Conte - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 05 Jun 2024 17:54:39 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Conte - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Conte sasa kocha mkuu Napoli https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/conte-sasa-kocha-mkuu-napoli/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/conte-sasa-kocha-mkuu-napoli/#respond Wed, 05 Jun 2024 17:54:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11235 Napoli, ItaliaKocha wa zamani wa timu za Chelsea na Tottenham Hotspur, Antonio Conte ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Napoli ya Italia kwa mkataba wa miaka mitatu.Conte, 54, amekabidhiwa jukumu hilo ikiwa ni takriban mwaka mmoja na miezi miwili sasa tangu aachane na Spurs baada ya kuwa na timu hiyo kwa mwaka mmoja na […]

The post Conte sasa kocha mkuu Napoli first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Napoli, Italia
Kocha wa zamani wa timu za Chelsea na Tottenham Hotspur, Antonio Conte ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Napoli ya Italia kwa mkataba wa miaka mitatu.
Conte, 54, amekabidhiwa jukumu hilo ikiwa ni takriban mwaka mmoja na miezi miwili sasa tangu aachane na Spurs baada ya kuwa na timu hiyo kwa mwaka mmoja na miezi minne.
Akiwa na Chelsea, Conte alifanikiwa kuiwezesha timu hiyo kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) katika msimu wa 2016-17 pamoja na lile la FA kabla ya kutimuliwa mwaka 2018.
“Napoli ni sehemu yenye umuhimu wake duniani, nina furaha na naona ufahari katika jambo hili, kukaa katika benchi la bluu,” alisema Conte ambaye pia aliwahi kuinoa Inter Milan na mwaka 2021 aliiwezesha timu hiyo kubeba taji la kwanza la Serie A baada ya miaka 11.

“Naweza kuahidi jambo moja, nitafanya kila ninaloweza kwa maendeleo ya timu na klabu hii, kujituma kwangu pamoja na maofisa wengine kutakuwa ni kwa mapana,” alisema Conte.


Conte ambaye ni Mtaliano si jina geni katika soka la Italia kwamba mbali na Inter Milan pia aliwahi kuinoa Juventus na kuiwezesha kubeba mataji matatu ya Serie A kati ya mwaka 2011 na 2014.
Napoli ambayo msimu uliopita ilibeba taji la Serie A ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 33, msimu huu imeshindwa kuonesha ubora wake na imemaliza ligi ya Serie A ikiwa nafasi ya 10.
Mwenendo mbaya wa timu hiyo msimu huu ulisababisha kutimuliwa kwa kocha Francesco Calzona ambaye alipewa jukumu hilo Februari mwaka huu akiwa kocha wa muda baada ya kutimuliwa kwa Walter Mazzarri.

The post Conte sasa kocha mkuu Napoli first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/conte-sasa-kocha-mkuu-napoli/feed/ 0
Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/#respond Mon, 10 Jul 2023 05:53:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6892 London, EnglandMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema kwamba kocha wa zamani wa timu hiyo, Antonio Conte alimkaripia kwa takriban saa mbili wakati wakiwa kwenye kikao cha timu hiyo.Richarlison ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Spurs msimu uliopita wa 2022-23 chini ya Conte kabla […]

The post Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison (pichani) amesema kwamba kocha wa zamani wa timu hiyo, Antonio Conte alimkaripia kwa takriban saa mbili wakati wakiwa kwenye kikao cha timu hiyo.
Richarlison ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Spurs msimu uliopita wa 2022-23 chini ya Conte kabla ya kocha huyo kutimuliwa mwezi Machi.
Utata baina ya Richarlison na Conte ulianza baada ya mchezaji huyo kumshushia lawama kocha huyo baada ya Spurs kutolewa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo baadaye Conte alisema kwamba mchezaji huyo ni mbinafsi.
Richarlison hata hivyo alikiri kwamba alikosea kumlaumu kocha wake hadharani na kujikuta akipewa adhabu mbele ya wachezaji wenzake.
“Ni kweli nilifanya upuuzi mimi mwenyewe kwa kusema katika mahojiano baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa lakini baadaye nilimuomba radhi,” alisema Richarlison.
“Nilifikia hatua ya kumwambia kwamba hata kama anataka kuniadhibu anaweza kufanya hivyo, tulimaliza lile pale,” alisema.
“Lakini alitaka pia aoneshe ukali wake mbele ya wachezaji, ni kama kusema kwamba yupo imara na ndiye kiongozi, hiyo ndiyo namna yake ya kukabiliana na watu, na kundi la wachezaji na alitumia kama saa mbili kunishambulia mimi tu kwenye kikao mbele ya kila mtu,” alisema Richarlison.
Richarlison alisema kwamba baada ya tukio lile baadhi ya wachezaji walimwambia asifanye tena alichokifanya na kila mmoja alitaka kuondoka.
Conte alimsajili Richarlison kutoka Everton mwanzoni mwa msimu wa 2022-23 lakini mchezaji huyo alipitia kipindi kigumu kidogo, hakuwa katika kiwango chake bora baada ya kuandamwa na majeraha hadi kuishia kufunga bao moja tu katika Ligi Kuu England.
Richarlison, 26, hata hivyo alisema kwamba baada ya Conte kutimuliwa Spurs aliwasiliana naye na kumuomba radhi. “Nilimtumia ujumbe wa kumuomba radhi kwa sababu ni mtu ambaye aliniajiri na sikumsaidia kwa kiwango alichofikiria, jambo pekee nililoona linafaa kulifanya ni kumuomba radhi.”

The post Richarlison: Conte alinifokea kwa saa mbili first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/10/richarlison-conte-alinifokea-kwa-saa-mbili/feed/ 0
Conte afanyiwa upasuaji, yuko poa https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/conte-afanyiwa-upasuaji-yuko-poa/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/conte-afanyiwa-upasuaji-yuko-poa/#respond Thu, 02 Feb 2023 06:18:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4962 London, EnglandKocha wa Tottenham, Antonio Conte amesema upasuaji wa kwenye kibofu aliofanyiwa umekwenda vizuri na anaendelea vizuri akisubiri kupona kabisa kabla ya kurudi katika kibarua chake.Conte alihitaji kufanyiwa upasuaji ambao ulifanyika jana Jumatano baada ya kukutwa na uvimbeuchungu hali iliyomfanya kujisikia mgonjwa kabla ya kubainika kwamba alihitaji kufanyiwa upasuaji.Haijaweza kufahamika mara moja ni lini kocha […]

The post Conte afanyiwa upasuaji, yuko poa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham, Antonio Conte amesema upasuaji wa kwenye kibofu aliofanyiwa umekwenda vizuri na anaendelea vizuri akisubiri kupona kabisa kabla ya kurudi katika kibarua chake.
Conte alihitaji kufanyiwa upasuaji ambao ulifanyika jana Jumatano baada ya kukutwa na uvimbeuchungu hali iliyomfanya kujisikia mgonjwa kabla ya kubainika kwamba alihitaji kufanyiwa upasuaji.
Haijaweza kufahamika mara moja ni lini kocha huyo atakuwa fiti na kurudi kibaruani ingawa inaaminika kwamba hatokuwepo katika mechi ya Jumapili ijayo dhidi ya Man City na hivyo msaidizi wake, Cristian Stellini ndiye atakayebeba majukumu.
“Ahsanteni kwa ujumbe wenu wa upendo, upasuaji niliofanyiwa ulikwenda vizuri na sasa tayari nimeanza kujisikia vizuri,” alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 kupitia mtandao wa Instagram.
Tottenham kwa sasa inashika nafasi ya tano katika Ligi Kuu England ikiwa na pointi 36, tofauti ya pointi 14 na Arsenal ambao ndio vinara wa ligi hiyo na mahasimu wao wa jiji la London.

The post Conte afanyiwa upasuaji, yuko poa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/conte-afanyiwa-upasuaji-yuko-poa/feed/ 0