Benjamin Sesko - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 15 Dec 2025 09:34:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Benjamin Sesko - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Majeruhi Sesko ahesabu siku https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/majeruhi-sesko-ahesabu-siku/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/majeruhi-sesko-ahesabu-siku/#respond Wed, 10 Dec 2025 18:45:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14156 Manchester, EnglandMshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko (pichani) anatarajia kurudi uwanjani hivi karibuni baada ya kuwa majeruhi wa goti.Sesko, 22, amekuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata Novemba 8 mwaka huu katika mechi dhidi ya Tottenham Hotspur iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.Kwa kipindi chote hicho, Sesko ambaye pia ni mshambuliaji wa […]

The post Majeruhi Sesko ahesabu siku first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Mshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko (pichani) anatarajia kurudi uwanjani hivi karibuni baada ya kuwa majeruhi wa goti.
Sesko, 22, amekuwa nje ya uwanja akisumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata Novemba 8 mwaka huu katika mechi dhidi ya Tottenham Hotspur iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Kwa kipindi chote hicho, Sesko ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Slovenia aliyejiunga na Man United majira ya kiangazi msimu huu akitokea RB Leipzig ya Ujerumani, amekosa mechi nne za Ligi Kuu England.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Dola 98 milioni, Man United wanamhitaji zaidi wakati huu ambao mastaa wake Bryan Mbeumo na Amad Diallo watajiunga na timu zao za taifa kwa ajili ya fainali za Afcon.
Hadi sasa kocha wa Man United, Ruben Amorim hajaweka wazi ni siku gani hasa ambayo Sesko atarejea dimbani lakini kwa mujibu wa wakala wake, mchezaji huyo atakuwa fiti wakati wowote katika siku za karibuni.

“Benjamin (Sesko) anajiona katika hali nzuri, matibabu yake yanakwenda kama yalivyopangwa, ana shauku kubwa ya kurejea uwanjani, anajiona ame-miss kucheza soka na katika hilo kidogo ni kama anachoka kusubiri, kwa hiyo ni matumaini atakuwa vizuri hivi karibuni,” alisema wakala wa mchezaji huyo.


Sesko ambaye hadi sasa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu England katika mechi 11, alisajiliwa Man United pamoja na Mbeumo na Matheus Cunha hatua ambayo ilikuwa ya kuijenga upya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

The post Majeruhi Sesko ahesabu siku first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/majeruhi-sesko-ahesabu-siku/feed/ 0
Majeruhi Sesko njia panda https://www.greensports.co.tz/2025/11/11/majeruhi-sesko-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/11/majeruhi-sesko-njia-panda/#respond Tue, 11 Nov 2025 09:25:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14092 Manchester, EnglandMshambuliaji majeruhi wa Man United, Benjamin Sesko atazikosa mechi muhimu za kufuzu Kombe la Dunia na timu yake ya taifa ya Slovenia huku pia kukiwa na hatihati kuhusu kuwa fiti na kuiwakilisha vyema United.Sesko aliumia Jumamosi iliyopita katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo […]

The post Majeruhi Sesko njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Mshambuliaji majeruhi wa Man United, Benjamin Sesko atazikosa mechi muhimu za kufuzu Kombe la Dunia na timu yake ya taifa ya Slovenia huku pia kukiwa na hatihati kuhusu kuwa fiti na kuiwakilisha vyema United.
Sesko aliumia Jumamosi iliyopita katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 na hivyo kuibua habari kwamba ameumia sana na mbali na timu ya taifa pia atakosa mechi kadhaa za Man United.
Baada ya kucheza kwa dakika 30 kwenye mechi na Tottenham, Sesko alitoka uwanjani huku akichechemea baada ya kuumia goti alipokuwa akikabiliana na Micky van de Ven.
Sesko aliyesajiliwa Man United kwa Pauni 73.7 milioni alionekana akiwa amekaa chini ya uwanja na ingawa muda mfupi baadaye aliinuka lakini utokaji wake uwanjani ulikuwa katika namna iliyotia shaka.
Alipoulizwa kuhusu Sesko, kocha wa Man United, Ruben Amorim alisema kwa sababu ni tatizo la goti ni vigumu kujua hivyo atafanyiwa vipimo na suala hilo huenda likaathiri mipango ya usajili wa mchezaji huyo wakati wa dirisha dogo la Januari.

Kuna hofu kubwa kwamba huenda mchezaji huyo akaongeza idadi ya wachezaji watakaokosekana katika kikosi cha Man United wakiwamo washambuliaji Bryan Mbeumo na Amad Diallo na beki Noussair Mazraoui.
Wahezaji hao watatu mwezi Desemba watakuwa na timu zao za taifa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Morocco.
Kwa upande wa timu ya taifa ni wazi kwamba Sesko atazikosa mechi mbili muhimu za timu hiyo dhidi ya Kosovo na Sweden, mechi ambazo watahitaji kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu Kombe la Dunia kupitia play offs.

The post Majeruhi Sesko njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/11/majeruhi-sesko-njia-panda/feed/ 0