Argentina - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 08 Oct 2024 06:35:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Argentina - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/#respond Tue, 08 Oct 2024 06:35:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11994 Manchester, EnglandWinga wa Man United, Alejandro Garnacho amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuumia goti la mguu wa kushoto.Argentina katika mbio za kufuzu fainali hizo itakuwa na mechi mbili dhidi ya Venezuela Alhamisi na dhidi ya Bolivia Jumanne ijayo, mechi ambazo, […]

The post Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Winga wa Man United, Alejandro Garnacho amejitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuumia goti la mguu wa kushoto.
Argentina katika mbio za kufuzu fainali hizo itakuwa na mechi mbili dhidi ya Venezuela Alhamisi na dhidi ya Bolivia Jumanne ijayo, mechi ambazo, Garnacho mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo atazikosa.
Garnacho, 20, Jumapili alicheza kwa dakika 90 mechi ya Man United dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana ingawa ilibainika kuwa hali yake haikuwa nzuri.
Tayari Argentina imetambua kuumia kwa mchezaji huyo na nafasi yake amepewa nyota wa Leicester City, Facundo Buonanotte.
Argentina katika mbio za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 inashika usukani katika kundi lake kwa tofauti ya pointi mbili ikifuatiwa na Colombia inayoshika nafasi ya pili.
Garnacho hadi sasa ameichezea timu ya taifa ya Argentina mara saba na alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kubeba taji la Copa America kwa mara ya 16 katika fainali zilizopigwa nchini Marekani Juni mwaka huu.

The post Goti lamtoa Garnacho kikosini Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/08/goti-lamtoa-garnacho-kikosini-argentina/feed/ 0
Argentina yabeba Copa America https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/#respond Mon, 15 Jul 2024 07:35:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11616 Miami, MarekaniArgentina wana kila sababu ya kujivunia soka lao, baada ya Kombe la Dunia 2022, wamebeba taji la Copa America kwa kuilaza Colombia bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii.Mechi hiyo ya fainali ililazimika kuchelewa kuanza kutokana na vurugu za nje ya uwanja na baadaye kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 […]

The post Argentina yabeba Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Argentina wana kila sababu ya kujivunia soka lao, baada ya Kombe la Dunia 2022, wamebeba taji la Copa America kwa kuilaza Colombia bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii.
Mechi hiyo ya fainali ililazimika kuchelewa kuanza kutokana na vurugu za nje ya uwanja na baadaye kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 za kawaida kushindwa kumpata mshindi.
Alikuwa ni Lautaro Martinez aliyefunga bao pekee la Argentina katika dakika ya 112 akiitumia pasi ya Giovani lo Celso na hivyo kuiwezesha timu hiyo kubeba taji la Copa America kwa mara ya 16.
Mechi hiyo hata hivyo ilikuwa ngumu kidogo kwa nahodha wa Argentina, Lionel Messi ambaye alijikuta akitokwa machozi alipotolewa kipindi cha pili baada ya kuumia wakati akiwania mpira.
Majeraha haya hata hivyo hayakumzuia Messi kufurahia ushindi wa taji hilo kwa Argentina mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo.
Vurugu zilizotokea nje ya Uwanja wa Hard Rock ilipochezwa mechi hiyo zinadaiwa kusababishwa na mashabiki ambao hawakuwa na tiketi lakini walikuwa wakihaha kutaka kuingia uwanjani.
Hali hiyo ilisababisha hata wale wenye tiketi kuchelewa kuingia wakisubiri nje ya uwanja kwa muda mrefu ili kupata nafasi ya kuingia ndani.
Katika tukio hilo polisi walilazimika kupambana na mashabiki hao ambao baadhi yao walikamatwa na wengine kulazimika kupatiwa matibabu hasa ya huduma ya kwanza.
Katika hali ambayo pia haikutarajiwa muda wa mapumziko ulichelewa kwa takriban dakika 25 kwa sababu ya burudani ya muziki kutoka kwa nyota wa miondoko ya pop, Shakira ambaye pia anatokea nchini Colombia.


Kitendo cah mwanamuziki huyo kuchelewesha mechi kilionekana kumkera kocha wa Colombia, Nestor Lorenzo na baadhi ya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo.
Kwa Messi taji hilo ni mwendelezo wa kufuta ukame wa mataji na timu yake ya taifa kwani kwa muda mrefu alikuwa hana taji la kujivunia na timu hiyo kabla ya kubeba taji lake la kwanza mwaka 2021 la Copa America wakati huo akiwa na miaka 34.
Mafanikio hayo yanamfanya awe amebeba mataji yote makubwa akiwa na timu yake ya taifa kwa miaka ya karibuni, kwani baada ya mwaka 2021, mwaka uliofuata wa 2022 alibeba Kombe la Dunia.
Messi ambaye kwa sasa ana miaka 37 kabla ya kuanza fainali hizi za Copa America alisema kwamba bado hajaamua ni lini atastaafu kuichezea timu yake ya taifa hivyo huenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 akaendelea kuiwakilisha timu hiyo.

The post Argentina yabeba Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/feed/ 0
Argentina yasaka taji la tatu https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/#respond Sat, 22 Jun 2024 12:46:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11405 Atlanta, MarekaniUshindi wa mabao 2-0 ilioupata Argentina dhidi ya Canada kwenye Copa America unatoa dalili za timu hiyo kubeba taji la tatu kubwa mfululizo baada ya Copa America 2021, Kombe la Dunia 2022 na sasa inataka tena Copa America 2024.Ijumaa hii kwenye dimba la Mercedes-Benz nchini Marekani, nahodha wa Argentina, Lionel Messi aliiongoza vyema timu […]

The post Argentina yasaka taji la tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Lionel Messi mara baada ya kushinda Kombe la Dunia

Atlanta, Marekani
Ushindi wa mabao 2-0 ilioupata Argentina dhidi ya Canada kwenye Copa America unatoa dalili za timu hiyo kubeba taji la tatu kubwa mfululizo baada ya Copa America 2021, Kombe la Dunia 2022 na sasa inataka tena Copa America 2024.
Ijumaa hii kwenye dimba la Mercedes-Benz nchini Marekani, nahodha wa Argentina, Lionel Messi aliiongoza vyema timu hiyo kuanza mbio za kulitetea taji hilo ambalo huenda timu yake ikalibeba kwa mara nyingine.
Kwa Messi ambaye Jumatatu alifikisha umri wa miaka 37 hiyo inakuwa mechi yake ya 35 kwenye fainali za Copa America na hivyo kumzidi mechi moja, Sergio Livingtone wa Chile.
Katika mechi hiyo Messi ndiye aliyekuwa mpishi wa bao la kwanza la Argentina baada ya kutoa pasi ya kichwa iliyomkuta Alexis Mac Allister kabla ya Alvarez kumalizia kazi ya kuujaza mpira wavuni.
Bao la pili la Argentina lilifungwa na Martinez na kwa mara nyingine lilitokana na mchango wa Messi aliyeunasa mpira katika eneo la kati la uwanja kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.
Baada ya ushindi huo, Argentina itajitupa uwanjani kwa mara nyingine Jumanne kuumana na Chile na kumalizia mzunguko wa kwanza kwa kuumana na Peru wakati Jumanne Canada itaumana na Peru kabla ya kumalizia mzunguko wa kwanza kwa kuivaa Chile.

The post Argentina yasaka taji la tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/feed/ 0
Familia ya Di Maria yatishiwa kifo https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/familia-ya-di-maria-yatishiwa-kifo/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/familia-ya-di-maria-yatishiwa-kifo/#respond Tue, 26 Mar 2024 07:30:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10362 Rosario, ArgentinaPolisi nchini Argentina wanachunguza kuwapo madai ya familia ya mwanasoka maarufu nchini humo, Ángel Di Maria kutishiwa kifo yeye na familia yake katika mji wa Rosario.Habari hizo zimekuba baada ya kuokotwa kifurushi chenye ujumbe wa kifo ulioelekezwa kwa Di Maria na familia yake kama mchezaji huyo atarudi Argentina na kuchezea moja ya klabu katika […]

The post Familia ya Di Maria yatishiwa kifo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rosario, Argentina
Polisi nchini Argentina wanachunguza kuwapo madai ya familia ya mwanasoka maarufu nchini humo, Ángel Di Maria kutishiwa kifo yeye na familia yake katika mji wa Rosario.
Habari hizo zimekuba baada ya kuokotwa kifurushi chenye ujumbe wa kifo ulioelekezwa kwa Di Maria na familia yake kama mchezaji huyo atarudi Argentina na kuchezea moja ya klabu katika mji wa Rosario.
Di Maria, 36 ambaye kwa sasa anaichezea Benfica ya Ureno, hivi karibuni alisema anaweza kurudi nyumbani Argentina na kuichezea klabu yake ya utotoni ya Rosario Central.
“Vitisho vya aina hii vinaleta hali ya wasiwasi katika jamii na hilo ndilo lengo lao, kuwafanya watu waogope, wanachofanya ni kuhusisha watu maarufu katika jamii,” alisema ofisa mmoja wa serikali.
Mji wa Rosario umekuwa ukiandamwa na matukio ya uhalifu kati ya makundi hasimu yanayodaiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya huku mji huo pia ukitajwa kuwa kama kitovu cha biashara hiyo kwenye nchi nyingine.
Di Maria, nyota wa zamani wa PSG ambaye pia alikuwamo katika kikosi cha Argentina kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2022, anakuwa mchezaji wa pili kukumbana na tishio hilo, kabla yake nahodha wa Argentina, Lionell Messi naye amewahi kujikuta katika hali kama hiyo.
Katika tukio la Messi, mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika alifyatua risasi katika duka kubwa (supermarket) inayomilikiwa na ndugu wa Messi na baadaye ukakutwa ujumbe uliosomeka, “Messi, tunakusubiri wewe.”
Wiki iliyopita, Serikali ya Argentina ilitangaza nia yake ya kuwasilisha muswada katika baraza la kutunga sheria wenye lengo la kuwaruhusu askari wenye silaha kuingilia kati operesheni ya kupambana na madawa ya kulevya na makosa ya jinai katika mji wa Rosario.

The post Familia ya Di Maria yatishiwa kifo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/26/familia-ya-di-maria-yatishiwa-kifo/feed/ 0
Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/#respond Sat, 25 Nov 2023 05:01:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8620 Rio de Janeiro, BrazilShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu […]

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.
Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu zilizosababisha polisi watumie virungu kuwatuliza mashabiki wa Argentina.
Mara tu baada ya kuanza kwa vurugu, nahodha wa Argentina Lionel Mess aliwaongoza wachezaji wake kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na baadaye alinukuliwa akisema kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu alihofia hali ingeweza kuwa mbaya zaidi.
Messi aliwalaumu polisi ambao walitumia virungu kuwakabili mashabiki hao ambao nao walivunja viti na kuvitumia kujihami wakati wengine walikimbilia katikati ya uwanja ambapo baadaye shabiki mmoja alionekana akiwa amebebwa kwenye machela na watu wa huduma ya kwanza.
Katika sakata hilo ambalo lilianza wakati nyimbo za taifa zikiimbwa, huenda vyama vya soka vya Brazil na Argentina vyote vikajikuta vikikumbana na adhabu ya Fifa.
Wakati vurugu zikiendelea, wachezaji wa timu zote walionekana kuwafuata mashabiki wao na kuanza kuwatuliza ambapo kipa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez alionekana akijaribu kumnyang’anya polisi mmoja kirungu.

“Fifa inathibitisha kwamba kamati ya nidhamu imeanza uchunguzi dhidi ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na Chama cha Soka Argentina (AFA),” ilieleza taarifa ya Fifa iliyopatikana Ijumaa.


Adhabu inayoweza kutolewa kwa kosa hilo ni faini au uwanja kufungiwa, Brazil inahusishwa na kosa la kushindwa kutuliza amani kwenye mechi wakati Argentina inahusishwa na kosa la vurugu za mashabiki.
Baadaye mechi hiyo iliendelea na kuchezwa kwa dakika 90 kama kawaida na Argentina ambao ndio mabingwa wa dunia, walitoka na ushindi wa bao 1-0.

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/feed/ 0
Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/#respond Wed, 22 Nov 2023 08:34:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8583 Rio de Janeiro, BrazilMechi ya Brazil na Argentina ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 ambayo Argentina imeshinda kwa bao 1-0 imechelewa kuanza kwa dakika 30 baada ya kutokea vurugu za polisi na mashabiki.Argentina katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Maracana ilipata bao hilo pekee kipindi cha pili lililofungwa na Nicolas Otamendi na […]

The post Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mechi ya Brazil na Argentina ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 ambayo Argentina imeshinda kwa bao 1-0 imechelewa kuanza kwa dakika 30 baada ya kutokea vurugu za polisi na mashabiki.
Argentina katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Maracana ilipata bao hilo pekee kipindi cha pili lililofungwa na Nicolas Otamendi na kuifanya Brazil ipoteze kwa mara ya kwanza mechi ya kufuzu ikiwa katika uwanja wa nyumbani.
Vurugu hizo ziliibuka baada ya mashabiki wa Argentina na Brazil kuanza kupambana wakati nyimbo za taifa zikiimbwa hali iliyowafanya polisi kutumia virungu kukabiliana na mashabiki wa Argentina.
Mashabiki wa Argentina nao walijibu mapigo kwa kuwarushia polisi viti hali iliyofanya Uwanja wa Maracana kuwa kama sehemu ya vita baada ya mashabiki wengine kukimbilia katikati ya uwanja ili kukwepa vurugu.
Wakati mapambano hayo yakiendelea, shabiki mmoja aliyejeruhiwa alionekana akiwa amebebwa kwenye machele na kutolewa nje ya uwanja na maofisa wa huduma wa kwanza.
Baadhi ya wachezaji wa Argentina walionekana wakiwataka mashabiki waliokuwa jukwaani kutulia ingawa muda mchache baadaye nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi aliwaongoza wenzake kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Kipa wa Argentina, Emiliano Martínez alikimbia hadi karibu na mashabiki wa timu yake kwenye jukwaa huku akiwataka polisi kuhakikisha wanatuliza vurugu.
“Tuliwaona polisi wakipiga watu, na wachezaji wengi hapa ndugu zao wa familia wapo maeneo hayo, hatukuweza kuendelea kucheza mpira,” alisema Messi baada ya mechi hiyo.
Wachezaji wa Argentina inadaiwa waliwaambia wenzao wa Brazil kwamba wangerudi uwanjani baada ya hali kutulia na hatimaye walirudi baada ya dakika 22 na kufanya mazoezi mepesi kwa dakika kama nne kabla ya mechi kuanza.

“Tuliamua kuondoka uwanjani kwa sababu haingewezekana kucheza mpira katika mazingira kama yale, na pia tulidhani kwa sisi kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingesaidia kutuliza hali,” alisema Messi.


Wakati mechi ikianza kundi kubwa la polisi liliwazingira mashabiki wa Argentina waliokuwa wakishangilia, polisi hao walikuwa wakiwadhibiti mashabiki hao katika eneo ambalo lilikuwa na mashabiki wapatao 3,000.
Tiketi zote 69,000 za mechi hiyo ziliuzwa, mashabiki wa Brazil ambao walionekana wakimzomea na wakati mwingine kumshangilia Messi kabla ya kuanza kwa vurugu, baada ya mechi kuanza walianza kuimba nyimbo za kumsakama.
“Timu hii inaendelea kuweka historia, ushindi mkubwa kwenye dimba la Maracana ingawa umekutana na vipigo kwa mashabiki wa Argentina kwa mara nyingine katika mechi dhidi ya Brazil, ukichaa huu hauwezi kuvumiliwa, na lazima uachwe sasa,” alisema Messi

The post Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/feed/ 0
Argentina kinara viwango vya Fifa https://www.greensports.co.tz/2023/04/07/argentina-kinara-viwango-vya-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/07/argentina-kinara-viwango-vya-fifa/#respond Fri, 07 Apr 2023 19:54:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5728 Davos, SwitzerlandMabingwa wa soka duniani Argentina wameshika usukani kwa mujibu wa viwango vya ubora vya Fifa vilivyotolewa jana Alhamisi ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka sita.Ushindi wa Argentina katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki mwezi uliopita umetosha kuifanya nchi hiyo ishike usukani na kuibwaga Brazil ambayo imepoteza mechi […]

The post Argentina kinara viwango vya Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Davos, Switzerland
Mabingwa wa soka duniani Argentina wameshika usukani kwa mujibu wa viwango vya ubora vya Fifa vilivyotolewa jana Alhamisi ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka sita.
Ushindi wa Argentina katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki mwezi uliopita umetosha kuifanya nchi hiyo ishike usukani na kuibwaga Brazil ambayo imepoteza mechi ya kirafiki na Morocco kwa kufungwa mabao 2-1 na kuangukia nafasi ya tatu.
Ufaransa mabingwa wa dunia wa mwaka 2018 na ambao mwaka 2022 walifikia fainali kabla ya kufungwa na Argentina waliobeba kombe, wanashika nafasi ya pili ikiwa imetoka kushinda mechi mbili za kuwania kufuzu Euro 2024 dhidi Uholanzi na Ireland.
Ubelgiji inashika nafasi ya nne wakati England ambayo imetoka kuifunga Italia inashika nafasi ya tano, Uholanzi ya sita, Croatia ya saba na Italia ya nane, Ureno ya tisa na Hispania inashika nafasi ya 10.
Katika nchi za Afrika, Morocco inayowania kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2030 na chini za Hispania na Ureno imechomoza ikiwa katika nafasi ya 11 ikizibeba nchi za Afrika katika orodha hiyo.
Japan inaongoza timu za Asia ikiwa nafasi ya 20 wakati wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2022, Qatar wameangukia katika nafasi ya 61.

The post Argentina kinara viwango vya Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/07/argentina-kinara-viwango-vya-fifa/feed/ 0
Messi ‘apewa uwanja’ Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/messi-apewa-uwanja-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/messi-apewa-uwanja-argentina/#respond Mon, 27 Mar 2023 08:20:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5610 Buenos Aires, ArgentinaLionel Messi amepewa heshima nchini Argentina baada ya chama cha soka nchini humo kutangaza uwanja wa mazoezi wa timu ya Taifa kuitwa kwa jina la mchezaji huyo.Messi ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina ambayo Desemba mwaka jana aliiongoza kubeba Kombe la Dunia, tangu mwaka 2005 hadi sasa ameichezea timu hiyo […]

The post Messi ‘apewa uwanja’ Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Lionel Messi mara baada ya kushinda Kombe la Dunia

Buenos Aires, Argentina
Lionel Messi amepewa heshima nchini Argentina baada ya chama cha soka nchini humo kutangaza uwanja wa mazoezi wa timu ya Taifa kuitwa kwa jina la mchezaji huyo.
Messi ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina ambayo Desemba mwaka jana aliiongoza kubeba Kombe la Dunia, tangu mwaka 2005 hadi sasa ameichezea timu hiyo mara 173.
Rais wa Chama cha Soka Argentina, Claudio Tapia, kocha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Lionel Scalloni na Messi mwenyewe, juzi Jumamosi walishiriki hafla ya uzinduzi wa jina hilo yalipo makao makuu ya timu ya taifa.
“Leo tunashuhudia tukio la kihistoria katika eneo hili, ambalo kuanzia sasa hapa patajulikana kwa jina la Lionel Andres Messi, kwa heshima ya mchezaji bora duniani,” alisema Tapia.
Makao makuu ya timu hiyo ambapo pia ndipo kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, ni eneo lililo umbali wa kilomita 40 kutoka katikati ya jiji maarufu la Buenos Aires nchini Argentina.
Messi ambaye Alhamisi iliyopita wakati akiiwakilisha Argentina katika mechi ya kirafiki na Panama, alifunga bao lake la 800 katika maisha yake ya soka la ushindani, aliguswa mno na tukio la uzinduzi huo.
“Nimekuwa nikija hapa kwa miaka 20 na wakati wote nimekuwa nikijiona mwenye nguvu mpya, hili ni jambo la kufurahisha kwangu, nina furaha sana, hii ni heshima ya kipekee,” alisema Messi.

“Hili ni eneo la aina yake, hata katika kipindi kigumu ambacho nami huwa napitia, nimekuwa nikija hapa na kusahau kila kitu, naweza kuja hapa na kujisikia furaha kwa kuwa kwenye eneo hili na bado naona hivyo, na ndio maana najisikia raha kweli kwamba baada ya siku nyingi hatimaye mahali hapa panapewa jina langu,” alisema Messi.


Messi, nyota wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anaichezea PSG ya Ufaransa, ni mshindi wa tuzo za Ballon d’Or kwa mara saba.

The post Messi ‘apewa uwanja’ Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/27/messi-apewa-uwanja-argentina/feed/ 0
Familia ya Messi yatishiwa maisha https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/familia-ya-messi-yatishiwa-maisha/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/familia-ya-messi-yatishiwa-maisha/#respond Thu, 02 Mar 2023 19:58:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5374 Rosario, ArgentinaSupermarket inayomilikiwa na familia ya mke wa mwanasoka, Lionel Messi imevamiwa na majambazi wenye silaha ambao wameacha ujumbe wa kuitishia maisha familia hiyo.Polisi mjini Rosario nchini Argentina iliyopo Supermarket hiyo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Alhamisi ambapo milio ya risasi ilisikika mara 14 kwenye mlango wa mbele na kwenye madirisha.Tukio hilo lilifanywa na […]

The post Familia ya Messi yatishiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rosario, Argentina
Supermarket inayomilikiwa na familia ya mke wa mwanasoka, Lionel Messi imevamiwa na majambazi wenye silaha ambao wameacha ujumbe wa kuitishia maisha familia hiyo.
Polisi mjini Rosario nchini Argentina iliyopo Supermarket hiyo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Alhamisi ambapo milio ya risasi ilisikika mara 14 kwenye mlango wa mbele na kwenye madirisha.
Tukio hilo lilifanywa na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki, na ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa risasi katika Supermarket hiyo ya Unico maarufu kwa kuuza vyakula hofu imekuwa kubwa.
Polisi pia walisema kwamba wavamizi hao baada ya kufyatua risasi waliacha taarifa iliyoandikwa kwenye ubao na kusomeka, “Messi tunakusubiri wewe, Javkin anajihusisha na madawa ya kulevya, hawezi kuwa makini na wewe.”
Uchunguzi unaendelea na Javkin ambaye jina lake ni Pablo Javkin ndiye meya wa mji wa Rosario, mji mkubwa katika jimbo la Santa Fe, kusini mwa mji mkuu wa Buenos Aires nchini Argentina.
Baada ya tukio hilo Javkin alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia ongezeko la matukio ya uhalifu na uhaba wa polisi na kutokuwapo ulinzi wa kutosha katika mji huo.
Hii si mara ya kwanza kwa Javkin kutoa malalamiko hayo, mapema wiki hii alizungumzia ukosefu wa ulinzi na umuhimu wa kuwa na polisi wengi katika mji huo ambao uhalifu umekuwa ukiongezeka.
Messi na mkewe Antonela Roccuzo hawajasema lolote kuhusu tukio hilo ambalo limetokea siku takriban siku nne baada ya Messi kutwaa tuzo ya Fifa ya mchezaji bora mwanaume baada ya kuiongoza Argentina kubeba taji la dunia Desemba mwaka jana.

The post Familia ya Messi yatishiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/familia-ya-messi-yatishiwa-maisha/feed/ 0
Martinez, kipa shujaa wa Argentina https://www.greensports.co.tz/2022/12/20/martinez-kipa-shujaa-wa-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2022/12/20/martinez-kipa-shujaa-wa-argentina/#respond Tue, 20 Dec 2022 14:24:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4390 Buenos Aires, ArgentinaJiji la Buenos Aires leo limechangamka, ni siku ya mapumziko, wananchi wanafurahia taji la dunia, wengi wamevaa jezi namba 10 ya Lionel Messi, wanajivunia nahodha wao, wanajivunia ushujaa wa kipa, Emiliano Martinez na timu yao kwa ujumla.Martinez ambaye pia ni kipa wa klabu ya Aston Villa ya England amefanya kazi kubwa katika mikwaju […]

The post Martinez, kipa shujaa wa Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kipa wa Argentina, Emiliano Martinez akidaka mkwaju wa penalti.

Buenos Aires, Argentina
Jiji la Buenos Aires leo limechangamka, ni siku ya mapumziko, wananchi wanafurahia taji la dunia, wengi wamevaa jezi namba 10 ya Lionel Messi, wanajivunia nahodha wao, wanajivunia ushujaa wa kipa, Emiliano Martinez na timu yao kwa ujumla.
Martinez ambaye pia ni kipa wa klabu ya Aston Villa ya England amefanya kazi kubwa katika mikwaju ya penalti, ubora wake golini ni sababu mojawapo kubwa iliyoiwezesha Argentina kutwaa kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia baada ya miaka 36.
Ubora wa Martinez ndio uliowafanya mashabiki waliokuwa wakiyaimba majina ya Messi na Kylian Mbappe kabla ya mechi kulazimia kubadili wimbo na kuanza kumtaja na kumjadili kwa namna ambavyo amekuwa msaada kwa timu yake hadi ikatoka na ushindi wa penalti 4-2.
Baada ya mpambano wa nguvu wa dakika 120 zilizoisha kwa sare ya 3-3, hatimaye ikafika zamu ya mikwaju ya penalti, vita ikahamia kwa watu wawili, kipa na mpigaji penalti na kwa namna ya kipekee kipa wa Argentina, Martinez akaibuka shujaa, ndiye aliyewavunja moyo Wafaransa na kuwafanya washindwe kulitetea kombe walilolibeba mwaka 2018 nchini Urusi.


Mbappe alikuwa wa kwanza kupiga penalti ya Ufaransa, bado kidogo Martinez amnyime bao kwa jinsi alivyoufuata mpira lakini ikashindikana. “Ningezuia shuti lake pia, niliruka vibaya lakini kila kitu nilikifanya kwa usahihi.”
Baada ya hapo akaokoa mkwaju wa Kingsley Coman kabla ya kuanza mbwembwe za kucheza golini ambazo inadhaniwa ‘zilimtoa mchezoni’, kiungo Aurelien Tchouameni aliyebeba matumaini makubwa ya Wafaransa lakini akapiga shuti lililotoka nje.
Hadi hapo Martinez akawa shujaa mwingine wa Argentina pengine baada ya Messi, na ingawa Kolo Muani alifunga penalti yake na Ufaransa kupata bao la pili, Argentina wakakamilisha hesabu baada ya Gonzalo Montiel kumalizia penalti ya mwisho iliyozaa bao lililotosha kuandika historia mpya ya Argentina kwenye fainali za Kombe la Dunia.


Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni alisema kwamba kabla ya mikwaju ya penalti, Martinez mwenye umri wa miaka 30 sasa aliwaambia wachezaji wenzake anenda kuokoa penalti.
Alipoulizwa kuhusu tukio la penalti lilivyokuwa, Martinez aliyetwaa tuzo ya kipa bora alisema,

“Sina la kusema, nilitulia wakati wa penalti na kila kitu kilienda kama nilivyokuwa nataka, yote yaliyokuwa kwenye ndoto zangu nimeyafanikisha.”

The post Martinez, kipa shujaa wa Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/12/20/martinez-kipa-shujaa-wa-argentina/feed/ 0