfungaji wa PSG mwenye mabao mengi msimu huu akiwa amefikisha mabao 33.
Arsenal ambao watakuwa ugenini watatakiwa kuhakikisha wanapata ushindi ili kusonga mbele baada ya kupoteza mechi ya kwanza wakiwa nyumbani.
Timu itakayosonga mbele itaumana katika mechi ya fainali na mshindi wa mechi kati ya Inter Milan na Barcelona ambazo zinaumana usiku wa Jumanne hii.

The post Dembele yuko fiti, aisubiri Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/06/dembele-yuko-fiti-aisubiri-arsenal/feed/ 0
Dembele ahamia PSG https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/#respond Wed, 02 Aug 2023 11:55:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7223 Las Vegas, MarekaniKocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Ousmane Dembele (pichani) anahamia PSG.Dembele mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barca mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 135 milioni na amefunga mabao 40 katika mechi 185 hadi sasa.Leo Jumatano Dembele alikuwa mmoja wa wachezaji wa […]

The post Dembele ahamia PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Las Vegas, Marekani
Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba mshambuliaji wa timu hiyo, Ousmane Dembele (pichani) anahamia PSG.
Dembele mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barca mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 135 milioni na amefunga mabao 40 katika mechi 185 hadi sasa.
Leo Jumatano Dembele alikuwa mmoja wa wachezaji wa akiba wa Barca katika mechi ya kirafiki dhidi ya AC Milan iliyopigwa mjini Las Vegas na Barca kutoka na ushindi wa bao 1-0 lakini mchezaji huyo hakucheza.
“Amesema kwamba hili ni wazo lake na ameamua kuondoka, ni uamuzi wake binafsi, napenda kuwa wazi katika hilo,” alisema Xavi.
“Ameamua kuwa muwazi, hilo ni wazo lake la kwenda Paris Saint Germain (PSG) kwamba ameitwa huko na sisi hapa hatuwezi kufanya lolote na ndio maana hakucheza hii leo,” alisema.

“Inaniuma mimi kwa sababu nafikiri tumekuwa tukimuangalia vizuri hapa ili awe mwenye furaha na kuwa nasi na kuendelea kuleta tofauti katika timu yetu,” aliongeza Xavi.


Mwaka jana, Dembele alisaini mkataba wa miaka miwili na Barca na kuweka rekodi ya kutoa asisti nyingi kwenye La Liga na Desemba mwaka jana alikuwamo kwenye timu ya Ufaransa iliyofikia hatua ya fainali ya Kombe la Dunia kabla ya kubwagwa na Argentina.
Msimu uliopita wa 2022-23 ambao Barca ilibeba taji la La Liga, Dembele alikosa sehemu kubwa ya nuus ya pili ya msimu huo kutokana na majeraha ya misuli yaliyokuwa yakimkabili.

The post Dembele ahamia PSG first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/02/dembele-ahamia-psg/feed/ 0