Antonio Rudiger - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 01 May 2025 20:49:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Antonio Rudiger - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rudiger afungiwa mechi 6, Bellingham afutiwa adhabu https://www.greensports.co.tz/2025/05/01/rudiger-afungiwa-mechi-6-bellingham-afutiwa-adhabu/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/01/rudiger-afungiwa-mechi-6-bellingham-afutiwa-adhabu/#respond Thu, 01 May 2025 16:28:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13347 Madrid, HispaniaBeki wa Real Madrid, Antonio Rudiger amefungiwa mechi sita baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya fainali ya Copa Del Rey dhidi ya Barcelona wakati mchezaji mwenzake, Jude Bellingham amefutiwa adhabu.Rudiger, Bellingham na Lucas Vázquez ambaye pia alifungiwa mechi mbili wote walitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika za nyongeza za mechi hiyo […]

The post Rudiger afungiwa mechi 6, Bellingham afutiwa adhabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Beki wa Real Madrid, Antonio Rudiger amefungiwa mechi sita baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya fainali ya Copa Del Rey dhidi ya Barcelona wakati mchezaji mwenzake, Jude Bellingham amefutiwa adhabu.
Rudiger, Bellingham na Lucas Vázquez ambaye pia alifungiwa mechi mbili wote walitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika za nyongeza za mechi hiyo ambayo Real Madrid ililala kwa mabao 3-2.
Wachezaji hao wote walitolewa baada ya kuibuka tafrani sababu ikiwa ni kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi wa mechi hiyo, Ricardo Bengoetxea.
Katika taarifa yake Bengoetxea alisema kwamba Rudiger ambaye tayari kocha wake alikuwa amemfanyia mabadiliko, alitolewa katika dakika ya 120 kwa kurusha kitu kwenye eneo la wasimamizi.
Katika tukio hilo la Jumamosi iliyopita ambalo mwamuzi alilitafsiri kuwa ni kuonesha tabia ya ukorofi, Rudiger alijikuta akizuiwa na wachezaji wenzake na maofisa wa benchi la Real Madrid.
Vázquez ambaye kama ilivyokuwa kwa Rudiger naye alikuwa amefanyiwa mabadiliko, kosa lake lilikuwa ni kuingia eneo la kuchezea wakati akijaribu kupinga baadhi ya maamuzi ya Bengoetxea.
Kuhusu Bellingham yeye alipewa kadi nyekundu mara baada ya mchezo kumalizika kwa kosa la kuwazonga waamuzi hadi kuzuiwa na wenzake wakati akipinga baadhi ya maamuzi yao, kosa ambalo Bengoetxea pia alilitaja kuwa ni tabia za ukorofi.
Mapema wiki hii, kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Hispania ilitangaza kwamba Rudiger atatumikia adhabu ya kukosa mechi sita wakati Vazquez atatumikia adhabu ya kukosa mechi mbili.
Baadaye Rudiger alijirudi kwa tukio hilo na kutumia mitandao ya kijamii kuomba msamaha kwa kilichotokea wakati wa mechi hiyo.

“Hakika hakuna msamaha kwa tabia yangu, samahani sana kwa hilo, baada ya dakika 111 sikuweza tena kuisaidia timu yangu na kabla ya filimbi ya kumaliza mchezo nilifanya kosa, samahani kwa mara nyingine kwa waamuzi na kila mmoja aliyesikitishwa,” alisema Rudiger.


Kamati ya nidhamu hata hivyo haikukubaliana na hoja ya klabu ya Real Madrid kudai kuwa kitendo cha Rudiger kujutia kosa lake baadaye kizingatiwe kabla ya kutoa adhabu badala yake ilisisitiza kwamba taarifa za kwenye mitandao ya kijamii haziwezi kutumiwa kuwa ushahidi unaojitosheleza.

The post Rudiger afungiwa mechi 6, Bellingham afutiwa adhabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/01/rudiger-afungiwa-mechi-6-bellingham-afutiwa-adhabu/feed/ 0
Rudiger kumdhibiti Haaland? https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/rudiger-kumdhibiti-haaland/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/rudiger-kumdhibiti-haaland/#respond Tue, 09 Apr 2024 08:35:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10563 Manchester, EnglandMan City leo Jumanne itaumana na Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi ambayo inatarajiwa pia kutawaliwa na mpambano baina ya mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland na beki wa Real Madrid, Antonio Rudiger.Rudiger alipata heshima akidaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kumdhibiti Haaland katika mechi ya kwanza ya nusu fainali […]

The post Rudiger kumdhibiti Haaland? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man City leo Jumanne itaumana na Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi ambayo inatarajiwa pia kutawaliwa na mpambano baina ya mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland na beki wa Real Madrid, Antonio Rudiger.
Rudiger alipata heshima akidaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kumdhibiti Haaland katika mechi ya kwanza ya nusu fainali msimu uliopita ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 kabla ya City kushinda kwa mabao 4-0 katika mechi ya marudiano.
Wakati mashabiki wakiwaza uwezekano wa kuwapo mpambano kati ya Rudiger na Haaland, kocha wa City, Pep Guardiola yeye anaamini wapinzani wao wataingia uwanjani kwa lengo la kulipa kisasi.
Kauli ya Pep inatokana na kumbukumbu ya matokeo ya mechi ya msimu uliopita yaliyoifanya City kusonga mbele hadi hatua ya fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 na hatimaye kubeba taji.
“Ni ngumu jambo hilo kujirudia mara ya pili, kuifunga Real Madrid mara mbili mfululizo ni jambo lisilowezekana, wamejifunza kitu na watataka kulipa kisasi, wana kitu cha kujivunia,” alisema Pep.
Kwa upande wake, Rudiger, beki wa zamani wa Chelsea alizungumzia jinsi walivyomdhibiti Haaland katika mechi ya kwanza ingawa alikosa nafasi katika mechi ya marudiano ambayo timu yake ilifungwa.
Akizungumzia hali ilivyokuwa katika mechi ya kwanza, Rudiger alisema mechi ilikuwa nzuri na walifanikiwa kumdhibiti Haaland kupewa pasi za kuzalisha mabao.

“Kocha hakuniomba radhi kwa kutonipa nafasi (mechi ya pili) na hahitaji kufanya hivyo, nalikubali hilo ingawa ni ngumu kulipokea, na sasa mpango wetu katika mechi hii ni kuwadhibiti wachezaji hatari kama Phil Foden, De Bruyne, na ipo wazi kwamba mwingine ni Haaland,” alisema Rudiger.


Rudiger pia alimsifia kiungo wao Jude Bellingham ambaye hakuwapo katika mechi iliyopita akisema kwamba atawaongeza nguvu kubwa katika timu yao kwenye mechi dhidi ya City.
“Awali nilishangaa sikuwa nikimjua sana, lakini acha tu jamaa yuko sawa, anakubalika hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, namna alivyo makini na mambo yake ni jambo zuri, ndio kwanza ana miaka 20 lakini ana mambo makubwa, kuna siku ataiongoza (timu ya taifa) England,” alisema Rudiger.
Mechi za leo Jumanne Ligi ya Mabingwa Ulaya
Arsenal v Bayern Munich
Real Madrid v Man City

The post Rudiger kumdhibiti Haaland? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/09/rudiger-kumdhibiti-haaland/feed/ 0