CHAN 2024 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 30 Aug 2025 18:36:24 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg CHAN 2024 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Morocco bingwa CHAN 2024 https://www.greensports.co.tz/2025/08/30/morocco-bingwa-chan-2024/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/30/morocco-bingwa-chan-2024/#respond Sat, 30 Aug 2025 18:36:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13856 Na mwandishi wetuMorocco imebeba taji la Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 baada ya kuilaza Madagascar mabao 3-2 katika mechi ya fainali iliyopigwa leo Jumamosi Agosti, 30, 2025 kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi, Kenya.Kwa ushindi huo, Morocco inakuwa timu ya kwanza kulibeba taji la michuano hiyo mara tatu ikiwa tayari imefanya hivyo […]

The post Morocco bingwa CHAN 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Morocco imebeba taji la Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 baada ya kuilaza Madagascar mabao 3-2 katika mechi ya fainali iliyopigwa leo Jumamosi Agosti, 30, 2025 kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi, Kenya.
Kwa ushindi huo, Morocco inakuwa timu ya kwanza kulibeba taji la michuano hiyo mara tatu ikiwa tayari imefanya hivyo mwaka 2018 na 2020.
Ushindi huo pia umeiwezesha Morocco kuondoka na kitita cha Dola milioni 3.5 na medali ya dhahabu wakati Madagascar kwa kushika nafasi ya pili wameondoka na Dola 1.2 milioni na medali ya fedha.
Shujaa wa Morocco katika mechi ya leo alikuwa ni Oussama Lamlioui aliyefunga mabao mawili wakati bao jingine likifungwa na Mehri huku mabao ya Madagascar yakifungwa na Manohantsoa na Rakotondraibe.
Madagascar licha ya kupoteza mchezo huo walionesha kila dalili za kutoka na ushindi baada ya kupata bao la kuongoza dakika ya tisa lililofungwa na Manohantsoa kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa Morocco, El Mehdi Al Harrar .
Bao hilo liliwaamsha Morocco walioongeza kasi ya mshambulizi kwenye lango la Madagascar na kupata bao la kusawazisha dakika ya 27 lililofungwa na Mehri kwa kichwa baada ya kuinasa krosi ya Khalid Baba.
Ikiwa imebaki dakika moja kabla ya timu kwenda mapumziko, Morocco waliandika bao la pili lililofungwa na Lamlioui ambaye aliinasa krosi ya Mohamed Boulacsout, akautuliza vyema mpira na kuujaza wavuni.
Madagascar walikianza kipindi cha pili kwa utulivu na kupata bao la kusawazisha dakika ya 68 lililofungwa na Toky Rakotondraibe aliyetokea benchi akiutumia mpira ulioanzia kwa Manohantsoa.

Baada ya bao hilo kila timu ilicheza kwa kujihami na kushambulia kwa tahadhari lakini walikuwa Morocco waliokamilisha vyema hesabu zao kwa kuandika bao la tatu na la ushindi lililofungwa na Lamlioui ambaye amefikisha mabao sita kwenye CHAN 2024.
Lamlioui ambaye pia ndiye nyota wa mchezo huo, alifunga bao hilo kwa shuti la mbali huku kipa wa Madagascar, Ramandimbisoa akiwa mbali na eneo lake.
Katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu iliyopigwa jana Ijumaa, Agosti 29, 2025, Senegal waliilaza Sudan 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Michuano ya CHAN 2024 iliyoanza kutimua vumbi Agosti 2, 2025 jijini Dar es Salaam, imefanyika katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

The post Morocco bingwa CHAN 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/30/morocco-bingwa-chan-2024/feed/ 0
Uganda Cranes yatolewa CHAN https://www.greensports.co.tz/2025/08/24/uganda-cranes-yatolewa-chan/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/24/uganda-cranes-yatolewa-chan/#respond Sun, 24 Aug 2025 13:09:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13852 Kampala, UgandaMatumaini ya timu ya taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’ kufuzu nuzu fainali ya michuano ya Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 yametoweka baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Senegal.Uganda, timu pekee mwenyeji wa michuano hiyo iliyobaki nayo ilishindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani na hivyo kutolewa kama ilivyokuwa kwa […]

The post Uganda Cranes yatolewa CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Kampala, Uganda
Matumaini ya timu ya taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’ kufuzu nuzu fainali ya michuano ya Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 yametoweka baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Senegal.
Uganda, timu pekee mwenyeji wa michuano hiyo iliyobaki nayo ilishindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani na hivyo kutolewa kama ilivyokuwa kwa majirani zake wa Kenya na Tanzania.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi hii Agosti 23, 2025 kwenye Uwanja wa Namboole, Senegal, ambao ni mabingwa watetezi waliandika bao hilo pekee dakika ya 62 lililofungwa na Oumar Ba.
Oumar Ba alifunga bao hilo akiwa ndani ya eneo la 18 kwa mpira uliomshinda kipa Joel Mutakubwa na kuwanyamazisha maelfu ya mashabiki waliofurika kwenye uwanja huo wakiwa na matumaini ya timu yao kusonga mbele.
Michuano hiyo inayofanyika katika nchi za Kenya Uganda na Tanzania ilianza kutimua vumbi Agosti 2 na itafikia tamati Agosti 30 kwa mechi ya fainali huku nchi hizo tatu wenyeji zikibaki kuwa mashuhuda.
Mechi za nusu fainali zitachezwa Jumanne Agosti 26, 2025 kati ya Madagascar dhidi ya Sudan kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na nusu fainali nyingine Morocco itaumana na Senegal kwenye Uwanja wa Namboole.
Washindi wa mechi hizo wataumana katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi, mechi ambayo itamtangaza bingwa mpya wa CHAN 2024.

The post Uganda Cranes yatolewa CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/24/uganda-cranes-yatolewa-chan/feed/ 0
Taifa Stars, Harambee zakwama CHAN https://www.greensports.co.tz/2025/08/23/taifa-stars-harambee-zakwama-chan/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/23/taifa-stars-harambee-zakwama-chan/#respond Sat, 23 Aug 2025 11:27:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13844 Na mwandishi wetuTimu za Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania, zimetolewa katika michuano ya Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024.Harambee imetolewa na Madagascar katika robo fainali baada ya kulala kwa penalti 4-3 wakati Taifa Stars nayo ikitolewa katika hatua hiyo hiyo na Morocco kwa kufungwa bao 1=0.Mechi zote za […]

The post Taifa Stars, Harambee zakwama CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu za Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania, zimetolewa katika michuano ya Ubingwa wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024.
Harambee imetolewa na Madagascar katika robo fainali baada ya kulala kwa penalti 4-3 wakati Taifa Stars nayo ikitolewa katika hatua hiyo hiyo na Morocco kwa kufungwa bao 1=0.
Mechi zote za timu hizo zimechezwa Ijumaa hii Agosti 22, 2025, Harambee ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi na Taifa Stars ikiwa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi ya Taifa Stars, timu hizo zilipambana katika dakika 45 za kwanza bila kufungana hadi dakika ya 65 Morocco walipopata bao hilo pekee lililofungwa na Oussama Lamlaoui.
Lamlaoui ambaye hadi sasa ana mabao matatu alifunga bao hilo baada ya kuinasa pasi ya Youssef Belammari kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa wa Taifa Stars, Yakoub Suleiman.


Taifa Stars ambao waliingia uwanjani wakitambia rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja hadi kufuzu robo fainali, walicheza kwa kujiamini wakishambulia lango la Morocco mara kadhaa lakini Morocco wakati wote walionesha utulivu na umakini.
Morocco nao walifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ukuta wa Taifa Stars ulikuwa mgumu hasa kipa Yakoub ambaye mara kadhaa alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi.
Nao Harambee Stars mambo yao hayakuwa mazuri mbele ya Madagascar baada ya kutolewa kwa penalti katika mechi ambayo hadi dakika 90 za kawaida na zile za nyongeza zinamalizika timu hizo zilikuwa sare ya bao 1-1.


Ikiwa mbele ya maelfu ya mashabiki kwenye dimba la Kasarani, Harambee ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 63 lililofungwa na Alphonce Omija aliyeruka juu kuuwahi mpira na kuujaza wavuni kwa kichwa.
Bao hilo liliibua kelele za furaha kwa mashabiki wa Harambee waliojazana kwenye dimba la Kasarani wakijiaminisha kuwa timu yao ilikuwa katika hatua nzuri ya kufuzu nusu fainali.
Utulivu wa Madagascar ulizaa matunda dakika ya 70 baada ya timu hiyo kupata penalti iliyotolewa baada ya Lewis Bandi kuunawa mpira uliopigwa na Toky Randriamirindra.
Madagascar hatimaye walifufua matumaini kupitia penalti hiyo baada ya Fenohasina Razafimaharo kuujaza mpira wavuni akimchambua kipa wa Harambee, Bryne Omondi na kuipatia Madagascar njia ya kuelekea kwenye mikwaju ya fainali tano tano.
Katika mikwaju ya penalti, kipa wa Madagascar, Ramandimbisoa Lalainiranjaka aliokoa penalti moja wakati Omondi wa Harambee naye aliokoa penalti moja huku penalti ya Alphonce Omija ikienda nje ya lango na hivyo kuipa Madagascar ushindi wa 4-3.


Michuano ya CHAN 2024 ilianza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu huku wenyeji wakiwa ni nchi majirani Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda ikitarajiwa kufikia tamati kwa mechi ya fainali itakayopigwa Jumamosi, Agosti 30, 2025.
Kushindwa kwa Harambee na Taifa Stars kunawafanya wenyeji hao kuaga mashindano hayo katika hatua ya robo fainali na kubaki mashuhuda wa michuano hiyo.
Uganda Cranes ndiyo timu pekee mwenyeji iliyosalia katika michuano hiyo na Jumamosi, Agosti 23, 2025 wataumana na Senegal katika mechi nyingine ya robo fainali.

The post Taifa Stars, Harambee zakwama CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/23/taifa-stars-harambee-zakwama-chan/feed/ 0
Stars, Afrika ya Kati hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/stars-afrika-ya-kati-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/stars-afrika-ya-kati-hakuna-mbabe/#respond Sun, 17 Aug 2025 06:09:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13835 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).Matokeo ya mechi hiyo ya mwisho ya hatua ya makundi iliyochezwa Jumamosi Agosti 16, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es […]

The post Stars, Afrika ya Kati hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Matokeo ya mechi hiyo ya mwisho ya hatua ya makundi iliyochezwa Jumamosi Agosti 16, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam yanaifanya Stars kumaliza hatua hiyo ikiwa kinara wa Kundi B.
Stars kabla ya mechi hiyo ilikuwa tayari imefuzu hatua ya robo fainali, katika kundi hilo lenye timu tano imeshinda mechi tatu na kutoka sare moja na hivyo kufikisha pointi 10.
Timu ya Madagascar ambayo imeifunga Burkina Faso mabao 2-1, imeshika nafasi ya pili ikiwa na pointi saba na hivyo kuungana na Stars katika hatua ya robo fainali.
Nafasi ya tatu katika kundi hilo inashikiliwa na Mauritania ambayo pia ina pointi saba sawa na Madagascar lakini Madagascar ina faida ya uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

The post Stars, Afrika ya Kati hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/17/stars-afrika-ya-kati-hakuna-mbabe/feed/ 0
Wachezaji Harambee kuzawadiwa nyumba https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/wachezaji-harambee-kuzawadiwa-nyumba/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/wachezaji-harambee-kuzawadiwa-nyumba/#respond Tue, 12 Aug 2025 18:47:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13826 Na mwandishi wetuRais wa Kenya, William Ruto ameendelea kutoa motisha kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ambao sasa amaehi kuwapa nyumba kila mmoja.Wachezaji hao watapewa nyumba za nyumba ya vyumba viwili kila mmoja iwapo watafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wandani (CHAN) […]

The post Wachezaji Harambee kuzawadiwa nyumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Kenya, William Ruto ameendelea kutoa motisha kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ambao sasa amaehi kuwapa nyumba kila mmoja.
Wachezaji hao watapewa nyumba za nyumba ya vyumba viwili kila mmoja iwapo watafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wandani (CHAN) inayoendelea nchini Kenya, Tanzania na Uganda.
Harambee ambayo ipo Kundi A hadi sasa imeshinda mechi mbili, sare moja na Jumapili itacheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Zambia.
Akizungumza na wachezaji hao Jumatatu hii Agosti 11, 2025 kwenye Hoteli ya Pullman mjini Nairobi, Rais Ruto pia aliahidi kumpa kila mchezaji Sh 2.5 milioni za Kenya iwapo wataifunga Zambia.
Ahadi ya Sh milioni 2.5 inakuwa motisha nyingine kubwa kwa wachezaji hao ambao awali aliwaahidi iwapo watashinda mechi yoyote atawapa Sh milioni moja ya Kenya kwa kila mchezaji.
Katika ahadi yake ya awali, mbali ya Sh milioni moja kwa kila mchezaji, Rais Ruto pia aliahidi kumpa kila mchezaji wa timu hiyo Sh 500,000 za Kenya kwa kila mechi ambayo watatoka sare.
Kuhusu ahadi ya nyumba, Rais Ruto ameahidi kuitekeleza kupitia mradi wa nyumba za bei nafuu ambao anaufanya nchini Kenya ambapo watakaonufaika katika ahadi hizo ni wachezaji wote 27 na viongozi 15 wa benchi la ufundi.
Taarifa ya nyongeza hiyo ya ahadi za Rais Ruto ilitolewa na msemaji wa Ikulu ya Kenya, Hussein Mohamed ambaye alisema wachezaji hao watajengewa nyumba kwenye maeneo ambayo watachagua wenyewe.
Ahadi za Rais Ruto kwa wachezaji wa Harambee zimeonekana kufurahiwa na wananchi wa Kenya hasa wapenda michezo ingawa wapinzani wake wa kisiasa wameanza kuhoji mantiki ya ahadi hizo.

The post Wachezaji Harambee kuzawadiwa nyumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/12/wachezaji-harambee-kuzawadiwa-nyumba/feed/ 0
Mzize aipeleka Stars robo fainali CHAN https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/mzize-aipeleka-stars-robo-fainali-chan/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/mzize-aipeleka-stars-robo-fainali-chan/#respond Sat, 09 Aug 2025 20:22:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13814 Na mwandishi wetuMabao ya Clement Mzize yameiwezesha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutoka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Madagascar katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).Stars imeibuka na ushindi huo leo Jumamosi, Agosti 9, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na hivyo kufuzu moja […]

The post Mzize aipeleka Stars robo fainali CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabao ya Clement Mzize yameiwezesha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutoka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Madagascar katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Stars imeibuka na ushindi huo leo Jumamosi, Agosti 9, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na hivyo kufuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea katika nchi za Tanzania, Uganda na Kenya.
Mzize ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Yanga na ndiye aliyetajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, aliandika bao la kwanza dakika ya 13, bao lililoanzia kwa mpira wa Iddi Suleiman Nado.
Mpira huo ulizua kizaazaa kwenye lango la Madagasrcar kabla ya kumkuta Mudathir Yahya ambaye shuti lake liligonga mwamba ndipo Mzize alipomalizia kwa kufunga goli.
Dakika saba baadaye, Mzize alindika bao la pili, safari hii akifunga kwa kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Feisal Salum au Fei Toto.
Madagascar walionesha utulivu licha ya kufungwa mabao hayo huku wakicheza pasi za uhakika na kuisumbua safu ya ulinzi ya Stars na juhudi zao kuzaa matunda kwa kupata bao pekee dakika ya 34 lililofungwa na Razafimahatana kwa pasi ya Rafanomezantsoa.
Stars hadi sasa haijapoteza hata mechi moja katika Kundi B, imeshashinda mechi zake za awali dhidi ya Burkina Faso, mabao 2-0 na dhidi ya Mauritania bao 1-0.
Timu hiyo imefikisha pointi tisa ikisubiri kumalizia mechi zake za makundi kwa kucheza na Afrika ya Kati, mechi itakayochezwa Jumamosi ijayo Agosti 16, 2025.

The post Mzize aipeleka Stars robo fainali CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/09/mzize-aipeleka-stars-robo-fainali-chan/feed/ 0
Harambee yalazimisha sare kwa Angola https://www.greensports.co.tz/2025/08/08/harambee-yalazimisha-sare-kwa-angola/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/08/harambee-yalazimisha-sare-kwa-angola/#respond Fri, 08 Aug 2025 20:12:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13804 Nairobi, KenyaIkiwa na wachezaji 10 uwanjani, timu ya taifa ya Kenya, imelazimisha sare ya bao 1-1 na Angola katika mechi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).Timu hiyo maarufu Harambee Stars ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kasarani, Alhamisi Agosti 7, 2025, ilianza kutikiswa nyavu zake dakika ya saba kwa […]

The post Harambee yalazimisha sare kwa Angola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Nairobi, Kenya
Ikiwa na wachezaji 10 uwanjani, timu ya taifa ya Kenya, imelazimisha sare ya bao 1-1 na Angola katika mechi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Timu hiyo maarufu Harambee Stars ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kasarani, Alhamisi Agosti 7, 2025, ilianza kutikiswa nyavu zake dakika ya saba kwa bao lililofungwa na Joao Paciencia.
Dakika tano baadaye juhudi za Harambee zilizaa matunda baada ya timu hiyo kupata bao la penalti lililofungwa na kiungo Austine Odhiambo aliyemchambua vyema kipa wa Angola, Adilson da Cruz.
Pernalti hiyo ilitolewa na mwamuzi, Sadou Ali Brahamou baada ya Odhiambo ambaye pia ni kiungo wa Gor Mahia, kuchezewa rafu katika eneo la penalti na mwamuzi kujiridhisha kwa kutumia VAR.
Baada ya bao la kusawazisha Harambee walipata pigo dakika ya 21 kwa nyota wao, Marvin Omondi kupewa kadi nyekundu na kuifanya timu hiyo ibaki na wachezaji 10 kwa dakika zilizobaki.
Omondi alipewa kadi hiyo kwa kucheza rafu, awali mwamuzi alimuonesha kadi ya njano lakini baada ya kutumia VAR alibadili maamuzi na kumpa mchezaji huyo kadi nyekundu.
Angola walitumia upungufu wa wachezaji wa Harambee kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara ambayo hata hivyo yalikutana na kikwazo baada ya wachezaji wa Harambee kucheza kwa kujihami zaidi na kushambulia mara chache.
Katika dakika za nyongeza Angola walipata bao lililofungwa kwa kichwa na Kaporal lakini mwamuzi baada ya kufanya marejeo kwenye VAR alikataa bao hilo kwa madai mfungaji aliotea.
Kwa sare hiyo, Harambee ambayo ipo Kundi A imefikisha pointi nne huku wachezaji wake wakiwa na uhakika wa kupata zawadi ya Sh 500,000 za Kenya (Sh 9.5 milioni za Tanzania) kwa kila mmoja ambayo ni ahadi ya Rais wa Kenya, William Ruto.

The post Harambee yalazimisha sare kwa Angola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/08/harambee-yalazimisha-sare-kwa-angola/feed/ 0
Stars yailaza Mauritania 1-0 https://www.greensports.co.tz/2025/08/07/stars-yailaza-mauritania-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/07/stars-yailaza-mauritania-1-0/#respond Thu, 07 Aug 2025 05:21:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13798 Na mwandishi wetuBao pekee la Shomari Kapombe limeiwezesha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mauritanni katika mechi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii Agosti 6, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Stars […]

The post Stars yailaza Mauritania 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la Shomari Kapombe limeiwezesha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mauritanni katika mechi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii Agosti 6, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Stars ilipata wakati mgumu kuipenya ngombe ya Mauritania kabla ya kupata bao hilo pekee dakika ya 89.
Mpira uliozaa bao la Stars ulianzia kwa kiungo Shekham Ibrahim aliyepiga pasi ndefu iliyotua kwa Idd Suleiman ‘Nado’ ambaye aliutuliza vizuri mpira kabla ya kupiga pasi nyingine ndefu iliyomkuta Kapombe aliyeujaza mpira wavuni.
Kocha wa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ aliwapongeza wachezaji wake kwa namna ambavyo walionesha upambanaji hadi kuivunja ngombe ngumu ya Mauritania.
Kwa ushindi huo Stars sasa inakuwa imefikisha pointi sita katika Kundi B baada ya ushindi wa awali wa mabao 2-0 mbele ya Burkina Faso na hivyo kuwa kinara wa kundi hilo ambalo pia lina timu za Afrika ya Kati na Madagascar.
Burkina Faso ambayo iliilaza Afrika ya Kati mabao 4-2 katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyochezwa awali, sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu.
Stars itajitupa tena uwanjani Jumamosi, Agosti 9, 2025 kuikabili Madagascar, mechi ambayo ushindi utaihakikishia timu hiyo tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

The post Stars yailaza Mauritania 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/07/stars-yailaza-mauritania-1-0/feed/ 0
Sonko awaahidi Harambee Stars milioni 400 https://www.greensports.co.tz/2025/08/04/sonko-awaahidi-harambee-stars-milioni-400/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/04/sonko-awaahidi-harambee-stars-milioni-400/#respond Mon, 04 Aug 2025 19:23:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13778 Nairobi, KenyaGavana wa zamani wa Nairobi, Mike Sonko ameahidi kutoa Sh 400 milioni za Kenya kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ iwapo watashinda taji la michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).Zawadi hiyo inawafanya wachezaji wa Harambee Stars kupata jumla ya Sh bilioni 1 za Kenya baada ya […]

The post Sonko awaahidi Harambee Stars milioni 400 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Nairobi, Kenya
Gavana wa zamani wa Nairobi, Mike Sonko ameahidi kutoa Sh 400 milioni za Kenya kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ iwapo watashinda taji la michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Zawadi hiyo inawafanya wachezaji wa Harambee Stars kupata jumla ya Sh bilioni 1 za Kenya baada ya Rais wa Kenya, William Ruto naye kuwaahidi Sh milioni 600 kama wakibeba taji hilo.
Sonko hata hivyo alisema kwamba ahadi aliyoitoa haina nia ya kushindana na Rais Ruto badala yake ni kumuunga mkono kiongozi huyo mkuu wa nchi.
“Rais amefanya jambo zuri la kuwahamasisha wachezaji, siko katika mashindano naye, nataka wabebe kombe na wakifanya hivyo nitawapa Sh milioni 400, vijana sasa mna bilioni 1,” alisema Sonko.
Sonko alisema kwamba bado anakumbuka siku za nyuma alivyokuwa akitoa ahadi kwa mchezaji mmoja mmoja anayeonesha juhudi badala yake anadhani jambo hilo si zuri kwani linaivunja moyo timu.

“Kuna siku nilikuwa natoa zawadi kwa wachezaji baada ya kufunga goli, lakini hilo kuna wakati linaleta ubinafsi kwenye timu, mchezaji anaweza akapoteza nafasi wakati angeweza kutoa pasi kwa mwingine ambaye yuko katika nafasi nzuri ya kufunga,” alisema Sonko.


Sonko pia aliwataka viongozi wengine nchini Kenya kuiunga mkono timu yao ya taifa kwa kutoa ahadi za kuwapa motisha wachezaji.
Wakati Sonko ameahidi kutoa Sh milioni 400 iwapo timu hiyo itabeba taji, Rais Ruto ahadi zake zinaanzia timu itakaposhinda Sh milioni moja kwa kila mchezaji, sare Sh milioni 500 na ahadi nyingine kuanzia robo fainali, nusu na fainali.
Michuano ya CHAN ambayo wenyeji wake ni nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, ilianza kutimua vumbi Agosti 2 jijini Dar es Salaam na Kenya tayari wametupa karata yao ya kwanza dhidi ya DR Congo na kutoka na ushindi wa bao 1-0 wakati Tanzania iliilaza Burkina Faso mabao 2-0.

The post Sonko awaahidi Harambee Stars milioni 400 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/04/sonko-awaahidi-harambee-stars-milioni-400/feed/ 0
Stars yaanza CHAN na mguu mzuri https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/stars-yaanza-chan-na-mguu-mzuri/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/stars-yaanza-chan-na-mguu-mzuri/#respond Sun, 03 Aug 2025 20:17:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13772 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza na mguu mzuri fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 kwa kuilaza Burkina Faso mabao 2-0.Katika mechi hiyo ya ufunguzi ya Kundi B iliyopigwa Jumamosi hii Agosti 2, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Stars waliandika […]

The post Stars yaanza CHAN na mguu mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza na mguu mzuri fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 kwa kuilaza Burkina Faso mabao 2-0.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi ya Kundi B iliyopigwa Jumamosi hii Agosti 2, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Stars waliandika bao lao la kwanza dakika chache kabla ya mapumziko.
Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Abdul Suleiman ‘Sopu’ baada ya Frank Tologo wa Burkina Faso kumchezea ndivyo sivyo Clement Mzize akiwa ndani ya eneo la 18.
Stars waliandika bao la pili katika dakika ya 74 lililofungwa na Mohamed Hussein Zimbwe Jr, aliyekuwa beki na nahodha wa timu ya Simba ambayo ameachana nayo siku za karibuni.
Katika mechi hiyo, Stars walionesha kila dalili za kusaka ushindi kwa kuanza kulisakama lango la Burkina Faso, mapema dakika ya nne ya mchezo huo.
Katika shambulizi hilo, Clement Mzize aliufumania mpira akiwa wingi ya kulia na kuambaa nao kabla ya kufumua shuti lakini umakini wa kipa wa Burkina Faso, Ladji Sanou ulikuwa kikwazo.
Dakika nne baadaye, Stars walifanya shambulzii lingine na safari hii, Mudathir Yahya alimuunganishia pasi Feisal Salum ‘Fei Toto’ambaye alifumua shuti lakini kwa mara nyingine uimara wa kipa Sanou uliinyima Stars bao.
Burkina Faso nao katika dakika ya 18 walifanya shambulizi katika lango la Stars lakini shuti lililopigwa na Souleymane Sangare liliokolewa na kipa wa Stars, Yakoub Ali.
Stars ambao wapo Kundi B watacheza mechi ya pili Agosti 6 dhidi ya Mauritania kabla ya kucheza mechi ya tatu Agosti 9 dhidi ya Madagascar na kukamilisha mechi za kundi hilo Agosti 16 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

The post Stars yaanza CHAN na mguu mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/stars-yaanza-chan-na-mguu-mzuri/feed/ 0