Bukayo Saka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 21 Mar 2024 19:14:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Bukayo Saka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Saka ajitoa kwenye kikosi cha England https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/saka-ajitoa-kwenye-kikosi-cha-england/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/saka-ajitoa-kwenye-kikosi-cha-england/#respond Thu, 21 Mar 2024 19:14:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10294 London, EnglandWinga wa Arsenal, Bukayo Saka amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kutokana na kuwa majeruhi na hivyo atazikosa mechi mbili za kirafiki za timu hiyo dhidi ya Brazil na Ubelgiji.Kwa mujibu wa FA, Saka, 22, ameshindwa kufanya mazoezi na timu hiyo tangu ajiunge nayo kwa ajili ya mechi hizo na hivyo […]

The post Saka ajitoa kwenye kikosi cha England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Winga wa Arsenal, Bukayo Saka amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kutokana na kuwa majeruhi na hivyo atazikosa mechi mbili za kirafiki za timu hiyo dhidi ya Brazil na Ubelgiji.
Kwa mujibu wa FA, Saka, 22, ameshindwa kufanya mazoezi na timu hiyo tangu ajiunge nayo kwa ajili ya mechi hizo na hivyo amerudi katika kikosi cha Arsenal kinachojinoa kwa ajili ya mechi kali dhidi ya Man City ambayo itapigwa Machi 31.
Kwa upande wa England itaanza kwa kuumana na Brazil mechi ambayo itapigwa Jumamosi ijayo kwenye dimba la Wembley na kufuatiwa na mechi dhidi ya Ubelgiji ambayo itapigwa Machi 26.
Hatua ya mchezaji huyo kujiondoa katika kikosi hicho bila shaka inakuwa pigo kwa kocha wa timu hiyo Gareth Southgate anayeiandaa timu hiyo kwa ajili ya fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
England baada ya mechi hizo itakuwa na mechi nyingine mbili za mwisho za kirafiki dhidi ya Bosnia-Herzegovina itakayopigwa Juni 3 na kufuatiwa na mechi nyingine dhidi ya Iceland itakayopigwa Juni 7.
Baada ya hapo timu hiyo itaelekea Ujerumani kwa ajili ya fainali hizo zitakazotimua vumbi kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Juni 11 mwaka huu.

The post Saka ajitoa kwenye kikosi cha England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/saka-ajitoa-kwenye-kikosi-cha-england/feed/ 0
Saka aachwa England https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/saka-aachwa-england/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/saka-aachwa-england/#respond Tue, 10 Oct 2023 18:44:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8034 London, EnglandWinga wa Arsenal, Bukayo Saka ameachwa katika kikosi cha England kinachojiandaa na mechi dhidi ya Australia na Italia kwa sababu ya kuwa majeruhi.Saka ambaye anasumbuliwa na matatizo ya misuli, aliikosa mechi ya juzi Jumapili ya Ligi Kuu England dhidi ya Man City ambayo Arsenal ilishinda kwa bao 1-0.Taarifa ya FA imethibitisha hilo ikieleza kuwa […]

The post Saka aachwa England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Winga wa Arsenal, Bukayo Saka ameachwa katika kikosi cha England kinachojiandaa na mechi dhidi ya Australia na Italia kwa sababu ya kuwa majeruhi.
Saka ambaye anasumbuliwa na matatizo ya misuli, aliikosa mechi ya juzi Jumapili ya Ligi Kuu England dhidi ya Man City ambayo Arsenal ilishinda kwa bao 1-0.
Taarifa ya FA imethibitisha hilo ikieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya timu ya madaktari wa England kumfanyia vipimo mchezaji huyo na kuongeza kwamba nafasi yake hatopewa mchezaji mwingine wakati huu kikosi cha England kikiwa na wachezaji 25.
Timu ya England inajiandaa kuuma na Australia Oktoba 13 na siku nne baadaye itaumana na Italia katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema baada ya mechi na Man City kwamba mchezaji huyo hawezi kuwamo kwenye kikosi cha England na kwamba hakufanya mazoezi hata simu moja tangu aumie.
Arteta hata hivyo hakuweka wazi ni lini hasa mchezaji huyo atakuwa fiti badala yake aliishia kusema kwamba kwa wakati huu hawezi kucheza soka.
Baada ya kukosa mechi na Man City, Saka anabaki na rekodi ya kucheza mfululizo mechi 87 za Ligi Kuu England akiwa na timu ya Arsenal.

The post Saka aachwa England first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/saka-aachwa-england/feed/ 0
Saka kusaini mkataba mpya https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/saka-kusaini-mkataba-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/saka-kusaini-mkataba-mpya/#respond Fri, 24 Feb 2023 09:05:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5297 London, England.Winga wa Arsenal, Bukayo Saka wakati wowote kuanzia sasa anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo inayoshika usukani kwenye Ligi Kuu England (EPL).Mazungumzo kati ya Saka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya England na vigogo wa Arsenal yanaendelea huku kukiwa na kila dalili za kufikia makubaliano ili mchezaji huyo aongeze mkataba.Saka […]

The post Saka kusaini mkataba mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England.
Winga wa Arsenal, Bukayo Saka wakati wowote kuanzia sasa anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo inayoshika usukani kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Mazungumzo kati ya Saka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya England na vigogo wa Arsenal yanaendelea huku kukiwa na kila dalili za kufikia makubaliano ili mchezaji huyo aongeze mkataba.
Saka ambaye ndio kwanza ana miaka 21, kwa sasa ni mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsenal kinachopigania taji la EPL akiwa tayari ameifungia timu hiyo mabao tisa na kutoa asisti 23.
Ni mchezaji aliyekulia katika akademi ya Arsenal na mkataba wake wa sasa unafikia ukomo mwaka 2024 huku ikidaiwa kwamba mkataba wake mpya na klabu hiyo utakuwa na thamani ya Pauni 10 milioni kwa mwaka.
Wanachotaka kufanya Arsenal ni kumpa mkataba utakaofikia ukomo mwaka 2028 ili waweze kuwa naye muda mrefu zaidi kuanzia sasa wakiwa wanafukuzia taji la kwanza kwa takriban miaka 19 iliyopita.
Saka akisaini mkataba huo atakuwa anaungana na kinda mwingine wa klabu hiyo ambaye pia ana miaka 21, Gabriel Martinelli wa Brazil ambaye mapema mwezi huu alisaini mkataba mpya Arsenal.

The post Saka kusaini mkataba mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/saka-kusaini-mkataba-mpya/feed/ 0