Coastal Union - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 10 Apr 2025 19:38:16 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Coastal Union - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Pacome aizamisha Coastal Union https://www.greensports.co.tz/2025/04/07/pacome-aizamisha-coastal-union/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/07/pacome-aizamisha-coastal-union/#respond Mon, 07 Apr 2025 19:44:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13224 Na mwandishi wetuBao pekee la Pacome Zouzoua limetosha kuizamisha Coastal Union na kuipa Yanga ushindi wa 1-0 na kuifanya iendelee kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 7, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam, Pacome alifunga bao hilo katika dakika ya 35 akiitumia krosi ya […]

The post Pacome aizamisha Coastal Union first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la Pacome Zouzoua limetosha kuizamisha Coastal Union na kuipa Yanga ushindi wa 1-0 na kuifanya iendelee kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 7, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam, Pacome alifunga bao hilo katika dakika ya 35 akiitumia krosi ya Maxi Nzengeli.
Bao hilo limetosha kuifanya Yanga kunyakua pointi zote tatu na kufikisha jumla ya pointi 64 wakati Pacome akiendelea kung’ara kwa mabao katika ligi hiyo.
Sambamba na bao hilo, Pacome ambaye sasa anakuwa amefikisha mabao manane katika ligi hiyo, pia ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi ya leo.
Ushindi huo pia umeifanya Yanga kuiacha Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi saba ingawa hadi sasa timu hiyo imecheza mechi 24 za ligi hiyo wakati Simba imecheza mechi 22.
Baada ya mechi hiyo kocha wa Yanga, Miloud Hamdi aliisifia timu yake kwa kupata ushindi ingawa alikiri kuwa wanahitaji kuiimarisha safu yao ya ushambuliaji kwa namna ambavyo wameshindwa kuzitumia nafasi walizotengeneza.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Coastal Union, Joseph Lazaro yeye aliwapongeza wachezaji wake kwa namna walivyocheza kwa kuwapa wakati mgumu Yanga.

The post Pacome aizamisha Coastal Union first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/07/pacome-aizamisha-coastal-union/feed/ 0
Mukwala atupia matatu Simba ikiilaza Coastal 3-0 https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/mukwala-atupia-matatu-simba-ikiilaza-coastal-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/mukwala-atupia-matatu-simba-ikiilaza-coastal-3-0/#respond Sun, 02 Mar 2025 06:58:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13068 Na mwandishi wetuSteven Mukwala ameipendezesha Simba katika Ligi Kuu NBC baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union.Kwa matokeo hayo yaliyopatikana Jumamosi hii, Machi Mosi, 2025 kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Simba sasa imefikisha pointi 54 ikiendelea kusalia nafasi ya […]

The post Mukwala atupia matatu Simba ikiilaza Coastal 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Steven Mukwala ameipendezesha Simba katika Ligi Kuu NBC baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union.
Kwa matokeo hayo yaliyopatikana Jumamosi hii, Machi Mosi, 2025 kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Simba sasa imefikisha pointi 54 ikiendelea kusalia nafasi ya pili.
Mukwala alianza kuzitikisa nyavu za Coastal katika dakika ya 30 akiunganisha kwa shuti la mguu wa kulia pasi ya David Kameta.
Wenyeji Coastal walipambana kutaka kusawazisha bao lakini Mukwala kwa mara nyingine aliipatia Simba bao la pili muda mfupi kabla ya mapumziko akiitumia pasi ya Elly Mpanzu.
Mukwala alikamilisha bao la tatu katika dakika ya 56 safari hii akinufaika na makosa ya kipa wa Coastal, Chuma Ramadhan ambaye aliutema mpira uliopigwa na Mpanzu kabla ya kumkuta mfungaji aliyeujaza wavuni.
Matokeo hayo yanaifanya Coastal kubaki nafasi ya tisa ikiwa na pointi 24 huku ikiwa na mwendelezo wa matokeo yasiyo ya kuvutia katika mechi tano zilizopita ambapo imeambulia sare na kufungwa mitatu.
Kwa upande wa Simba ambayo Jumamosi ijayo itacheza na mahasimu wao Yanga, pamoja na kupata ushindi huo dhidi ya Coastal lakini bado imeachwa na Yanga kwa pointi nne ingawa Yanga imecheza mechi moja zaidi ya Simba.
Mechi hiyo ambayo itakuwa ya mwisho kwa msimu huu wa ligi baina ya timu hizo mahasimu inatajwa na wadau wengi wa soka kuwa ndiyo yenye kutoa mwelekeo wa nani atavuna nini msimu huu.

The post Mukwala atupia matatu Simba ikiilaza Coastal 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/mukwala-atupia-matatu-simba-ikiilaza-coastal-3-0/feed/ 0
Simba, Coastal zatoka sare ya 2-2 https://www.greensports.co.tz/2024/10/05/simba-coastal-zatoka-sare-ya-2-2/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/05/simba-coastal-zatoka-sare-ya-2-2/#respond Sat, 05 Oct 2024 12:07:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11984 Na mwandishi wetuSimba imeanza kuonja ugumu wa Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2024-25 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Coastal Union katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.Hayo ni matokeo ya kwanza yasiyovutia kwa Simba tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi baada ya kuwa tayari […]

The post Simba, Coastal zatoka sare ya 2-2 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeanza kuonja ugumu wa Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2024-25 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Coastal Union katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.
Hayo ni matokeo ya kwanza yasiyovutia kwa Simba tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi baada ya kuwa tayari imeshinda mechi zake nne za awali na hivyo kujikuta ikikusanya pointi 13 badala ya 15 zilizotarajiwa na mashabiki wake.
Katika mechi hiyo, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ dakika ya 25 na Lionel Ateba kuongeza la pili kwa penalti dakika tano kabla ya timu kwenda mapumziko.
Matarajio ya Simba kutoka na pointi zote tatu yalianza kuvurugwa katika dakika ya 47 kwa bao lililofungwa na Abdallah Hassan wakati lile la kusawazisha lilifungwa na Ernest Malonga katika dakika ya 71.
Simba sasa itakuwa na kibarua kigumu cha kufunika kosa hilo hapo Oktoba 19 itakapoumana na hasimu wake wa soka nchini Yanga, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Ken Gold ikiwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, iliilaza JKT Tanzania kwa bao 1-0 wakati Mashujaa ikiwa nyumbani Lake Tanganyika ililala kwa bao 1-0 mbele ya Singida BS.

The post Simba, Coastal zatoka sare ya 2-2 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/05/simba-coastal-zatoka-sare-ya-2-2/feed/ 0
Coastal kusajili wapya watano https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/coastal-kusajili-wapya-watano/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/coastal-kusajili-wapya-watano/#respond Tue, 25 Jun 2024 19:36:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11436 Na mwandishi wetuKlabu ya Coastal Union inajipanga kufanya usajili wa wachezaji takriban watano kuelekea msimu ujao wa 2024-25 ili kuendelea kuleta hali ya utulivu na umakini kikosini.Wagosi Wakaya hao wameeleza hayo leo Jumanne kuwa usajili huo utalenga wachezaji wenye wasifu wa kupita kwenye timu zilizoshiriki michuano ya Shirikisho la Soka Afrika ili kuongeza tija.“Kuna majina […]

The post Coastal kusajili wapya watano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Coastal Union inajipanga kufanya usajili wa wachezaji takriban watano kuelekea msimu ujao wa 2024-25 ili kuendelea kuleta hali ya utulivu na umakini kikosini.
Wagosi Wakaya hao wameeleza hayo leo Jumanne kuwa usajili huo utalenga wachezaji wenye wasifu wa kupita kwenye timu zilizoshiriki michuano ya Shirikisho la Soka Afrika ili kuongeza tija.
“Kuna majina takriban ya wachezaji wachache sana ambao tutawasajili na yote kwa yote ni kwa sababu hatutaki tuingize maingizo mengi ili kujenga kwa umakini kikosi chetu kuelekea msimu ujao,” alisema ofisa habari wa Coastal, Abbas El Sabri.

“Ubora na uzuri wa kikosi chetu tayari umeshajionesha tupo vizuri eneo gani, na tuko dhaifu eneo gani kwa hiyo tutakayofanyia kazi ni maeneo machache sana na kusajili wachezaji watano ambao kwanza lazima wawe na uzoefu wa michuano ya Caf,” alieleza Sabri.


Alifafanua kuwa kutafuta ubora wa wachezaji hao ndiko kunakowachelewesha kuweka wazi usajili mpya kwani mchakato wa kunasa wachezaji wazuri wenye wasifu kama huo huwa mgumu kidogo.
Coastal na Simba zitawakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wakati Yanga na Azam zitapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao wa 2024-25.

The post Coastal kusajili wapya watano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/coastal-kusajili-wapya-watano/feed/ 0
Ouma aiweka Coastal top four https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/ouma-aiweka-coastal-top-four/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/ouma-aiweka-coastal-top-four/#respond Sat, 16 Mar 2024 20:27:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10229 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma amesema timu yake itamaliza msimu kwenye nafasi nne za juu kutokana na kiwango walichokuwa nacho na idadi ya mechi zilizobaki.Juzi mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu (daraja la kwanza) waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC wakiwa uwanja wao wa nyumbani, CCM […]

The post Ouma aiweka Coastal top four first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma amesema timu yake itamaliza msimu kwenye nafasi nne za juu kutokana na kiwango walichokuwa nacho na idadi ya mechi zilizobaki.
Juzi mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu (daraja la kwanza) waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC wakiwa uwanja wao wa nyumbani, CCM Mkwakwani na kurudi nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 30.
“Naridhishwa sana na kiwango tunachokionesha, wachezaji wangu wamekuwa wasikivu sana kwa kufuata kile ninachowaelekeza, tupo nafasi ya nne na ninaamini tutaipigania hadi mwisho,” alisema Ouma.
Kocha huyo alisema mikakati yao kwa sasa ni kuhakikisha wanashinda mechi zao tisa zilizobaki ili kufikia kwa vitendo kile ambacho wamekikusudia cha kushiriki michuano ya kimataifa.
Coastal ambao ni mabingwa wa taji la ligi kuu mwaka 1988 (wakati huo ligi daraja la kwanza) wamesema endapo lengo lao la kushiriki michuano ya kimataifa litatimia msimu ujao wataimarisha kikosi kwa ajili ya kuwania taji la Ligi Kuu NBC.

The post Ouma aiweka Coastal top four first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/ouma-aiweka-coastal-top-four/feed/ 0
Simba yaiadhibu Coastal 2-1 https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/simba-yaiadhibu-coastal-2-1/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/simba-yaiadhibu-coastal-2-1/#respond Sun, 10 Mar 2024 09:55:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10116 Na mwandishi wetuSimba imepata ushindi wa kupunguza presha katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-1 ikiwa ni siku chache zimepita tangu ipokee kichapo kama hicho mbele ya Prisons.Ushindi huo uliopatikana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini, Tanga unaifanya Simba kufikisha pointi 39 katika mechi 17 ingawa timu hiyo inabaki […]

The post Simba yaiadhibu Coastal 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imepata ushindi wa kupunguza presha katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-1 ikiwa ni siku chache zimepita tangu ipokee kichapo kama hicho mbele ya Prisons.
Ushindi huo uliopatikana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini, Tanga unaifanya Simba kufikisha pointi 39 katika mechi 17 ingawa timu hiyo inabaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Simba ilianza kuzitingisha nyavu za Coastal Union katika dakika ya kwanza tu ya mchezo kwa bao lililofungwa na nyota wa timu hiyo kutoka Ivory Coast, Freddy Koublan.
Coastal Union walipambana na kufanikiwa kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa kiungo wa timu hiyo, Lucas Almeida katika dakika ya 24 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Bao la ushindi lililoihakikikishia Simba pointi tatu muhimu za kwenye mechi hiyo lilipatikana katika dakika ya 73 mfungaji akiwa Willy Onana.
Matokeo hayo yanaifanya Coatal Union ibaki na pointi zake 27 katika mechi 20 ilizocheza hadi sasa na kujichimbia nafasi ya nne ikiwa pia imetanguliwa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili na Yanga inayoshika usukani.

The post Simba yaiadhibu Coastal 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/10/simba-yaiadhibu-coastal-2-1/feed/ 0
Ouma akiri mechi na Tabora ngumu https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:06:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9948 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma, (pichani) amesema mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa mgumu lakini anakiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanapata ushindi.Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo […]

The post Ouma akiri mechi na Tabora ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma, (pichani) amesema mchezo wao dhidi ya Tabora United utakuwa mgumu lakini anakiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanapata ushindi.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Ni mchezo mgumu ukizingatia tutakuwa ugenini lakini malengo yetu ni ushindi na tutahakikisha tunacheza kwa juhudi kuhakikisha hatupotezi mchezo huu, ni mchezo muhimu, kila mmoja anajiandaa vya kutosha,” alisema Ouma raia wa Kenya.
Kocha huyo alisema wanataka kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao hivyo ni lazima wapambane ili kubaki kwenye nafasi za juu za kushiriki michuano hiyo mwisho wa msimu.
Wagosi wa Kaya hao wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC wakikusanya pointi 26 katika michezo 17 waliyocheza hadi sasa.

The post Ouma akiri mechi na Tabora ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ouma-akiri-mechi-na-tabora-ngumu/feed/ 0
Coastal ya Ouma yaacha wengine watatu https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/coastal-ya-ouma-yaacha-wengine-watatu/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/coastal-ya-ouma-yaacha-wengine-watatu/#respond Fri, 29 Dec 2023 17:57:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9062 Na mwandishi wetuCoastal Union ya Tanga inayonolewa na kocha David Ouma (pichani) imeendelea na timuatimua ya wachezaji katika dirisha hili dogo la usajili baada ya kuwaacha wachezaji wengine watatu akiwamo kiungo wa kati, Abdulswamad Kassim.Sambamba na kiungo huyo wa zamani wa Simba, wachezaji wengine wawili ambao nao hawatakuwa katika timu hiyo ya Ouma ni pamoja […]

The post Coastal ya Ouma yaacha wengine watatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Coastal Union ya Tanga inayonolewa na kocha David Ouma (pichani) imeendelea na timuatimua ya wachezaji katika dirisha hili dogo la usajili baada ya kuwaacha wachezaji wengine watatu akiwamo kiungo wa kati, Abdulswamad Kassim.
Sambamba na kiungo huyo wa zamani wa Simba, wachezaji wengine wawili ambao nao hawatakuwa katika timu hiyo ya Ouma ni pamoja na Daud Mbweni na Yakubu Abdallah.
Kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kuhusiana na Abdulswamad, Coastal ilieleza: “Kiungo mkabaji bora, mshambuliaji pia na mwenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na akili ya zaida ni vitu ulivyojaaliwa, ila muda si rafiki. Tunasikitika muda ndio umeamua, tuseme asante.”
Abdulswamad alitua Coastal mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mlandege ya Zanzibar aliyoisaidia kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi msimu uliopita.
Kabla ya hapo kiungo huyo aliitumikia Simba kabla ya kutimkia Ruvu Shooting alikodumu kwa miezi sita na kutua Mlandege.
Baada ya tamko hilo, Coastal sasa imeachana na jumla ya wachezaji sita baada ya hivi karibuni kutangaza kuachana na Balama Mapinduzi, Juma Mahadhi na Fran Golubic.

The post Coastal ya Ouma yaacha wengine watatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/coastal-ya-ouma-yaacha-wengine-watatu/feed/ 0
Coastal yawaacha wachezaji watatu https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/coastal-yawaacha-wachezaji-watatu/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/coastal-yawaacha-wachezaji-watatu/#respond Mon, 25 Dec 2023 09:30:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9008 Na mwandishi wetuTimu ya Coastal Union imeachana na nyota wake watatu katika dirisha hili la usajili baada ya kushindwa kulishawishi benchi la ufundi chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, David Ouma (pichani).Wachezaji hao waliooneshwa mlango wa kutokea na Wagosi wa Kaya ni Fran Golubic, Juma Mahadhi na Mapinduzi Balama.Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa […]

The post Coastal yawaacha wachezaji watatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Coastal Union imeachana na nyota wake watatu katika dirisha hili la usajili baada ya kushindwa kulishawishi benchi la ufundi chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, David Ouma (pichani).
Wachezaji hao waliooneshwa mlango wa kutokea na Wagosi wa Kaya ni Fran Golubic, Juma Mahadhi na Mapinduzi Balama.
Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Coastal, Abbas Elsabri alisema kuwa wanataka kutumia dirisha dogo la usajili kupunguza wachezaji walioshindwa kuwa kwenye mipango ya kocha mkuu.
“Tumeachana na wachezaji hawa kwa makubaliano ya pande mbili na yenye maslahi kwa kila mmoja tunawatakia kila la heri kwenye majukumu yao huko waendako, tunaheshimu mchango wao walipokuwa na sisi.

“Malengo yetu ni kuwa na kikosi chenye ushindani ambacho kitaenda kutimiza malengo yetu ya msimu hivyo lazima tuwe imara kwani ligi imekuwa ngumu kwa kila timu kupambana kupata matokeo,” alisema Elsabri.


Alisema kuwa wanatarajia kuongeza nyota wanne wapya kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao na mambo yakiwa tayari watawaweka wazi wachezaji wao wapya.

The post Coastal yawaacha wachezaji watatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/25/coastal-yawaacha-wachezaji-watatu/feed/ 0
Kocha mpya Coastal kurudisha heshima https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/kocha-mpya-coastal-kurudisha-heshima/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/kocha-mpya-coastal-kurudisha-heshima/#respond Tue, 14 Nov 2023 19:13:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8465 Na mwandishi wetuKocha mpya wa Coastal Union, David Ouma (pichani katikati) ameahidi kuirudisha timu hiyo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu NBC.Ouma aliyetangazwa na timu hiyo wiki iliyopita, amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwao Kenya alipokuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa, Harambee Stars.Akizungumza leo Jumanne, kocha huyo alisema kinachompa matumaini ni […]

The post Kocha mpya Coastal kurudisha heshima first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa Coastal Union, David Ouma (pichani katikati) ameahidi kuirudisha timu hiyo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu NBC.
Ouma aliyetangazwa na timu hiyo wiki iliyopita, amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwao Kenya alipokuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa, Harambee Stars.
Akizungumza leo Jumanne, kocha huyo alisema kinachompa matumaini ni ubora waliokuwa nao wachezaji wengi wa timu hiyo pamoja na vipaji murua walivyojaaliwa navyo.

“Nimevutiwa na vitu vingi kwa muda mfupi tangu nimejiunga na Coastal, kikubwa ni uwezo waliokuwa nao wachezaji wangu, wengi wana umri mdogo na ni wapambanaji, naamini nikiongeza mbinu zangu tutakuwa miongoni mwa timu zinazopigania ubingwa msimu huu,” alisema Ouma.


Kocha huyo alisema anajua hawapo nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi lakini malengo yake ni kutumia mapumziko ya kalenda ya Fifa kukiimarisha kikosi hicho ili ligi itakapoendelea wapate matokeo mazuri.
Coastal ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikikusanya pointi saba katika michezo tisa iliyocheza hadi sasa, ikiwa imeshinda mchezo mmoja, imefungwa minne na kutoka sare mechi nne pia.

The post Kocha mpya Coastal kurudisha heshima first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/14/kocha-mpya-coastal-kurudisha-heshima/feed/ 0