Chama - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 03 Jul 2024 19:41:04 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Chama - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Chama aaga rasmi Simba https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/chama-aaga-rasmi-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/chama-aaga-rasmi-simba/#respond Wed, 03 Jul 2024 19:41:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11497 Na mwandishi wetuHatimaye kiungo fundi Mzambia, Clatous Chama amevunja ukimya na kuwashukuru Simba katika muda wote aliokaa nao mpaka alipotangazwa kuibukia kwa mahasimu wao Yanga.Chama ameeleza hisia zake hizo akiwaaga Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii leo Jumatano huku akiwashukuru kwa muda wote wa miaka sita waliodumu na kuandika historia pamoja.“Wapendwa familia ya […]

The post Chama aaga rasmi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye kiungo fundi Mzambia, Clatous Chama amevunja ukimya na kuwashukuru Simba katika muda wote aliokaa nao mpaka alipotangazwa kuibukia kwa mahasimu wao Yanga.
Chama ameeleza hisia zake hizo akiwaaga Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii leo Jumatano huku akiwashukuru kwa muda wote wa miaka sita waliodumu na kuandika historia pamoja.
“Wapendwa familia ya Simba, miaka sita iliyopita nilikuja kwenu kama mgeni. Mlinipa kusudi na changamoto ya kuwa toleo bora zaidi ya nilivyokuwa.
“Tuliteka ardhi hii pamoja, tukapanua utawala wetu hadi sehemu nyingine za Afrika, na kilichobaki ni historia.
“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na kusudi, hatima zetu zilizounganishwa huchukua uelekeo tofauti, sina chochote ila heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na msaada mlionipa miaka yote hii, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja,” ilifafanua sehemu ya ujumbe huo.
Hata hivyo, Chama ambaye tangu atangazwe kutua Yanga juzi alikuwa hajabadili wasifu wake kwenye mitandao ya kijamii, sasa ameelekeza yeye ni mchezaji wa Yanga na si Simba kama ilivyokuwa ikisomeka awali.

The post Chama aaga rasmi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/chama-aaga-rasmi-simba/feed/ 0
Yametimia, Chama asaini Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/07/01/yametimia-chama-asaini-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/01/yametimia-chama-asaini-yanga/#respond Mon, 01 Jul 2024 06:38:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11477 Na mwandishi wetuHatimaye ile habari ya kiungo Clatous Chota Chama au Triple C kuachana na klabu ya Simba na kujiunga na Yanga imetimia baada ya habari hiyo kuthibitishwa leo Jumatatu asubuhi.Habari ya Chama kujiunga na Yanga imekuwa ikijadiliwa mitandaoni na kwenye vijiwe vya mashabiki kwa muda mrefu sasa lakini mapema leo picha za mchezaji huyo […]

The post Yametimia, Chama asaini Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye ile habari ya kiungo Clatous Chota Chama au Triple C kuachana na klabu ya Simba na kujiunga na Yanga imetimia baada ya habari hiyo kuthibitishwa leo Jumatatu asubuhi.
Habari ya Chama kujiunga na Yanga imekuwa ikijadiliwa mitandaoni na kwenye vijiwe vya mashabiki kwa muda mrefu sasa lakini mapema leo picha za mchezaji huyo zimeonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akisaini kuichezea Yanga.
Picha iliyoonekana katika chanzo kimoja cha Yanga ilimuonesha mchezaji huyo akiwa anasaini na kuandamana na maneno yaliyosomea kwa herufi kubwa, ‘NYIE HAMUOGOPI?
Haikuweza kueleweka mara moja maneno hayo alikuwa akiambiwa nani au kundi gani lakini kwa uzoefu wa timu mahasimu za Simba na Yanga ni dhahiri swali hilo lina mtazamo wa kuwadhihaki Simba.
Habari ya Yanga kumsajili Chama inakuwa imemaliza majigambo na kozodoana kwa mashabiki wa timu hizo mbili mahasimu kwa kila mmoja kumpinga mwenzake kuhusu wapi angeelekea mchezaji huyo fundi wa kuuchezea mpira.
Katika taarifa ya Yanga hata hivyo haikuwekwa wazi mkataba wa mchezaji huyo ni wa muda gani na umeigharimu klabu hiyo kiasi gani cha fedha ingawa zipo habari kwamba Chama anakuwa mmoja wa wachezaji ghali katika klabu hiyo.

The post Yametimia, Chama asaini Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/01/yametimia-chama-asaini-yanga/feed/ 0
Chama aibeba Simba Mwanza https://www.greensports.co.tz/2024/02/10/chama-aibeba-simba-mwanza/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/10/chama-aibeba-simba-mwanza/#respond Sat, 10 Feb 2024 08:34:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9669 Na Mwandishi wetuClatous Chama ameibuka shujaa baada ya kufunga bao la kusawazisha lililoiwezesha Simba kutoka sare ya bao 1-1 na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Katika mechi hiyo iliyopigwa Ijumaa hii, Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 14 mfungaji akiwa […]

The post Chama aibeba Simba Mwanza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Mwandishi wetu
Clatous Chama ameibuka shujaa baada ya kufunga bao la kusawazisha lililoiwezesha Simba kutoka sare ya bao 1-1 na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Katika mechi hiyo iliyopigwa Ijumaa hii, Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 14 mfungaji akiwa Prince Dube.

Bao hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza na licha ya Simba kupambana kutaka kusawazisha lakini juhudi zao ziligomba mwamba mbele ya ukuta wa Azam.

Chama ambaye klabu yake ilimsimamisha hivi karibuni kwa kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu kabla ya kumsamehe, alisawazisha bao hilo katika dakika tatu za nyongeza akitumia vizuri mpira wa adhabu.

Bao hilo lilipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Simba ambao waliingiwa na hofu ya timu yao kupoteza mchezo ingawa pia walishindwa kuzitumia nafasi kadhaa walizotengeneza ambazo zingeweza kuwafanya watoke na pointi zote tatu.

Kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo wakati Azam inabaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 katika mechi 14.

Yanga ambayo inasubiri kuumana na Prisons kesho Jumapili hadi sasa ndiyo inayoshika usukani wa ligi hiyo ikiwa imejikusanyia pointi 37 katika michezo 14.

The post Chama aibeba Simba Mwanza first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/10/chama-aibeba-simba-mwanza/feed/ 0
Chama asahau yaliyopita https://www.greensports.co.tz/2024/02/03/chama-asahau-yaliyopita/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/03/chama-asahau-yaliyopita/#respond Sat, 03 Feb 2024 18:30:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9569 Na mwandishi wetuKiungo wa Simba, Clatous Chama amesema amesahau yaliyopita na yupo nchini kwa ajili ya kuitumikia na kuipa mataji timu hiyo bila kinyongo.Akizungumza na GreenSports, mchezaji huyo alisema anatambua maneno mengi yamesemwa kutokana na adhabu ya kusimamishwa na timu hiyo kwa utovu wa nidhamu, lakini anaushukuru uongozi wa Simba kwa kukubali msamaha wake.“Nipo hapa […]

The post Chama asahau yaliyopita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Clatous Chama amesema amesahau yaliyopita na yupo nchini kwa ajili ya kuitumikia na kuipa mataji timu hiyo bila kinyongo.
Akizungumza na GreenSports, mchezaji huyo alisema anatambua maneno mengi yamesemwa kutokana na adhabu ya kusimamishwa na timu hiyo kwa utovu wa nidhamu, lakini anaushukuru uongozi wa Simba kwa kukubali msamaha wake.
“Nipo hapa kwa ajili ya kuipigania Simba kubeba mataji katika mashindano yote, changamoto za hapa na pale ni vitu vya kawaida kwenye kazi, nafurahi yamepita na sasa nipo kazini,” alisema Chama.
Kiungo huyo alisema hataki kuendeleza malumbano ambayo hayana msingi sababu suala la msingi lilishamalizika na yupo kazini.
Chama alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo pamoja na Nassoro Kapama kwa madai ya utovu wa nidhamu lakini baadaye yeye alirudishwa kundini baada ya kuomba msamaha kwa viongozi na benchi la ufundi la timu yake.

The post Chama asahau yaliyopita first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/03/chama-asahau-yaliyopita/feed/ 0
Chama: Tusinyoosheane vidole https://www.greensports.co.tz/2023/11/09/chama-tusinyoosheane-vidole/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/09/chama-tusinyoosheane-vidole/#respond Thu, 09 Nov 2023 19:01:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8415 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amewaomba Wanasimba kuacha kunyoosheana vidole na kupeana lawama, badala yake waungane ili kurejea katika ari ya ushindani wanayopaswa kuwa nayo.Chama ameeleza hayo leo Alhamisi, saa chache kabla ya timu hiyo kuumana na Namungo ya Lindi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Kiungo huyo ameeleza hayo zikiwa zimepita […]

The post Chama: Tusinyoosheane vidole first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amewaomba Wanasimba kuacha kunyoosheana vidole na kupeana lawama, badala yake waungane ili kurejea katika ari ya ushindani wanayopaswa kuwa nayo.
Chama ameeleza hayo leo Alhamisi, saa chache kabla ya timu hiyo kuumana na Namungo ya Lindi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kiungo huyo ameeleza hayo zikiwa zimepita siku nne tangu wachezee kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa mahasimu wao, Yanga hali iliyoibua tafrani na kuondoshwa kwa kocha wao, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ huku baadhi ya wachezaji wakitupiwa lawama wakidaiwa kuhusika kuizorotesha timu hiyo siku hiyo.
“Katika nyakati hizi hakuna haja ya kunyoosheana vidole na kutupiana lawama, haitotusaidia kwa namna yoyote ile. Huu ni wakati sahihi wa kushikamana pamoja na kuunganisha nyoyo zetu. Twendeni tena leo tukiwa na nguvu moja na kufanyabkazi ili kurejea katika ari yetu,” aliandika Chama katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Kipigo cha Jumapili kilichafua rekodi ya timu hiyo ya kutofungwa kwenye michuano yoyote tangu kuanza kwa msimu huu lakini pia kushindwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi na kuiacha Yanga ikijitanua kwa pengo la pointi sita kabla ya Wekundu hao kushuka dimbani leo.

The post Chama: Tusinyoosheane vidole first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/09/chama-tusinyoosheane-vidole/feed/ 0
Matokeo Simba yamkera Chama https://www.greensports.co.tz/2023/09/18/matokeo-simba-yamkera-chama/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/18/matokeo-simba-yamkera-chama/#respond Mon, 18 Sep 2023 06:34:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7785 Na mwandishi wetuMwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama amekerwa na matokeo ya sare ya mabao 2-2 ambayo Simba iliyapata mbele ya Power Dynamos ya Zambia licha ya yeye kucheza vizuri na kufunga mabao yote ya timu yake.Chama ambaye kwa mara nyingine alionesha uwezo binafsi katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa nchini Zambia, […]

The post Matokeo Simba yamkera Chama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama amekerwa na matokeo ya sare ya mabao 2-2 ambayo Simba iliyapata mbele ya Power Dynamos ya Zambia licha ya yeye kucheza vizuri na kufunga mabao yote ya timu yake.
Chama ambaye kwa mara nyingine alionesha uwezo binafsi katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa nchini Zambia, Jumamosi iliyopita, alisema kwamba hayo hayakuwa matokeo waliyoyataka.
Mchezaji huyo hata hivyo aliwatoa hofu mashabiki wa Simba akiwaambia kwamba wanajiandaa kujibu mapigo wakiwa nyumbani katika mechi ya marudiano.

“Huu si mwanzo tulioutaka lakini tutafanya vizuri nyumbani ambapo hakuna anayekuja na kuacha kupewa kichapo,” ilisomeka kauli ya mchezaji huyo kupitia mitandao ya kijamii.


Mbali na Chama mchezaji mwingine wa Simba aliyeumizwa na matokeo hayo ni kipa wa timu hiyo, Ayoub Lankerd ambaye aliwaomba radhi mashabiki kwa kuruhusu mabao mawili kwenye lango lake.
Kipa huyo ambaye hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kubwa na Simba naye alinukuliwa kupitia mitandao ya kijamii akisema, “samahani mashabiki Simba, sikuwa vizuri kwenye ile mechi, niliruhusu mabao mawili lakini naahidi mechi ijayo nitakuwa bora.”
Kipa huyo alionekana kuwakera mno mashabiki wa Simba hasa kwa namna ambavyo aliruhusu bao la pili lililofungwa na kwa shuti la mbali la chinichini ambalo ilionekana mapema angeweza kulidaka lakini alikosa umakini.
Simba sasa inasubiri kurudiana na vinara hao wa Zambia katika mechi ya marudiano ambayo itapigwa jijini Dar es Salaam ambapo timu hiyo itakuwa ikiwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

The post Matokeo Simba yamkera Chama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/18/matokeo-simba-yamkera-chama/feed/ 0
Chama, Ngoma waelekea Uturuki https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/chama-ngoma-waelekea-uturuki/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/chama-ngoma-waelekea-uturuki/#respond Thu, 20 Jul 2023 12:17:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7032 Na mwandishi wetuNyota wa Simba, Clatous Chama na kiungo mpya wa timu hiyo, Fabrice Ngoma kesho Ijumaa wanatarajia kuungana na wachezaji wenzao mazoezini nchini Uturuki.Wachezaji hao waliondoka Dar es Salaam, alfajiri ya leo kwa ajili ya kuungana na wenzao kwenye kambi hiyo ya wiki tatu ambayo inatarajiwa kuvunjwa Julai 31, mwaka huu.Chama hakusafiri na wenzake […]

The post Chama, Ngoma waelekea Uturuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nyota wa Simba, Clatous Chama na kiungo mpya wa timu hiyo, Fabrice Ngoma kesho Ijumaa wanatarajia kuungana na wachezaji wenzao mazoezini nchini Uturuki.
Wachezaji hao waliondoka Dar es Salaam, alfajiri ya leo kwa ajili ya kuungana na wenzao kwenye kambi hiyo ya wiki tatu ambayo inatarajiwa kuvunjwa Julai 31, mwaka huu.
Chama hakusafiri na wenzake kutokana na kuwa na madai yake ya kuomba aboreshewe maslahi kwenye mkataba wake na baada ya kukutana na kumalizana na uongozi wa Simba, mchezaji huyo amekubali kwenda kambini kujiunga na wenzake.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema nyota hao walitarajiwa kuwasili Uturuki jioni na kesho asubuhi wataungana na wenzao kwenye mazoezi.
“Chama na Ngoma kesho wataanza mazoezi na wenzao baada ya kuondoka nchini alfajiri ya leo na kutarajiwa kuwasili Uturuki jioni,” alisema Ally ambaye alieleza kuwa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kikosi chao kinafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
Ally pia alisema kwamba baada ya idadi kubwa ya wachezaji wao kuwasili kambini wanatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki.
Alisema wamepanga kucheza mechi tatu hadi nne za kirafiki lakini hiyo itategemea na muda kama utawaruhusu pamoja na kupata timu za kucheza nazo.

The post Chama, Ngoma waelekea Uturuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/20/chama-ngoma-waelekea-uturuki/feed/ 0
Mashabiki Simba wamkosoa Chama https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mashabiki-simba-wamkosoa-chama/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mashabiki-simba-wamkosoa-chama/#respond Fri, 26 May 2023 19:08:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6296 Na mwandishi wetuKiungo wa Simba, Cletous Chama amesema amekuwa akitumiwa jumbe mbalimbali za kumkosoa kutoka kwa mashabiki baada ya timu yao kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa msimu huu.Nyota huyo alisema hayo yote ni kwasababu wameteleza msimu huu kwa kushindwa kuwapa mashabiki zao furaha iliyostahili.Alisema mashabiki wamekuwa pamoja nao na kuna wakati wanawatia moyo na kuwasapoti na […]

The post Mashabiki Simba wamkosoa Chama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Simba, Cletous Chama amesema amekuwa akitumiwa jumbe mbalimbali za kumkosoa kutoka kwa mashabiki baada ya timu yao kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa msimu huu.
Nyota huyo alisema hayo yote ni kwasababu wameteleza msimu huu kwa kushindwa kuwapa mashabiki zao furaha iliyostahili.
Alisema mashabiki wamekuwa pamoja nao na kuna wakati wanawatia moyo na kuwasapoti na wakati mwingine amekuwa akipata ujumbe wa kumpinga na kumkosoa, akikiri kwamba maisha ndivyo yalivyo wakati mwingine.
“Nawashukuru mashabiki msimu huu wamekuwa na sisi, kuna muda wanalalamika ndio maana kama hawajapenda lazima waongee. Kwangu tunathamini mchango wao kwenye timu na maisha yetu, tumeteleza kidogo lakini ndivyo maisha yalivyo,” alisema Chama.
Chama alisema mashabiki wamekuwa wakitaka kuona mambo makubwa kutoka kwake ndio maana changamoto za kukosolewa zimekuwa zikitokea pale ambapo wanashindwa kuona walichotarajia.

“Sisi kama wachezaji lazima tufanye tathmini kuona nini tumechangia kwenye msimu. Tuangalie vitu vibaya tulivyofanya tujirekebishe na vile vizuri tuendelee navyo kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao,” alisema Chama.


Huu ni msimu wa pili mfululizo miamba hiyo inashindwa kuondoka na kombe lolote baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu NBC, kutolewa nusu fainali Kombe la FA (ASFC), pia wakiishia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post Mashabiki Simba wamkosoa Chama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mashabiki-simba-wamkosoa-chama/feed/ 0
Chama: Tulifanya kila tulichoweza lakini… https://www.greensports.co.tz/2023/04/29/chama-tulifanya-kila-tulichoweza-lakini/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/29/chama-tulifanya-kila-tulichoweza-lakini/#respond Sat, 29 Apr 2023 15:14:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5974 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amesema kwenye mechi waliyofungwa jana Ijumaa na Wydad kwa penalti 4-3, walifanya kila walichokijua ili wapate ushindi lakini mwisho wamekubali matokeo.Simba ilitolewa na Wydad katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana kwenye Uwanja wa Mohamed V, Casablanca baada ya matokeo ya jumla ya […]

The post Chama: Tulifanya kila tulichoweza lakini… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amesema kwenye mechi waliyofungwa jana Ijumaa na Wydad kwa penalti 4-3, walifanya kila walichokijua ili wapate ushindi lakini mwisho wamekubali matokeo.
Simba ilitolewa na Wydad katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana kwenye Uwanja wa Mohamed V, Casablanca baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1 ambapo kila timu ilishinda bao 1-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Chama aliandika ujumbe huo leo Jumamosi kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kueleza kuwa matokeo hayo wanayachukulia kama chachu ya kuzidi kuimarika zaidi kimapambano.
“Imekuwa safari ndefu yenye mambo mengi ndani yake na hisia mchanganyiko. Jana tulifanya kila kitu tunachokijua lakini mwisho wa siku ilibidi tukubaliane na ukweli ili tuweze kusonga mbele,” alisema.

“Tutachukulia matokeo ya jana kama chachu ya kuendelea kuimarika zaidi. Asanteni kwa ushauri na jumbe zenu za kututia moyo. Mungu awabariki sana,” aliandika Chama aliyefunga mabao manne kwenye michuano hiyo.


Mchezaji huyo pia alikosa penalti yake aliwashukuru kwa dhati wachezaji wenzake, benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, mwekezaji wao, Mohammed Dewji na mashabiki wa Wekundu hao akifafanua maombi na upendo wao ndio umewafikisha walipo sasa.
Timu hiyo pia imeripotiwa kuanza safari yake leo Jumamosi mchana ya kutoka jijini Casablanca nchini Morocco kurejea Tanzania kuendelea na ratiba za michuano mingine inayowakabili.
Katika safari hiyo, timu hiyo ilitarajia kupitia Doha, Qatar kabla ya kikosi hicho kutua jijini Dar es Salaam asubuhi ya kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Katika misimu mitano iliyopita Simba imeishia robo fainali mara nne. Ilitolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Ligi ya Mabingwa wakati msimu uliopita kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ilitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 4-3.

The post Chama: Tulifanya kila tulichoweza lakini… first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/29/chama-tulifanya-kila-tulichoweza-lakini/feed/ 0
Chama, Kapombe wapendeza CAF https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/chama-kapombe-wapendeza-caf/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/chama-kapombe-wapendeza-caf/#respond Tue, 14 Mar 2023 17:35:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5496 Na mwandishi wetuKiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amechaguliwa kwenye kikosi cha wiki cha mechi ya nne ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na beki wa timu hiyo, Shomari Kapombe.Sambamba na hilo, kiungo huyo Mzambia pia ameingia kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo ambayo Simba inashiriki ikishika nafasi ya […]

The post Chama, Kapombe wapendeza CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amechaguliwa kwenye kikosi cha wiki cha mechi ya nne ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na beki wa timu hiyo, Shomari Kapombe.
Sambamba na hilo, kiungo huyo Mzambia pia ameingia kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo ambayo Simba inashiriki ikishika nafasi ya pili.
Mbali na Chama, beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe pia amejumuishwa kwenye kikosi hicho kilichowekwa wazi na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Katika kikosi hicho Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Casablanca na Wydad Casablanca za Morocco zilitoa wachezaji wawili-wawili pia huku Al Hilal ya Sudan, JS Kabilye (Algeria) na Zamalek (Misri) zikitoa mchezaji mmoja kila moja.
Kwenye mechi ya wiki hiyo, Simba ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Vipers kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, bao hilo likifungwa na Chama na kuifanya Simba kukaa nafasi ya pili ya Kundi C ikiwa na pointi sita dhidi ya 12 za vinara Raja.
Katika kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki ambacho mshindi anatarajiwa kutangazwa leo, Chama alikuwa akiwania dhidi ya Walid Sabar wa Raja, Peter Shalulile wa Mamelodi na Ahmed Zizo wa Zamalek.
Chama pia amejumuishwa kwenye wachezaji watano waliofunga mabao mazuri zaidi katika wiki hiyo pamoja na Mohamed Nahiri wa Raja walipoiadhibu Horoya mabao 3-1, Marouf Tchakei (AS Vita) walipofungwa na Kablyie mabao 2-1 na Marcelo Allende na Teboho Mokoena wa Mamelodi walipoiadhibu Al Ahly mabao 5-2.
Kwenye kikosi cha wiki za mechi za tatu za michuano hiyo Simba iliwakilishwa na beki wao Henock Inonga, aliyefunga bao pekee dhidi ya Vipers walipokuwa ugenini.

The post Chama, Kapombe wapendeza CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/14/chama-kapombe-wapendeza-caf/feed/ 0