Bayern - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 08 Jul 2024 06:58:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Bayern - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Winga wa Palace atua Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/winga-wa-palace-atua-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/winga-wa-palace-atua-bayern/#respond Mon, 08 Jul 2024 06:58:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11561 Munich, UjerumaniKlabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imemsajili kwa mkataba wa miaka mitano winga, Michael Olise kutoka klabu ya Crystal Palace ya England kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 60 milioni.Olise, 22, mzaliwa wa England ambaye ni Mfaransa na amekuwa akiichezea timu ya Ufarnsa ya vijana chini ya miaka 21, katika misimu mitatu na Palace hadi […]

The post Winga wa Palace atua Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imemsajili kwa mkataba wa miaka mitano winga, Michael Olise kutoka klabu ya Crystal Palace ya England kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 60 milioni.
Olise, 22, mzaliwa wa England ambaye ni Mfaransa na amekuwa akiichezea timu ya Ufarnsa ya vijana chini ya miaka 21, katika misimu mitatu na Palace hadi sasa amecheza mechi 90 za mashindano yote.
Hatua ya Bayern kukamilisha usajili wa Olise linakuwa pigo kwa klabu za Chelsea na Newcastle United ambazo zote ziliweka wazi nia yao ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye hata hivyo aliamua kuichagua Bayern ambako atakuwa chini ya kocha Vincent Kompany.

“Nina furaha kubwa kwa sasa kuwa katika klabu hii kubwa, ni changamoto ya kipekee, hicho ndicho kitu pekee ninachokitaka, nataka kuthibitisha uwezo wangu katika kiwango hiki na kutoa mchango wangu kuhakikisha tunashinda mataji mengi kadri iwezekanavyo kwa miaka ijayo,” alisema Olise.


Akiwa na Palace ambayo ilimaliza nafasi ya 10 kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu England, Olise aliifungia timu hiyo mabao 10 katika ligi hiyo.
Kabla ya kuanza kuiwakilisha Bayern, Olise atakuwa na kikosi cha Ufaransa ambacho kitashiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika baadaye mwezi huu katika jiji la Paris.
“Tunajivunia kwa kiasi kikubwa kile ambacho Michael amekifanikisha akiwa Crystal Palace, klabu ambayo ameendeleza soka lake na kuwa bora, tunaheshimu uamuzi wake wa kujipima katika soka la hadhi ya juu duniani,” alisema Steve Parish, mwenyekiti wa Eagles, timu ya zamani ya Olise.
Bayern pia inadaiwa kuwa katika mkakati wa kumsajli kiungo wa Ureno, Joao Palhinha anayekipiga Fulham kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 42 milioni.

The post Winga wa Palace atua Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/winga-wa-palace-atua-bayern/feed/ 0
Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/#respond Fri, 10 May 2024 07:34:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10901 Madrid, HispaniaKocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema kitendo cha mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya timu yake kufunga bao la kusawazisha katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid ni mfano wa usaliti.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano usiku kwenye dimba la Bernabeu, Bayern walikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi […]

The post Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amesema kitendo cha mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya timu yake kufunga bao la kusawazisha katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid ni mfano wa usaliti.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano usiku kwenye dimba la Bernabeu, Bayern walikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi dakika ya 88 baada ya Joselu aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la kwanza na kuongeza la pili katika dakika tatu.
Wakati Bayern ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 katika dakika za nyongeza, Matthijs de Ligt aliifungia Bayern bao na kudhani kuwa alisawazisha lakini mshika kibendera tayari aliinua kidendera kuashiria kwamba mfungaji alikuwa ameotea.
Mabeki wa Real Madrid, walisimama kabla ya De Ligt kuujaza mpira wavuni na baadaye marudio ya kwenye televisheni yalionesha kuwa uamuzi wa awali usingekuwa wa mchezaji kuotea na hilo lingeweza kufanyiwa mapitio ya VAR.
Hata hivyo kwa kuwa mchezo ulishasimamishwa, VAR haikuweza kutumiwa jambo ambalo Tuchel amelitaja kuwa ni uamuzi mbaya mno na ambao pia ni kinyume na taratibu.
“Kumekuwa na uamuzi wa hovyo kutoka kwa mshika kibendera na mwamuzi, mwisho wa yote tunaona kama ni kusalitiwa,” alisema Tuchel.

“Mshika kibendera alisema samahani lakini hilo halisaidii kitu, kuinua kibendera katika kipindi kama hicho, mwamuzi aliona tulikuwa tunaupata mpira na kuupiga golini, ni ngumu kukubali lakini hivyo ndivyo mambo yalivyo,” alisema Tuchel.


Baadaye Tuchel alisema kwamba mwamuzi Szymon Marciniak ambaye pia ndiye aliyechezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2022 pia aliomba msamaha lakini kwa Tuchel jambo hilo pia haliwezi kusaidia kitu.
Kwa ushindi huo, Real sasa inasubiri kuumana na Borussia Dortmund katika mechi ya fainali ambayo itapigwa Juni Mosi mwaka huu kwenye dimba la Wembley.

The post Tuchel: Mwamuzi kaisaliti Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/tuchel-mwamuzi-kaisaliti-bayern/feed/ 0
Bayern wataka Spurs itoe jibu kuhusu Kane https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/bayern-wataka-spurs-itoe-jibu-kuhusu-kane/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/bayern-wataka-spurs-itoe-jibu-kuhusu-kane/#respond Fri, 04 Aug 2023 20:17:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7237 Munich, UjerumaniBayern Munich imewataka mabosi wa Tottenham Hotspur wawe hadi leo Ijumaa wameamua kama wanajiandaa kumuuza mshambuliaji wao na nahodha wa England Harry Kane.Hatma ya Kane katika kikosi cha Spurs imekuwa mjadala kwa siku za karibuni baada ya klabu kadhaa kubwa barani Ulaya kumtaka huku mwenyewe akidai kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern.Bayern tayari imeshawasilisha […]

The post Bayern wataka Spurs itoe jibu kuhusu Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Bayern Munich imewataka mabosi wa Tottenham Hotspur wawe hadi leo Ijumaa wameamua kama wanajiandaa kumuuza mshambuliaji wao na nahodha wa England Harry Kane.
Hatma ya Kane katika kikosi cha Spurs imekuwa mjadala kwa siku za karibuni baada ya klabu kadhaa kubwa barani Ulaya kumtaka huku mwenyewe akidai kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern.
Bayern tayari imeshawasilisha ofa ya kumtaka Kane ambaye kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini Ujerumani, mchezaji huyo amekubali ofa hiyo ingawa mabosi wake wanasita kutoa uamuzi.
Kitendo cha mabosi wa Bayern kutaka jibu kuhusu mchezaji huyo ni ishara ya kukerwa na mazingira ya yaliyogubila usajili wa mchezaji huyo na haitokuwa ajabu wakiamua kuachana naye kama Spurs haitowapa jibu la uhakika.
Kane ambaye ametimiza miaka 30, ndiye mfungaji wa mabao wa wakati wote Spurs na ana mwaka mmoja katika mkataba wake na timu hiyo, licha ya Bayern kuonekana kumtaka hadi kutaka ipewe jibu lakini mabosi Spurs hawajatoa jibu lolote hadi sasa.
Mchezaji huyo pia hayupo tayari kuongeza mkataba na Spurs na kama klabu hiyo haitompiga bei wakati huu ijiandae kumuona akiondoka msimu ujao akiwa huru na wao kutovuna chochote kwa mkali huyo wa kuzifumania nyavu.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy na maofisa waandamizi wa Bayern walikutana hivi karibuni lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa licha ya mmiliki mwenye hisa nyingi katika klabu hiyo, Joe Lewis kunukuliwa siku chache zilizopita akitaka Kane auzwe.

The post Bayern wataka Spurs itoe jibu kuhusu Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/bayern-wataka-spurs-itoe-jibu-kuhusu-kane/feed/ 0
Kane agomea mkataba mpya Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/07/21/kane-agomea-mkataba-mpya-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/21/kane-agomea-mkataba-mpya-spurs/#respond Fri, 21 Jul 2023 07:12:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7052 London, EnglandMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na yuko wazi katika mpango wake wa kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani.Kane mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo na nahodha wa timu ya Taifa ya England, atakuwa tayari kuondoka kama Spurs itakubali ada ya uhamisho lakini […]

The post Kane agomea mkataba mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na yuko wazi katika mpango wake wa kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani.
Kane mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo na nahodha wa timu ya Taifa ya England, atakuwa tayari kuondoka kama Spurs itakubali ada ya uhamisho lakini hatolazimisha kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Msimamo huo wa Kane umekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu atangaze kwamba yuko tayari kujiunga na timu hiyo ya Ujerumani lakini hatokuwa tayari kuichagua PSG ambayo pia inamtaka.
Mkataba wa Kane na Spurs unafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao na kilichopo ni kwamba kama timu hiyo haitomuuza sasa itajikuta ikimshuhudia akiondoka bila ya wao kupata chochote pale atakapomaliza mkataba wake labda kama atabadili mawazo na kusaini mkataba mpya wakati huu.
Tayari Bayern imeshawasilisha ofa mbili ambazo zimekataliwa na Spurs hapo hapo kukiwa na habari kwamba Real Madrid ambayo pia inadaiwa kumtaka mshambuliaji huyo inafuatilia kwa karibu maendeleo hayo kabla ya kufanya maamuzi.

The post Kane agomea mkataba mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/21/kane-agomea-mkataba-mpya-spurs/feed/ 0
Rais Bayern ajitetea kumtimua Kahn https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/rais-bayern-ajitetea-kumtimua-kahn/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/rais-bayern-ajitetea-kumtimua-kahn/#respond Tue, 30 May 2023 19:02:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6378 Munich, UjerumaniKlabu ya Bayern Munich imetetea uamuzi wa kumfuta kazi aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wake klabu hiyo, Oliver Kahn ingawa Kahn amechukizwa na uamuzi huo akidai kafanyiwa kitu kibaya.Bayern ilitangaza kumfuta kazi Kahn dakika chache baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya FC Cologne na kutwaa taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga […]

The post Rais Bayern ajitetea kumtimua Kahn first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich imetetea uamuzi wa kumfuta kazi aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wake klabu hiyo, Oliver Kahn ingawa Kahn amechukizwa na uamuzi huo akidai kafanyiwa kitu kibaya.
Bayern ilitangaza kumfuta kazi Kahn dakika chache baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya FC Cologne na kutwaa taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga na Kahn akidai kukatazwa kwenda na timu mjini Cologne kufurahia taji hilo na wachezaji.
Mwingine aliyefutwa kazi na Kahn ni mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Hasan Salihamidzic na muda huo huo klabu hiyo ikamtangaza Jan-Christian Dreesen kuwa CEO mpya.
Wakati Kahn akilalamikia uamuzi huo, rais wa klabu hiyo, Herbert Hainer amejitetea akidai ulikuwa uamuzi sahihi na kwamba Kahn na Salihamidzic waliarifiwa mapema juu ya uamuzi huo.
Heiner alisema kwamba timu yao haikucheza kwa namna ambayo wangependa iwe na walitilia shaka uwezo wa Kahn na Salihamidzic kubadili mambo katika timu hiyo.
Kwa Kahn namna uamuzi huo ulivyochukuliwa ni kama vile umefunika sherehe za ubingwa ikiwamo ule wa timu ya wanawake ambayo ilikuwa katika kujiandaa na mechi yake ya Jumapili dhidi ya Turbine Potsdam kabla ya kutwaa ubingwa.
Kahn alitumia mtandao wa Twitter kulalamika akidai kwamba ilikuwa siku mbaya katika maisha yake kwa kunyimwa nafasi ya kusherehekea ubingwa na watu wake.
Hainer hata hivyo alisema kwamba Kahn na Salihamidzic wote walipewa taarifa juu ya uamuzi huo siku ya Alhamisi na Salihamidzic aliuchukulia vizuri uamuzi huo na kusafiri na timu hadi Cologne ingawa kwa Kahn mambo hayakuwa hivyo.
“Ni jambo lililotugusa na mwishowe hatukuweza kukubaliana na Oliver lakini yote kwa yote tulimaliza kwa kukubaliana na Ijumaa tulikaa na bodi katika kikao cha dharura na kuamua kumfuta kazi Oliver Kahn, ni kweli Jumamosi hakwenda Cologne kufurahia ubingwa.” alifafanua Hainer.
Kahn alipingana na hoja kwamba alichukia na kujawa hasira baada ya kuarifiwa kwamba klabu hiyo imemfuta kazi.

“Yalikuwa mazungumzo yaliyojaa utulivu, Jumamosi asubuhi nikapata ujumbe kwamba siwezi kwenda kwenye mechi mjini Cologne, niliukubali uamuzi kiungwana, japo ni kweli nilisikitishwa lakini nina furaha hasa baada ya kubeba taji, nina furaha na timu, kocha na mashabiki,” alisema Kahn kipa wa zamani wa Bayern na timu ya Taifa ya Ujerumani.


The post Rais Bayern ajitetea kumtimua Kahn first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/rais-bayern-ajitetea-kumtimua-kahn/feed/ 0
Lewandowski, Bayern wazika tofauti https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/#respond Tue, 02 Aug 2022 19:16:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2103 Munich, UjerumaniMshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski hatimaye leo amekutana na kuagana rasmi na wachezaji na maofisa wa klabu yake ya zamani ya Bayern Munich na hivyo kuzika hali ya utata uliotokana na kuondoka kwake.Lewandowski ambaye akiwa Bayern amejiwekea rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji mbalimbali zikiwamo tuzo […]

The post Lewandowski, Bayern wazika tofauti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski hatimaye leo amekutana na kuagana rasmi na wachezaji na maofisa wa klabu yake ya zamani ya Bayern Munich na hivyo kuzika hali ya utata uliotokana na kuondoka kwake.
Lewandowski ambaye akiwa Bayern amejiwekea rekodi ya kuvutia ya kufunga mabao 344 katika mechi 375 na kutwaa mataji mbalimbali zikiwamo tuzo za mfungaji bora kwa miaka minane, amejiunga na Barca mwezi uliopita kwa ada inayofikia Euro milioni 45, uhamisho ambao aliulazimisha baada ya Bayern kuonekana kuwa wagumu na hivyo kuibua sintofahamu kati yake na klabu hiyo.
Tangu kuondoka Bayern, Lewandowski ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Poland, alijikuta katika hali ya kushutumiana na mabosi wake wa zamani huku mchezaji huyo akidai kwamba uhamisho wake ulijaa siasa nyingi kutoka Bayern ambao aliwashutumu kwa kujaribu kutafuta hoja ili wamuuze.
Bayern nao kwa upande wao walisema kwamba hali hiyo ilisababishwa na mchezaji huyo ambaye alikuwa akisisitiza kutaka kuhama licha ya kwamba alikuwa na mkataba ambao ulikuwa unafikia ukomo mwaka 2023.
“Kwa sasa kila kitu kiko vizuri, nimekutana na kila mtu na kuwashukuru, sitosahau nilichokipata hapa na uzoefu nilioupata, hilo ni jambo muhimu sana kwangu, wiki iliyopita kidogo kulikuwa na hali ya utata lakini kuna wakati haya ni mambo yanayotokea kwenye soka,” alisema Lewandowski katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Sky.
Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic alizungumza na Lewandowski kwa muda mfupi ambao mchezaji huyo alifika katika klabu hiyo na wameyaweka mambo sawa na hatimaye kuondoa utata uliojitokeza.
“Robert alikuja ofisini kwangu kuniaga na tumezungumza kwa dakika 15, nilimueleza kila kitu na tumeyaweka mambo sawa, Robert amefanya mambo makubwa hapa Bayern na hilo litabaki kuwa hivyo, naye pia anajua kwamba kwa nini anatakiwa kuishukuru Bayern,” alisema Salihamidzic.

The post Lewandowski, Bayern wazika tofauti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/lewandowski-bayern-wazika-tofauti/feed/ 0
Lewandowski: Bayern waongo https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/#respond Sat, 30 Jul 2022 12:05:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2047 Barcelona, HispaniaMshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Bayern Munich ameishutumu klabu yake ya zamani kwa kusema uwongo kuhusu kuondoka kwake kwa lengo la kuwatuliza mashabiki.Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Lewandowski aliulizwa sababu hasa iliyomfanya aihame Bayern kuwa ni uvumi ulioenea kwamba timu hiyo ilipanga kumsajili […]

The post Lewandowski: Bayern waongo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji mpya wa Barcelona, Robert Lewandowski aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Bayern Munich ameishutumu klabu yake ya zamani kwa kusema uwongo kuhusu kuondoka kwake kwa lengo la kuwatuliza mashabiki.
Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Lewandowski aliulizwa sababu hasa iliyomfanya aihame Bayern kuwa ni uvumi ulioenea kwamba timu hiyo ilipanga kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ambaye hata hivyo baadaye alijiunga na Man City.
“Hapana, hakuna uhusiano wowote na usajili wa Erling, mimi ni mtu ambaye hata kama jambo fulani si zuri kwangu ukweli unabaki kuwa muhimu, sitaki kuzungumzia nini hasa kilichotokea lakini kama sababu ya kuhama ni Erling, hiyo hapana, mimi sikuona tatizo lolote kama yeye angejiunga na Bayern Munich.
“Lakini kuna aina ya watu ambao hawasemi ukweli kuhusu mimi, wanasema vitu tofauti, lakini kwangu wakati wote ni muhimu kuwa wazi, kusema ukweli na labda kwa baadhi ya watu wachache hilo lilikuwa tatizo, ni sawa lakini mwisho wa siku niliona ni wakati sahihi kwa mimi kuondoka Bayern Munich na kujiunga na Barcelona,” alisema.
“Nilikuwa na uhusiano mzuri na wachezaji wenzangu, maofisa, kocha na haya yote ni mambo ambayo nitayakosa kwa sababu nilikuwa na wakati mzuri pale na hatukuwa marafiki uwanjani tu bali ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini hatimaye ukurasa umefungwa na nafungua ukurasa mpya wa maisha yangu.”
“Kwa hiyo najiona niko katika msimamo sahihi, mahali sahihi lakini yote ambayo yalijitokeza mwishoni, wiki chache kabla sijaondoka Bayern Munich ni siasa nyingi, klabu ilikuwa inajaribu kutafuta hoja ya kwanini wanaweza kuniuza mimi katika klabu nyingine, kwa sababu hapo kabla labda kulikuwa na ugumu kulieleza hilo kwa mashabiki, na lazima nikubali kwamba kuna uwongo mwingi umesemwa kuhusu mimi, lakini yote kwa yote bado najua ukweli kwamba mashabiki hata katika wakati huu bado wananiunga mkono.
Lewandowski ameondoka Bayern baada ya kuichezea timu hiyo kwa mafanikio kwa miaka minane akifunga mabao 344 katika mechi 375, awali klabu yake ilikuwa ikipata tabu kumruhusu aondoke licha ya mwenyewe kusisitiza azma yake ya kutaka changamoto mpya kwingineko Ulaya.

The post Lewandowski: Bayern waongo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/lewandowski-bayern-waongo/feed/ 0