Bajana - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 12 Dec 2023 17:39:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Bajana - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bajana ataka tuzo ya mfungaji bora https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/bajana-ataka-tuzo-ya-mfungaji-bora/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/bajana-ataka-tuzo-ya-mfungaji-bora/#respond Tue, 12 Dec 2023 17:39:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8850 Na mwandishi wetuNahodha msaidizi wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema amejipanga kubeba tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu NBC msimu huu.Akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania ambao walishinda kwa mabao 2-1 yeye akiwa mfungaji wa bao la kwanza, alisema pamoja na kucheza eneo la kiungo lakini amekuwa akijiongeza kwenda mbele kuwasaidia […]

The post Bajana ataka tuzo ya mfungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha msaidizi wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema amejipanga kubeba tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu NBC msimu huu.
Akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania ambao walishinda kwa mabao 2-1 yeye akiwa mfungaji wa bao la kwanza, alisema pamoja na kucheza eneo la kiungo lakini amekuwa akijiongeza kwenda mbele kuwasaidia washambuliaji wao.

“Napenda sana kufunga na malengo yangu msimu huu ni kuwa mfungaji bora wa ligi kuu, naamini inawezekana kutokana na juhudi zangu ndani ya uwanja,” alisema Bajana.


Kiungo huyo mkabaji alisema anatambua haitokuwa kazi rahisi kutimiza lengo hilo kutokana na kuwepo washambuliaji wazuri kwenye timu yake na timu nyingine za Simba na Yanga lakini hilo halimpi presha ya kumfanya ashindwe kupambania malengo yake.
Alisema atahakikisha anapambana kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake cha Azam na kisha kupigania kutimiza ndoto yake ya ufungaji bora.
Bajana anayeshika nafasi ya tatu kwa ufungaji ndani ya kikosi cha Azam akiwa amefunga mabao matatu, winga Kipre Junior akifunga matano huku kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ akiwa kinara wa timu hiyo kwa mabao yake saba.

The post Bajana ataka tuzo ya mfungaji bora first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/12/bajana-ataka-tuzo-ya-mfungaji-bora/feed/ 0
Bajana asifia mazoezi Azam https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/#respond Wed, 19 Jul 2023 12:27:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7019 Na mwandishi wetuNahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema mazoezi na mbinu wanazopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Yossoufa Dabo zimekuwa zikiwasuka vilivyo hasa kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.Azam ambayo imejichimbia Sousse, Tunisia kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki na Al Hilal, na leo wakitaraji […]

The post Bajana asifia mazoezi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Nahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana amesema mazoezi na mbinu wanazopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Yossoufa Dabo zimekuwa zikiwasuka vilivyo hasa kuelekea michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam ambayo imejichimbia Sousse, Tunisia kwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao tayari imeshacheza mechi moja ya kirafiki na Al Hilal, na leo wakitaraji kuikabili Esperance ya nchini humo.
“Mazoezi ni magumu, kama inavyofahamika mazoezi ya utimamu wa mwili yanahitaji uvumilivu na tumeonesha hilo, tunaomba tuendelee kuwa hivi hivi tuweze kukipata tunachokitaka kuelekea msimu ujao.
“Mazoezi yamekuwa na utofauti kidogo, walimu wapya wanasisitiza zaidi nidhamu na mbinu ambazo wanatuelekeza na sisi tupo tayari kuchukua vitu vyao vipya kwa ajili ya kufanya vizuri tuendako pia tuna michuano mikubwa iliyo mbele yetu,” alisema Bajana.
Alifafanua kuwa michezo yao ya kimataifa pia imekuwa ikiwasaidia mno kuwaweka vizuri ikizingatiwa wanakutana na timu kubwa, hivyo inawajenga vilivyo na inasaidia benchi la ufundi kufahamu mapungufu yao kwa timu kama hizo.

The post Bajana asifia mazoezi Azam first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/bajana-asifia-mazoezi-azam/feed/ 0
Bajana aongezewa mkataba Azam FC https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/bajana-aongezewa-mkataba-azam-fc/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/bajana-aongezewa-mkataba-azam-fc/#respond Thu, 22 Jun 2023 14:33:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6671 Na mwandishi wetuKlabu ya Azam FC imemuongezea mkataba wa miaka motatu kiungo wake, Sospeter Bajana (pichani) utakaomuweka katika timu hiyo hadi mwaka 2026.Azam imeeleza juu ya hilo Jumatano hii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusiana na hilo wakiandika: “Mkata umeme halisi na nahodha wetu, Sospeter Bajana ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex […]

The post Bajana aongezewa mkataba Azam FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imemuongezea mkataba wa miaka motatu kiungo wake, Sospeter Bajana (pichani) utakaomuweka katika timu hiyo hadi mwaka 2026.
Azam imeeleza juu ya hilo Jumatano hii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusiana na hilo wakiandika: “Mkata umeme halisi na nahodha wetu, Sospeter Bajana ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026.”
Taarifa za kuongeza mkataba kwa Bajana ambaye msimu uliopita alikuwa na msimu bora kwa kiwango alichokionesha, kunazima tetesi zilizokuwa zikizagaa kwenye duru za michezo kuwa anatarajia kutua Simba SC.
Bajana anakuwa mchezaji wa kwanza kuelezwa kuongezewa mkataba na timu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya hivi karibuni timu hiyo kuwatema wachezaji wake sita mpaka sasa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kurekebisha kikosi chao wakijiweka tayari kwa michuano ya ndani na yale ya Afrika.
Wachezaji waliotemwa mpaka sasa ni Wilbol Maseke, Ismail Aziz, Cleophas Mkandala, Rodgers Kola, Kenneth Muguna na Bruce Kangwa.

The post Bajana aongezewa mkataba Azam FC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/22/bajana-aongezewa-mkataba-azam-fc/feed/ 0