Coastal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 30 Oct 2024 04:53:24 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.7 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Coastal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaibutua Coastal 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/yanga-yaibutua-coastal-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/yanga-yaibutua-coastal-1-0/#respond Sat, 26 Oct 2024 16:01:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12087 Na mwandishiYanga imepanda hadi nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union ya Tanga bao 1-0 mechi iliyochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Bao hilo pekee la Yanga lilipatikana dakika ya 24 mfungaji akiwa ni Jean Baleke ambaye hilo ni bao lake la kwanza katika ligi kuu msimu […]

The post Yanga yaibutua Coastal 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi
Yanga imepanda hadi nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union ya Tanga bao 1-0 mechi iliyochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Bao hilo pekee la Yanga lilipatikana dakika ya 24 mfungaji akiwa ni Jean Baleke ambaye hilo ni bao lake la kwanza katika ligi kuu msimu huu tangu ajiunge na timu hiyo.
Baleke alifunga bao hilo kutokana na mpira wa kona iliyochongwa na Maxi Nzengeli na kuokolewa vibaya na Haroub Mohamed kabla ya kumkuta Khalid Aucho aliyemsogezea Baleke na kuujaza wavuni.
Coastal licha ya kufungwa bao hilo walilichachafya mara kadhaa lango la Yanga ambalo katika mechi ya leo lililindwa vyema na kipa namba mbili Aboubakar Khomeini.
Kwa upande wa Coastal kipa wao Chuma Mgeni naye hakuwa nyuma katika kudhibiti mashambulizi ya mara kwa mara ya Yanga na haikushangaza hadi dakika 90 zinamalizika Yanga walipata bao moja tu.
Coastal nusura wasawazishe bao baada ya Ernest Malongo kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu dakika chache kabla ya kutimia dakika 90 lakini wakati akiupiga mpira huo alikuwa tayari ameotea.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 21 katika mechi saba ikiwa haijapoteza hata mechi moja na kutua nafasi ya pili iliyokuwa ikishikiliwa na mahasimu wao, Simba huku Singida BS wakiendelea kushikilia usukani.
Baada ya kuona mambo hayaendi kama ilivyotarajiwa, kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alifanya mabadiliko kadhaa akiwatoa Baleke, Maxi Nzengeli na Aziz Ki na nafasi zao kuingia Pacome Zouzoua, Clatous Chama na Prince Dube.
Mabadiliko hayo bado hayakubadili matokeo hata pale alipomtoa Yao Kouasi aliyeumia na nafasi yake kuingia Duke Abuya na Clement Mzize ambaye nafasi yake aliingia Aziz Andambwile lakini matokeo yalibaki 1-0.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, KMC ikiwa ugenini iliilaza Tanzania Prisons mabao 2-1, mabao ya washindi yakifungwa na Daruwesh Saiboko dakika za 16 na 60 wakati bao la Prisons lilifungwa na Oscar Mwajanga dakika ya 74.

The post Yanga yaibutua Coastal 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/yanga-yaibutua-coastal-1-0/feed/ 0
Coastal yataja sababu kumuacha Mulumba https://www.greensports.co.tz/2024/06/30/coastal-yataja-sababu-kumuacha-mulumba/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/30/coastal-yataja-sababu-kumuacha-mulumba/#respond Sun, 30 Jun 2024 12:12:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11464 Na mwandishi wetuSiku kadhaa baada ya Coastal Union kutangaza kuachana na beki wake, Felly Mulumba, (pichani) uongozi umefunguka kuwa kikwazo ni umri wa beki huyo.Akizungumza hivi karibuni na GreenSports, Ofisa Habari wa Coastal, Abbas El Sabri alisema mashabiki wa Wagosi Wakaya hao hawapaswi kuvunjika moyo kwa kuondoka kwa Mulumba kwani huo ni mchakato wa kuisuka […]

The post Coastal yataja sababu kumuacha Mulumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku kadhaa baada ya Coastal Union kutangaza kuachana na beki wake, Felly Mulumba, (pichani) uongozi umefunguka kuwa kikwazo ni umri wa beki huyo.
Akizungumza hivi karibuni na GreenSports, Ofisa Habari wa Coastal, Abbas El Sabri alisema mashabiki wa Wagosi Wakaya hao hawapaswi kuvunjika moyo kwa kuondoka kwa Mulumba kwani huo ni mchakato wa kuisuka Coastal bora zaidi.
“Hapana tatizo katika hilo, inafahamika Mulumba ni beki mkubwa, muhimu na alikuwa nguzo ya kutuliza timu lakini kwa kuangalia umri wake tumeona anahitaji kwamba tutafute vijana ambao wataleta nguvu na changamoto mpya,” alisema El Sabri.
Alieleza kuwa kwa sasa wanatengeneza kikosi ambacho kitadumu kwenye michuano ya kimataifa kwa takriban misimu mitatu baada ya msimu huu kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Coastal mbali na Mulumba, 36, pia imeondokewa na beki wake mwingine, Lameck Lawi, 18 aliyetangazwa kujiunga na Simba SC huku ikielezwa tayari kuna beki kisiki kutoka Uganda yupo kwenye mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo ya mjini Tanga ili kuendeleza moto msimu ujao.

The post Coastal yataja sababu kumuacha Mulumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/30/coastal-yataja-sababu-kumuacha-mulumba/feed/ 0
Yanga yainyuka Coastal 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/yanga-yainyuka-coastal-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/yanga-yainyuka-coastal-1-0/#respond Sun, 28 Apr 2024 09:35:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10761 Na mwandishi wetuBaada ya sare tasa dhidi ya JKT, Yanga imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii jioni.Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Azam Complex, bao hilo pekee lililoihakikishia Yanga pointi tatu lilifungwa na Joseph Guede dakika ya 75 akimalizia pasi […]

The post Yanga yainyuka Coastal 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya sare tasa dhidi ya JKT, Yanga imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii jioni.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Azam Complex, bao hilo pekee lililoihakikishia Yanga pointi tatu lilifungwa na Joseph Guede dakika ya 75 akimalizia pasi ya Kennedy Musonda.
Dakika tano kabla ya kuingia kwa bao hilo, mambo yalianza kuwaharibikia Coastal walipolazimika kubaki wachezaji 10 uwanjani baada ya mwamuzi kumpa kadi nyekundu beki wa timu hiyo, Lameck Lawi.
Lawi alijikuta akipewa kadi hiyo baada ya kumvuta jezi kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ambaye alikuwa anaelekea kuipatia Yanga bao.
Kwa ushindi huo Yanga inaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 62 katika mechi 24 wakati Coastal Union inabaki katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 33 nayo hadi sasa ikiwa imecheza mechi 24.
Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 54 katika mechi 24 wakati mahasimu wa Yanga, Simba wao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 46 katika mechi 21.

The post Yanga yainyuka Coastal 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/yanga-yainyuka-coastal-1-0/feed/ 0
Pembele wa DR Congo asaini Coastal https://www.greensports.co.tz/2022/07/28/pembele-wa-dr-congo-asaini-coastal/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/28/pembele-wa-dr-congo-asaini-coastal/#respond Thu, 28 Jul 2022 12:37:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2032 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Coastal Union inazidi kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23 baada ya leo kumtambulisha kiungo mshambuliaji Riguene Pembele raia wa DR Congo.Mchezaji huyo anayeelezwa kusajiliwa kutoka Don Bosco ya nchini kwao amemwaga wino wa kuwatumikia Wagosi wa Kaya hao kwa mkataba wa miaka miwili baada ya uongozi wa […]

The post Pembele wa DR Congo asaini Coastal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Coastal Union inazidi kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23 baada ya leo kumtambulisha kiungo mshambuliaji Riguene Pembele raia wa DR Congo.
Mchezaji huyo anayeelezwa kusajiliwa kutoka Don Bosco ya nchini kwao amemwaga wino wa kuwatumikia Wagosi wa Kaya hao kwa mkataba wa miaka miwili baada ya uongozi wa timu hiyo kuridhishwa na kiwango chake.
Ofisa Habari wa Coastal, Jonathan Tito ameeleza kuwa safari hii usajili wao umelenga zaidi wachezaji wanaokipiga timu za taifa kama ilivyo kwa Pembele kwa kuwa wanaunda kikosi chenye ushindani maradufu kuelekea msimu ujao.
“Ujio wa Pembele kwetu una maana kubwa kutokana na kiwango chake na tumekuwa tukimfuatilia kwa muda sasa kabla ya kujiridhisha kumsajili, baadhi ya watu wetu ambao wanaufahamu mpira waliupa uongozi taarifa juu yake na baada ya kujiridhisha tumemchukua.
“Kiuhalisia bado hatujamaliza usajili, tutaendelea na zoezi hilo kwa sababu tuna wachezaji sita tutawatambulisha na wote ni wachezaji wenye tija, baada ya hapo tutakuwa tumefunga usajili tayari sasa kwa msimu ujao,” alisema Tito.
Mbali na Pembele anayemudu kucheza winga ya kushoto, kulia na kiungo mshambuliaji wa kati, wengine waliotambulishwa na timu hiyo ni Khatib Kombo kutoka Kipanga FC ya Zanzibar, kiungo mshambuliaji wa KMKM, Optatusy Lupekenya na mshambuliaji Omar Mbaruk kutoka Fountain Gate.
Pia yumo kiungo mshambuliaji, Djibril Olatoundji kutoka ASVO Benin, mshambuliaji kutoka KVZ ya Zanzibar, Maabad Maulid pamoja na kipa wa timu ya taifa ya Comoro, Mahmoud Mroivili.

The post Pembele wa DR Congo asaini Coastal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/28/pembele-wa-dr-congo-asaini-coastal/feed/ 0
Coastal yasajili kiungo wa Benin https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/coastal-yasajili-kiungo-wa-benin/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/coastal-yasajili-kiungo-wa-benin/#respond Wed, 27 Jul 2022 11:52:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=1988 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Coastal Union ya Tanga leo imetambulisha wachezaji watatu wapya wanaomudu nafasi tatu tofauti uwanjani akiwamo kiungo kutoka nchini Benin lengo likiwa ni kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2022/23.Coastal imeweka wazi kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Djibril Olatoundji kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa kwamba mchezaji huyo ametoka […]

The post Coastal yasajili kiungo wa Benin first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Coastal Union ya Tanga leo imetambulisha wachezaji watatu wapya wanaomudu nafasi tatu tofauti uwanjani akiwamo kiungo kutoka nchini Benin lengo likiwa ni kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa 2022/23.
Coastal imeweka wazi kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Djibril Olatoundji kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa kwamba mchezaji huyo ametoka katika klabu ya ASVO Benin ya nchini Benin anakotoka mchezaji huyo.
Mwingine aliyetambulishwa ni mshambuliaji kutoka KVZ ya Zanzibar, Maabad Maulid ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufanya vizuri akiwa Zanzibar na kuibuka mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.
Wagosi wa Kaya hao pia wamemnasa kipa wa timu ya taifa ya Comoro, Mahmoud Mroivili na sasa kufanya idadi ya makipa kutoka Comoro kuwa wawili kwenye Ligi Kuu Bara baada ya awali Azam kumtambulisha Ali Ahmada kutoka taifa hilo pia.
Mbali na wachezaji hao, pia Coastal inatajwa kumalizana na beki wa kati, Khatib Kombo kutoka Kipanga FC ya Zanzibar, kiungo mshambuliaji wa KMKM, Optatusy Lupekenya na mshambuliaji Omar Mbrauku kutoka Fountain Gate.
Msimu uliopita Coastal ilionesha ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara wakimaliza nafasi ya saba licha ya kuyumba mwanzoni mwa ligi huku ikitinga fainali ya Kombe la FA ikipoteza kwa matuta 4-1 dhidi ya Yanga baada ya sare ya 3-3 ya dakika 90, hivyo sasa timu hiyo inaonekana kujipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao.

The post Coastal yasajili kiungo wa Benin first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/27/coastal-yasajili-kiungo-wa-benin/feed/ 0