Dar Derby - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 08 Mar 2026 10:37:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Dar Derby - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Refa aliyekataa bao la Simba afungiwa https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/refa-aliyekataa-bao-la-simba-afungiwa/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/refa-aliyekataa-bao-la-simba-afungiwa/#respond Sun, 08 Mar 2026 08:59:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14402 Na mwandishi wetuMwamuzi msaidizi namba moja wa mechi ya mahasimu wa soka Yanga na Simba, Kassim Mpanga (pichani) wa Dar es Salaam amefungiwa miezi sita kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za soka kwa kukataa bao halali la Simba.Taarifa ya kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu iliyopatikana Machi 6, […]

The post Refa aliyekataa bao la Simba afungiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwamuzi msaidizi namba moja wa mechi ya mahasimu wa soka Yanga na Simba, Kassim Mpanga (pichani) wa Dar es Salaam amefungiwa miezi sita kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za soka kwa kukataa bao halali la Simba.
Taarifa ya kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu iliyopatikana Machi 6, 2026 ilieleza kuwa katika dakika ya 70 ya mchezo huo, mwamuzi huyo alikataa bao hilo kwa kuonesha kuwa kuna mchezaji aliotea wakati haikuwa hivyo.
Bao hilo la Simba lilifungwa na Seleman Mwalim na baadaye wataalam wa kutafsiri sheria za soka baada ya kufanyia tathmini kupitia video wamebainisha kuwa hakukuwa na kosa lolote kabla ya kufungwa bao hilo.
Naye mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi hiyo, Hamdan Said wa Mtwara amefungiwa miezi mitatu pia kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria za soka ambapo dakika ya 61 aliashiria mshambuliaji wa Yanga Prince Dube alikuwa ameotea.
Katika kipindi hicho Yanga walifanya shambulizi langoni mwa Simba na kitendo cha mwamuzi huyo kutoa ishara ya kuotea maana yake ni kwamba shambulizi hilo la Yanga lilikwama wakati mchezaji huyo hakuwa katika mazingira ya kuotea.
Adhabu nyingine katika mechi hiyo hiyo pia ilitolewa kwa klabu ya Simba ambayo imetozwa faini ya Sh milioni tano kwa kuingia Uwanja wa New Amaan kwa kutumia mlango usio rasmi.
Simba pia wametozwa faini nyingine ya Sh milioni tano kwa kosa la kukataa kutumia vyumba vya kubadilishia nguo na badala yake kutumia chumba kinachotumiwa kwa ajili ya mikutano na wanadishi wa habari.
Klabu hiyo pia imetakiwa kulipia gharama za matengenezo ya mlango wa kuingia katika chumba cha mikutano na waandishi wa habari baada ya walinzi wake kuvunja mlango huo na kulazimisha kuingia humo badala ya kutumia chumba cha kubadilishia nguo.
Katika tukio jingine la mechi hiyo, klabu za Simba na Yanga kila moja imetozwa faini ya Sh milioni tano kwa kosa la walinzi wao kugombana na kutoleana lugha chafu jambo lililozua taharuki na kuchafua taswira ya mchezo huo wakati klabu ya Simba ikiingia uwanjani.

The post Refa aliyekataa bao la Simba afungiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/refa-aliyekataa-bao-la-simba-afungiwa/feed/ 0
Yanga, Simba hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/#respond Mon, 02 Mar 2026 08:22:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14389 Na mwandishi wetuVigogo wa soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga wametoka sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa usiku wa Jumapili, Machi Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.Kwa matokeo hayo, Yanga wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 29 na Simba kushika nafasi ya […]

The post Yanga, Simba hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Vigogo wa soka la Tanzania, timu za Simba na Yanga wametoka sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa usiku wa Jumapili, Machi Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, Yanga wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 29 na Simba kushika nafasi ya tatu na pointi zao 24, timu zote hizo kila moja imeshacheza mechi 11.
Matokeo hayo pia yanaifanya Yanga kufikisha mechi ya saba mfululizo bila kufungwa na Simba ingawa matokeo ya sare siyo yaliyotegemewa na mashabiki walio wengi wa timu hiyo bingwa mtetezi wa ligi.
Simba waliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo walionesha dhamira yote ya kufuta uteja wa mechi saba zilizopita kwa kutengeneza nafasi kadhaa langoni mwa Yanga lakini hazikuzaa matunda.
Shambulizi la kwanza kabisa la kutisha la Simba langoni mwa Yanga lilifanyika dakika ya nne baada ya Jospin Loemba kuinasa pasi ya Nickson Kibabage na kufumua shuti lakini kipa Djigui Diarra alikuwa makini na kuokoa mpira huo.
Nao Yanga walijibu shambulizi hilo dakika tano baadaye, Mohamed Damaro akiwa katika nafasi nzuri aliufumania mpira na kufumua shuti ambalo hata hivyo lilitoka nje ya lango la Simba.
Katika dakika ya 70, Simba walifanya shambulizi la maana langoni mwa Yanga na kupata bao lililofungwa na Seleman Mwalimu lakini wakati mashabiki wao wakishangilia mwamuzi alipuliza filimbi kuashiria mfungaji aliotea.
Tukio hilo liliibua mzozo miongoni mwa wachezaji wa timu zote mbili na waamuzi kabla ya hali kutulia na mchezo kuendelea kama kawaida.
Wakizungumza baada ya mechi hiyo makocha wa timu hizo, Steve Barker wa Simba aliwasifia wachezaji wake licha ya kushindwa kupata ushindi wakati Pedro Concalves wa Yanga alisema mechi ilikuwa ngumu na kwamba Simba walitawala zaidi kipindi cha kwanza lakini wao Yanga walifanikiwa kuwadhibiti.
Mara ya mwisho Simba kutoka na ushindi mbele ya Yanga ilikuwa mwaka 2023 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, ushindi ambao ulipatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.

The post Yanga, Simba hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/02/yanga-simba-hakuna-mbabe/feed/ 0
Mwinchui kuzihukumu Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/mwinchui-kuzihukumu-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/mwinchui-kuzihukumu-simba-yanga/#respond Sat, 28 Feb 2026 07:25:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14373 Na mwandishi wetuMwamuzi Nassoro Mwinchui wa Tanga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati katika mechi ya Ligi Kuu NBC kati ya watani wa jadi nchini Tanzania, Simba na Yanga itakayopigwa Machi Mosi, 2026 kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar.Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana Februari 27, 2026 ilielezxa kuwa mwamuzi huyo atasaidiwa na Kassim […]

The post Mwinchui kuzihukumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwamuzi Nassoro Mwinchui wa Tanga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati katika mechi ya Ligi Kuu NBC kati ya watani wa jadi nchini Tanzania, Simba na Yanga itakayopigwa Machi Mosi, 2026 kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana Februari 27, 2026 ilielezxa kuwa mwamuzi huyo atasaidiwa na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam ambaye atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja na Hamdan Said wa Dodoma ambaye atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.
Sambamba na waamuzi hao, mwamuzi wa akiba atakuwa Ramadhan Kayoko wa Dar es Salaam na mthamini waamuzi katika mechi hiyo atakuwa Israel Mjuni pia wa Dar es Salaam.
Uteuzi wa Mwinchui kuwa mwamuzi wa kati umekuja wakati presha ya mechi hiyo ikiwa juu miongoni mwa mashabiki wa klabu hizo ambapo wapo wanaohoji kama ataweza kukabiliana na presha za mechi hiyo kubwa.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Juni 25, 2025 katika mechi ya ligi hiyo, Yanga ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 na mechi hiyo ilichezeshwa na mwamuzi wa kati Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.
Mwamuzi huyo wa kimataifa alipewa jukumu hilo baada ya kuibuka mzozo wa muda mrefu kuhusu mechi hiyo ambayo iliahirishwa mara kadhaa hadi viongozi wa serikali kuingilia kati na hatimaye makubaliano yakafikiwa.

The post Mwinchui kuzihukumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/28/mwinchui-kuzihukumu-simba-yanga/feed/ 0
Pacome aipa Yanga Ngao ya Jamii https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/pacome-aipa-yanga-ngao-ya-jamii/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/pacome-aipa-yanga-ngao-ya-jamii/#respond Tue, 16 Sep 2025 19:20:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13913 Na mwandishi wetuBao pekee la Pacome Zouzoua limeifanya Yanga kuendelea kuwanyanyasa mahasimu wao Simba kwa kutoka na ushindi wa 1-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa leo Jumanne Septemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.Huu ni ushindi wa sita mfululizo wanaupata Yanga dhidi ya Simba lakini ushindi wa leo umekuwa mtamu […]

The post Pacome aipa Yanga Ngao ya Jamii first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la Pacome Zouzoua limeifanya Yanga kuendelea kuwanyanyasa mahasimu wao Simba kwa kutoka na ushindi wa 1-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa leo Jumanne Septemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.
Huu ni ushindi wa sita mfululizo wanaupata Yanga dhidi ya Simba lakini ushindi wa leo umekuwa mtamu baada ya Yanga kubeba Ngao ya Jamii na hivyo kuashiria mwanzo mzuri wa timu hiyo katika msimu mpya wa 2025-26 ambao pazia lake limefunguliwa rasmi kwa mechi hiyo.
Yanga inabeba taji hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo wakati wakiukaribisha msimu uliopita wa 2024-25 kwa kuichapa Azam FC mabao 4-1.
Ushindi wa leo ulipatikana katika dakika ya 53 baada ya kipa wa Simba, Muosa Camara kushindwa kuumiliki mpira uliopigwa na Maxi Nzengeli na kumkuta Pacome ambaye alionesha utulivu na kupiga mpira uliojaa wavuni.
Timu zote ziliuanza mchezo kwa kasi na kuonesha shauku ya kutaka ushindi huku Kibu Denis akishindwa kuipatia Simba bao dakika ya 27 na beki Shomari Kapombe akishindwa kuitumia vyema nafasi aliyoipata dakika ya 40, Kibu na Kapombe wakiwa karibu na kipa Djigui Diarra walipiga mashuti yaliyotoka nje ya lango.
Yanga nao walifanya shambulizi la maana kipindi hicho hicho lakini mshambuliaji wake Prince Dube alishindwa kuunganisha vizuri krosi iliyochongwa na Aziz Andambwile kwa kuupiga mpira kwa bega na hivyo kudakwa kiulaini na kipa wa Simba, Camara.

Dakika chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza, kipa wa Yanga, Djigui Diarra alifanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Seleman Mwalimu na hivyo kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuingia Mamadou Doumbia mabadiliko ambayo yalionekana kuongeza kasi ya mchezo kabla ya Yanga kupata bao la Pacome.
Bao hilo lilionekana kuitia hasira Simba ambayo iliongeza kasi ya mashambulizi lakini ukuta wa Yanga chini ya Ibrahim Bacca na wenzake ulikuwa imara katika kuhakikisha mashambulizi hayo hayaleti madhara.
Yanga iliendelea kufanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa, Shadrack Boka, Maxi Nzengeli, Duke Abuya na Prince Dube na kuwaingiza, Balla Conte, Celestine Ecua, Clement Mzize na Mohamed Hussein.
Simba nao katika mabadiliko yao waliwatoa Elly Mpanzu, Stephen Mukwala na Allasane Cante na nafasi zao kuchukuliwa na Neo Maena, Anthony Mligo na Mwalimu.

The post Pacome aipa Yanga Ngao ya Jamii first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/pacome-aipa-yanga-ngao-ya-jamii/feed/ 0
Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/#respond Sun, 13 Jul 2025 20:20:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13700 Na mwandishi wetuKwa mara ya kwanza mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ilichezeshwa na mwamuzi Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.Katika mechi hiyo iliyopigwa Juni 25, 2025 na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-0, bila shaka hakukuwa na matukio yaliyoacha maswali au kuzua mijadala kuhusu ubora wa mwamuzi.Ukiachana […]

The post Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kwa mara ya kwanza mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ilichezeshwa na mwamuzi Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Juni 25, 2025 na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-0, bila shaka hakukuwa na matukio yaliyoacha maswali au kuzua mijadala kuhusu ubora wa mwamuzi.
Ukiachana na tukio la kipa wa Simba, Mousa Camara kugongana na kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua na kuzaa penalti iliyozaa bao, hakuna tukio jingine lililozua mijadala, mechi ilikwenda vizuri na kwa utulivu wa hali ya juu.
Mjadala wa tukio la Pacome na Camara, kwa Simba wanaamini haikuwa penalti kwa kuwa kipa aliruka kuufuata mpira wakati Yanga wanaamini ilikuwa penalti kutokana na mgongano uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na mruko wa kipa.
Nje ya tukio hilo, mwenendo wa mchezo na jinsi mwamuzi alivyokuwa uwanjani kila eneo na kufuatilia kwa umakini ni kati ya mambo ambayo yameacha somo kwa waamuzi wa Tanzania.
Ukiachana na umakini huo, mwamuzi huyo pia alituonesha namna mwamuzi anavyotakiwa kuutawala mchezo kwa kutokubali kuchezewa au kujaribiwa na wachezaji pale anapoamini kwamba amefanya uamuzi sahihi.
Mfano hakukubali mchezaji kuonesha kwa ishara ya kutoridhika na maamuzi anayoyachukua kwa kujifanya ameonewa au kufanya tukio lolote baada ya filimbi kupulizwa.
Mifano ya hiyo ilijionesha kwa Kibu Denis wa Simba pale mwamuzi alipopuliza filimbi kuashiria mpira umetoka na urushwe kuelekea lango la Simba.
Kibu pengine kwa kutaka kumjaribu, akaonesha kuchukizwa na maamuzi hayo kwa kuudunda mpira chini kwa hasira ili ionekane kama Simba ndio waliotakiwa kurusha mpira huo kuelekea kwa Yanga.
Mwamuzi alimfuata kwa karibu Kibu huku akionekana mwenye hasira na kumuonya kwa ishara ya kukataa kujaribiwa.
Tukio kama hilo pia lilitokea kwa Duke Abuya wa Yanga aliyeanguka chini kama vile aliyechezewa rafu mbaya na kutaka kumshawishi mwamuzi apulize filimbi lakini mwamuzi huyo alimtolea macho na kumpa ishara ya kutotaka kujaribiwa.
Tukio kama hilo linanikumbusa kisa alichowahi kusimulia mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool ya England, Steven Gerard wakati akimsifia mwamuzi Pierluigi Collina wa Italia kwa umakini.
Katika moja ya mechi, Steven Gerard akiwa nahodha Liverpool alijaribu kwa uwongo kujifanya kaumizwa ili kumshawishi mwamuzi apulize filimbi kuibeba timu yake lakini mwamuzi huyo alibaini tukio hilo na kumtolea macho ya ukali huku akimwambia ‘stop fuck around with me’ (acha kuniletea mzaha, au acha kunijaribu).
Kitu hicho pia ndicho nilichokiona kwa Amin Mohammed Omar, hakuruhusu wachezaji wafanye mzaha na kazi yake au wamjaribu.
Clement Mzize wa Yanga aliubutua mpira nje wakati mwamuzi alishapuliza filimbi, Shadrack Boka naye hivyo hivyo alipiga mpira kwa lengo la kufunga goli baada ya mwamuzi kupuliza filimbi kuashiria kuotea.
Katika matukio yote hayo mawili, Amin Mohammed Omar alionesha jinsi asivyotaka masihara kazini, wote akawaonya kwa ishara ya ukali.
Kuyasimamia matukio hayo kama alivyofanya Amin Mohammed Omar ni sababu tosha inayosaidia kulinda hadhi na heshima ya mwamuzi kwa kutokubali kuchezewa, hiyo ni mbali na umakini ambalo ni jambo la lazima kwa mwamuzi yeyote.
Kwa hiyo ni vyema kwa waamuzi wetu mbali na somo la umakini lakini wawapo uwanjani wasikubali kuchezewa au kujaribiwa na wachezaji.

The post Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/feed/ 0
Yanga yaua Mnyama, yabeba taji ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/yanga-yaua-mnyama-yabeba-taji-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/yanga-yaua-mnyama-yabeba-taji-ligi-kuu/#respond Wed, 25 Jun 2025 16:48:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13664 Na mwandishi wetuYanga imemchapa hasimu wake Simba au Mnyama mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatano Juni 25, 2025 na kufanikiwa kubeba moja kwa moja taji la ligi hiyo kwa mara ya nne mfululizo.Ushindi huo uliopatikana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam unaifanya Yanga kubeba taji la msimu […]

The post Yanga yaua Mnyama, yabeba taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga imemchapa hasimu wake Simba au Mnyama mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatano Juni 25, 2025 na kufanikiwa kubeba moja kwa moja taji la ligi hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Ushindi huo uliopatikana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam unaifanya Yanga kubeba taji la msimu huu wa 2024-25 ikiwa na pointi 82 na kuiacha Simba nafasi ya pili ikiwa na pointi 78.
Alikuwa ni Pacome Zouzoua aliyeanza kuzamisha jahazi la Simba dakika ya 66 kwa bao la mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa ndivyo sivyo na kipa wa Simba, Mousa Camara.
Pacome alikuwa wa kwanza kuuchukua mpira huo na kuuweka katika eneo sahihi kabla ya kupiga kiufundi na kumhadaa kipa Camara ambaye alikuwa kama aliyevurugwa na kujikuta akiuangalia mpira ukiingia wavuni kwa upande wake wa kushoto.
Yanga waliandika bao la pili katika dakika ya 86 mfungaji akiwa Clement Mzize, kwa mara nyingine juhudi za Pacome zilionekana kwa namna alivyotoa pasi iliyozaa bao hilo.
Simba ndio walioanza mapema kulisakama lango la Yanga, dakika ya pili baada ya Khalid Aucho kuporwa mpira lakini Steven Mukwala aliyefanya kazi hiyo alishindwa kuutumia mpira huo kuipatia timu yake bao.
Yanga nao wakajibu mapigo dakika mbili baadaye, Shedrack Boka aliambaa na mpira kabla ya kupiga krosi iliyofika eneo la kipa Camara lakini utulivu wa mabeki wa Simba ukasaidia kuepusha madhara kwenye lango la timu hiyo.
Dakika ya 11, Mudathir Yahya alionesha ubora wake baada ya kumzunguka Chamou Karaboue na kupiga pasi iliyomkuta Prince Dube ambaye alimpasia Pacome lakini shuti lake lilipaa juu ya lango.
Yanga waliendelea na mashambulizi safari hii dakika ya 18, Israel Mwenda alipiga krosi ambayo ilimkuta Boka lakini shuti lake lilitoka nje ya lango.
Mashambulizi hayo yaliendelea hadi kipindi cha kwanza kinamaliza na Simba kuanza kipindi cha pili kwa mabadiliko wakimtoa Joshua Mutale na nafasi yake kuingia Kibu Denis na baadaye kumtoa Kagoma na nafasi yake kuingia Abdulrazak Hamza na Mukwala ambaye nafasi yake aliingia Leonel Ateba.
Mabadiliko hayo yaliimarisha Simba ambayo ilianza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Yanga mfano dakika ya 60 Elly Mpanzu alifumua shuti ambalo lilitoka sentimita chache nje ya lango la Yanga.
Yanga nayo ilifanya mabadiliko kadhaa ikiwamo kumtoa Mudathir, Pacome, Dube na Duke Abuya na nafasi zao kuchukuliwa na Clatous Chama, Mzize, Salum Aboubakar na Jonathan Ikangalombo.
Ushindi wa Yanga unakuwa umemaliza mijadala na mizozo iliyotawala kwa takriban miezi mitatu sasa tangu kuahirishwa mechi hiyo ambayo awali ilipangwa kuchezwa Machi 8 lakini ikaahirishwa hadi Juni 15 kabla ya kuahirishwa tena hadi Juni 25.
Mijadala hiyo miongoni mwa mashabiki ikiwamo kutokuwa na imani na waamuzi wa Tanzania, inaaminika kuwa sababu ya TFF kuchukua uamuzi mgumu wa kuwapa mechi hiyo waamuzi kutoka nchini Misri walioongozwa na Amin Mohammed Omar aliyekuwa mwamuzi wa kati.

The post Yanga yaua Mnyama, yabeba taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/yanga-yaua-mnyama-yabeba-taji-ligi-kuu/feed/ 0
Waamuzi wa Misri wapewa mechi ya Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2025/06/24/waamuzi-wa-misri-wapewa-mechi-ya-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/24/waamuzi-wa-misri-wapewa-mechi-ya-simba-yanga/#respond Tue, 24 Jun 2025 06:40:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13653 Na mwandishi wetuMwamuzi Amin Mohammed Omar (pichani) kutoka Misri ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi ya mahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba, itakayochezwa Jumatano, Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.Uteuzi wa mwamuzi huyo wa kigeni umekuja baada ya kuwapo mjadala kuhusu nani mwamuzi sahihi wa kuchezesha mechi hiyo […]

The post Waamuzi wa Misri wapewa mechi ya Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Mwamuzi Amin Mohammed Omar (pichani) kutoka Misri ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi ya mahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba, itakayochezwa Jumatano, Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Uteuzi wa mwamuzi huyo wa kigeni umekuja baada ya kuwapo mjadala kuhusu nani mwamuzi sahihi wa kuchezesha mechi hiyo ambayo mshindi wake atakabidhiwa taji la Ligi Kuu NBC msimu wa 2024-25.
Mbali na mwamuzi huyo wengine watakaomsaidia ambao pia wanatokea Misri ni Mahmoud Ahmed na Samir Gamal wakati mwamuzi msaidizi atakuwa Ahmed Mahrous na kamisaa wa mchezo huo atakuwa Salim Singano ambaye anatokea Tanga.
Kabla ya waamuzi hao kutangazwa majina kadhaa ya waamuzi wakiwamo Ahmed Arajiga, Ramadhan Kayoko, Kefa Kayombo na wengineo yamekuwa yakijadiliwa katika siku za karibuni hasa kwenye mitandao ya kijamii.
Hatimaye TFF wamekuja na uamuzi tofauti kwa kuwakabidhi mechi hiyo waamuzi kutoka Misri ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mechi hiyo maarufu Dar Derby kuchezeshwa na waamuzi kutoka taifa hilo.
Yanga wanamkumbuka mwamuzi Omar kwa kuwa ndiye aliyekuwa mwamuzi katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mechi iliyopigwa Machi mwaka jana kwenye Uwanja wa Benjamina Mkapa na kumalizika kwa sare ya 0-0.
Simba nao wanamkumbuha mwamuzi huyo katika mechi yao ya Ligi ya Mabngwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea, iliyopigwa Februari 2023 nchini Guinea na Simba kulala kwa bao 1-0.
Mechi ya Simba na Yanga itachezwa baada ya kuahirishwa mara mbili kufuatia mivutano iliyojitokeza, awali ilikuwa ichezwe Machi 8, 2025 lakini ukaibuka mvutano baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi.
Kitendo hicho kiliwafanya viongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuiahirisha kwa sababu walizozitaja kuwa ni za kiusalama huku Simba wakidai kwamba wasingecheza mechi siku hiyo hadi waliowazuia kufanya mazoezi watakapoadhibiwa.
Baadaye TPLB walitangaza kuahirisha mechi hiyo kwa sababu kadhaa kubwa ikiwa ni ya kiusalama na ndipo Yanga nao walipoibuka wakisema hawako tayari kucheza siku nyingine hadi waliohusika kuahirishwa kwa mechi hiyo watakapoadhibiwa.
TPLB walitangaza mechi hiyo ingechezwa Juni 15, 2025 kabla ya kuahirishwa kwa mara nyingine na kutangaza tarehe ya sasa ambayo ni Juni 25 na waamuzi kutoka Misri kupewa majukumu.
Yanga wameonesha utayari wa kucheza mechi hiyo wakati Simba wakionekana kutoonesha msimamo wao kama watacheza au hawatacheza badala yake wamekuwa wakitoa madai kwamba mamlaka za soka zinaibeba Yanga.

The post Waamuzi wa Misri wapewa mechi ya Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/24/waamuzi-wa-misri-wapewa-mechi-ya-simba-yanga/feed/ 0
Mechi Yanga, Simba yaahirishwa https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/#respond Sat, 08 Mar 2025 12:41:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13102 Na Hassan KinguMechi ya Ligi Kuu NBC baina ya mahasimu wa soka nchini Tanzania, Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025, imeahirishwa.Uamuzi huo umetangazwa leo Jumamosi Machi 8 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na taarifa zake kutufikia saa takriban nne kabla ya muda wa kuchezwa mechi hiyo.Mechi ilipangwa kuchezwa majira […]

The post Mechi Yanga, Simba yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Mechi ya Ligi Kuu NBC baina ya mahasimu wa soka nchini Tanzania, Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025, imeahirishwa.
Uamuzi huo umetangazwa leo Jumamosi Machi 8 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na taarifa zake kutufikia saa takriban nne kabla ya muda wa kuchezwa mechi hiyo.
Mechi ilipangwa kuchezwa majira ya saa moja na robo usiku kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam na uamuzi huo umefikiwa baadhi ya mashabiki wakiwa tayari wamefika uwanjani hapo.
Uamuzi wa bodi hiyo umekuja baada ya kuibuka sintofahamu kutokana na kitendo cha Simba ambao ni timu mgeni kuzuiwa na timu mwenyeji ambao ni Yanga kuutumia uwanja husika kwa ajili ya mazoezi kama taratibu zinavyotaka.
Simba baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi iliwasilisha malalamiko yake TPLB huku ikielezea nia yake ya kutoshiriki mechi hiyo baada ya kunyimwa haki yao ya kikanuni ya kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.
Bodi kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya TPLB iliitisha kikao cha dharura na baada ya taarifa mbalimbali kuwafikia kutoka kwa maofisa wake na vyanzo husika ilibaini mambo kadhaa.
Kamati hiyo ilibaini kuwa Simba wakati wakielekea uwanjani kuitumia haki yao ya kuutumia uwanja huo kwa mazoezi haikuwasiliana na ofisa yeyote wa mchezo.


Simba pia haikuwasiliana na timu mwenyeji wala mamlaka ya uwanja kuhusu nia yao ya kuutumia uwanja huo kwa mazoezi ili maandalizi yafanyike kikanuni.
Kamati pia ilibaini kuwa walinzi ambao baadhi yao walifahamika kwa sura kuwa ni wa Yanga walishiriki tukio la kuzuia basi la Simba kuingia uwanjani kinyume na taratibu za mchezo wa ligi kuu.
Bodi pia ilipokea taarifa ya ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyoambatana na tukio la Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.
Kutokana na matukio yote hayo bodi imeona yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati na hivyo imeamua kuiahirisha mechi hiyo.
“Kutokana na matukio hayo bodi, kupitia kamati ya uendeshaji imeamua kuahirisha mchezo husika ili kutoa nafasi ya kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki,” ilieleza kwa ufafanuzi sehemu ya taarifa ya bodi.
Bodi pia imeahidi kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kutangaza tarehe ya mchezo huo mapema iwezekanavyo.
Pigo kwa Yanga, mashabiki
Uamuzi wa kuahirisha mechi hiyo utakuwa pigo kubwa kwa mashabiki ambao baadhi yao wamesafiri kutoka mikoani na hata nje ya nchi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo.
Mashabiki hao bila shaka wengi wao waliamini kuwa mechi inapochezwa Jumamosi, wnaaweza kuwa na muda wa kutosha kurejea mikoani kuendelea na shughuli zao kama kawaida kuanzia Jumatatu.
Kwa upande wa Yanga pia haijulikani hali itakuwaje kutokana na uamuzi huo kwani walishaahidi mapema katika taarifa yao kwamba hawatokuwa tayari kucheza mechi siku nyingine zaidi ya leo.
Je wataafikiana na uamuzi wa bodi kuahirisha mechi au watasimamia msimamo wao wa kutokuwa tayari kucheza mechi hiyo siku nyingine zaidi ya leo?

The post Mechi Yanga, Simba yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/feed/ 0
Mechi Yanga, Simba njia panda https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/#respond Sat, 08 Mar 2025 11:26:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13095 Na Hassan KinguUtata umeibuka kuhusu mechi ya Simba na Yanga ambayo imepangwa kuchezwa leo Jumamosi Machi 8, 2025 na huenda mechi hiyo isichezwe baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.Yanga ambao ni wenyeji wa mechi hiyo wanadaiwa kuwazuia Simba kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi ingawa nao wametoa taarifa leo […]

The post Mechi Yanga, Simba njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Utata umeibuka kuhusu mechi ya Simba na Yanga ambayo imepangwa kuchezwa leo Jumamosi Machi 8, 2025 na huenda mechi hiyo isichezwe baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.
Yanga ambao ni wenyeji wa mechi hiyo wanadaiwa kuwazuia Simba kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi ingawa nao wametoa taarifa leo Jumamosi wakisisitiza mechi ipo kama kawaida.
Simba katika raarifa yao walielezea kitendo cha kuzuiwa kufanya mazoezi na kuitaja kanuni ya ligi kuu inayotaka timu mgeni kufanya mazoezi kwenye uwanja itakayochezwa mechi angalau siku moja kabla ya mechi.
Katika hoja yao Simba wanadai kunyimwa fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na wenyeji wa mechi Yanga kwa makusudi licha ya kufika uwanjani katika muda husika.
Baada ya kufika uwanjani Ijumaa kwa ajili ya mazoezi, waliarifiwa na meneja uwanja kuwa hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila ya taarifa ya kamishna wa mchezo husika.


Katika hali ambayo haikutarajiwa, Simba katika taarifa yao wanadai kuwa hata baada ya kamishna wa mchezo kufika, mabaunsa wanaoaminika kuwa wa Yanga walizuia msafara wa Simba kuingia uwanjani hapo kufanya mazoezi.
Iliwachukua Simba saa takriban mbili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda na hatimaye wakaamua kuondoka eneo hilo kwa sababu walizozitaja kuwa ni za kiusalama.
Kutokana na sakata hilo, Simba wameahidi kutoshiriki katika mchezo wao na Yanga na kutaka hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika wote.
Taarifa ya Yanga
Baada ya uamuzi huo wa Simba, Yanga nao wametoa taarifa wakisisitiza kwamba mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika leo Jumamosi ya Machi 8, 2025 upo pale pale kama ilivyopangwa na hakuna mabadiliko yoyote.
Yanga kama wenyeji wa mchezo wamedai kufuata taratibu zote husika kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za ligi hiyo na maandalizi yote yapo tayari.


Zaidi ya hilo uongozi wa Yanga umeahidi kupeleka timu uwanjani na hautakuwa tayari kucheza mchezo huo siku nyingine tofauti na leo yaani Jumamosi ya Machi 8, 2025.
Wakati Yanga wakitoa kauli hiyo, kiongozi mmoja mwandamizi wa Simba amenukuliwa katika vyanzo mbalimbali vya habari akisema kwamba Simba hawatopeleka timu hadi wahusika wa kadhia hiyo watakapoadhibiwa na mamlaka husika za soka.
Mazingira yote hayo yanaifanya mechi hiyo maarufu kwa jina la Kariakoo au Dar Derby kuwa njia panda hadi wakati huu.

The post Mechi Yanga, Simba njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/feed/ 0
Namba ngumu Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/#respond Sat, 08 Mar 2025 09:12:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13091 Na Hassan KinguMashabiki Simba na Yanga wanacharurana kuelekea mechi yao ya Jumamosi Machi 8, 2025, kila upande ukitamba kuwa bora kumshinda mwenzake lakini namba ambazo haziongopi zina jibu tofauti.Kwa mujibu wa namba ubora wa timu hizo katika Ligi Kuu NBC msimu huu hautofautiani kwa sana, ukweli wa namba unatupa picha tofauti kuhusu majigambo na kuzodoana […]

The post Namba ngumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Mashabiki Simba na Yanga wanacharurana kuelekea mechi yao ya Jumamosi Machi 8, 2025, kila upande ukitamba kuwa bora kumshinda mwenzake lakini namba ambazo haziongopi zina jibu tofauti.
Kwa mujibu wa namba ubora wa timu hizo katika Ligi Kuu NBC msimu huu hautofautiani kwa sana, ukweli wa namba unatupa picha tofauti kuhusu majigambo na kuzodoana kunakoendeea mitaani baina ya mashabiki wa timu hizo.
Mashabiki wangezifanyia tafakuri namba, wangekuwa na hofu kuelekea mechi ya Machi 8 badala ya kujigamba na kuzodoana kwa kuwa ukiziangalia timu zote 16 za kwenye ligi, Yanga na Simba ndizo zenye muendelezo mzuri wa ushindi.
Yanga inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 58 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 54, hivyo tofauti baina ya timu hizo ni pointi nne.
Pointi nne ni nyingi lakini Simba ipo nyuma kwa mchezo mmoja, imecheza mechi 21, Yanga imecheza mechi 22, kutokana na ubora wa timu hizo kwa namna zinazovyoshinda mechi zao tofauti yao kimsingi ni pointi moja.
Tunaamini Simba watashinda kama wanavyoshinda Yanga dhidi ya timu nyingine, hivyo tofauti itabaki pointi moja ambayo kimsingi ni ndogo na rahisi kuipoteza wakati wowote.
Maana yake ni kwamba mashabiki Yanga hawana sababu ya kujiamini kwamba wameshalibeba taji la ligi kwa mtaji wa pointi moja ambayo wanaweza kuipoteza wakati wowote, ni hivyo hivyo kwa Simba wapo nyuma kwa pointi moja na wana kazi ya kuisaka.
Kwa kuziangalia namba maana yake ni kwamba mechi ya Machi 8 inabaki kuwa muhimu kwa timu zote kuhakikisha zinashinda, ikishinda Yanga itakuwa faida zaidi kwani tofauti itakuwa ya pointi nne zenye uhakika si sawa na hizi za sasa wakati Simba ina kiporo cha mechi moja.


Ni hivyo hivyo ikishinda Simba itakuwa imeisogelea Yanga na kujitofautisha kwa pointi moja ya uhakika na kama wote wataendelea kushinda mechi zao hadi ligi itakapofikia tamati maana yake ni kwamba Simba italibeba taji ikiitangulia Yanga kwa pointi mbili.
Kwa shabiki ambaye ataziangalia timu hizo kwa kuzichambua namba atauona ukweli wa pointi hizo ulivyo na ambavyo utazitesa timu hizo, tofauti kwa sasa ni pointi moja au mbili.
Matokeo ya sare baina ya timu hizo kidogo yatakuwa msaada kwa Yanga kwa kuwa itajinasua katika tofauti ya pointi moja na kutanguliwa mechi moja badala yake itakuwa pointi moja ya uhakika ambayo hata hivyo ugumu wake upo pale pale. Ukipoteza mechi moja tu umwekwisha, ukitoka sare moja tu umejiweka pabaya.
Vyovyote itakavyokuwa Yanga inatakiwa kushinda mechi ya leo ili kujiweka pazuri katika kulibeba taji kama ambavyo Simba inatakiwa kushinda ili kuwaweka Yanga pagumu katika mbio za kulibeba taji.
Nje ya namba za pointi kuna namba za magoli, hapa ndipo Yanga wanapoweza kujivunia kwani wamewaacha Simba kwa tofauti ya mabao 12, Yanga wana mabao 48, Simba 36, hii inaweza kuwa faida kubwa kama timu zitafungana pointi.
Yanga hata hivyo hawawezi kuangalia idadi ya mabao hayo ni kujiaminisha kuwa ni mtaji wa kulibeba taji badala yake wanatakiwa kuendelea na wimbi la ushindi katika mechi zao zilizobaki, hapo tu wataweza kulitetea vyema taji hilo.

Namba nyingine
Namba nyingine ni za mabao ya kufungwa, Simba ina ahueni kwani imefungwa mabao manane dhidi ya Yanga iliyofungwa mabao tisa, lakini pia hii haiwezi kuwa na maana yoyote badala yake kila timu inatakiwa kushinda mechi zilizo mbele yake.
Pia kuna namba za uwiano wa mabao, Yanga ikiwa 49 Simba 38, hizi namba mwisho wa siku pia haziwezi kuwa na maana yoyote badala yake la muhimu ni timu kupata ushindi.
Ukiachana na namba za pointi ambazo ni muhimu kuliko namba zozote kwenye ligi, namba nyingine yaani za mabao ya kufunga, kufungwa na uwiano zitakuwa na maana tu pale timu zitakapofungana pointi katika mechi zao za mwisho.
Ili kujitoa katika namba hizo ngumu na zinazoleta hofu za kulibeba taji, tunajikuta tukirudi katika hoja ile ile ya kwamba kila timu inatakiwa ishinde kila mechi, na mtaji wa kwanza muhimu kuushinda ni hii mechi yao ya Machi 8.

The post Namba ngumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/feed/ 0